Kassim Majaliwa anatoa wapi mamlaka ya kubadili sheria za TRA?

seedfarm

JF-Expert Member
Feb 9, 2020
260
2,654
Tuache siasa kwenye mambo yaliyotungiwa sheria na bunge na ambayo mtu binafsi kama waziri mkuu hawezi kuyatengua kwa maneno ya jukwaani bila barua au muongozo

Matamko ya waziri mkuu kassim Majaliwa kariakoo kuwa TRA wafanye kazi kwa kauli zao za majukwaani bila barua au marekebisho ya sheria bungeni ni kuwahadaa wafanyabiashara

Kuna tuhuma kuwa watoto wa viongozi kariakoo wanauza matairi na hawalipi kodi kwa kigezo cha matamko ya Baba na Mama zao viongozi wakuu wa kitaifa mtaa wa livingstone street

Vijana wa TRA wanatishwa na watoto hawa wa vigogo kwa matamko ya simu na memo

Kwanini Kassim Majaliwa anaogopa kuwapa barua TRA ya kupindisha sheria za kodi bali analazimisha watekeleze matamko ya maneno yake mdomoni

Waziri mkuu majaliwa ameshangaza uma wa watanzania kuitaka mamlaka ya mapato Tanzania kufanya kazi kwa matamko ya wanasiasa na sio kwa kufuata sheria na utaratibu za fedha

Kassim Majaliwa analazimisha TRA wafanye kazi kwa maneno yao ya majukwaani na sio kwa maandishi au taratibu za fedha zilizotungwa na bunge

TRA ni taasisi ya uma sio mali ya wanasiasa,Ipo kisheria na inafanya kazi kwa kufuata sheria za kodi zilizotungwa na bunge

Kassim Majaliwa aache kuwadanganya wafanyabiashara awaambie ukweli kuwa hizo kodi zimetungwa na bunge lao na yeye hana uwezo wa kurekebisha sheria za kodi kwa matamko ya jukwaani

Kassim Majaliwa anapaswa kutambua walioanzisha TRA walianzisha kwa kufuata sheria na akitaka kurekebisha afuate sheria au yeye anataka kuturudisha kwenye kodi ya kichwa ya kufukuzana mitaani
 
Tuache siasa kwenye mambo yaliyotungiwa sheria na bunge na ambayo mtu binafsi kama waziri mkuu hawezi kuyatengua kwa maneno ya jukwaani bila barua au muongozo...
Yaani mtanzania anafanya jambo lenye nafuu kwa Watanzania wenyewe wewe unatuambia mambo ya sheria zilizotungwa na Bunge? Mazingira rahisi yakufanya biashara kwa wakati huu ni muhimu, kodi za mjerumani na zisizokuwa na tija hatuzitaki. Nyie ndio mnataka sheria za kuolewa na wanaume wenzenu sababu ni haki zenu binadamu.

Tunataka mazingira rahisi na rafiki ya kufanya biashara katika nchi hii, kama kuna sheria ndio muambiane nyie wenyewe mrekebishe, hatutaki kamata kamata za kifala kariakoo sio kama watu hawawezi kuwapasua ndio wameona heri nusu shari na PM kaelewa.

Watu wa karikaoo hawaongei na Mbwa wanataka mwenye mbwa, Makala leo ameamkia station kuelekea kituo kipya cha kazi.

Bado wewe na wenzako
 
Moja ya tatizo sugu kwa Tanzania ni watu hasa viongozi kutokuheshimu sheria tulizojiwekea. Pia kutokuwajibishana kwa kutoheshimu huko Sheria.

Kwenye kodi TRA wako sawa kusimamia Sheria. Matamko ya Viongozi wa nchi awe Rais au Waziri Mkuu kamwe hayawezi kuwa Sheria. Na nchi inaongozwa kwa Katiba na Sheria ( Utawala wa Sheria)
 
Regulations, hizi ni sheria ndogo zinazotungwa na waziri, ila sheria mama ya bunge hawezi
Sahihi kuna sheria mama hawezi badili , ila regulations anaweza kuzitoa kwa mamlaka aliyonayo kutoa risiti EFD hawezi kuifuta ila kuna hizi kodi sijui za store, nk zinaweza kuangaliwa upya

Alivyo ongea ni kama kuna mwanga mzuri ila tu isiwe siasa katika hili
 
Sheria tu Hana uwezo huo kikatiba Ila kanuni anaweza kuzisimamisha kwa muda na ndo alichosema
 
Mtoa mada ni afisa wa TRA ambaye kwa sasa kibarua kimenuka ile njia yao ya kirushwa rushwa K/Koo imekomeshwa

Lazma upanic bro hata ningekuwa mimi
Ila usijali fungua duka acha kazi
Baada ya miezi m3 titaongea lugha moja
Nakazia hoja Mkuu
 
Back
Top Bottom