Rais wa WBC, Mauricio Suleiman ataka uwepo wa V.A.R na majaji watano kwenye pambano kati ya Oleksandr Usyk na Tyson Fury

Hance Mtanashati

JF-Expert Member
Sep 7, 2016
17,456
21,167
Rais wa WBC Mauricio Suleiman atoa pendekezo kuwe na V.A.R kwenye pambano la wababe kati ya Tyson Fury (Gypsy King) na Oleksandr Usyk (The cat).

Mauricio hakuishia hapo apendekeza pia kuwe na majaji watano kwenye hilo pambano la wababe litakalofanyika May 18 Riyadh Saudi Arabia.

Sababu kuu ya kufanya hivyo ni kuondoa lawama au dosari zozote zile za upendeleo ili mtu akipigwa apigwe kihalali kusitokee malalamiko ya aina yoyote ile kama malalamiko yaliyotokea kwenye pambano la mwisho la Tyson Fury dhidi ya Francis Nganou.

Ikumbukwe pambano hili ni kubwa sana kwa kuwa wanaunganisha mikanda yote minne mikubwa kidunia kupata undisputed champion katika uzito wa juu zaidi
(heavyweight division).

Wote wawili hawana historia ya kupigwa .

Tyson Fury ana jumla ya mapambano 35 ameshinda 34 ,24 kwa K.O na moja ametoa sare.

Usyk anajumla ya mapambano 21 ameshinda yote ,14 kwa K.O.

Ikumbukwe Usyk alikuwa Undisputed champion kwenye uzito wa cruiserweight na baada ya kuona hana tena mpinzani baada ya kumchapa swahiba wa Anthony Joshua anaitwa Anthony Bellew ambaye angalau kidogo alikuwa anaonekana Bora kwenye uzito huo ndipo akapanda uzito mpaka heavyweight kupata challenge mpya.

Usyk ameendeleza ubabe kwenye heavyweight na kufanikiwa kuchukua mikanda mbalimbali ikiwemo mikanda mitatu mikubwa ya kidunia ambayo ni WBA,WBO na IBF amebakisha mkanda mkubwa mmoja ambao ni WBC unaoshikiliwa na Tyson Fury.

Hakika hili pambano la wababe na rais hataki kabisa kuona mbeleko ya aina yoyote atakayeshinda basi ashinde kihalali.

#ENJOY THE SWEET SCIENCE OF BOXING#.

Save the date May 18 2024.

🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥
 
Pambano la Fury vs Usyk ilibidi lifanyike tangu desemba 2023 lilasogezwa mbeleni mpaka februali 17 2024 kutokana fury alipata pambano dhidi ya Francis Nganou na Usyk alipata pambano dhidi ya Daniel dynamite Dubois (triple D) .

februal 17 napo limesogezwa mpaka may 18 kutokana na fury kupata majeraha kambini.
 
Rais wa WBC Mauricio Suleiman atoa pendekezo kuwe na V.A.R kwenye pambano la wababe kati ya Tyson Fury (Gypsy King) na Oleksandr Usyk (The cat).

Mauricio hakuishia hapo apendekeza pia kuwe na majaji watano kwenye hilo pambano la wababe litakalofanyika May 18 Riyadh Saudi Arabia.

Sababu kuu ya kufanya hivyo ni kuondoa lawama au dosari zozote zile za upendeleo ili mtu akipigwa apigwe kihalali kusitokee malalamiko ya aina yoyote ile kama malalamiko yaliyotokea kwenye pambano la mwisho la Tyson Fury dhidi ya Francis Nganou.

Ikumbukwe pambano hili ni kubwa sana kwa kuwa wanaunganisha mikanda yote minne mikubwa kidunia kupata undisputed champion katika uzito wa juu zaidi
(heavyweight division).

Wote wawili hawana historia ya kupigwa .

Tyson Fury ana jumla ya mapambano 35 ameshinda 34 ,24 kwa K.O na moja ametoa sare.

Usyk anajumla ya mapambano 21 ameshinda yote ,14 kwa K.O.

Ikumbukwe Usyk alikuwa Undisputed champion kwenye uzito wa cruiserweight na baada ya kuona hana tena mpinzani baada ya kumchapa swahiba wa Anthony Joshua anaitwa Anthony Bellew ambaye angalau kidogo alikuwa anaonekana Bora kwenye uzito huo ndipo akapanda uzito mpaka heavyweight kupata challenge mpya.

Usyk ameendeleza ubabe kwenye heavyweight na kufanikiwa kuchukua mikanda mbalimbali ikiwemo mikanda mitatu mikubwa ya kidunia ambayo ni WBA,WBO na IBF amebakisha mkanda mkubwa mmoja ambao ni WBC unaoshikiliwa na Tyson Fury.

Hakika hili pambano la wababe na rais hataki kabisa kuona mbeleko ya aina yoyote atakayeshinda basi ashinde kihalali.

#ENJOY THE SWEET SCIENCE OF BOXING#.

Save the date May 18 2024.

Ila heavyweight boxing imekuwa so desperate asee. Yaani mtu akiniambia eti Fury na Usyk ni bonge la pambano huwa nacheka sana. I really miss the goiden era ya kina Tyson, Evander, Bowe, Lewis, Mercer, Botha, Tua et al.
 
Hao uliowataja wana sifa gani za ziada kuliko Fury na Usyk?
 
Wana uwezo sio sifa. Huyo Fury na kitambi chake cha bia hata David Tua tu anamtosha. Asingeweza kuhimili mawe ya Samoan tornado.
Uwezo kwenye nini ambao Usyk na Fury hawana?

Defence? Powerful punches, movements? Techniques ? accurate punches? Iron Chin? au kitu gani?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom