Simulizi ya kipelelezi: Document number 72 (Nyaraka namba 72)

FEBIANI BABUYA

JF-Expert Member
Mar 5, 2022
1,035
1,925
Simulizi hii inahusu utafutwaji wa NYARAKA namba 72 waweza kuiita DOCUMENT namba 72 ambayo ina siri nzito sana ndani yake.

DOCUMENT hiyo inadaiwa kuwa na majina ya watu ambao wanatakiwa kupatikana kwa gharama yoyote ile hata kama ni kwa kuyatoa maisha ya watu wengine.

Watu hao ambao wanatafutwa, wanahusishwa na tukio la kikatili ambalo muda mfupi uliokuwa umepita lilikuwa limetokea ndani ya nchi ya Tanzania. Ni tukio ambalo liliondoka na maisha ya wana siasa zaidi ya miamoja na tisini (190) ndani ya siku moja tu pekee.

Watu hao ambao walikufa kwenye hilo tukio waliponzwa na bwana mdogo mmoja tu mwisho wa siku kiongozi mmoja akapakaziwa kuhusika na hilo tukio hali iliyo pelekea yeye kunyongwa.

Kufanikiwa kwa tukio hilo anahusishwa daktari mmoja mkubwa sana ambaye anatokea ndani ya nchi ya RWANDA hivyo inapaswa afanyiwe uchunguzi mkali kama sio kukamatwa kama ushahidi ukipatikana.

Daktari huyo anahisiwa kuwa mmoja kati ya watu hao ambao wanatakiwa kupatikana, ukweli na ushahidi wote wa nani yupo nyuma ya hiyo michezo yote upo ndani ya hiyo DOCUMENT namba 72. Hapo ndipo shirika la kijasusi la nchi ya Tanzania linaamua kumtuma jasusi wa kike ambaye anajulikana kama Tina ili kwenda huko kufanya upepelezi kwa sababu mtuhumiwa anadaiwa kwamba anaihusudu sana ngono, ndiyo sababu anatumwa jasusi wa kike.

Tina kusafiri kwenda ndani ya jiji la Kigali, Rwanda unakuwa mwanzo wake mbaya wa kuingia kwenye mikono ya hao watu akiwa kwenye mbio za kuisaka hiyo NYARAKA/ DOCUMENT namba 72 ambayo inalindwa na mwanaume anaye semekana kuwa KICHAA (hana akili timamu).

Tina anapitia mateso makali na unyama wa kutisha ikiwa ni kubakwa kila baada ya siku mbili ili aweze kusema yeye ni nani haswa na nani kamtuma. Mateso hayo yanamkutanisha na binti mmoja ambaye anamsaidia kutoroka ambapo anaishia kwenye msitu mmoja, ambako nako anatekwa na kukutana na unyama mwingine lakini anafanikiwa kutoroka pia akili yake ikiwa haipo sawa.

Anafanikiwa kufika ndani ya ardhi ya nchi yake na kukutana na mkurugenzi wa shirika la kijasusi la nchi ya Tanzania pamoja na mdogo wake wa damu kabisa.

Sasa baada ya kusimulia aliyo yapitia huko pamoja na siri kadhaa ambazo alifanikiwa kuzijua, anatumwa mdogo wake kwenda kuichukua hiyo DOCUMENT namba 72 huko RWANDA. Huo unakuwa mwanzo wa matukio ya kutisha na ya kikatili sana ndani ya hii simulizi.

Najua unataka kujua kwamba DOCUMENT hiyo ina nini ndani yake! Najua unataka kujua ilikuwaje mpaka wakauawa viongozi zaidi ya miamoja na tisini ndani ya siku moja na sababu hasa zilikuwa ni zipi?

Unatamani kumjua huyo mdogo wake na Tina? Una hamu ya kujua nini kilitokea ndani ya Rwanda na historia nzima ya watu ambao walikuwa huko na hawa majasusi walio tumwa huko na kuonekana kuwa ndugu wa damu?

Basi niazime muda wako tulisome kwa pamoja moja kati ya andiko bora sana la mwaka 2023.

Chao.

Episode 1
Episode 2
Episode 3
Episode 4
Episode 5
Episode 6
Episode 7
Episode 8
Episode 9
Episode 10
Episode 11
Episode 12
Episode 13
Episode 13(2)
Episode 14
Episode 15

1693571840266.jpg

Simulizi ya kipelelezi: Document number 72 (Nyaraka namba 72)
 
STORY: DOCUMENT NUMBER 72
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
WHATSAPP: 0621567672
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
AGE: 18+
EPISODE 1.

RWANDA,
Chumba kilichokuwa na mwanga hafifu, kikitawaliwa na kiza kinene ndipo ilipokuwa hofu ya moyo wake.

Hakuwa akiogopa kuhusu kufa kwake au kupoteza kwake maisha, lahasha! bali alikuwa anaogopa kushuhudia yale matukio ambayo yalikuwa yamatokea ndani ya hicho chumba.

Mwanga wa blue ambao ulikuwa unamulika kwa mbali, ulimfanya asitamani muda mwingi kuweza kuyafungua macho yake, kwa maana yalikuwa yanamuuma. Chumba hakikuwa rafiki sana kwa mwanadamu kuishi na huenda haikutakiwa kabisa kukaliwa na mtu kwa muda mrefu kwa namna kilivyokuwa kimechakaa. Huenda kwa mtu mwenye maisha ya chini angekitumia kama nyumbani kwake ila kwa mtu mwenye maisha yake hakikustahili kuishi kabisa.

Kwenye kiti kimoja ambacho kilikuwa kimekunjwa lakini kuna muda kilikuwa kinaweza kukunjuliwa na kikalazwa kama kitanda na mtu akapumzika hapo, alikuwa amefungwa mtu mmoja ambaye bila shaka licha ya kile kiza lakini alionekana kuwa ni mwanamke ambaye usoni kwake nywele zilikuwa zimejaa sana. Ilionyesha kwamba ni muda mrefu kidogo tangu kichwa chake hicho kiweze kufanyiwa usafi kama sio nywele kuoshwa vizuri.

Pembeni kidogo ya ile sehemu ambayo mwanamke huyo alikuwa amefungwa kwenye kiti, palikuwa na kitanda ambacho kilikuwa ni kisafi mno na kilionekana kwa mbali kwa jinsi mashuka yake yalivyokuwa yaking'aa kwa ule mwanga hafifu wa blue ambao ulikuwa unamulika humo ndani. Sehemu ya mbele yake kwa juu, sehemu ambayo ilikuwa na TV ndogo ya zamani, maana ilikuwa na tumbo kwa nyuma, palionekana kuwa na mpauko mkubwa sana isivyokuwa kawaida, rangi kuu kuu iliyo banduka banduka ukutani ilionekana kwa mbali.

Tv hiyo ilikuwa inaendelea kupiga kelele lakini mwanamke huyo ambaye alikuwa humo ndani, alikuwa ameinamisha kichwa chake chini. TV hiyo haikuwa na faraja yoyote mwake zaidi ya kumuongezea maumivu makali kwenye nafsi yake, kilichokuwa kinasikika kwenye TV hiyo ni miguno tu ya watu wakiwa wanafanya mapenzi, ilizidi kumpa hasira sana kwenye moyo wake akajikuta anadondosha chozi lisilokuwa na thamani gizani.

Hicho chumba kwake hakikuwa kigeni kabisa kwani alikuwa ana muda mrefu sana tangu aanze kuishi humo ndani hivyo hata bila kiza mazingira hayo alikuwa anayajua vizuri sana. Chozi lake lilikuwa linamshuka kwa sababu alikuwa anajua kile ambacho kilikuwa kinaenda kumkuta kwa muda mchache ujao.

Mlio wa TV hiyo na miguno ya mahaba ilikuwa inawekwa kwa sababu maalumu ambayo ilikuwa inamuuma sana kwenye nafsi yake huku ikimpelekea majuto makubwa sana ya yeye kuingia kwenye mikono ya hao watu ambao walimfanya aishie ndani ya hicho chumba alicho kuwepo kwa wakati huo.

Alikuwa anatamani ni bora hata angejiua au angeuliwa lakini sio kwa unyama ambao alikuwa anakutana nao hapo ndani, hivyo hakuwa na namna ya kulizuia chozi lisilo na mkingaji wa kulipooza kwa wakati huo ambapo hakujua kama nje ni usiku au mchana japo kwa ndani kulikuwa na kiza totoro.

Hakupewa nafasi ya kuweza kujidhuru ama kutoka kwenye mikono ya watu hao ambao walikuwa wamemuhifadhi hiyo sehemu. Akiwa anatoa chozi la uchungu, mlango wa hiyo sehemu ulifunguliwa na taa nyeupe zikawashwa, alichukua dakika nzima mpaka kufungua macho yake ili kuangalia nani aliyekuwa ameingia.

Aliye ingia humo ndani, alikuwa ni mwanamke mmoja ambaye asili yake ilikuwa ni ya Rwanda, alikuwa ni mwanmke mrembo sana. Alionekana kuwa mwenyeji wa hilo eneo ndiyo maana hakusita hata kufanya shughuli ambazo zilimleta hapo baada tu ya kuingia. Mwanga uliowashwa ulisaidia kuweza kukimulika vyema chumba hicho ambacho hakikuwa na ubora wowote ule.

Chumba cha zamani sana ambacho kilichoka, rangi ilikuwa imechubuka mno kiasi kwamba kikapoteza mvuto wa mtu mwenye afya salama kuishi, kilionekana vyema. Upande wa kushoto kulikuwa na mlango ambao bila shaka ulikuwa wa uani japo ulifungwa kwa komeo iliyo choka, licha ya kuwa na ubaya ulio kithiri lakini, chumba hicho kilikuwa kimepambwa na kitanda cha gharama isivyokuwa kawaida.

Kitanda kilicho nakshiwa na mashuka ya gharama bila kusahau friji la bei ghali ambalo liliwekwa mkabala na pembe moja ya kitanda lilileta maswali mengi sana juu ya siri iliyopo kwenye hicho chumba. Mwanamke ambaye alikuwa ameingia wakati huo, mkononi mwake alikuwa ana vifaa vya kuogea, vipodozi kiasi pamoja na beseni kubwa lenye maji huku akiwa amevaa bikini tu pekee kwenye mwili wake.

Alimwangalia mwanamke mwenzake kwa umakini sana, hakueleweka kama alikuwa anamuonea huruma au alikuwa anamsanifu. Aliinama na kulowanisha taulo dogo kwenye maji na wakati huo yule mwanamke ambaye alikuwa amefungwa pale kwenye kitu aliinua uso wake na kumtazama mwenzake ambaye alikuwa hapo chumbani kwa ajili yake, huku naye kwenye mwili wake akiwa na bikini tu pekee ila kuinua kwake sura alionyesha moja kwa moja kwamba ni mtanzania.

"Sorry do you speak swahili? ( samahani unaongea kiswahili?" yule mwanamke ambaye alikuwa kwenye kiti alimuuliza mrembo huyo ambaye alikuwa na taulo mkononi huku akiwa ameanza kumfuta kwenye uso wake. Alimwangalia sana kabla ya kumjibu.

"Yes, I'm not native but somehow i try cuz i once lived in Tanzania back in days (ndiyo mimi sio mzawa ila naongea kwa kiasi chake maana niliwahi kuishi Tanzania huko nyuma)" jibu lake lilionyesha kwamba anajua kuongea japo sio sana maana aliwahi kuishi Tanzania kwa miaka kadhaa huko nyuma.
"Unaweza kuniambia lolote kuhusu Tanzania?" Alimuuliza kwa kiswahili baada ya kuonekana kwamba anakiweza.

"Unajua nyi watu mko na janja janja sana ndicho nilicho jifunza about Tanzania" alijibu kuonyesha kwamba hakuwa anakijua sana kila neno kuongea japo alikuwa anaelewa kila kitu. Mwanamke huyo ambaye alifungwa kwenye kiti alitoa tabasamu hafifu kwani kilichokuwa kimezungumzwa, ni ukweli mtupu. Watanzania wanaogopeka kwa maneno maneno na ujanja mwingi sana mdomoni.

"Hii sehemu mimi ndiye wa kwanza kufanyiwa hivi na kuletwa?"
"Hapana, watu mingi sana waliwahi kuletwa kama wewe ila janja zao zinawafanya kufa haraka"
"Wanaweza kuwa wangapi ambao waliwahi kuletwa hapa?"
"Sijui, tangu anze mimi kuja, watu mingi kama kumi meona wakikuja kwa hapa"
"Huwa huwaonei huruma wanawake wenzako kifanyiwa huu ukatili?"

"Onea wapi huruma watu wengine? Wewe lini onea huruma mimi navyofanywa mbele yako? Ishi maisha ya wewe, acha kufuatilia yangu mimi" alijibu kwa hasira sana akiona kama mwenzake anataka mazoea ambayo yeye hakuyapenda kabisa. Alimkanda kanda na kumfuta uchafu ambao ilikuwa kwenye mwili wake na kumpaka vipodozi.

Baada ya kumaliza,alisogea na kuufungua ule mlango wa uani na kwenda kumwaga maji aliyokuwa akimsafishia mwenzake. Alirudi na kwenda kujilaza kitandani huku akivua nguo zote, dakika kama tatu zilipita akaingia mwanaume mmoja mwenye kitambi akiwa kifua wazi na kipensi kifupi, mkononi mwake alikuwa ameshika sigara yake akiivuta taratibu.

Ni bwana mmoja mfupi lakini kibonge, hakuwa na wasiwasi, utulivu na nuru ilikuwa sawa machoni pake, huenda ni kwa sababu ya maisha kama siyo mamlaka aliyokuwa nayo juu ya hiyo sehemu ambayo alikuwepo kwa wakati huo.

Alisogea mpaka pale kwenye kiti na kumbusu yule mwanamke ambaye alikuwa amefungwa kisha akaenda mpaka kitandani na kuvua kipensi chake, akaanza kufanya mapenzi kwa fujo sana na yule dada wa kinyarwanda mpaka alipo fika safari yake.

Mwanamke yule wa kinyarwanda aliinuka na kuanza kumnyonya sehemu za siri tena mwanaume huyo ambaye baada ya dakika tano alimvamia yule mwanamke wa kwenye kiti ambaye mpaka wakati huo alikuwa akitoa machozi.

Aliichana ile bikini na kukilaza kile kiti kisha akawa anambaka kwa nguvu bila huruma mpaka pale alipo tosheka akasimama, yule dada wa kinyarwanda alimsogelea mwanaume yule na kuanza kunyonyana naye midomo yake mpaka walipo tosheka, bwana yule mfupi akavaa kipensi chake na kumsogelea yule mwanamke wa kwenye kiti baada ya kukiinua akiwa bado yupo uchi.

"Tina" mwaaume huyo aliita kwa dharau huku akicheka.
"Mara ya kwanza tu nakuona, nilijua kuna kitu hakipo sawa, mwanamke mrembo kama wewe huwezi kumpenda mwaaume mfupi kama mimi, huo ni uongo na najua hilo. Nilishangaa siku ile ukisema kwamba unanipenda sana mimi na unataka nikuoe niwe na wewe kama mke wangu, nilishangaa sana kwa maana nilijua mrembo kama wewe kuna wanaume wengi sana wenye maisha yao mazuri hata zaidi yangu wangetamani wakuite mke"

"Kwanini mimi? Hahahahah kumbe ulikuwa na malengo yako kuniweka kwenye mtego? Bibie umefanya moja kati ya kosa ambalo litayagharimu maisha yako na mwili wako kwa ujumla mpaka akili yako. Umejiingiza kwenye upelelezi wa vitu ambavyo haujui hata madhara yake wala kujua historia yake ya kweli ipoje"

"Ulitakiwa kwanza kujua kwamba;.. kwanini haya mambo yanatokea! Kwanini hawa watu waaishi hivi na ni nani ambaye yupo nyuma ya maisha haya ambayo sisi tunayaishi?. Unajua kwanini nilikimbia Tanzania? Unajua maisha yamekuwaje mpaka nipo hapa na haya maisha mazuri ambayo unaniona nayo?"

"Pengine kiongozi wako alikutuma bila kukwambia yaliyopo nyuma ya makaratasi au alikutuma makusudi ili ufe, na kitu kibaya na cha kushangaza wanakutumaje mtoto mzuri kama wewe? Umeletwa ili ufe? Sasa mimi nataka nikuhakikishie kwamba wewe hautakufa kirahisi sana namna hii kama unavyo dhani, nitahakikisha kwamba unakufa huku ukijuta na ukitamani hata kujiua mwenyewe ila hautakuja kupata hiyo nafasi kabisa hususani ya kuishi kwa furaha tena" Bwana huyo aliongea kwa msisitizo akihitaji kueleweka kwa mwanamke huyo ambaye hakujulikana amemkosea nini.

"Kesho ratiba inaendelea kama kawaida ila mimi sina ratiba na mwili wako, nikijisikia tu nakuja, ndiyo maana hata kondomu situmii ila hao wanaokuja kesho lazima watumie kondomu maana vinginevyo nawaua mwenyewe kwa mkono wangu"

"This is Rwanda not beautiful Tanzania. Hahahahah" Mwanaume huyo alicheka sana huku akiwa anatoka ndani ya hicho chumba akiongozana na yule dada wa kirwanda huku mlango ukifungwa na rangi zikibadilishwa na kubakia kama zile za mwanzo.

Kuna kipi kimemkuta mwanamke huyu Tina? Yeye ni nani na alikuwa akiwapeleleza hao wanaume kwa sababu zipi? Na ni kiongozi wake yupi huyo aliye mtuma huko? Huyo mwanaume anadai alikimbia Tanzania kwa kipi?....nini sababu ya wao kuwepo Rwanda?

Maswali ni mengi sana ila ndiyo kwanza tunaufungua ukurasa wa kwanza kabisa wa simulizi yetu safi ya DOCUMENT namba 72. Twende pamoja tuweze kujibiwa maswali yetu.

Hii ni moja kati ya simulizi bora sana ya kipelelezi utakayo isoma kwenye maisha yako.

Kalamu ni yangu mwenyewe,

FEBIANI BABUYA.
1693571840266.jpg


Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
STORY: DOCUMENT NUMBER 72
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
WHATSAPP: 0621567672
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
AGE: 18+
EPISODE 2.

Tina alibaki amejiinamia akiwa anayatoa machozi ambayo ni kama alikuwa anayatoa baharini kwa maana hakuna kitu cha maana chochote ambacho yangemsaidia. Nafsi yake ilikuwa inamuuma sana, watu hao ukatili ambao walikuwa wanamfanyia ulikuwa umevuka mipaka, licha ya kuwa mpelelezi mahiri lakini kifo alikiogopa mno kwa maana naye alijiona kuwa mwanadamu wa kawaida kama vile walivyokuwa wengine.

Aligeuzwa kuwa chombo cha starehe kwa wanaume hao ambao hata hakujua kuhusu afya zao, ila kilicho kuwa kinamuumiza zaidi ni yeye kuwa kama dala dala ambayo abiria wangepanda hapa na kushuka pale asielewe mwisho wa kituo chake ni wapi.

Kumbukumbu zake zilishindwa kumkumbusha kabisa kwamba alikuwa yupo ndani ya eneo gani mpaka wakati huo, alichokuwa anakumbuka ni kwamba mara ya mwisho alikuwa na mwanaume mmoja kitandani wakifanya mapenzi. Hakuwa na nguvu za kumzuia yule mwanaume kumfanya kile ambacho alikuwa ameazimia kukifanya kwa maana mwili wake haukuwa na nguvu kabisa zaidi ya mwili huo kuzidiwa na hamu ya mapenzi ambayo hata yeye ilimshangaza sana kwamba ilitoka wapi.

Hakujua kwamba ni kipi kiliendelea mpaka pale alipokuja kushtuka akiwa ndani ya hicho chumba, sasa maswali mengi yalikuwa yanapita kwenye kichwa chake kwamba alikuwa wapi ila alikata tamaa kwa maana swali hilo alikuwa amejiuliza mara nyingi sana na hakuwa na jibu wala mtu wa kumpa hilo jibu.

Mara ya kwanza aliwahi kuchukulia mambo kawaida sana hivyo akataka kujaribu kutoroka ndani ya jengo hilo ambapo alifanikiwa kufungua mlango tu, baada ya kutoka nje ya mlango wa chumba alicho kuwepo, alikutana na mwaaume mmoja ambaye alikuwa kwenye vazi la bukta huku kifua chake kikiwa wazi.

Alihisi anaweza kumdhibiti huyo mtu kisha angetoka lakini kilicho mkuta, alitaka kupoteza jicho lake ambalo lingeharibu urembo wake wote ambao alikuwa nao. Mwanaume huyo alimpiga vibaya bila kujali kwamba huyo alikuwa ni mtoto wa kike na ndiyo hiyo siku ambayo alipangiwa ratiba ya kulala na wanaume watano kila baada ya siku mbili kwa ukaidi ambao alikuwa ameufanya.

Alibakwa kwa nguvu sana siku ile na hicho ni kitu ambacho kwenye maisha yake hawezi kukisahau kabisa hata kama angeamshwa ndotoni, maana maumivu ambayo alikuwa anayapitia kwenye moyo wake yalimfanya ahisi kwamba yeye siyo mwandamu wa kawaida akaishia kumlaumu sana MUNGU.

Siku ile ambayo alikamatwa akihitaji kutoroka, alishuhudia mwenzake mmoja akipigwa kisu cha moyo mbele yake baada ya kubakwa, kisha watu hao wakakipasua kichwa cha mwanamke huyo kwa risasi nyingi ikiwa ni kama onyo kwake kwamba kama akija kujaribu tena kufanya huo ujinga wake basi angefanywa kile kile ambacho mwenzake alifanywa japo yeye hatauawa ila angepitia mateso ambayo angetamani yeye mwenyewe kutafuta nafasi ya kujiua.

"Uko wapi kaka?!" aliongea kwa sauti ya kichovu ambayo imekosa furaha na nuru kwenye uso wake. Alitamani mtu ambaye alikuwa akimuita kaka angekuwa karibu yake wakati huo ambao yeye hakuwa na tumaini lolote lile la kuwa salama. Kumbukumbu zilimbeba na kumrejesha mbali sana akiwa na huyo ndugu yake wa kiume.

"Dada bado unayo nafasi ya kufanya maamuzi yako upya, kwa sasa unatakiwa uwe na familia yako utulie na kulea watoto wako, haya mambo ebu kaa nayo mbali dada yangu, maisha ya huku siyo ya kawaida halafu wewe ni mtoto wa kike" mdogo mtu alikuwa anamshauri dada yake aweze kuacha kile ambacho alikiamua ili akatengeneze familia yenye furaha siku zote.

"Calvinjr unajua kwanini niliichagua hii kazi?"
"Hapana"
"Basi unatakiwa kujua kitu kimoja, dada yako ni mwanamke jasiri sana ambaye anaipenda sana nchi yake, mimi sijaja kwenye hii kazi kwa kubahatisha bali nimeamua kukabiliana na watu ambao wanaikosesha nchi yetu amani. Watoto wa kike wananyanyaswa sana lakini hakuna hatua kubwa zinazo chukuliwa, kuna watu kwa maslahi yai wanaifilisi hii nchi na sioni watu wakiwa na uchungu kwenye haya mambo mdogo wangu"

"Nadhani una ujua kwa ukubwa uwezo wa dada yako, mimi sio yule mwanmke wa kushinda na vipodozi mezani bali mimi ni yule mwanamke ambaye nimejitoa kulipambania taifa langu. Kama MUNGU akijaalia basi familia nitakuwa nayo wakati ujao, maana hata mama huwa ananisimbua sana kwa hilo" dada mtu ambaye alikuwa anafanya kazi ya upelelezi alionyesha msimamo kwa mdogo wake kwamba hayupo tayari kuachana na hiyo kazi bali alitaka kuwafichua wote ambao walikuwa wanayafanya maovu.

"Sister please naomba usiende huko, tumezaliwa wawili tu unaendaje pekeyako kwenye nchi ambayo haujawahi hata kuishi? Haujui watu wake wanaishi vipi? Na mama unamuaga unaenda wapi? Vipi kama ukipatwa na tatizo huko unahisi nani atakusaidia? Nipo tayari kubadili plani nzima nikaenda mwenyewe" Calvinjr hakuwa tayari kumuacha dada yake aende huko pekeyake, alikuwa na hofu sana kuhusu maisha ya dada yake wa pekee huyo.

Tina alimsogelea mdogo wake na kwenda kumkumbatia akiwa na tabasamu, alijua ni kwa namna gani yeye na ndugu yake walikuwa wakipendana sana ndiyo sababu hakuwa tayari kumruhusu kwenda ndani ya nchi hiyo tena akiwa hana mtu wa kumpa msaada.

"Kaka, kweye maisha yako usitumie sana hisia kufanya maamuzi mahali ambapo inahitajika akili zaidi, haitajalisha kwamba hisia zitakuumiza ila kuna muda unapaswa kufanya maamuzi magumu ili kupata matokeo ambayo yapo sahihi. Mimi kwenda Rwanda sio mpango wangu tu, ni kiongozi amefanya hayo maamuzi kwa sababu anajua mazingira ya kazi yalivyo"

"Kule inatakiwa niende mimi mwenyewe maana kama tukienda wote itakuwa ni rahisi sana kufuatiliwa na kujulikana kitu ambacho kitafanya tupoteze kila kitu ambacho tumekianza hivyo natakiwa kwenda kwanza halafu baadae kama kutakuwa na ulazima wa nyie kunifuata itakuwa sawa"

"Kumbuka Calvinjr, wameuliwa viongozi wengi sana, nchi imechafuka saivi, raia wanailaumu serikali kwa uzembe wake mkubwa ambao imeufanya mpaka kuruhusu idadi ya wanasiasa wengi kufa namna hiyo kwa siku moja. Hatutakiwi kulala kabisa na huu ndio muda ambao inabidi tuhakikishe tunafanya jambo lolote lile ili kuwapata hawa watu ambao wamehusika na hili jambo"

"Tukitanguliza hofu ya kuogopa kupoteza maisha basi jua kwamba kazi haitafanyika na ni kitu ambacho kitakuwa ni hatari sana kwa usalama wa taifa letu. Kumbuka tu ni jambo la hatari sana pale inapotokea wananchi wanaacha kuiamini serikali yao, hilo huenda ndilo jambo la hatari zaidi ndani ya nchi kwa maana kuna watu wanaweza kuutumia mwanya huo kufanya yale ambayo wanayataka wao"

"Mimi nakwenda Rwanda kuanza kazi ya kuwatafuta hawa watu kwa namna yoyote ile ila kila nikiwa huko nitakuwa na amani kwa kitu kimoja tu, kwamba bado ninaye wewe hapo, wewe ndiye mtu ambaye ninakutagemea sana kwenye hii kazi.

Huenda mimi naanza ila nitahitaji sana msaada wako hapo baadae"
"Pale nitakapokuwa sipo, usinitafute kabisa mpaka pale nitakapo kutafuta mimi, na hakikisha unamtunza mama, maana ndicho kitu cha pekee cha thamani ambacho MUNGU ametupatia kwenye haya maisha yetu"

"Kumbuka tu kwamba dada yako nakupenda sana". Tina alilia kwa kwikwi na sauti ya chini baada ya kukumbuka maongezi ya mwisho mwisho akiwa anahitaji kuianza safari yake ya kwenda Rwanda ambako kulimfanya akaishia ndani ya hicho chumba alicho kuwepo.

Kazi yake kubwa ilikuwa ni kuweza kutafuta ushahidi wa hayo mauaji ambayo yalihusisha vifo vya wanasiasa wengi sana ndani ya Tanzania ila ni kama alikuwa na bahati mbaya baada ya kukamatwa na sasa alikuwa analipa kwa mateso makali mno.

Aliinua uso wake kutazama kila kona ya hicho chumba na kuishia kusonya kwa fadhaiko la kukata tamaa, hakuwa na imani ya kuendelea kuishi zaidi ya kumuomba MUNGU aweze kumchukua haraka sana. Hakuona mahali pa kuupatia msaada wowote wala mtu wa kujali kuteseka Kwake hivyo kupambana na hali yake ndio ulikuwa msingi wa kila kitu kwa huo wakati.

Alijaribu bahati yake kwa mwanamke yule wa Kirwanda lakini hakusikilizwa, aliona kabisa kwamba mwanamke yule angeweza kumsaida kwa namna moja ama nyingine ya kumjulisha hata tu lile eneo ambalo alikuwepo ila kwa bahati iliyokuwa mbaya mwanamke huyo alimkataa kabisa kwa kumtaka apambane na maisha yake mwenyewe! Kwa maisha yapi? alibaki anajicheka mwenyewe huku chumba kikimzomea kwa kile ambacho alikuwa anakipitia.

Akiwa analia huku anacheka kama mtu aliye changanyikiwa, mlango wa chumba hicho ulifunguliwa tena lakini hakuona mtu akiingia zaidi ya kusikia kishindo cha sauti kama vile kuna mzigo umetupwa humo ndani. Taa iliwaka ghafla sana na kumfanya afumbe macho yake ili yasiumie, lakini baada ya kuyafumbua hakuona mtu yeyote akiwa amesimama mbele yake.

Baada ya kuona hivyo akaamua kuinamisha macho chini ili kuona ile sehemu ambayo alihisi kwamba kuna mzigo ukitupwa kuna nini, alicho kiona kilimtisha kiasi kwamba alishindwa kuvumilia, akawa anatokwa na jasho jingi huku akihema kwa nguvu na kwa taabu kubwa. Alipiga kelele mara moja tu na kutulia. Haikueleweka kama alipoteza maisha au alikuwa amezimia kwa ule mshtuko mkubwa ambao aliupata kwa kipe ambacho alikuwa anakishuhudia pale.

Unahisi aliona nini mbele yake cha kumshtua sana kiasi hicho? Je huko Rwanda kilimpata nini kwenye harakati zake hizo za upelelezi? Na alikuwa anampeleleza nani mpaka aangukie kwa hao watu? Ni wanasiasa wapi hao wa Tanzania ambao walidaiwa zaidi ya 100 waliuliwa na kwanini wauliwe?

Twende sawa ndani ya DOCUMENT namba 72 taratibu tutayapata majibu yetu. Episode 2, inafika mwisho.

Kalamu ni yangu mwenyewe.

Febiani Babuya.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
mkuu simulizi inaonekana kuwa nzuri sana lakini hofu na mashaka yangu ni kama itaisha na hata kama itaisha muendelezo utakua unauleta kwa mtindo upi wa daily au
 
STORY: DOCUMENT NUMBER 72
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
WHATSAPP: 0621567672
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
AGE: 18+
EPISODE 3.

MIAKA MIWILI ILIYO PITA (2 YEARS AGO)

Ndani ya ofisi moja kubwa kwenye kampuni kubwa iliyokuwa ikijishughulisha na ujenzi. Alionekana mwanaume mmoja ambaye kwa mwonekano alikuwa bado ni kijana mdogo tu ambaye alikuwa ndani ya suti yake nzuri na safi sana.

Macho yake hayakubanduka kabisa kwenye simu ya mezani ambayo ilionekana kwamba alikuwa anaisubiri kwa hamu kubwa mno iweze kuita kwa wakati huo lakini palikuwa kimya tu, ni sauti ya kiyoyozi tu kwa mbali ndiyo ilikuwa inasikika ndani ya chumba hicho. Kwenye meza yake kibao kiliandikwa CEO, kumaanisha kwamba yeye ndiye mtendaji mkuu wa kampuni hiyo.

Calvinjr ndilo jina ambalo liliandikwa mbele ya neno CEO, bila shaka ndilo lilikuwa jina lake yeye mwenyewe, juu ya ukuta paliandikwa maneno makubwa Cal-Tina investment likiwa ndilo jina la kampuni hiyo ambayo yeye alikuwa akiiongoza. Akiwa kwenye hayo mawazo yake ya kuisubiri kwa hamu hiyo simu ambayo ilikuwa mbele yake.

Hatimaye hamu yake ilitolewa na mlio wa nguvu wa simu hiyo ambao ulimfanya atabasamu kwa mbali na kuipokea haraka sana kiasi kwamba mtu ambaye alikuwa upande wa pili asije akaikata simu hiyo.

"Hello" aliongea kwa sauti ya utulivu.
"You have won the bid, na sasa mkataba wewe ndiye unayepatiwa, hongera sana Mr Calvinjr. Mradi wote wa ujenzi utasimamiwa na kampuni yako" ni sauti nyororo kutoka upande wa pili wa simu ambayo ilimpa shangwe lisilo kuwa ka kawaida. Alicheka kwa furaha sana na kuhema kwa nguvu.

"Mrs William, sitakusahau kwa hili, nakushukuru sana na nitahakikisha narudisha fadhila hizi ulizo nitendea leo. Naomba MUNGU akubariki na nakuahidi sitakuangusha katika hili" Calvinjr aliongea kwa utulivu kama kushukuru kwa mwanamke huyo ambaye alionekana kumfanyia jambo kubwa sana.

"Unahisi utanipatia nini Mr Calvinjr kama asante kwangu?" sauti nyororo ilizidi kusikika upande wa pili na kumfanya mwanaume agune kwanza kabla ya kuongea.

"Nahitaji kutuliza kichwa ili nijue ni zawadi gani inaendana na mtu wa mhimu kama wewe ila tu sitakuangusha, nakuahidi hilo"

"Ok nasubiri ukiitimiza hiyo ahadi yako ila kumbuka tu kwamba huu mradi ni wa mabilioni ya pesa na ni watu wengi sana ambao walikuwa wanauhitaji huku wengine wakiwa tayari hata kulipia mabilioni ili waupate ila mimi nimekupa wewe bila malipo yoyote yale. Nimefanya hivyo kwa sababu najua ulivyo smart kwenye kazi yako lakini huenda kuna mengine zaidi ya haya.

Nakutakia utelelezaji mwema na kama ukinihitaji, nadhani unajua kwa kunipata" sauti hiyo iliongea kwa upole na mamlaka, hakuonekana kuwa mtu wa kawaida sana mbele ya jamii ndiyo maana hata CEO Calvinjr alikuwa anaongea naye kwa heshima sana.

"Ah....ah mheshima sitakuangusha niami....." alibaki anajikanyaga kanyaga, kabla hajamaliza sentensi yake, simu hiyo ilikuwa imeshakatwa muda mrefu sana. Alisimama na kuanza kushangilia pekeyake humo ndani, kwa maana yalikuwa ni mafanikio makubwa isivyokuwa kawaida.

Alikuwa amefanikiwa kupata moja ya mikataba mikubwa mno ambayo alikuwa na uhakika kwamba ingeyabadilisha maisha yake kwa kiasi kikubwa pamoja na kampuni yake kwa ujumla. Sasa alihitaji kuongea na msaidizi wake kumpa hizo habari juu ya mradi wao kufanikiwa, kwani kwa pamoja waliupambania sana isivyokuwa kawaida.

Hakutaka kumpigia simu mtu huyo zaidi ya yeye mwenyewe kuhitaji kwenda ofisini kwake kumpatia taarifa hizo na kumpa pongezi kwa kuhusika moja kwa moja kukamilisha jambo hilo. Alijongea taratibu mpaka upande wa pili wa ofisi yake ambako huko ilikuwepo ofisi ya msaidizi wake, wakati anasogea ili afungue mlango, alisita baada ya kusikia kama ndani watu walikuwa wanaongea kwa sauti ya chini sana ambayo bila shaka hawakutaka watu wawasikie kabisa. Ikamlazimu kusikiliza kwanza kiumakini ili ajue ni kipi kilikuwa kinaendelea humo ndani.

"Kuna kitu hakipo sawa kwa kiongozi" ni sauti ya mwanaume ambaye bila shaka alikuwa ni mtu wa makamo, alisikika akiongea na kijana wake ndani ya ofisi hiyo.

"Una maanisha nini mzee kuongea hivyo?" Kijana huyo aliuliza huku akiacha kila kitu na kumsikiliza mzee huyo maana kumzungumzia bosi wa kampuni haikuwa rahisi sana namna hiyo. Ilionyesha kulikuwa na mambo ambayo hayakuwa ya kawaida kwake hususani kwenye kulinda kibarua chake.

"Unajua kijana wangu, mimi nipo kwenye hii nchi kwa miaka mingi sana. Nimeishi na kujifunza mengi sana mpaka leo unapo niona hapa, na kuna vitu vingi sana ambavyo navijua kuhusu historia ya nchi hii ambavyo nyie vijana hamvijui kabisa" Mzee huyo aliongea mambo ambayo kijana wake huyo hakumuelewa kabisa zaidi aliongeza hofu kwenye moyo wake akihisi huenda wanataka kupunguzwa kazini.
"Bosi wetu anafanana kama sio mimi namfananisha na mwanaume mmoja ambaye amewahi kuishi kwenye nchi hii miaka kadhaa iliyopata kupita huko nyuma"

"Mzee mbona kama sikuelewi unamaanisha nini kuongea hivyo? Huoni kama itakuwa hatari kwako kama bosi akikusikia?"

