Mambo usiyoyajua kuhusu Nyumbu

Mambo usiyoyajua kuhusu Nyumbu

Kwa hiyo unatuambia nini?
Ana tabia kama chama fulani?
Kina Kichwa cha Radar
Miguu ya Richmond
Pembe za IPTL
Mgongo wa Escrow
Usahaulifu wa kutoka scandal moja hadi nyingine?
 
kwa hapa dar nenda pale breakpoint kijitonyama hakuna bucha ila unakuta zimeshaandaliwa ila nadhani wanatuchakachulia kwa mikoani sijui

Si ajabu mnakula wo wo wo bila kujijua...........
 
Haya sasa.......
 

Attachments

  • image.jpg
    image.jpg
    9.8 KB · Views: 302
Wuh wuh wuh......agrrrrrr.......wuh........
ohhh kale kamnyama basi kuna mama mmoja muuza supu kumbe alikuwa anatumixia siku hiyo supu ikaisha mapema tukamuuliza vipi akasema mwanangu ka mbwa kenyewe leo kalikuwa kadogo
 
Hahahaha! kuna Kaka yangu mmoja alikua anapenda kutuita nyumbu!!!
 
Kwa hiyo unatuambia nini?
Ana tabia kama chama fulani?
Kina Kichwa cha Radar
Miguu ya Richmond
Pembe za IPTL
Mgongo wa Escrow
Usahaulifu wa kutoka scandal moja hadi nyingine?

umeipanga vizuri sna
 
umbile la
Nyumbu (Wild Beast). Nyumbu ana
maumbile ya wanyama kadhaa.
1. Miguu
ya nyuma na kiuno ni umbile la Fisi;
2. mkia ni umbile la Farasi;
3. michirizi ya
Pundamilia;
4. pembe ni za Nyati;
5.ndevu
ni za Pofu;
6. nywele za mgongoni ni za
pundamilia.
7.Nyumbu kwa jina lingine
anaitwa "Zero Brain". Hii inatokana na
tabia yake ya usahaulifu. Kwa mfano: Nyumbu anaweza kuwa anafukuzwa
na Simba, akikuta majani mazuri
anajisahau kuwa anafukuzwa
anasimama na kuanza kula majani.
Very amazing story

Ingependeza zaidi ungeeka na picha ya huyo nyumbu!!!
 
umbile la
Nyumbu (Wild Beast). Nyumbu ana
maumbile ya wanyama kadhaa.
1. Miguu
ya nyuma na kiuno ni umbile la Fisi;
2. mkia ni umbile la Farasi;
3. michirizi ya
Pundamilia;
4. pembe ni za Nyati;
5.ndevu
ni za Pofu;
6. nywele za mgongoni ni za
pundamilia.
7.Nyumbu kwa jina lingine
anaitwa "Zero Brain". Hii inatokana na
tabia yake ya usahaulifu. Kwa mfano: Nyumbu anaweza kuwa anafukuzwa
na Simba, akikuta majani mazuri
anajisahau kuwa anafukuzwa
anasimama na kuanza kula majani.
Very amazing story

Bwana Mziwanda, hayo yote uliyoyaelezea ni uongo mtupu??! Sijui hata hizo info umezitolea wapi?
-kwanza kabisa nyumbu haitwi wild beast? Bali anaitwa wildebeest.
-pia hana michilizi kama ya punda milia,kwani punda milia michilizi yake(stripes)ni Nyeusi na nyeupe.
-kwa jina jingine haitwi zero brain hilo jina umembatiza wewe tu.
- kwa taarifa yako wanyama wanaoliwa(herbivores) hawawaogopi wanyama wanaokula nyama(carnivores) kwani wameishi pamoja miaka nenda rudi.unapomuona nyumba kamkimbia simba na mbele kidogo anasimama haimaanishi kuwa amesahau bali wanachofanya huwa ni ku keep distance ambayo atajiona kuwa yuko salama kwani simba anapotaka kuwinda huwa kuna sign ambazo hawezi kuzificha zitakazo muonyesha mliwa kuwa yuko hatarini hivyo uamuzi wa mliwa ni either kukimbia au kuzidi ku keep distance. Na signal anazo zionyesha simba ni pamoja na concentration, shorten distance,squatting nk. Kwa kufanya hvyo mliwa lazima achukue tahadhali.lkn kama simba anapita zake bila kuonyesha moja ya signal hizo basi huyu mliwa hana haja ya kukimbia kwani wanajuana tokea zamani sna.simba akiwa na njaa ni lazima aonyeshe signal hizo nilizozitaja hapo juu.
- pia pembe hizo sio za nyati bali ni za nyumbu mwenyewe ila zinataka kufanana na za nyati.

Kwa faida ya wengine pia. Huyu nyumbu sifa yake nyingine ni pamoja na kuwa na uwezo wa ku locate mvua umbali ka km 50.wakisha jua hilo eneo linamvua bali huama na kuelekea huko na ndio sababu kati ya maajabu ya dunia kwa Tanzania tuna uhamaji wa nyumbu(wildebeest migration)ambao huama kutoka mbuga ya serengeti na kuelekea Masai mara(Kenya) na idadi yao wahamapo yapata nyumbu milion 3 pamoja na punda milia.
-pia umbali wanao zunguka kuhama eneo moja kwenda jingine wanakimbia umbali wa km 5000(elfu tano) ili kukamilisha mzunguko wote.
-sababu inayowafanya wahame ni utafutaji wa chakula, maji na malisho mazuri.
-nyumbu hawezi fanana na fisi hata sku moja

Karibuni wadau kuhusu kuuliza swali lolote kuhusu wanyama wa porini na sifa zao. ImageUploadedByJamiiForums1418335435.579521.jpg ImageUploadedByJamiiForums1418335497.921969.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom