Mambo ya Kuzingatia Kabla ya Kutafuta Leseni ya Biashara ya Duka la Dawa

Mambo ya Kuzingatia Kabla ya Kutafuta Leseni ya Biashara ya Duka la Dawa

youngkato

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2014
Posts
3,638
Reaction score
3,641
1*ibZzeKfYXcrovDfq8besIg.jpeg

Kabla hujawekeza muda na fedha kwenye kufungua duka la dawa, ni muhimu ujue vigezo na masharti yanayoelekezwa na Baraza la Famasi. Kukosa kuyafuata kunaweza kukugharimu muda, pesa na hata kusababisha maombi yako kukataliwa. Hapa chini tumekuletea mwongozo:

1. REJAREJA / COMMUNITY PHARMACY​

Kama unataka kufungua famasi ya rejareja, zingatia masharti haya:

  • Ukubwa wa jengo: Lile eneo la famasi lazima liwe na angalau mita za mraba 30 (30m²). Eneo dogo zaidi halitakubalika.
  • Umbali kutoka famasi nyingine: Duka lako liwe si chini ya mita 150 kutoka famasi nyingine ya rejareja. Hii inalenga kupunguza ushindani usio na tija na kuhakikisha upatikanaji wa huduma katika maeneo mengi.
  • Ukaribu na maeneo hatarishi: Epuka kujenga karibu na bar, kituo cha mafuta, dampo la taka, mifereji ya maji taka au gereji. Umbali wa angalau mita 100 unatakiwa. Pia, hakikisha unakuwa umbali wa mita 50 kutoka maabara.
  • Umbali na vituo vya huduma za afya za Serikali:
  • Angalau mita 500 kutoka Hospitali ya Taifa au Hospitali ya Kanda.
  • Angalau mita 400 kutoka Hospitali ya Mkoa.
  • Angalau mita 300 kutoka Hospitali ya Wilaya.
  • Angalau mita 200 kutoka kituo cha afya au zahanati.
Ukishajiridhisha na masharti hayo:

  • Jaza fomu ya maombi ya ukaguzi wa awali (Approval of Location Form — PCF.5a) kwa umakini.
  • Lipia TZS 100,000/= kupitia control number kwa ajili ya ukaguzi na hifadhi risiti ya Baraza kama uthibitisho.

2. JUMLA / WHOLESALE PHARMACY​

Kama ndoto yako ni kuuza dawa kwa jumla, basi utahitaji:

  • Ukubwa wa jengo: Liwe na angalau mita za mraba 60 (60m²).
  • Vigezo vingine: Fuata hatua zote kuanzia (iii) hadi (vii) zilizotajwa kwenye sehemu ya rejareja.

3. MAELEKEZO MUHIMU YA KUZINGATIA​

  • Usifanye matengenezo kabla ya ukaguzi: Kabla ya ukaguzi wa awali, huruhusiwi kufanya marekebisho yoyote makubwa ya jengo.
  • Mamlaka ya mwisho: Baraza lina uamuzi wa mwisho kuhusu kama eneo lako linafaa kwa famasi au la. Jukumu lako ni kuhakikisha unazingatia masharti yote.
  • Mawasiliano: Hakikisha namba za simu unazojaza kwenye maombi zinapatikana muda wote. Ukipatikana kirahisi, unaongeza nafasi ya maombi yako kuchakatwa haraka.
1*vDPpi0SUu-pkvu99MWrwBA.jpeg

Kama tayari umetimiza masharti haya yote, basi usipoteze muda. Victoria Agency ipo kwa ajili ya kukusaidia kupata leseni ya biashara yako haraka na bila usumbufu. Tunakusaidia kuandaa nyaraka, kufuata taratibu na kuhakikisha unapata kibali cha kuendesha duka lako kwa uhalali.

Fika ofisini kwetu au piga simu sasa hivi kupitia +255693880325. Usichelewe anzisha safari ya kufungua duka lako la dawa kwa uhakika na amani ya akili.
 
Back
Top Bottom