Mamlaka gani zinawajibika kufanya marekebisho ya barabara za mitaani?

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
1,817
4,568
Salaam Wadau,

Nimekuwa nikikutana na barabara mbovu mitaa mingi katika sehemu ninazoishi. Kunaweza kutokea sehemu Kuna dimbwi kubwa au korongo ambalo linaleta changamoto kwa wapitanjia au wenye magari.

Kwa mtaa ninaoishi imekuwa busara tu ya wanakikiji kumwaga vifusi au kuweka mawe ili kurahisisha uvukaji wa maeneo Mbalimbali.

Je, ni mamlaka au viongozi wa ngazi gani hasa wanapaswa kuwajibika kurekebisha barabara za mitaani ambazo si lami?
 
CCM bana!

Kwanza mkuu pole na changamoto ya barabara za mitaani kwako.

Magufuli aliapa kuuwa upinzani (upinzani hapa alimaanisha Chadema).

Alipoingia madarakani 2015 alikuta halmashauri nyingi (kama sio zote) zenye mapato makubwa zinaongozwa na wapinzani, na maendeleo yanafanyika. Sababu nia yake haikuwa maendeleo bali kuuwa upinzani, akachukua mapato mengine ya ndani ya halmashauri yawe yanaenda serikali kuu, ili ule wimbo wake wa 'ukichagua upinzani sahau maendeleo ' upate mantiki.

Sasa uwezo wa halmashauri kufanya yale mambo madogo madogo, eg kuwe dizeli kwenye greda la halmashauri ili likarekebishe barabara za mitaani kwako, uwezo huo haupo Tena.

Anyway, kuna mtalii mmoja anaitwa Paul makonda, siku akipita mtaani hapo muoneni anaweza akawawekea lami.
 
Back
Top Bottom