Uchaguzi 2020 Mambo yatakayomrudisha Dkt. Magufuli ofisini tarehe 28 Oktoba

Elius W Ndabila

JF-Expert Member
Jul 17, 2019
322
645
MAMBO YATAKAYOMRUDISHA JPM OFISINI TR 28 OCTOBER.

Na Elius Ndabila
0768239284

Mh Dkt Magufuli Rais wa JMT jana amechukua fomu ya kugombea Urais kwa awamu ya pili kupitia Chama Cha Mapinduzi. Mh Magufuli anayeelezwa kuwa mzalendo namba moja wa Tanzania baada ya kuchukua fomu aliwaasa wanaCCM kufanya kampeni za kistaarabu na siku ya kupiga kura kujitokeza kwa wingi.

Wachambuzi wa masuala ya kisiasa tunauona Uchaguzi wa mwaka huu utakuwa ni uchaguzi rahisi kwa Mh JPM ukilinganisha na uchaguzi wa awamu yake ya kwanza. Watanzania wengi wanasema hatuwezi kuacha kumchagua Magufuli kwa kuwa sasa yeye ndiye jicho la Afrika. Watanzania wanasema watamchagua JPM kwa matendo yake na maneno yake. Wanasema miradi mikubwa na midogo midogo ndiyo itakayo mrudisha JPM kwa kipindi cha pili.

Niwakumbushe tu Watanzania moja ya miradi ambayo itaibeba CCM na ambayo inawafanya wapinzani wa CCM kuwa stressed muda wote.

MIUNDOMBINU, Kwa kipindi cha miaka mitano ya uongozi wa JPM ameendelea kuboresha miundombinu koto nchini. Watanzania wanatambua kuwa nchini kote Barabara za lami zinatandikwa na barabara za kawaida zinaboreshwa. Watanzania wameona barabara za juu Dar es salaam alimaarufu fly over, Watanzania wameona madaraja makubwa yaliyojengwa hapa nchini ambayo ni ngumu kuyataja yote likiwemo la Kilombero. Watanzania wanajua sasa kuna ujenzi wa reli ya mwendo kasi Dar to Mwanza, Watanzania wanajua kumalizika kwa reli hii itakuwa mwarobaini wa usafiri kwani itatumia muda mfupi kufika Mwanza.

Watanzania wanatambua kuwa karibu mikoa mingi viwanja vya ndege vinajengwa na vya zamani kuimarishwa, hii ni kutokana na JPM kununua ndege 11 ambazo kwa muda mwingi hazikuwepo. Watanzania wanajua usafiri wa majini umeboreshwa mara dufu kwa kununua meli mpya na kukarabati za zamani. Nenda ziwa Nyasa, Ziwa Tanganyika, Victoria utaambiwa JPM MITANO TENA. Kwa miaka mitano ya JPM suala la miundombinu linaenda kubaki kwenye kumbu kumbu za kihistoria.

AFYA, MH Magufuli akiwa anaingia madarakani alitambua afya ni jambo la muhimu katika kuchochea maendeleo. Kwa kutambua hilo alikazia mpango wa kujenga zahanati kwenye kila kijiji nchini. Leo hii tunazungumza kila kijiji kina zahanati inayotumika au inayoendelea kumaliziaa. Vituo vya afya vimejengwa na kuboreshwa. Leo hii ukienda Wilayani kwangu Ileje hususani kata ya Ibaba ukikiona kile kituo cha afya utadhani umefika kwenye hospitali ya Rufaa.

Hospitali za Wilaya zimejengwa nchini kote, kwa mara ya kwanza sisi Ileje tumejengewa hospitali ya Wilaya ambayo jengo tu la OPD Utadhani upo Mhimbili hizi zote ni kura za JPM. Hospital za rufaa na ndo usipime na vifaa vyake. Zamani hata CT scan ilikuwa mpaka Mhimbili, leo ukienda Rufaa Mbeya kazi inaishia pale pale. Katika uboreshwaji huu wa afya leo safari za India ambazo tulikuwa tunapoteza fedha nyingi zimeisha. Nani asiyejua kitengo cha moyo Dar es salaam sasa kinafanya kazi kubwa ambazo tulizoea kutumia fedha nyingi kwenda nje? Hii ni kazi za JPM na wanufaika wote watampatia kura za ndiyo.

ELIMU, JPM kwa miaka yake mitano ameboresha elimu kwa kiwango kikubwa. Inasemekana zaidi ya shule mpya 900 zimejengwa, shule za zamani zimeboreshwa, bajeti ya mikopo chuo kikuu imeogezeka mara dufu, haya ni tisa tu lakini kumi kipindi chake elimu ni bure kutoka chekechea hadi kidato cha nne. Huyu ndiye JPM ambaye watu wanasubiria kwa hamu kwenda kumpatia zawadi mwezi Oktoba.

HUDUMA ZA JAMII, Upatikanaji wa huduma za jamii umeboreshwa na kuwezeshwa. Kwa mfano suala la maji limetatuliwa kwa kiwango kikubwa. Kuna miradi mikubwa ya maji imetengenezwa na mingine inaendelea kuboreshwa. Upande wa Umeme kati ya vijiji 12000+ hadi sasa ni vijiji 9000+ vina Umeme.JPM ndiye jasiri na kinara anaye jenga mradi mkubwa wa Umeme kule mto Rufiji. Mradi huu ukikamilika pamoja na kelele za Wafuasi wa mabeberu shida ya umeme Tanzania itakuwa historia. Mradi huu ni mkubwa na utaifanya Tanzania kuuza umeme nje. Only JPM! JPM ndani ya miaka mitano amepeleka umeme zaidi ya vijiji 6000+, hii ndiyo inafanya wananchi wamsubirie kwa hamu kumpatia zawadi kunako OCTOBER 28.

Yapo mambo mengi, kila unapokanya unakutana na kazi ya JPM. Hawa wengine wanagombea tu kwa kuwa ni haki ya kikatiba, lakini wanatambua fika hawawezi kumtikisa JPM. Kuonyesha kuwa mwaka huu kuna kazi rahisi, Jana Katibu Mkuu ameziachia Jumuiya za chama kufanya kampeni ili Mh Rais aendelee na majukumu mengine. Maeneo mengi jumuiya zitafika kutoa elimu ya kazi za JPM.

#JPMMITANOTENA.
 
Uchaguzi ukiwa JPM vs Lissu. Basi Lissu atashinda. Ila Membe nae akirudisha form basi nichelee kusema Magufuli atashinda.
 
Hivi unakumbuka wakati mnamzika mkapa mlisema yeye ndie aliyejenga foundation wengine wote wametembelea miguu take? Basi Hakuna jipya kwa JPM zaidi ya kuzindua miradi waliyoanzisha wengine.
 
Uchaguzi ukiwa JPM vs Lissu. Basi Lissu atashinda. Ila Membe nae akirudisha form basi nichelee kusema Magufuli atashinda.
Naona ulikiw ukiwaza kama kidgo,kama mimi. Huenda hizi games za kugawanya kura.
 
Kama Uchaguzi utakuwa bila kushikisha Polisi na Tume na Wakurugenzi kukimbia na Kufunga Ofisi ili Wasipokee Fomu za Wapinzani Uko sahihi
 
Nakuona mtendaji wa kata bwana Shilatu, ukiendelea kujipendekeza na namba ya cm juu Hahahaaaaa kaazi kweli kweli!
Unaishi Kakonko unashangila fly over ya dar?

Siku huyo jiwe wenu akipigwa chini mtaishi maisha mabaya sana, na ni bahati nzuri tunawafahamu. Time will tell
 
Hivi unakumbuka wakati mnamzika mkapa mlisema yeye ndie aliyejenga foundation wengine wote wametembelea miguu take? Basi Hakuna jipya kwa JPM zaidi ya kuzindua miradi waliyoanzisha wengine.

Kama ni nyumba ukijenga fondesheni ukaaicha kuendeleza utakaa humo?
 
Hivi unakumbuka wakati mnamzika mkapa mlisema yeye ndie aliyejenga foundation wengine wote wametembelea miguu take? Basi Hakuna jipya kwa JPM zaidi ya kuzindua miradi waliyoanzisha wengine.
Hivi huwa mnafikiria kwa kutumia nini...?
 
Basi mpe credit na fundi aliyedizaini na kujenga hiyo foundation. Sio ww umepaka rangi tu ndio unaona umefanya kazi kuuubwaa

Hilo neno kupiga rangi limeniguza kwelikweli maana mimi ni fundi mchundo rangi. Ila ni kuulize SGR ni kupiga rangi?
 
MAMBO YATAKAYOMRUDISHA JPM OFISINI TR 28 OCTOBER.

Na Elius Ndabila
0768239284

Mh Dkt Magufuli Rais wa JMT jana amechukua fomu ya kugombea Urais kwa awamu ya pili kupitia Chama Cha Mapinduzi. Mh Magufuli anayeelezwa kuwa mzalendo namba moja wa Tanzania baada ya kuchukua fomu aliwaasa wanaCCM kufanya kampeni za kistaarabu na siku ya kupiga kura kujitokeza kwa wingi.

Wachambuzi wa masuala ya kisiasa tunauona Uchaguzi wa mwaka huu utakuwa ni uchaguzi rahisi kwa Mh JPM ukilinganisha na uchaguzi wa awamu yake ya kwanza. Watanzania wengi wanasema hatuwezi kuacha kumchagua Magufuli kwa kuwa sasa yeye ndiye jicho la Afrika. Watanzania wanasema watamchagua JPM kwa matendo yake na maneno yake. Wanasema miradi mikubwa na midogo midogo ndiyo itakayo mrudisha JPM kwa kipindi cha pili.

Niwakumbushe tu Watanzania moja ya miradi ambayo itaibeba CCM na ambayo inawafanya wapinzani wa CCM kuwa stressed muda wote.

MIUNDOMBINU, Kwa kipindi cha miaka mitano ya uongozi wa JPM ameendelea kuboresha miundombinu koto nchini. Watanzania wanatambua kuwa nchini kote Barabara za lami zinatandikwa na barabara za kawaida zinaboreshwa. Watanzania wameona barabara za juu Dar es salaam alimaarufu fly over, Watanzania wameona madaraja makubwa yaliyojengwa hapa nchini ambayo ni ngumu kuyataja yote likiwemo la Kilombero. Watanzania wanajua sasa kuna ujenzi wa reli ya mwendo kasi Dar to Mwanza, Watanzania wanajua kumalizika kwa reli hii itakuwa mwarobaini wa usafiri kwani itatumia muda mfupi kufika Mwanza. Watanzania wanatambua kuwa karibu mikoa mingi viwanja vya ndege vinajengwa na vya zamani kuimarishwa, hii ni kutokana na JPM kununua ndege 11 ambazo kwa muda mwingi hazikuwepo. Watanzania wanajua usafiri wa majini umeboreshwa mara dufu kwa kununua meli mpya na kukarabati za zamani. Nenda ziwa Nyasa, Ziwa Tanganyika, Victoria utaambiwa JPM MITANO TENA. Kwa miaka mitano ya JPM suala la miundombinu linaenda kubaki kwenye kumbu kumbu za kihistoria.

AFYA, MH Magufuli akiwa anaingia madarakani alitambua afya ni jambo la muhimu katika kuchochea maendeleo. Kwa kutambua hilo alikazia mpango wa kujenga zahanati kwenye kila kijiji nchini. Leo hii tunazungumza kila kijiji kina zahanati inayotumika au inayoendelea kumaliziaa. Vituo vya afya vimejengwa na kuboreshwa. Leo hii ukienda Wilayani kwangu Ileje hususani kata ya Ibaba ukikiona kile kituo cha afya utadhani umefika kwenye hospitali ya Rufaa. Hospitali za Wilaya zimejengwa nchini kote, kwa mara ya kwanza sisi Ileje tumejengewa hospitali ya Wilaya ambayo jengo tu la OPD Utadhani upo Mhimbili hizi zote ni kura za JPM. Hospital za rufaa na ndo usipime na vifaa vyake. Zamani hata CT scan ilikuwa mpaka Mhimbili, leo ukienda Rufaa Mbeya kazi inaishia pale pale. Katika uboreshwaji huu wa afya leo safari za India ambazo tulikuwa tunapoteza fedha nyingi zimeisha. Nani asiyejua kitengo cha moyo Dar es salaam sasa kinafanya kazi kubwa ambazo tulizoea kutumia fedha nyingi kwenda nje? Hii ni kazi za JPM na wanufaika wote watampatia kura za ndiyo.

ELIMU, JPM kwa miaka yake mitano ameboresha elimu kwa kiwango kikubwa. Inasemekana zaidi ya shule mpya 900 zimejengwa, shule za zamani zimeboreshwa, bajeti ya mikopo chuo kikuu imeogezeka mara dufu, haya ni tisa tu lakini kumi kipindi chake elimu ni bure kutoka chekechea hadi kidato cha nne. Huyu ndiye JPM ambaye watu wanasubiria kwa hamu kwenda kumpatia zawadi mwezi Oktoba.

HUDUMA ZA JAMII, Upatikanaji wa huduma za jamii umeboreshwa na kuwezeshwa. Kwa mfano suala la maji limetatuliwa kwa kiwango kikubwa. Kuna miradi mikubwa ya maji imetengenezwa na mingine inaendelea kuboreshwa. Upande wa Umeme kati ya vijiji 12000+ hadi sasa ni vijiji 9000+ vina Umeme.JPM ndiye jasiri na kinara anaye jenga mradi mkubwa wa Umeme kule mto Rufiji. Mradi huu ukikamilika pamoja na kelele za Wafuasi wa mabeberu shida ya umeme Tanzania itakuwa historia. Mradi huu ni mkubwa na utaifanya Tanzania kuuza umeme nje. Only JPM! JPM ndani ya miaka mitano amepeleka umeme zaidi ya vijiji 6000+, hii ndiyo inafanya wananchi wamsubirie kwa hamu kumpatia zawadi kunako OCTOBER 28.

Yapo mambo mengi, kila unapokanya unakutana na kazi ya JPM. Hawa wengine wanagombea tu kwa kuwa ni haki ya kikatiba, lakini wanatambua fika hawawezi kumtikisa JPM. Kuonyesha kuwa mwaka huu kuna kazi rahisi, Jana Katibu Mkuu ameziachia Jumuiya za chama kufanya kampeni ili Mh Rais aendelee na majukumu mengine. Maeneo mengi jumuiya zitafika kutoa elimu ya kazi za JPM.

#JPMMITANOTENA.
Miundombinu haimrudishi magu, watu wamemchoka hana jipya na hatuoni maendeleo ya kweli kwa watu, tunasikia tu maendeleo ya madaraja na viwanda visivyoonekana wala kuwa na impact kwenye maisha ya watu.
 
Atake Asitake Tutamwongezea Miaka Mingine Atakapomaliza.
Mpaka Afie Kwenye Kiti
 
Atake Asitake Tutamwongezea Miaka Mingine Atakapomaliza.
Mpaka Afie Kwenye Kiti
 
Nakuona mtendaji wa kata bwana Shilatu, ukiendelea kujipendekeza na namba ya cm juu Hahahaaaaa kaazi kweli kweli!
Unaishi Kakonko unashangila fly over ya dar?
Siku huyo jiwe wenu akipigwa chini mtaishi maisha mabaya sana, na ni bahati nzuri tunawafahamu. Time will tell
Time has already told
 
Back
Top Bottom