Mamlaka naomba iunde kikosi maalumu kichunguze tukio la kupotea kwa Askari Emmanuelle Govella

Nyanje

JF-Expert Member
Jul 25, 2013
278
250
Unajitoa mwenyewe, unadhani Askari officer WA nyota mbili anawezaje kupotea kienyeji hivo, zingatia maelezo hapo juu alikuwa mkuu wa Kituo fulani,alikuwa hapendelei kuvaa uniform akienda kazini badala yake alikuwa akibeba begi jeusi mgongoni, jiulize Kwa nini alikuwa anaficha identity? Defenitly was an agent undercover, jiulize Askari wa level officer commanding station anawezaje kupotea polisi wasitoe tamko mpaka ndg zake ndo wamtafute? Anzia hapo kujiuliza kama alivuruga mission huyo ndo umsahau, formula ni moja tu kwamba if the law doesn't work, Eliminate.
Nafkiri mimi na wewe wote hatujui ZAIDI ya kubashiri ndiyo maana nikaomba mamlaka zifanye uchunguzi tupate ripoti ya kweli.
 
mbu wa dengue

JF-Expert Member
Jun 2, 2014
6,406
2,000
Unajitoa mwenyewe, unadhani Askari officer WA nyota mbili anawezaje kupotea kienyeji hivo, zingatia maelezo hapo juu alikuwa mkuu wa Kituo fulani,alikuwa hapendelei kuvaa uniform akienda kazini badala yake alikuwa akibeba begi jeusi mgongoni, jiulize Kwa nini alikuwa anaficha identity? Defenitly was an agent undercover, jiulize Askari wa level officer commanding station anawezaje kupotea polisi wasitoe tamko mpaka ndg zake ndo wamtafute? Anzia hapo kujiuliza kama alivuruga mission huyo ndo umsahau, formula ni moja tu kwamba if the law doesn't work, Eliminate.
Huwa wanapotezwa milele au kuna muda ukifika wanaachiwa?

Sent from my SM-C7000 using JamiiForums mobile app
 
Nyanje

JF-Expert Member
Jul 25, 2013
278
250
hapana hapo kuna kimchezo kimechezeka inavyoonekana.
vinginevyo askari wenzake wangepiga makelele nchi nzima tungejua.
Ukiona wapo kimya ujue wanajua aliko.
Ukiwa mkuu wa kituo ni mtihani sana hasa pale unapotaka kutenda haki,kuna polisi wa chini yako ambao ni wakongwe wa madili wanakuangalia wewe,kuna wakuu wa polisi wilaya wanakuangalia wewe

Sent from my SM-C7000 using JamiiForums mobile app
Tuanzie hapo labda kama nimekuelewa
 
Rusumo one

JF-Expert Member
Oct 4, 2018
1,646
2,000
Nyanje kuwa muelewa Kuna kozi ya ASP inaendelea Kurasini na wanasongoka kwa sasa ukifeli inakula kwako hao ndg waeleze waende watamkuta ananyakua nyakua
 
Nyanje

JF-Expert Member
Jul 25, 2013
278
250
Nyanje kuwa muelewa Kuna kozi ya ASP inaendelea Kurasini na wanasongoka kwa sasa ukifeli inakula kwako hao ndg waeleze waende watamkuta ananyakua nyakua
Rusumo one nimefuatilia comments zako karibu zote nimegundua wewe ni empty headed nafkiri unachanganya fb na jf,jf ni home of Great thinkers.
 
ilala yetu

JF-Expert Member
Apr 10, 2015
688
1,000
Kwa hiyo binadamu ni polisi pekee,azori alivyopotea Igp akadai labda yupo anatafuta maisha sehemu,so i stand with igp huyo askari yupo anatafuta maisha sehemu au yupo kwa hawara
Hapa ndipo mnapokosea nyie watu wasiasa sio kila jambo lakuleta mizaha ya ccm na chadema,,..
Wengne hivyo vyama tunaviona f*** kbsa vyote sbbu ya ujinga ujinga ka huo,,..
Tujadili suala la mtu huyu kupotea,,..
Anzisha thread ya ndugu azory tutakuja kuchangia pia
 
Franco2

JF-Expert Member
Oct 20, 2019
225
500
Haieleweki ndugu yangu kwanza Sisi majirani tuliowengi miezi yote hatukuweza kujua kama jamaa ni askari mpaka ulipovunjwa mlango wake na kukuta uniform Tena alikuwa na nyota Mbili wenzake walisema alikuwa mkuu wa kituo Cha mtumba mji wa kiserikali nafkiri hakutaka watu wamjue kama ni askari.
alikuwa hata hafui hizo uniform
 
Nyanje

JF-Expert Member
Jul 25, 2013
278
250
Hapa ndipo mnapokosea nyie watu wasiasa sio kila jambo lakuleta mizaha ya ccm na chadema,,..
Wengne hivyo vyama tunaviona f*** kbsa vyote sbbu ya ujinga ujinga ka huo,,..
Tujadili suala la mtu huyu kupotea,,..
Anzisha thread ya ndugu azory tutakuja kuchangia pia
Hakika mkuu Kuna watu wanawaza ujinga wa siasa za maji taka muda wote wanafkiri kila mtu anahitaji masiasa siasa mtu kapotea badala ya kuchangia namna nini kifanyike yaani ni ccm v/s chadema+chuki basi ni upuuzi tu.
 
MTAZAMO

JF-Expert Member
Feb 8, 2011
16,712
2,000
Askari anapotea mwezi mzima bila Polisi kutoa taarifa yoyote? Hii ni issue kubwa kama ni kweli.
 
Mtanzatozo

JF-Expert Member
Mar 2, 2016
860
1,000
Mh rais nianze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kukupa Afya njema na kuweza kutekeleza vyema majukumu yako ya kitaifa,mh rais Nina ombi maalum kwako kama mwananchi wako ambaye nimeguswa Sana na tukio la kupotea kwa askari polisi Emmanuelle Govella wa kituo kidogo cha mtumba mji wa kiserikali hapa Dodoma.

Mimi ni jirani hapa Nkuhungu Dodoma na Nyumba ambayo polisi huyu alikuwa amepanga siku ambayo ndugu wa huyo polisi walifika na polisi wa kituo Cha kati dodoma kuvunja mlango ili kujua kwanini askari huyo hapatikani muda mrefu nilikuwepo karibu.

Ilikuwa kati ya tarehe 19| 20 mwezi huu wa saba baada ya kuingia ndani walikuta simu ikiwa na laini zake zote Mbili lakini pia walikuta wallet yake ikiwa na vitambulisho vyake vyote mpaka kadi ya benki pamoja na fedha tasrimu sikujua kiasi gani, namba yake 0768243998 inaonyesha alikuwa hewani mala mwisho ni tarehe 26june hata ukiangalia WhatsApp inaonyesha hivyo mpaka siku wanabomoa kwake zilisha pita siku 24 Sasa Kuna maswali najiuliza ni kweli kwamba askari anapotea ZAIDI ya wiki 3 bila wenzake kujua?

Ombi langu kwako MH RAIS uunde kikosi maalum kichunguze upoteaji wa askari huyu Emmanuel govella Mpaka Leo hii nakutumia maombi haya ni takribani mwezi mmoja na siku 5 askari huyu hajaonekana ,nakutakia majukumu mema na Mwenyezi Mungu akutangulie.
NAOMBA TU RAIS ASISAHAU KUWAHOJI VIZURI MAJIRANI WA HYU POLISI MPOTEVU..
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom