Mambo yanayothibitisha ushamba wa Mwanaume mwenye miaka 30-45

mwanyaluke

JF-Expert Member
Jan 22, 2015
473
1,448
Kuna vitu ukivifanya au ukawa unaviongelea huwa vina proove ushamba wako na ulimbukeni, na kumbuka kila rika na umri una vitu vinavyopendwa kwa wakati huo, so ukifanya kinyume na hapo jua tu wanaokuzunguka wanakuona mshamba.

1. Kujisifu elimu au kazi yako, tunakula bia tumekaa tupumzishe vichwa unanza kuleta stori za degree yako au kazi yako ilivyo nzuri, katika umri huu kila mtu ana elimu na kazi yake.

2. Mavazi, hapa huwa tunatambuana sana zipo nguo za kuvaa kulingana na mazingira, hapa unaweza chomekea vizuri na ukapita mahali wasikushangae, unaweza vaa njisi, boot nk wata wakakuelewa, ila sijui umevaa suruali la kitambaa tena rangi zile wasukuma wanapenda mara suruali au shati vina rangi ya dhambarau jua watu wanakuona mshamba tu( dress code muhimu na kiatu kinamua kila kitu kuhusu wewe)

3. Kujisifia mkeo au mchumba wako mzuri, umri huu watu waisha ona mengi relax hawako na interest ya sura ya mkeo.

4. Kujifanya msomi, kutuchanganyia lugha (code switching) watu lazima wakuone wewe fala flani hivi.

5. Kujisifia pesa, magari au nyumba, tukikaa wahuni sio stori za kusema sijui IST yangu inakimbia hiyo, hizi stori za magari nyumba au nina pess wanapenda kuzungumza wale wenzangu wajiriwa wa TAMISEMI hawa wanapenda kuzungumza kwa sababu ya kipato chao duni so anapomililki ist , spacio na kibanda huwa anaona ametoboa so anataka awe mtu wa mfano.

6. Kutuletea stori za wasanii wasanii Mboso sijui anapiga Wema Sepetu, ukiona hizi ni stori zako jua tunakuona wewe fala sana na mshamba. 7. kujisifu kuwa wewe umepiga demu flani ,aisee umri huu hatuoneani wivu eti umepiga ngare flani , umri huu kila mtu ana nafasi ya kuchukua yoyote , sema ni umri ambao wanawake wapo wengi ila wanaume hatuna muda 8. leta mengine watanzania wapunguze ushamba , stori hizi zinakufanya uonekane mwenzetu 1. zungumza mpira,ngumi , 2. zungumza ibada na njisi gani unapambana na shwetani 3.tuambie kuhusu deal za biashara 4. sema changamoto za malezi ya watoto,ndoa na migogoro ya familia na wewe unashinda vip hizo changamoto 5. leta stori za njisi ya kuishi vizuri kwenye vipato vyetu, wengi tuna vipato ila hatujui tutumie vip
 
Acha ushamba...

Namba 1, 2 na 3 umezificha ili iweje..? Nimetumia torch kuzitafuta.

Panga vizuri uzi wako
 
  • Kicheko
Reactions: EEX
Kijana inaonekana huna future na maisha, unaonekana maisha yamekupiga sana... Nikushauri tu fanyakazi kwa maarifa na bidii, halafu anza kuwaona wenzako ktk muonekano chanya ili nawewe ufanikiwe... Sikuhiz hivyo vitu ulivyo vitaja ni vya kawaida sana mtu kuwa navyo ushamba wako na umasikini wako ndio unakufanya uone watu kwa namna hasi
 
Kijana inaonekana huna future na maisha, unaonekana maisha yamekupiga sana... Nikushauri tu fanyakazi kwa maarifa na bidii, halafu anza kuwaona wenzako ktk muonekano chanya ili nawewe ufanikiwe... Sikuhiz hivyo vitu ulivyo vitaja ni vya kawaida sana mtu kuwa navyo ushamba wako na umasikini wako ndio unakufanya uone watu kwa namna hasi
Ni kweli nimepigwa na maisha na sina future, ila usishangae maisha yangu yakawa ndio mfano wako na nilipofika ikawa ni future unayoitamani na huwa unawambia wenzanko kuwa ukifika level flan utakuwa sawa
 
.........bila kujali umri kama ulivyodokeza, jambo ulilolisema lina pande mbili......kwamba linaweza kuwa sahihi Kwa upande mmoja lakini lisiwe sahihi Kwa upande mwingine........hoja yako ni sahihi kwa sababu kibusara huwa si sahihi kujisifu au kujitangaza mbele za watu unamiliki nini au wewe ni nani, hii inasense kama kujikweza na kuringa.......

Hoja yako inaweza isiwe sahihi Kwa msingi wa kwamba wengi wetu tusio na mafanikio japo kidogo, huwa hatupendi kusikia wala kuona ustawi wa wenzetu....sasa utagundua kumbe tulio wengi hatupendi kusikia kwa sababu ya wivu na si lingine, ndo ile unasikia mtu kanunua gari watu wanataka kila siku akipita karibu na kijiwe chao ashushe vioo awasalimie then aendelee....

Hivi vingine vya wasanii au kuvaa nguo za dhambarau ni very minor and too personal......yaani mtu amevaa zake nguo udhurungi na mke wake kamwambia umependeza we mwingine unaumia!!......
 
ni kweli nimepigwa na maisha na sina future, ila usishangae maisha yangu yakawa ndio mfano wako na nilipofika ikawa ni future unayoitamani na huwa unawambia wenzanko kuwa ukifika level flan utakuwa sawa
😂😅 Wee ng'ombe tu tena ng'ombe shoga... Huna maisha ndiyo maana unaonea wivu wanaume...
 
Hapa kuna hoja ila naona wadau mnashambulia mleta mada. Binafsi nimejisifu na mambo karibia yote uliyo yataja nikiwa under 30. Vp mkuu sasa hivi itakuwa vibaya nikijisifu na company niliyo isajili au nipotezee.
 
Kuna vitu ukivifanya au ukawa unaviongelea huwa vina proove ushamba wako na ulimbukeni, na kumbuka kila rika na umri una vitu vinavyopendwa kwa wakati huo, so ukifanya kinyume na hapo jua tu wanaokuzunguka wanakuona

Katiba mpya hamna hapo? Upi utakuwa mchango wako kwa taifa hili?
 
ni kweli nimepigwa na maisha na sina future, ila usishangae maisha yangu yakawa ndio mfano wako na nilipofika ikawa ni future unayoitamani na huwa unawambia wenzanko kuwa ukifika level flan utakuwa sawa
Kuna mahali nimeosoma na wewe unajisifu umejenga nyumba tatu,umerithi nyumba moja etc na wewe ni mshamba?
 
Back
Top Bottom