Mambo ya kuzingatia kwa waleta simulizi na wafuatiliaji wake

Mkwawe

JF-Expert Member
Jun 10, 2016
2,345
4,168
'Chai'
Aisee hili neno linakata mdadi sana humu jamiiforums. Mtu ameamua kuleta kisa chake ambacho anaamini kwa uzoefu alioupitia anaweza kuwasaidia watu wengine kimtazamo na yeye binafsi kupata mawazo mapya maana kujifunza hakujawahi kuisha.

Binafsi mimi ni mpenzi sana wa simulizi hasa mikasa ambayo ni ya kweli inayowasilishwa na watu, na katika mitandao ambayo ninaiamini kwa asilimia zaidi ya tisini kwa kuwa na visa vya ukweli ni hapa Jamiiforums. Sio kwamba mitandao mingine hakuna visa vya kweli HAPANA, ila vingi kati ya hivyo hupikwa, japo hata baadhi ya visa c vingine vya kutungwa hufunza sana.

Kwenye hili jukwaa la burudani binafsi ninachota maarifa sana na ndiyo maana huwa sichagui mada ya kusoma kwa sababu mazingira hayamchagui mtu ila mtu ndo huchagua mazingira. Mimi husoma visa vya mapenzi, mikasa, siasa, harakati za kiusalama na uchumi, elimu, uchawi na kadhalika kwa kuwa jamii yetu imekusanya vyote hivyo.

Basi baada ya kutangulia kusema hayo nianze kwa kutoa pongezi kwa watunzi wote wa simulizi mnaozileta humu Jamiiforums iwe za kubuni au za kweli kwa sababu namna moja au nyingine zitapuna kampani kubwa sana tunapokuwa wenyewe kwahiyo watunzi wote heshima yenu nawapa kwa kazi kubwa ya kutenga muda wenu na kutuletea burudani na mafunzo bila malipo.

Mbali na hayo Kuna vitu vya kuzingatia kwa wasimuliaji wote wanaoleta simulizi humu...
•Kwanza kabisa ni lazima uwe imara kisaikolojia pindi unapoleta simulizi humu maana mbali na kazi nzuri ambayo utakuwa umeleta sio wote watakaopokea katika mtazamo unaoutarajia, wapo watakaokukosoa hata bila tija na wapo watakaokusifu ( hawa huwa ni wengi na wengi wao sio wachangiajia sana)
•Kuwa na ratiba ambayo itawatayarisha wafuatiliji wako kuzingatia, kama ni muda maalamu ambao pia utakupa uhuru hata wewe binafsi
•Zingatia maoni chanya (japo hasi hayawezi katu kukosekana). Binafsi hakuna hadithi niliyowahi kuisoma humu ikakosa kukosolewa kwa hiyo ni kawaida hivyo ni vizuri ukazipuuza jumbe hasi na kuzipa kipaumbele zile chanya na nadhani Kuna namna ya kumpuuza mtu kama hupendi michango yake kwa kubofya neno 'ignore' kwenye wasifu wake baada ya kuuchungulia
•Na jambo la mwisho ni katika kujibu michango nadhani ni vyema kujibu ile yenye ulazima na hata ikitokea Kuna mchango umekukera ni vyema ukauacha maana hata huo mchango hasi pia hisaidia kwenye kuuchangamsha uzi na kuwa na ukubwa kwa wafuatiliaji

Kwa wasomaji Kuna vitu kadhaa vya kuzingatia wakati unafuatilia simulizi...
•Kwanza inabidi umheshi mleta simulizi kwa kuaxha yote na kutenga muda ili wewe upate wasaa wa kuburudika na kujifunza huku ukisogeza muda mbele.
•Kuwa na subira katika simulizi unayoifuatilia, lazima tijue kuwa mleta simulizi naye ana shughuli kando ambazo hufanya hivyo lazima Kama mtu mzima unapoona uzi haujaja kwa muda uliotarajia ukawa mvumilicu na kutafualta chanzo kingine cha kukuweka 'busy'. Habari ya kushinikiza kisa arosto na kutoa lugha isiyofaa si njema
•Kama simulizi hujaipenda achana nayo, hata zipo simulizi nyingi sana sikizipenda ila sijawahi kutoa hoja udhi kwa kuwa tu haukufikia matamanio yangu

Na ziada ni kuhusu wasimamizi wa mtandao inabidi wawalinde waleta simulizi kwa kuwa moja ya majukwaa yanayotembelwa Sana na wanachama ni jukwaa la burudani na sababu kuu ikiwa ni simulizi kwa inabidi mliangalie kwa namna ya kipekee kama lilivyo jukwaa la siasa

Mwisho nitoe heko kwa watunzi wote kwa kuendelea kutupa burudani, baadhi yao ni
CK Allan
SteveMollel
Analyse
JBourne59
UMUGHAKA
Jack Daniel
INSIDER MAN
mireille
KigaKoyo
singanojr
FEBIANI BABUYA

Na wengine wengine wengi
 
Mimi huwa sisomi comment ya mtu, kazi yangu ni scrolling nikiona comment ndefu najua nyama hizi hapa nakula, imenisaidia sana maana hata uzi wa insider nilikuja kugundua hauendelei baada ya kuona comments nyingi alaf sioni story ndo nikaona kuna simtofahamu
But Analyse ana story za kufundisha maisha sana hasa kwa sisi ambao bado familia zetu hazina ata umeme.
 
Mimi huwa sisomi comment ya mtu, kazi yangu ni scrolling nikiona comment ndefu najua nyama hizi hapa nakula, imenisaidia sana maana hata uzi wa insider nilikuja kugundua hauendelei baada ya kuona comments nyingi alaf sioni story ndo nikaona kuna simtofahamu
But Analyse ana story za kufundisha maisha sana hasa kwa sisi ambao bado familia zetu hazina ata umeme.
Sometimes inabidi watu waapply uchawa kwenye hizi simulizi kwa ajili ya kuenda nao sambamba uawa taste spoilers
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom