Ukamataji wa polisi na kupotea kwa wahusika serikali bado kimya

Kaka yake shetani

JF-Expert Member
Feb 1, 2023
3,611
8,746
Kila kukicha ni vilio vya wananchi kuhusu ndugu zao na mazingira wanayochukuliwa kwa njia ya kupitia jeshi la polisi.

Je ili tatizo litakishwa lini maana ujui yupo wapi ?.mikoa yote sasa ni vilio

ATEKWA KARIAKOO NA KUPOTEZWA KABISA!

Bw. Chande Kizenga (pichani) alitekwa na watu wasiojulikana siku ya tarehe 18 Agosti 2022 akiwa dukani kwake Machinga Complex, Ilala jijini Dar es Salaam. Kaka yake anasema kuwa alitekwa na watu waliodaiwa kuwa ni Askari Polisi na baada ya kumvamia dukani kwake waliondoka naye wakitumia gari aina ya Land Cruiser Hardtop yenye namba za kiraia na hata hawakumpa nafasi ya kufunga duka lake.

Mke wake alipopata taarifa alikwenda Polisi na akafika hadi Central akaonana na RCO ambaye alimpatia Askari wa kufuatilia. Inasemekana mke wa Chande Kizenga aliombwa rushwa ya shilingi milion 3 na mmoja wa Askari Polisi ili amsaidie kumnasua mumewe kwa madai kuwa jambo lilikuwa chini ya wakubwa. Lakini mke wa Kizenga hakuwa na hiyo fedha ila akataka kujua mume wake yuko Kituo gani cha Polisi lakini hakuambiwa. Miezi 6 sasa imepita tangu atekwe na hayupo kituo chochote cha Polisi, Magereza na hata Mochwari.

Taarifa zilieleza kuwa waliokamatwa siku hiyo walikuwa watu 9 na habari zao hazijajulikana hadi sasa walipo. Katika kufuatilia, kwa mujibu wa kaka yake Chande Kizenga, simu za watu wale wengine zilionekana kuzimiwa eneo la Salenda Bridge na wengine eneo ya Sitaki Shari karibu na Majumba Sita. Anasema kuna taarifa kuwa waliowakamata walitoka Kikosi Maalum kutoka Kituo cha Polisi cha Sitaki Shari. Hata hivyo, taarifa zinaarifu kuwa Askari wa Kikosi Maalum kutoka Sitaki Shari hawapo tena pale na kwamba wote wametawanywa mikoani.

Baada ya muda mwingi sana kupita na mke wa Chande Kizenga kufuatilia pasipo mafanikio, mmoja wa Askari Polisi alimwambia kuwa afanye dua kwani hakudhani Chande Kizenga kama angali bado anaishi. Mtu wa pili kusema maneno kama hayo alikuwa ni Polisi mmoja wa Kituo cha Tazara ambaye baada ya mke wa Chande Kizenga kwenda pale na kumsikiliza na yeye akamueleza kuwa aendelee kuomba dua na ikiwezekana waite kikao cha ukoo kumaliza mambo!

Taarifa hii ni kwa mujibu wa maelezo ya kaka yake Chande Kizenga. Sisi Askofu Mwamakula tunatoa wito kwa wahusika kutoa taarifa wapi Chande Kizenga na wenzake wengine 8 walipo.

Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!
Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula

Dar es Salaam, 25 Februari Anno Domino 2023.
FB_IMG_1677323162669.jpg
 
Back
Top Bottom