matunduizi
JF-Expert Member
- Aug 20, 2018
- 6,587
- 15,373
1: Nyota
2: MAOMBEZI NA VILINGE VYA MAOMBI
3: Maneno mengi.
4: Vikundivikundi vingi vya kusaidiana wakati wa kufa
Huu ni ushirikina. Kuamini mambo ya nyota ni kuamini mambo ya kishirikina. Stori za mtu kuchukua nyota ya mwenzake au kufunga nyota ni mbinu za kutia ujinga raia ili wawe wavivu.
Unakuta mtu amekaa kizembe ukiuliza unaambiwa eti alikiwa na nyota sana huyo imechukuliwa. Hizo story China, US, Japan na kwa watu wanaoendelea hazipo. Bill gate, Carlos Slim, Mo, Buffet, Dangote hawana pesa kwa sababu ya nyota, ni mipango.
Unakuta mtu amekaa kizembe ukiuliza unaambiwa eti alikiwa na nyota sana huyo imechukuliwa. Hizo story China, US, Japan na kwa watu wanaoendelea hazipo. Bill gate, Carlos Slim, Mo, Buffet, Dangote hawana pesa kwa sababu ya nyota, ni mipango.
2: MAOMBEZI NA VILINGE VYA MAOMBI
Mambo mengi yanayoombwa ni matokeo ya kukiuka taratibu za Mungu au kanuni za Mungu. Kama wachungaji wangekuwa siriasi wangewafundisha waumini maombi na kutimiza wajibu ni vitu visivyotengana. Wajiombee wenyewe hukohuko.
Ukila vibaya utakufa kwa magonjwa ya kujitakia. Usipokuwa siriasi na Mungu utanyukwa na majini na wachawi hadi akili zikae sawa. Ukiwa muhuni utavuruga familia. Hakuna maombezi ni kufuata kanuni. Mimi ukija nikuombee lazima nikufanyie interview, na kukuelekeza ulichokosea ukarekebishe hakuna kuchoshana. Matatizo mengi ya wanaopenda maombi ni ukosefu wa maarifa. Wanatakiwa kuelimishwa sio kuombewa.
Hii inajumuisha na maombezi ya kiganga.

Vitu vya kutenda, tunapiga maneno mengi sana. Yaani kila mtu anajifanya pundit wa maisha. Maneno yanatakiwa kuwa machache vitendo vingi. Kila kitu tunataka tukijadili. Hata mwenyezi Mungu wakati anaumba dunia alitumia maneno machache kuleta matokeo makubwa. Hii ndio model aliyotuachia sisi tulioumbwa kwa mfano wake.
4: Vikundivikundi vingi vya kusaidiana wakati wa kufa
Yaani nchi nzima tunawaza kufakufa tu au kufiwa. Unakuta mtu anaMkoba sita, za Form four, chuoni, majirani, kazini, vikoba na utitiri wa vijikundi vya jusaidiwa wakati wa shida. Akili inayowaza na kujihami na shidashida hizo taabu na vifo vitakuwa vinakufuatilia kama unavyovifuatilia.
Tunatumia muda mwingi sana kujihami tusife, au tusionekane wabaya. Lazima tuwe na kiasi. Vikundi vingi vilipaswa vile vya kutuvusha kimaisha. Vikundi vya maendeleo. Ulaya ilifanikiwa kwa watu wenye akili zinazofanana kuunda vikundi na kubuni mambo ya maana bila kujali umbali wao. Sio vikundi vya misiba, birthday, majanga, kujifungua mtoto, harusi na kitchen party.
Ni hayo tu.