"Nisikilize kwa umakini sana kijana wangu, mimi sio mjinga kiasi hicho na huwa sikurupuki kabisa kufanya maamuzi yangu wala taarifa zangu kuzitoa pasipo ushahidi wowote ule. Kabla ya kukwambia jambo hili, nimemfuatilia kwa umakini na ukaribu mkubwa sana na kuna vitu vinanipa uhakika kwamba mawazo yangu kwa asilimia nyingi sana yapo sahihi"

"Kuna mwanaume mmoja amewahi kuishi kwenye nchi hii zaidi ya miaka ishirini ambayo imekwisha kupita. Alikuwa ni kijana mdogo tu ambaye bila shaka kama yupo hai kwa sasa ni mtu mzima kabisa, kijana huyo ni moja ya watu ambao walibahatika kuzaliwa kwenye familia za kitajiri mno ila kuzaliwa kwake kwenye maisha hayo kulimfanya akazichukia pesa kwa baadae"

"Alizichukia pesa kwa sababu ndizo zilimfanya abakie yatima asiye na ndugu wala mzazi yeyote wa kumfariji. Mama yake na baba yake waliuliwa na watu ambao walikuwa wanazihitaji mali za baba yake na inasemakena kwamba yeye alitoroka, alipotea kabisa kwenye macho ya watu na kurudi baada ya miaka miwili"

"Alirudi tofauti na alivyo ondoka, kwani anadaiwa kwamba alikuja kuwa muuaji wa kutisha ambaye kila akionekana mahali watu walikuwa wanamkimbia japo alikuwa anafanya mambo yake kizani. Aliwaua watu wote ambao walihusika na mauaji ya familia yake kisha baadae akaondoka na familia yake mpya wakiwemo wake zake wawili na watu wengine wachache ambao aliwapata kwenye harakati zake za kupigania haki ya wazazi wake"

"Inasemakana kwamba tangu aondoke, hakuwahi kurudi tena Tanzania, na hapa ndipo kichwa changu kinapo uma sana, kama mtu huyo aliondoka na hakuwahi kurudi nchini kwanini azaliwe kijana ambaye anafanana naye? Na kwa mwanamke mwingine kabisa? tena kijana huyo anaonekana amezaliwa kipindi mtu huyo alisha ondoka Tanzania kwa muda mrefu?"

"Hesabu zinagoma kabisa lakini kuna nafsi inaniambia hawa watu wanafanana ukiwaangalia kwa umakini, hapo ndo napata shaka sana. Bosi wetu ni mlaini sana kama angekuwa ni mtoto wake huenda kuna roho ngumu angeirithi kwake, lakini haipo hivyo, bosi wetu ni mpole na mwenye huruma sana japo bado naamini hapa kuna kitu kinaendelea sio bure.

Nahitaji kufuatilia hili jambo mpaka nione mwisho wake unakuwaje na kama ni kweli ndiye mtoto wake basi kuna mambo makubwa na mabaya yanakuja siku zijazo" Mzee huyo aliongea vitu ambavyo hata yeye vilikuwa vinamchanganga na kumpeleka kukosa jibu la moja kwa moja asijue kwamba anayo yaongea yote kuna mtu alikuwa anamsikiliza mlangoni, ambaye ndiye huyo mlengwa mwenyewe Calvinjr.

Kijana wake alibaki anamshangaa sana, maana Mzee huyo ni kama alikuwa anamtisha stori alizokuwa anampa.

"Bosi hayo mambo unayo yaongelea ni mazito sana na kama yakifika huko kwa bosi basi yanaweza kutuletea matatizo tukakosa hata kazi. Kama ambavyo kuna nafsi inakuwa inasita kukufanya uyaamini mawazo yako basi iamini hiyo nafsi yako kwani hilo jambo haliwezekani bosi"

"Haliwezakani kwa sababu duniani watu wanafanana sana, hata wewe hapo lazima kuna nafsi yako ipo inaishi mahali pengine tofauti na hapa. Inaweza kuwa ndani ya Tanzania au hata nje ya nchi ila niamini mimi, duniani huwa tupo wawili wawili au hata zaidi ya hapo.

Kipindi nasoma sekondari kuna rafiki yangu wa Tabora aliwahi kuniambia kwamba huko kwao kuna mtu ambaye anafanana kwa kila kitu na mimi mpaka tabia, kitu kilicho mfanya ahisi kwamba mimi ni huyo mtu ila alishangazwa na mimi kutomjua kabisa hapo akawa na uhakika kwamba mimi siye"

"Hivyo hilo jambo lisikuchangaye sana ukawa na mawazo ambayo yanaweza kukufikisha sehemu mbaya, bosi hawezi kuwa hivyo, angalia alivyo mpole, mwenye huruma na mchapakazi. Jizuie bosi wangu usiwe na mawazo kama hayo.

Unaweza kutumia muda wako kusoma vitabu au kufanya unacho kipenda, kinaweza kukuweka mbali na haya mawazo ambayo upo nayo leo" kijana huyo alionekana kuwa mstaarabu, hakuyaamini kabisa maneno ya mzee huyo ambaye alionekana kuwa kiongozi wake ndani ya hiyo ofisi yao.

Hivyo alimjibu kistaarabu kahisa ili aachane na hayo mawazo na afanye mambo mengine ambayo yangekuwa ya mhimu kwake kwa wakati huo.

Huku mlangoni Calvinjr alisikia kila kitu, maneno ambayo yalimshtua sana nafsi yake, aliogopa mno alichokuwa anakisikia na ndiyo ilikuwa mara yake ya kwanza kusikia maneno kama hayo kwenye maisha yake yote. Alikitoa kitambaa kwenye mfuko na kujifuta kidogo usoni ili kupunguza hali ya ujoto ambayo ghafla ilimuandama.

Hakuona kama inafaa kuendelea kubaki tena hilo eneo, alisogea taratibu mpaka kwenye ofisi yake huku akighairi kuongelea kile ambacho alitaka kuongea na mzee huyo na kuacha wote waje kuambiwa kwenye kikao cha bodi.

Hakuwa na hamu tena ya kuendelea kukaa ofisini, kichwani mwake alikuwa na hesabu ya mtu mmoja tu ambaye ndiye alipaswa kumwambia ukweli wa hayo mambo ulikuwaje. Mama yake ndiye mtu pekee ambaye angeweza kumjibu maswali yake mengi ambayo yalizaliwa ghafla sana kama sio kutokupatiwa kabisa majibu kuhusu historia yake.

Alibeba mkoba wake na kutoka humo ndani bila kumuaga hata katibu wake ambaye alimshangaa kiongozi wake anampita kama vile hamjui, mwanaume hakuwa na muda wa kupoteza, alikuwa anawahi nyumbani.

Je kuna ukweli wowote kuhusu mambo ambayo yamezungumzwa? Na mama yake anaenda kumjibu nini?
Episode ya 3 inafika mwisho hapa. Tukutane sehemu inayo fuata.

Febiani Babuya

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
STORY: DOCUMENT NUMBER 72
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
WHATSAPP: 0621567672
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
AGE: 18+
EPISODE 4

Calvinjr aliendesha gari lake kuelekea nje kidogo ya mji, Mbezi Temboni ndiko alikokuwa anaelekea majira hayo ya jioni kwenda kuonana na mama yake mzazi ambaye alikuwa akiishi huko.

Gari yake ilikuwa inaenda kwa spidi kali sana, baada ya kufika sehemu ambayo ilikuwa na mgawanyiko wa barabara nyingi, alichepuka na kuishika njia ambayo ilikuwa na mabonde bonde mengi sana, hakuwa akipenda kabisa mama yake aweze kuishi eneo kama hilo lakini mwanamke huyo yeye aliona ni sahihi kuishi huko na hakutaka kabisa mtu yeyote apingane na hayo maamuzi yake.

Calvin aliendesha gari kwa nusu saa nzima kwenye hiyo njia mbovu mpaka alipo kutana na tambalale, hapo aliendesha gari kwa kasi kwa dakika zipatazo kumi akawa analiangalia geti la blue ambalo lilikuwa mbele yake. Lilikuwa ni jumba la kifahari mno ambalo lilijengwa nje ya mji huko na hapo ndipo palikuwa nyumbani kwao, geti lilifunguliwa baada ya kipiga honi mara tatu, aliliingiza ndani na kushuka ili aelekee ndani.

"Waooo mziwanda wangu, naona leo umekuja bila hata taarifa bila shaka umeniletea taarifa za kuniletea mkwe hapa" mama huyo aliongea kwa furaha huku akimkumbatia mwanae wa kiume na kumbusu kwenye baji lake la uso, huyo ndiye alikuwa mtoto wa mwisho kwenye familia hiyo.
"Aaah! mama wewe unawaza kuoa tu"

"Ebu kelele na wewe, ujue wewe na dada yako siwaelewi. Umri wangu unazidi kwenda lakini cha ajabu sioni hata dalili ya kuletewa wajukuu humu ndani, mnajifanya mko busy na kazi ambazo hata sijui mnamfanyia nani kama hamtaki familia. Naye dada yako anajifanya yuko busy na masomo ambayo hata sijui anasomea nini, sitaki huo ujinga kwenye nyumba yangu" mama huyo aliongea huku akiwa anampa kijana wake maziwa.

Alikuwa anawapenda sana wanae ila alikuwa anaumia umri unaenda na hawamletei wajukuu wa kucheza nao, Calvinjr alitabasamu tu huku akikaa kwenye sofa, kwa maana alikuwa na mazungumzo marefu kidogo na mama yake.

"Sawa mama nimekuelewa kwa hilo lakini kwa leo nimekuja kuongea na wewe jambo la mhimu sana tena zaidi ya sana. Naomba usinidanganye tafadhali, mimi nakuamini sana hivyo nategemea utakacho niambia utakuwa ni ukweli na nitakuamini mama yangu" maneno ya Calvinjr yalimshtua mama yake, kiasi kwamba akaacha alichokuwa anakifanya na kusogea kwenye kiti ili amsikilize mwanae wa mwisho alihitaji kujua kuna nini mpaka akamuomba asimdanganye.

"Mama yako nipo hapa, nambie ni kipi hicho kinacho kusibu mwanangu" mama aliongea kwa upole na kumpa nafasi mwanae huyo kuweza kuyasema yale ambayo yalionekana kuutesa mtima wake.
"Mama nataka kuujua ukweli kuhusu baba yangu, kwani mimi ni nani mama? Nafanana na nani, je kuna maisha yangu mengine ambayo huenda siyajui mama yangu unanificha labda?" Maswali aliyo ulizwa yalimuacha mama huyo mdomo wazi, hakutarajia ama kutegemea kama angeulizwa kwa namna kama hiyo.

Alibaki ameganda kama sanamu ambalo linasubili kuhamishwa kutoka lilipo ili kwenda mahali pengine, machozi yakikuwa yanamshuka kwenye macho yake akiwa haelewi afanye nini kwa maana maneno ambayo yalitoka kwa mwanae ilikuwa ni haki yake kujijua yeye ni nani lakini kwake ulikuwa ni mwiba mkali sana kwenye nafsi yake.

"Mwanangu kuna mtu amekwambia kwamba wewe unafanana na mtu?" Mama huyo ambaye jina lake alifahamika kama Dainesi Mtandu aliuliza akiwa anajifuta machozi taratibu kwenye macho yake. Calvinjr hakumficha kitu kwa sababu alidhamiria kumwelekeza kila kitu ambacho alikisikia wale wafanyakazi wake wakiongea kule ofisini hususani kwa mzee Bakezi (alifanya kosa kubwa sana kumtaja huyo mzee).

Mama huyo alimsogelea mwanae na kumbusu kwenye shavu lake kisha akatoka na kwenda chumbani ambako alirudi na kitabu kimoja kikiwa kwenye mkono wake.

"Hii ndiyo zawadi pekee ambayo baba yako aliniachia kabla ya kupotea siku ya mwisho kwenye macho yangu" alikuwa anaongea huku anampatia mwanae kitabu hicho.

Kitabu ambacho alikishika kwenye mkono wake kiliandikwa, INNOCENT KILLER (THE REVENGE), kikiwa na maana ya MUUAJI ASIYE NA HATIA (KISASI). Calvinjr alikipokea kwa mara kwanza kabisa kwani hakuwahi kujua kama kuna kitabu ambacho baba yake aliwahi kukipenda sana kukisoma.

"Kitabu hicho mimi nimekisoma baada ya yeye kutoweka, sikuwahi kukigusa, aliwahi kunikataza kabisa kukisoma kwani alisisitiza kwanza kama nitataka kukisoma kitabu hicho basi inanibidi nisome kwanza kitabu ambacho kinaitwa ULIMWENGU WA WATU WABAYA ila kwa bahati mbaya sana niliwahi kukitafuta sana kitabu hicho bila mafanikio na hakipo sehemu yoyote ile ndani ya maktaba zote kubwa zilizopo hapa nchini"

"Baada ya muda mrefu kupita niliamua kukisoma hivyo hivyo na nilicho kutana nacho ndani, ni kwamba kilikuwa kinamhusu mwanaume mmoja ambaye alikuwa anaishi maisha ya kawaida sana na alikuwa ni ndugu wa jaji mkuu wa nchi ila aligeuka kuwa mnyama wa kutisha sana baada ya baadhi ya watu kumuua ndugu yake na familia yake nzima"

"Mwanangu, sijui kitabu hicho mpaka leo kinahusu nini hasa ila nadhani kuna ujumbe ambao una maana fulani humo ndani japo ukikisoma unaweza usijue lolote kama ambavyo mimi sina nilijualo mpaka leo hii. Sina mengi juu ya hicho kitabu ila tu nitakujibu swali lako kama ifuatavyo"

"Mimi na baba yenu tuliwahi kupendana sana isivyokuwa kawaida, mapenzi yetu mazito ndiyo yaliyo pelekea nyie kuzaliwa. Licha ya sisi kupendana sana na kuwa tayari kuishi kwenye mazingira magumu pamoja kwa hali yoyote ila ila tulikuwa ndani ya umaskini mkubwa sana, tulikuwa na maisha ambayo hayakuridhisha kabisa hasa kwa sisi ambao tulikuwa tumepata familia kubwa hasa baada ya wewe kuongezeka ukiacha dada yako ambaye alizaliwa miaka miwili kabla yako"

"Ukubwa wa familia uliongeza mzigo mkubwa ambao ulimfanya baba yenu kuchukua maamuzi magumu sana, maamuzi ambayo mimi binafsi sikuyaridhia ila sikuwa na namna zaidi ya kuheshimu kile ambacho alikiamua. Baba yenu aliamua kwenye kuitafuta bahati yake kwenye machimbo ya madini huko Shinyanga, kwa wakati huo alipata taarifa kwamba mashimo ya madini yanatema sana"

"Ila kama ningejua basi huenda ningelazimisha tu abaki, tangu alipo ondoka siku ile, ule ndio ulikuwa mwisho wa kumuona mume wangu, sikuwahi hata kuisikia japo sauti yake kwa mara nyingine na ni miaka ishirini na mitano imepita kwa sasa."

"Baada ya muda mrefu sana kupita nililazimika kuanza kufuatilia ili nijue tatizo lilikuwa nini? Niliamini hata kama angekuwa amezidiwa sana na kazi, bado asingekosa muda wa kunitafuta na kunijulia hali ikiwa nina mtoto mchanga kabisa ambaye ulikuwa ni wewe hapo."

"Baada ya kufuatilia kwa wiki nzima bila kupata majibu, ilitolewa taarifa kwenye mitandao na vyombo vya habari kwamba zaidi ya machimbaji wadogo hamsini walikuwa wamefukiwa na vifusi vya mgodi na kupoteza maisha.

Jitihada za kuwatafuta zilifanyika lakini walifanikiwa kuipata miili ishirini tu, hiyo mingine thelathini walitafuta bila mafanikio wakaamua kutangaza kwamba watu hao wamefia huko ndani na hivyo kuliko kuendelea kupoteza pesa ambazo zingesaidia kusomesha wanafunzi, basi mgodi huo unafungwa kwa heshima ya watu waliofukiwa na hilo eneo linatengwa kama kaburi maalumu kama heshima kwa nchi kwa kuwapoteza wapambanaji hao"

"Nilichanganyikiwa kiasi kwamba nikawa natamani niyachukue hata maisha yangu baada ya watu wote ambao walipona kuruhusiwa kurudi nyumbani lakini cha ajabu baba yenu hakurudi kabisa, kwa maana hiyo ni kwamba baba yenu alikuwa moja ya watu ambao walifukiwa na vifusi hivyo huko kwenye machimbo. Kwangu mimi sikutaka kuamini kwamba mume wangu amekufa kwa sababu sikuona hata mwili wake nikathibitisha mwenyewe ila kwa asilimia sabini ni kwamba hakuwa hai"

"Kama mume wangu angekuwa mtu aliye changanyikiwa na dunia ningeamini kwamba alipata madini na akaamua kuitelekeza familia yake kwenda kuishi maisha mazuri mbali na sisi, lakini baba yenu aliipenda familia yake kuliko kitu chochote kile hivyo asingeweza kabisa kufanya jambo la hovyo kama hilo"

"Kilicho nifanye nighairi yale maamuzi ya kujiua, ni nyie hapo wewe na dada yako, niliwaza nitamuachia nani watoto wangu mwenyewe? Hakuwepo. Nikawaza kwa namna dunia ilivyo na watu wabaya nani atawalea wanangu kwa mapenzi ya dhati? Sikuona. Ndipo nikagundua kwamba mzigo ulikuwa ni wangu, tena wangu pekeangu!"

"Ningefanya kosa kubwa saba kama ningeamua kuwaacha pekeenu bila msaada wowote, hapo ndipo yale mawazo yalipo toweka kabisa kwenye kichwa changu ya kujiua"

"Maisha yalikuwa magumu sana pekeangu bila msaada wowote ule, nilizunguka kila sehemu huku nikiwa nimekubeba mgongoni na dada yako anatembea taratibu nikitafuta vibarua. Kuna watu walinisaidia na kuna watu walikuwa wakinitukana, yote ilikuwa kheri kwangu na nilishukuru kwa uzima"

"Nilibahatika kupata kazi ya kuuza kwenye mgahawa ambayo ndiyo ilibadilisha maisha yangu, nilifanya kazi kwa bidii sana maana kila nikiwaangalia nyie nilikuwa napata uchungu mkubwa sana moyoni mwangu.

Nilijitahidi kuhifadhi mpaka nilipo pata mtaji wa kuuza maji, niliuza maji na bidhaa za nyumbani ambazo zilileta tumaini jipya mpaka nikafanikiwa kuinunua kampuni yangu ambayo ndiyo unaisimamia mpaka leo na imebadilisha maisha yetu yote mpaka leo" mama huyo alimaliza kusimulia akiwa anamuangalia mwanae usoni.

Calvinjr alimsogelea mama yake na kumfuta machozi, hakutakiwa kuuliza hayo yote kwa maana ni kama alikitonesha kidonda kwenye moyo wa mama yake.

"Nimekuelewa mama na naomba sana unisamehe. Mimi nakuamini sana wewe mama kuliko mtu yeyote yule kwenye maisha yangu" Calvinjr alimbusu mama yake kwenye paji la uso huku akitoka nje na kuondoka. Hicho ndicho kitu pekee kilicho mpeleka kwa mama yake hivyo kukaa naye karibu huenda angeendelea kuiharibu furaha ya mwanamke huyo wa zamani kidogo.

Dainesi Mtandu baada ya mwanae kuondoka, alijibeba hapo na kuelekea chumbani kwake ambapo baada tu ya kuingia aliufunga mlango wa chumba hicho. Aliusogelea ukuta, sehemu ambayo usinge idhania palikuwa na mlango wa siri ambapo alisogeza jicho lake kwenye sehemu ya ukuta ambayo ilikuwa na nukta ndogo sana.

Sehemu hiyo ilifunguka, akaingia huko ndani. Kwenye ukuta zilikuwa zimebandikwa picha nyingi sana kubwa za mwanaume ambaye alikuwa ndani ya suti ya bei lakini kwenye picha zote mtu huyo alikatwa upande wa kwenye kichwa.

"Sitaruhusu huyu mtoto aje kujua lolote kuhusu wewe kamwe, hatakiwi kuijua historia ya maisha ya asili yake wala hatakiwi kukufahamu wewe. Acha aishi maisha ya kawaida kama waishivyo watoto wengine, nipo tayari kuibeba dhambi ya kumdanganya huyu mtoto mpaka naingia kaburini ila sio kumwambia ukweli wowote kuhusu wewe. Hata wewe huko uliko naomba unisamehe sana kuhusu hili maana sina namna." Mama huyo alitamka maneno hayo huku akiwa anatoa chozi.

Aliinama kwenye droo moja humo ndani na kuitoa simu. Aliiwasha simu hiyo na kupiga namba ambayo ndiye pekee ilikuwa imehifadhiwa kwenye simu nzima. Simu iliita upande wa pili na kupokelewa.
"Uko wapi?"
"Nakuja hapo sasa hivi mambo yameaanza kuharibika" mama huyo aliongea mfululizo baada ya mtu wa upande wa pili kumwelekeza alipokuwepo.

Hakuonekana kuwa na amani kabisa maana hofu ilimtawala moyoni, alifunga hiyo sehemu haraka sana na kujifunga mtandio usoni kisha akatoka ndani kwake. Nje aliwakuta walinzi wake wanamsubiri lakini cha ajabu aliwaambia kwamba gari ataendesha mwenyewe na asifuatwe na mtu yeyote.

Unahisi huyu mama ana siri gani moyoni? Anajaribu kumficha nini mwanae? Yule mwanaume kwenye kile chumba ni nani? Anaenda kukutana na nani na kwa sababu zipi?

Bado ni mapema sana, episode ya 4 inafika tamati.

Wasalaam.

Febiani Babuya.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom