SoC01 Mambo ya kujifunza kwenye mafanikio ya Diamond Platnumz

Stories of Change - 2021 Competition

Mancobra

Member
May 31, 2021
54
95
Naseeb Abdul Juma Issack (maarufu kama Diamond Platnumz; majina mengine ya kisanii ni Chibu, Simba au Dangote; alizaliwa dar es salaam, 2 october 1989 ni mwimbaji wa nyimbo za Bongo flava kutoka Tanzania. Diamond ni msanii mwenye mafanikio makubwa kuliko wasanii wengine Tanzania na Afrika mashariki. Hii inatokana na juhudi alizonazo Diamond tangu alipoanza rasmi kuingia kwenye hii tasnia ya muziki wa Bongoflava. Mafanikio ya Diamond yameonekana kwenye nyanja mbalimbali za maisha ambapo tumeshuhudia mafanikio ya Diamond kwenye muziki, uchumi, kijamii na kimataifa. Mafanikio ya Diamond yametokana na kazi ya muziki anayofanya. kwenye muziki, Diamond amefanikiwa kupata tuzo nyingi za ndani ya nchi na nje ya nchi, kumiliki lebel ya WCB na kufanya collabo na wasanii wakubwa mfano; Rick Ross na Burna boy. mafanikio ya Diamond kiuchumi yanaonekana kutokana na kumiliki vitega uchumi vingi kama radio, Tv, Diamond karanga na kufanya matangazo ya biashara. Lakini pia, mafanikio ya Diamond kijamii yanaonekana kulingana na kuwa na followers wengi social nertworks, kusafiri nchi mbalimbali na kutengeneza urafiki na jamii za watu wenye tamaduni tofaut na Tanzania. kimataifa Diamond platnumz anajulikana kutokana na kazi yake ya muziki na ni miongoni wa watanzania wachache wanaopeperusha bendera ya Tanzania kimataifa. Mafanikio ya Diamond yanazidi kuongezeka kila siku na kumfanya kuwa msanii wa kwanza Afrika Mashariki kwa utajiri na kuwa msanii wa pili Afrika kwa kumiliki radio baada ya Youssou Ndour wa Senegal.

Mafanikio ya Diamond ni moja ya kiu ya vijana wengi wa Tanzania kufikia mafaniko yake; mafanikio ya kumiliki nyumba nzuri, vitega uchumi vya uhakika, magari ya kifahari na kutambulika kimataifa. Hii inatokana na ukweli kuwa Diamond ni msanii aliyetoka maisha ya kawaida sana na kwa aina ya kazi aliyochagua kufanya(muziki) kwa mazingira ya Tanzania huwa ni ngumu kufikia mafanikio ya juu sana. Lakin Diamond ameonesha unaweza kufanikiwa pasipo kujali mazingira unayotoka. hivyo basi kupitia mafanikio ya Diamond, vijana watanzania tunapata kuelewa mambo yafuatayo;​
  1. Kusoma(elimu) sio kigezo cha kupata utajiri ila ni njia ya kufikia mafanikio: Elimu ya diamond platnumz ni form four, ila kiwango cha mafanikio yake ni zaidi ya wasomi wengi wenye Phd, masters, degree na diploma. Kwa baadhi ya watanzania, watu huamini bila kuwa na elimu kubwa huwezi kuwa tajiri au wanaamini huwezi kuishi maisha unayopenda, kitu ambacho sio kweli. mwalimu nyerere alishawahi kusema "kusoma sio kupata utajiri ila ni njia itakayokuwezesha kupata utajiri". Huu msemo umethibitishwa na Diamond platnumz kwani kiwango cha elimu yake na mafanikio yake ni tofauti na fikra za watanzania wanaoamini bila elimu kubwa hakuna mafanikio. lakin kupitia mziki,Diamond ameweza kupata elimu ya kukabiliana na changamoto za maisha. hii inaonesha bila kujali kiwango cha elimu ya darasan uliyonayo unaweza kujifunza fani yoyote itakayokupa maarifa ya kukabiliana na changamoto za maisha.​
  2. Mazingira sio kikwazo kufikia ndoto zako: Kuna dhana imejengeka miongoni mwa vijana watanzania kuwa ningezaliwa ulaya, china au marekani ningefanikiwa kimaisha na nisingekua na maisha ya dhiki kiasi hiki. Hii inapelekea baadhi ya vijana kwenda ughaibuni kutafuta maisha, wengine hufanikiwa na wengne huambulia patupu. kwa wale wanaoshindwa kufikia ndoto zao baada ya kwenda ulaya, Diamond platnumz anaweka wazi kwamba bongo sio bahati mbaya, unaweza kupambana ukiwa ardhi ya bongo na ukafanikiwa sana pengine hata kushinda walioenda ulaya. Diamond amezaliwa na kukulia Tandale, mitaa wanayoishi watu wa tabaka la kawaida sana nchi Tanzania, lakini kutokana na bidii na nidhamu ya kazi, leo Diamond anaweza kwenda sehemu yoyote duniani bila kuhofia gharama za maisha na pia ameitangaza tandale na Tanzania. Hivyo basi, mazingira sio sababu ya kushindwa kwako kikubwa ni kuwa mbunifu na kujifunza kitu ambacho dunia inataka ukiwa kweny mazingira yako. mfano, tumeona Diamond akifanya collabo na wasanii wa marekani, south Africa na Nigeria bila kukimbilia kwenda kuchukua uraia wa nchi hizo na kubaki Tanzania huku akiendelea kujitangaza.​
  3. kuna kundi la watu nyuma ya mafanikio yako: Nyuma ya mafanikio kuna watu waliowezesha mafanikio yako au waliojaribu kukwamisha mafanikio yako. Mafanikio ya Diamond yamechangiwa na sisi mashabiki, management yake( babu Tale, Salam na mkubwa Fella), familia yake (mama) yake, media(radio na social media) na wasanii wenzake. Kuwa na kundi kubwa la watu mnaofahamiana, kuheshimiana na kuthaminiana ni muhimu kwenye maisha ya leo kwani kupitia watu, unaweza kupata connections za maisha. Collabo alizofanya Diamond platnumz ni zao la kufahamiana na watu wa aina tofauti tofauti. Lakini pia, mama mzazi wa Diamond amechangia kwa kiasi kikubwa mafanikio ya Diamond kwa kutomzuia kuimba mziki wakati anasoma shule ya msingi na kumnunua CD za album za wasanii wa kipind hicho. hii sapoti kutoka kwa mama imechangia mafaniko ya Diamond. Hivyo basi, kuishi vizuri na watu wa aina na tamaduni tofauti ni msingi wa kutengeneza njia nzuri ya mafanikio.​
  4. Matatizo ya kifamilia yasiwe kikwazo cha mafanikio: Ni ukweli usiopingika kuwa matatizo ya kifamilia ni chanzo cha watoto wengi kushindwa kufikia ndoto zao nchini Tanzania. matatizo ya kifamilia kama wazazi kutengana, baba kumkataa mtoto hupelekea watoto wengi kuishi na mzazi wa kike pekee. Hii husababisha kukosekana kwa mahitaji ya msingi ya mtoto na kukatisha ndoto zao. Diamond ametoka kwenye familia ambayo ina migogoro mingi sana baada ya wazazi wake kutengana. Kama tunavyojua changamoto za kulelewa na mama asiyekuwa na kipato kikubwa, lakini Diamond alipambana na kushinda changamoto hizo na kufikia malengo yake. Hivo basi, kama vijana migogoro isiwe sababu ya kukatisha ndoto zetu, kikubwa ni kufocus kwenye unachoamini. Lakini pia, wazazi wasiache kutoa sapoti kwa watoto wao hata kama wameshatengana, mama Diamond ni mfano mzuri wa kuigwa kwasababu aliendelea kumsapoti Diamond.​
  5. Kubali kujifunza kama unataka mafanikio: One incredible kwenye soga za mzawa anasema "hakuna maisha bora kwa kijana asiyejifunza, kujifunza hakuna maana kwa kijana asiyejituma". Kujifunza huja baada ya kukubali kitu flani huna na unatamani kukijua au kukipata. Diamond amezaliwa na kukulia Tandale ambapo amesoma shule ya msingi na sekondari za kawaida ambazo wahitimu wengi wa form four huwa hawawezi kuongea kiingereza na yeye akiwa mmoja wao. lakini mpaka sasa hivi Diamond amefanikiwa kuimba nyimbo kwa kiingereza, kufanya interview kwenye media kubwa kwa kiingereza na kuwasiliana na wasanii wa nchi mbalimbali kwa kiingereza mfano, Wiz khalifa, Busta Rhymes na wengne wengi. Sio hvyo tu, Diamond amejifunza style za wasanii wa nje kama nigeria, Congo na south Afrika ili kusudi apate mashabiki kila kona ya dunia. Cha kuzingatia kama kijana mchapakazi ni jambo la kheri kujifunza zaidi kwenye kitu unachofanya ili uongeze maarifa na kuweza kufanya kwa umakini zaidi.​
  6. Ubunifu kwenye kazi ni jambo la muhimu sana: Kuna interview moja, diamond aliwaambia wanachuo wasome ila wasisahau kuwa wabunifu kwenye kazi watakazofanya wakikosa ajira maana elimu ya darasani pekee haitoshi. Ubunifu wa Diamond unaonekana kwenye kazi yake ya mziki na huu ubunifu ndo unamfanya kuwa tofauti na wasanii wengne wa bongoflava. kuna kauli za baadhi ya watanzania husema mfano; kuna baadhi ya nyimbo Diamond akitoa utasikia mtaani watu wanasema " nyimbo yenyewe mbaya ila video ndo nzuri" , kauli za aina hii zinaonesha ubunifu kwenye kazi za Diamond na watu kutambua kitu anachofanya. Mfano mwingine wa ubunifu wa Diamond ni kwenye tuzo za BET alivyovaa kimasai ili kuvuta attention, hii ilimpa credit sana. Kwenye maisha ya kawaida hasa kwenye biashara na kazi, ubunifu ni muhimu sana kwani unakutofautisha na wengine mliopo kwenye tasnia moja.​
Hitimisho, kwenye kila mafanikio ya mtu kuna vitu vingi vya kujifunza ambavyo vinaweza kukusaidia wewe kufanikisha malengo yako. Bila kujali aina ya kazi mtu anayofanya unaweza kupata maarifa na ukiamua kutumia hayo maarifa unaweza kufika mbali kwenye safari ya kutimiza ndoto yako. Palipo na mafanikio kuna bidii na nidhamu ya hali ya juu sana mpaka mafaniko yakatokea. Hata Diamond pia, amefika hapo alipo kutokana na kufanya kazi kwa bidii na kuheshimu watu na mamlaka za mziki mfano; Diamond aliomba msamaha BASATA sababu ya wimbo wa nyegezi. Kwenye kila fani, bidii na heshima ni muhimu sana kwenye kutimiza malengo. Lakini pia kwenye kila mafanikio ya mtu kuna madhaifu mengi, ni vizuri kuchukua yale yaliyo mazuri na kuacha mabaya, Nikki mbishi anasema " nami sijakamilika sometime nakosea, msije mkahamasika na kuiga mkapotea". Kwa kujifunza na kuona mafanikio ya watu wanaotoka mazingira yako, kijana utakua kwenye nafasi nzuri ya kuamini kuwa hata wew mwenyewe unaweza na kuona hakuna kitu chochote cha kukuzuia usinunue Rolls Royce, lamborghin au usipate mafanikio makubwa.​
 
Kuna cha kujifunza kikubwa hapa.

Tukiacha unafiki, wivu na ushabiki. Huyu jamaa ni inspiration ya wengi. From zero to international
 
Naseeb Abdul Juma Issack (maarufu kama Diamond Platnumz; majina mengine ya kisanii ni Chibu, Simba au Dangote; alizaliwa dar es salaam,2 october 1989 ni mwimbaji wa nyimbo za Bongo flava kutoka Tanzania. Diamond ni msanii mwenye mafanikio makubwa kuliko wasanii wengine Tanzania na Afrika mashariki. Hii inatokana na juhudi alizonazo Diamond tangu alipoanza rasmi kuingia kwenye hii tasnia ya muziki wa Bongoflava. Mafanikio ya Diamond yameonekana kwenye nyanja mbalimbali za maisha ambapo tumeshuhudia mafanikio ya Diamond kwenye muziki, uchumi, kijamii na kimataifa. Mafanikio ya Diamond yametokana na kazi ya muziki anayofanya. kwenye muziki, Diamond amefanikiwa kupata tuzo nyingi za ndani ya nchi na nje ya nchi, kumiliki lebel ya WCB na kufanya collabo na wasanii wakubwa mfano; Rick Ross na Burna boy. mafanikio ya Diamond kiuchumi yanaonekana kutokana na kumiliki vitega uchumi vingi kama radio, Tv, Diamond karanga na kufanya matangazo ya biashara. Lakini pia, mafanikio ya Diamond kijamii yanaonekana kulingana na kuwa na followers wengi social nertworks, kusafiri nchi mbalimbali na kutengeneza urafiki na jamii za watu wenye tamaduni tofaut na Tanzania. kimataifa Diamond platnumz anajulikana kutokana na kazi yake ya muziki na ni miongoni wa watanzania wachache wanaopeperusha bendera ya Tanzania kimataifa. Mafanikio ya Diamond yanazidi kuongezeka kila siku na kumfanya kuwa msanii wa kwanza Afrika Mashariki kwa utajiri na kuwa msanii wa pili Afrika kwa kumiliki radio baada ya Youssou Ndour wa Senegal.
Mafanikio ya Diamond ni moja ya kiu ya vijana wengi wa Tanzania kufikia mafaniko yake; mafanikio ya kumiliki nyumba nzuri, vitega uchumi vya uhakika, magari ya kifahari na kutambulika kimataifa. Hii inatokana na ukweli kuwa Diamond ni msanii aliyetoka maisha ya kawaida sana na kwa aina ya kazi aliyochagua kufanya(muziki) kwa mazingira ya Tanzania huwa ni ngumu kufikia mafanikio ya juu sana. Lakin Diamond ameonesha unaweza kufanikiwa pasipo kujali mazingira unayotoka. hivyo basi kupitia mafanikio ya Diamond, vijana watanzania tunapata kuelewa mambo yafuatayo;​
  1. kusoma(elimu) sio kigezo cha kupata utajiri ila ni njia ya kufikia mafanikio: Elimu ya diamond platnumz ni form four, ila kiwango cha mafanikio yake ni zaidi ya wasomi wengi wenye Phd, masters, degree na diploma. Kwa baadhi ya watanzania, watu huamini bila kuwa na elimu kubwa huwezi kuwa tajiri au wanaamini huwezi kuishi maisha unayopenda, kitu ambacho sio kweli. mwalimu nyerere alishawahi kusema "kusoma sio kupata utajiri ila ni njia itakayokuwezesha kupata utajiri". Huu msemo umethibitishwa na Diamond platnumz kwani kiwango cha elimu yake na mafanikio yake ni tofauti na fikra za watanzania wanaoamini bila elimu kubwa hakuna mafanikio. lakin kupitia mziki,Diamond ameweza kupata elimu ya kukabiliana na changamoto za maisha. hii inaonesha bila kujali kiwango cha elimu ya darasan uliyonayo unaweza kujifunza fani yoyote itakayokupa maarifa ya kukabiliana na changamoto za maisha.​
  2. Mazingira sio kikwazo kufikia ndoto zako: Kuna dhana imejengeka miongoni mwa vijana watanzania kuwa ningezaliwa ulaya, china au marekani ningefanikiwa kimaisha na nisingekua na maisha ya dhiki kiasi hiki. Hii inapelekea baadhi ya vijana kwenda ughaibuni kutafuta maisha, wengine hufanikiwa na wengne huambulia patupu. kwa wale wanaoshindwa kufikia ndoto zao baada ya kwenda ulaya, Diamond platnumz anaweka wazi kwamba bongo sio bahati mbaya, unaweza kupambana ukiwa ardhi ya bongo na ukafanikiwa sana pengine hata kushinda walioenda ulaya. Diamond amezaliwa na kukulia Tandale, mitaa wanayoishi watu wa tabaka la kawaida sana nchi Tanzania, lakini kutokana na bidii na nidhamu ya kazi, leo Diamond anaweza kwenda sehemu yoyote duniani bila kuhofia gharama za maisha na pia ameitangaza tandale na Tanzania. Hivyo basi, mazingira sio sababu ya kushindwa kwako kikubwa ni kuwa mbunifu na kujifunza kitu ambacho dunia inataka ukiwa kweny mazingira yako. mfano, tumeona Diamond akifanya collabo na wasanii wa marekani, south Africa na Nigeria bila kukimbilia kwenda kuchukua uraia wa nchi hizo na kubaki Tanzania huku akiendelea kujitangaza.​
  3. kuna kundi la watu nyuma ya mafanikio yako: Nyuma ya mafanikio kuna watu waliowezesha mafanikio yako au waliojaribu kukwamisha mafanikio yako. Mafanikio ya Diamond yamechangiwa na sisi mashabiki, management yake( babu Tale, Salam na mkubwa Fella), familia yake (mama) yake, media(radio na social media) na wasanii wenzake. Kuwa na kundi kubwa la watu mnaofahamiana, kuheshimiana na kuthaminiana ni muhimu kwenye maisha ya leo kwani kupitia watu, unaweza kupata connections za maisha. Collabo alizofanya Diamond platnumz ni zao la kufahamiana na watu wa aina tofauti tofauti. Lakini pia, mama mzazi wa Diamond amechangia kwa kiasi kikubwa mafanikio ya Diamond kwa kutomzuia kuimba mziki wakati anasoma shule ya msingi na kumnunua CD za album za wasanii wa kipind hicho. hii sapoti kutoka kwa mama imechangia mafaniko ya Diamond. Hivyo basi, kuishi vizuri na watu wa aina na tamaduni tofauti ni msingi wa kutengeneza njia nzuri ya mafanikio.​
  4. Matatizo ya kifamilia yasiwe kikwazo cha mafanikio: Ni ukweli usiopingika kuwa matatizo ya kifamilia ni chanzo cha watoto wengi kushindwa kufikia ndoto zao nchini Tanzania. matatizo ya kifamilia kama wazazi kutengana, baba kumkataa mtoto hupelekea watoto wengi kuishi na mzazi wa kike pekee. Hii husababisha kukosekana kwa mahitaji ya msingi ya mtoto na kukatisha ndoto zao. Diamond ametoka kwenye familia ambayo ina migogoro mingi sana baada ya wazazi wake kutengana. Kama tunavyojua changamoto za kulelewa na mama asiyekuwa na kipato kikubwa, lakini Diamond alipambana na kushinda changamoto hizo na kufikia malengo yake. Hivo basi, kama vijana migogoro isiwe sababu ya kukatisha ndoto zetu, kikubwa ni kufocus kwenye unachoamini. Lakini pia, wazazi wasiache kutoa sapoti kwa watoto wao hata kama wameshatengana, mama Diamond ni mfano mzuri wa kuigwa kwasababu aliendelea kumsapoti Diamond.​
  5. Kubali kujifunza kama unataka mafanikio: One incredible kwenye soga za mzawa anasema "hakuna maisha bora kwa kijana asiyejifunza, kujifunza hakuna maana kwa kijana asiyejituma". Kujifunza huja baada ya kukubali kitu flani huna na unatamani kukijua au kukipata. Diamond amezaliwa na kukulia Tandale ambapo amesoma shule ya msingi na sekondari za kawaida ambazo wahitimu wengi wa form four huwa hawawezi kuongea kiingereza na yeye akiwa mmoja wao. lakini mpaka sasa hivi Diamond amefanikiwa kuimba nyimbo kwa kiingereza, kufanya interview kwenye media kubwa kwa kiingereza na kuwasiliana na wasanii wa nchi mbalimbali kwa kiingereza mfano, Wiz khalifa, Busta Rhymes na wengne wengi. Sio hvyo tu, Diamond amejifunza style za wasanii wa nje kama nigeria, Congo na south Afrika ili kusudi apate mashabiki kila kona ya dunia. Cha kuzingatia kama kijana mchapakazi ni jambo la kheri kujifunza zaidi kwenye kitu unachofanya ili uongeze maarifa na kuweza kufanya kwa umakini zaidi.​
  6. Ubunifu kwenye kazi ni jambo la muhimu sana: Kuna interview moja, diamond aliwaambia wanachuo wasome ila wasisahau kuwa wabunifu kwenye kazi watakazofanya wakikosa ajira maana elimu ya darasani pekee haitoshi. Ubunifu wa Diamond unaonekana kwenye kazi yake ya mziki na huu ubunifu ndo unamfanya kuwa tofauti na wasanii wengne wa bongoflava. kuna kauli za baadhi ya watanzania husema mfano; kuna baadhi ya nyimbo Diamond akitoa utasikia mtaani watu wanasema " nyimbo yenyewe mbaya ila video ndo nzuri" , kauli za aina hii zinaonesha ubunifu kwenye kazi za Diamond na watu kutambua kitu anachofanya. Mfano mwingine wa ubunifu wa Diamond ni kwenye tuzo za BET alivyovaa kimasai ili kuvuta attention, hii ilimpa credit sana. Kwenye maisha ya kawaida hasa kwenye biashara na kazi, ubunifu ni muhimu sana kwani unakutofautisha na wengine mliopo kwenye tasnia moja.​
Hitimisho, kwenye kila mafanikio ya mtu kuna vitu vingi vya kujifunza ambavyo vinaweza kukusaidia wewe kufanikisha malengo yako. Bila kujali aina ya kazi mtu anayofanya unaweza kupata maarifa na ukiamua kutumia hayo maarifa unaweza kufika mbali kwenye safari ya kutimiza ndoto yako. Palipo na mafanikio kuna bidii na nidhamu ya hali ya juu sana mpaka mafaniko yakatokea. Hata Diamond pia, amefika hapo alipo kutokana na kufanya kazi kwa bidii na kuheshimu watu na mamlaka za mziki mfano; Diamond aliomba msamaha BASATA sababu ya wimbo wa nyegezi. Kwenye kila fani, bidii na heshima ni muhimu sana kwenye kutimiza malengo. Lakini pia kwenye kila mafanikio ya mtu kuna madhaifu mengi, ni vizuri kuchukua yale yaliyo mazuri na kuacha mabaya, Nikki mbishi anasema " nami sijakamilika sometime nakosea, msije mkahamasika na kuiga mkapotea". Kwa kujifunza na kuona mafanikio ya watu wanaotoka mazingira yako, kijana utakua kwenye nafasi nzuri ya kuamini kuwa hata wew mwenyewe unaweza na kuona hakuna kitu chochote cha kukuzuia usinunue Rolls Royce, lamborghin au usipate mafanikio makubwa.

Jamani, hili jina la hapo juu sio la diamondplatnumz, baba mzazi wa diamond ni Nyange
 
Back
Top Bottom