Ushauri kwa vijana

KJ07

JF-Expert Member
Dec 17, 2021
2,243
5,000
Nimeikuta mahala na nina inukuu kama ifuatavyo

NAMNA WAZAZI WANAVYOONGEA NA MABINTI ZAO KATIKA UMRI TOFAUTI.
Miaka 13: Usipende wavulana ni wabaya sana.
Miaka 16. Sitaki kukuona na yule kijana.
Miaka 23. Lini utatuletea mchumba wako.
Miaka 26. Wenzako wanaolewa umebaki wewe.
Miaka 30. Tumekuambia kwamba acha kuchagua wanaume sana, hutaki kusikia.
Miaka 33. Kuna mtumishi wa Mungu yupo kule anaombea sana watu unaweza ukapata mchumba.
Miaka 36. Umri unakwenda At least pata mtoto mmoja basi.
Miaka 39. We will take care of all the wedding bills. Leta yeyote sawa sisi tutagharamia kila kitu mwenetu.
Miaka 40. Hivi ni nani aliyekuloga kweli?
Prove, Take Care!πŸƒπŸ‚πŸ„πŸ‡πŸ‡

ANGALIA UMRI WAKO, UPO SAHIHI? UMEKOSEA? UNAHITAJI KUJIREKEBISHA?!!!

20 - 25 = Kama ni kielimu hujafikia malengo yako, sitisha mara moja tafuta kazi/biashara ya kufanya, pigana kufa na kupona ili kama vipi urudi shule kwa pesa yako.

25 - 30 = Hakikisha uwe na angalau KAZI RASMI kama umeajiriwa au umejiajiri au una shughuli yeyote ya kukuingizia kipato.

30 - 35 = Uwe na angalau kama sio nyumba basi kiwanja, tena ujitahidi uwe umeoa/umeolewa. Ni vema ukiwa na familia, kwa maana ya kuwa na watoto kama Mungu kakuwezesha.

35 - 40 = Ni wakati kiwanja kiwe kimejengwa na kama ni tayari basi nenda step nyingine ya kumiliki kama ni Gari au kuongeza nyumba na hakikisha vinaenda sambamba na ongezeko la familia. Hapa inabidi upambane sana kuweka misingi.

40 - 45 = Ni umri wa masahihisho, kama hukuwahi kununua kiwanja, kama hukujenga basi hapa pambana afe kipa afe beki, ni umri wa masahihisho. Ila kwa wale ambao wameenda vizuri huko nyuma basi hapa watoto wapo kwenye level tofauti za elimu, kwahiyo ni muda wa kuwawekea malengo ya kimasomo watoto wao.

45 - 50 = Kwa yule ambae hakukosea huko nyuma basi umri huu ni wa kuanza kuwatengenezea mazingira watoto wako, kama ni shughuli zako ni kuanza kuwahusisha, huku wewe ukijiweka pembeni taratibu na kuangalia fursa za umri wako. Lakini kwa wale waliokosea hapa ni kupitia zile hatua za 35 - 40.

50 - 60 = Ni kujiandaa na maisha mapya ya kustaafu au kujiweka mbali na kazi zinazotumia nguvu au akili nyingi.

60 - 70 = Kula matunda yako huku ukiangalia misingi ya wanao inaendaje.

70 - 80 = Kula matunda

80 - nk = Umri wa kusubiria mauti

Yote kwa yote, maisha yetu yapo mikononi mwa MUNGU, kumbuka kufanya Ibada wakati wote...

Wengi itakuwa bado miaka miwili, mitatu au minne kabla ya kutimiza miaka 30. Natambua kuwa kuna waliokwisha fikisha na kuna uwezekano kuna walio nyuma kidogo.
Kama katika umri tulionao sasa kuna mtu anakuambia wewe bado ni mdogo/mtoto, basi huyo mtu hakupendi na anakulemaza kiakili. Kua! Acha utoto! Mambo yafuatayo kwa vigezo vya kibinadamu mwenye akili timamu, mtu mwerevu lazima uwe ushayatimiza.

1) Kuweka misingi ya kifamilia:
Katika umri huo unatakiwa uwe umeoa, umechumbia au uko katika uhusiano wenye kueleweka unaelekea kwenye kujenga familia. Kama katika umri huu bado unabadilisha wanawake na kudandia vicheche, basi sahau kuwa na familia imara. Mambo yafuatayo yatakuwa yanakunyemelea;
– Kuoa/kuolewa msichana/mvulana mdogo sana ambaye atakuona unamzeesha
– Kuoa /kuolewa chapchap bila kuwaza
-Kuokoteza magonjwa ya hatari
– Kunogewa na usela na kusahau kuoa/kuolewa

2)Kujitegemea kiuchumi:
Hapa simaanishi kufanya kazi na kupata mshahara pekee, la hasha! Hapa nalenga wale watoto wa mama ambao pamoja na kuwa wana kazi na mishahara, bado wanalalama mishahara haitoshi na kukimbilia kuomba hela nyumbani wanapoishiwa mara kwa mara. Wale ambao bado wanakaa nyumbani hii inawahusu pia. Pia wale wanaotumia 100% ya mishahara kununua vitu vinavyoisha (consumption) wakingoja wapate hela nyingi au wazazi, ndugu na jamaa wawasaidie kwenye uwekezaji. Africa tunachelewa sana kwenye hii sector.

3) Kuwa na kitega uchumi:
Kama unadhani mshahara wako wa milioni kadhaa ni mwingi sana, ngoja augue mtu wa karibu au wewe mwenyewe halafu daktari akuambie mgonjwa wako/wewe ana/unatakiwa ape/upelekwe nje ya nchi kwa matibabu zaidi wakati huna bima ya afya inayolipia hilo ndo utajijua kama mshahara wako heshima yake inaishia samaki samaki au inavuka border. Kitega uchumi si lazima uwe na mkampuni mkubwa, la hasha! Ila uwe na kitu cha kueleweka na chenye malengo ya kukua kuwa kitu cha maana. Kwa wale wagumu kuelewa, UNATAKIWA UWE NA PATO LA PEMBENI NJE YA MSHAHARA.

4) Makazi:
Uwe hata na kiwanja hapo Bunju Arif! Huezi kunywa bia kila weekend halafu wenzio wakiongelea issues za nyumba/viwanja/mashamba yao unakimbilia kubadilisha mada (Eti Huyu LVG wamuondoe kabisa anaharibu timu). Kumbe unazuga kupotezea story za viwanja/nyumba.

5)Uwe na professional qualification
ACCA, CPA, CFA, CSIA, CPB, LAW SCHOOL ETC wale wa procurement wana ya kwao n.k. Ikifika huu umri kama CPA imekataa, tafuta hata mitihani za marketing upige, CPA sio issue zako. Lazima uwe na defined career (Kama hukubahatika kwenda kidato kingi, uwe na namna ya halali na ya kudumu ya kukupatia kipato). Umri huu kama huna utaalam katika fani yako, jiandae kuwa frustrated ofisini. Madogo wanasoma jamaa angu! Halafu wako tayari kupewa salary ndogo wapige kazi kuliko wewe.. So take care!

6) Uwe ushaamua ka hicho kitambi unakiondoa au unakilea:
Hapa sichekeshi! Kitambi kina madhara mengi. Suruali haikai vizuri, UTAPIGIWA, Kisukari, pressure n.k. Ukikinyamazia muda huu jua kitakuwa kishakomaa na majukumu yatakuwa mlima. Ukikiachia kijiamulie, kitakuganda kama β€œroba ya mbao” till death does you apart! Kama unakipenda endelea nacho, kama hukipendi uwe ushaweka program ya kukiondoa.

7)Uwezo wa kusaidia wanaokutegemea:
Kama we ni wa kishua, hapa hapakuhusu. Wewe ambaye si wa kishua, wazazi walikuwa na mategemeo flani walipokuwa wanakusomesha. Kama umefika miaka 30 hujaanza kuyatimiza mategemeo yao bila sababu ya msingi, jua watakuwa washakata tamaa na wewe.

8) Uwe na busara.
Kuwa mtu wa kufikiri kabla ya kutenda. Tengeneza haiba nzuri na ya kuheshimika kwa wanaokuzunguka. Kama huna busara hadi umri huu basi we sahau suala la busara ukiwa hai.. Labda utakutana nayo akhera.!

9) Savings:
Hapa nimeweka kizungu kuonyesha msisitizo. Kila mtu ana kipato chake. Ila formula ni kwamba angalau uwe ushahifadhi fedha sawa na mishahara yako ya mwaka na nusu gross of Tax kwa kipindi hicho. Kwa wale wagumu kuelewa namaanisha Ukiacha kazi au kusimamishwa kazi, uwe na uwezo wa kukaa mwaka na nusu bila kuingiza kitu chochote lakini uendelee kuishi maisha yale yale.

10) Umjue Mungu:
Nimeliweka hili mwisho si kwamba ni la mwisho kwa umuhimu, La hasha! Ni ili ulikumbuke zaidi. Mjue Mungu, mpende na umuogope. Nenda ibadani, soma neno lake na umuombe. Uwe na desturi ya kusali nyumbani kwako angalau kila unapoamka na wakati wa kulala. Kama humuogopi Mungu katika umri huu, basi wewe kwenda Mbinguni ni ngumu kuliko ngamia kupenya tundu la sindani (hata kama ni masikini).
πŸ’–πŸ’–πŸ’žπŸ’žπŸ’žπŸ’•πŸ’•πŸ’•πŸ’•πŸ’πŸ’

12 Mtu awaye yote asiudharau ujana wako, bali uwe kielelezo kwao waaminio, katika usemi na mwenendo, na katika upendo na imani na usafi.

1Timothy 4:12
πŸ•ŠπŸ•ŠπŸ•ŠπŸ•ŠπŸ•Š
 
Ntaelezea nikitulia ila aging is inevitable all you need is to control ur mind and not focus on ur Age and fear of death toward success
Lakini kwa mtazamo wa watu wazima wa makamo(50-70)
Wanaamini kwamba vijana kuna vitu hawavistahili au hawatakiwi kufika maeneo hayo.
Binafsi namshukuru mzee wangu kwani hajawahi kunionyesha dalili za kuwa na mitazamo hiyo na ananisupport kwa kila hali
 
Lakini kwa mtazamo wa watu wazima wa makamo(50-70)
Wanaamini kwamba vijana kuna vitu hawavistahili au hawatakiwi kufika maeneo hayo.
Binafsi namshukuru mzee wangu kwani hajawahi kunionyesha dalili za kuwa na mitazamo hiyo na ananisupport kwa kila hali
Miaka 50-70 sio miaka mingi Sana unachobidi ni kuhakikisha unakuwa na ukomavu wa MAARIFA na hekima


Umri mkubwa sio tatizo maana huwezi kuzuia ila tatizo litaanza kujitoneza pale utakapojikuta una umri mkubwa ila hauna hekima na ukomavu wa MAARIFA hili ndo tatizo maana huwezi kuwa tunu au hadhina Kama hauna ukomavu wa MAARIFA na hekima.


Ikiwa utawaza sana kuhusu umri utapotea njia ila kila kunapokucha waza kuongeza Maarifa na kuwa na hekima ,ukarimu na kujua thamani yako .


Kitu unachobidi kujua Binadamu Akili yake huwa haizeeki kinachozeeka ni mwili wa Nyama Sasa usije ukasema una miaka 50-70 eti hauna mchango hiyo sio Kwel


Pia kitu kibaya kinachowafanya wazee wa Africa washindwe kuishi vizuri ni pale wanapoamini wao wanajua kila kitu na kuacha kujifunza mambo mapya ya kuijenga Akili Yao na mwisho kuonekana hawana mchango katika jamii.
 
Back
Top Bottom