Mambo Unayotakiwa Kuyaepuka Ukiwa Desperate Sana Kupata Pesa

Kainetics

Senior Member
Jun 20, 2022
131
259
Hello wakuu,

Katika maisha huwa kuna mambo mengi, sisi kama binadamu huwa tunapitia, na baadhi ya haya mapito, yanaweza kukuvuruga kabisa kiakili kupelekea kufanya au kujaribu kufanya mambo ambayo hata hukuwahi kudhania.

Moja ya mambo haya ni "Being So Desperate To Earn Money"

Nimecheck tafsiri ya neno Desperate, nikakuta kwa Kiswahili kilicho sanifu ni kukata tamaa. Ila feeling nayojaribu ongelea ni tofauti; so nita rephrase kidogo...



Leo nimeweza litatua jambo moja lililokua linaniletea utata baada ya siku kadhaa nikakumbuka baadhi ya experiences huko nyuma ambako nlifanya mambo kinyume kabisa, hivyo nikaona sio mbaya kushare. Kama utakua unapitia kipindi kigumu/similar natumai hii thread itasaidia, hata kidogo. Hivyo basi, bila kupoteza muda;


'Mambo ambayo hutakiwi kufanya ukiwa na uhitaji mkubwa mno wa pesa.'

(Uhitaji mkubwa mno wa pesa- inaweza kua kiasi chochote kile, kwendana na situation uliyopo. Shida kubwa kwenye hizi scenarios huwa sio kiasi chenyewe bali ugumu unaokutana nao kwenye kukipata. Pia uhitaji huu huongezeka mara kadhaa kwa kua hua kinaongezwa kikomo cha muda kwenye equation. Mfano; Deadline ya siku mbili)

1. Kubet

Kubet kama kubet au aina yeyote ile ya kamari ni mambo unayopaswa kuepuka ukiwa kwenye matatizo yoyote yale yanayohitaji uwe na kiasi kikubwa cha fedha ndani ya muda fulani.

Wengi kwenye situations kama hizi akili zetu hua zinafunga kabisa. Unajiambia ningekua na namna ya kuzalisha hii Million haraka haraka iwe million 15 kufikia kesho mchana. Nitakua nimesolve mambo yote.

Na hakuna kitu inaweza kukushawishi ukiwa that desperate, kama wazee wa Fixed Matches. Sure Odds, Sjui Correct Scores, all that. Nliwahi kua na dharura kubwa hapo nyuma, muda umepita , na pesa nliyo kua nayo mfukoni, na ile iliyokua ikihitajika vilikua hata havikaribiani hata kidogo.

Hivyo kwenye kuhangaika huku na kule, since I knew some of my friends walokua wana bet na wanapata pesa ndefu, nikawaambia wanifundishe basics. Nikaelekezwa, na nikaanza suka mikeka ya ajabu ajabu. Randomly naweka hela nione kama nitakula ila zote zikawa zinageuka losses.

Nikajaribu tafuta Groups za wanako share odds and all that nikitumaini maybe ntakua na chance nikitumia odds za pro's. Kwenye kutafuta huku na kule, nikakuta Booking Codes kama nne hivi kwenye group moja nazo nikawekea stake na kubet absent mindedly. Odds zilikua ndogo hivyo nikawa disappointed. Hela nliyokua natafuta ilikua kubwa kidogo hivyo nikaendelea surf walau nikutane booking codes za mikeka mirefu mirefu.

Ndipo nikakutana na matangazo ya hawa wanaojiita Pro's upande wa Correct Scores. Screenshot zilikua zinaonesha wins za kuridhisha, na stake ilikua ya kawaida elfu kumi, kumi na tano. Nikasema hapa nimetoboa.

Ukiwa na shida, unakuwa mwepesi wa kupata matumaini.

Nlipomcheck huyo jamaa, akanambia correct scores zake n za uhakika. Na anazinunua kwa pesa ndefu mno. Hivyo hatoi bure. Nikamuuliza kiasi, akanambia anauza timu mbili kwa 250,000/- ananipa mimi naweka stake na kusubiri matokeo.

Hela io nlikua nayo. Nikajiambia akinipea hizo na zikapita , tatizo langu litakua limemalizika na naweza ifanya kua my part time source of income. So nikaomba nimpigie kuhakiki kama ni authentic, tukaongea. Nikauliza namba ya malipo. Nikatuma hela. Teams na scores zake nikapewa.

Nikabet, stake ya 10k. Zilikua mechi za usiku huko, so I didn't wait nikalala na amani kabisa kua ntaamka na hela ya kutosha. Nikaamka kucheck mkeka umechanika. Na jamaa kaniblock. Haha. Nikatafuta mwingine nae akanitapeli. Na mwingine. Na mwingine. Ndani ya siku tatu nlikua naishatapeliwa kama laki 9 hivi. Pesa niliyokua natafuta ilikua million 5. Hivyo nikawa nimerudi nyuma.

Ilinichukua muda kukubaliana na hali kua mambo za correct score ni utapeli. Na hakuna ukweli kwenye Fixed Matches. So, ushauri wangu usijaribu. Unaweza ingiwa na matumaini ghafla na kuhisi umepata suluisho kumbe ndo unaenda kupigwa.


2. Mikopo ya Microfinance

Hapa sitoongelea kiundani. Na sio mikopo ya Microfinance peke ake. Mkopo wowote utakao hitaji uweke dhamana ya kitu chenye thamani maradufu /isiyoendana na kiasi unachokopeshwa. Mfano kuweka hati ya nyumba, gari lako, na kadhalika.

Mikopo yenye riba zaidi ya 35% ndani ya muda mfupi mno. Epukana nayo. Maana unakua umeliwa siku hio hio utakayo sign kukubaliana na hizo terms/conditions.

Shida yako utaweza itatua lakini, utajkuta kwenye shida zaidi na majuto mengi.

3. Ulozi wa Aina Yeyote Ile

Unaweza usishawishike na hio mikopo yenye riba kubwa (Pasua Kichwa) au hao jamaa wana o promise Correct Scores zenye 200+ Odds, ila ukaja kudakwa na matangazo ya kitapeli ya hawa wagaganga wa kienyeji.

Nitakuomba, hata uwe na shida kubwa kiasi gani; yapuuze tafadhali.

Sitoshare story zangu kuhusu hili coz nyingi ni vituko tu, nlikua soo desperate kipindi hicho na kutaka nishike hela nyingi in such a very short time ikapepekewa nitapeliwe na Mnigeria, Msouth, Mcongo na ilibaki nitapeliwe hadi na Msukuma akili ndipo ikanikaa sawa.

Now I look back, and just laugh. But shida zinakufanya uwe mtu wa ajabu at times.


4. Any Get-Rich-Quick Business

Hizi ziko nyingi mno. I can't list them all. Ila kama utakutana na aina yeyote ya biashara iwe offline au online itakayo promise returns za 50% , 65% 100% ,nk. Ndani ya muda mfupi mno (siku moja, siku tatu, week, etc) kimbia.

Ukiwa na shida/uhitaji. Kuna common sense switches zinajizima, unakua easily convinced. Partly, because unataka kuamini kua kitu husika kitakutatulia tatizo, na mwishowe utaishia kwenye vilio zaidi.

Ushauri wangu ni usijaribu kitu chochote kipya, hadi matatizo yako yatakapo tuama/kua manageable. And even then, approach everything new with a curious mind. Lah sivyo utaishia kupigwa.

5. Kuhusisha Watu Wengi/Ndugu

Ndio. Hautosolve matatizo yako/kuzipata hela zenyewe kwa kumshirikisha kila mtu matatizo yako. Chagua watu wachache unaoamini wanaweza kukusaidia (na uwe na sababu zenye mashiko za kukufanya uamini hivyo) ikiwa hawawezi tulizana.

Ila usimtangazie kila mtu shida zako, na uhitaji wako wa hela. You'll be surprised ni wangapi utawafuraisha kusikia uko kwenye matatizo.

6. Loosing Your Cool/ Kupanic

Usiwaze sana. Haisaidii. Jipatie muda wa kutosha kupumzima. Na jaribu kutumia muda wako kufikiria, na sio kuwaza. Ukiwa kwenye situation mbovu kuwaza kwenyewe hakukusaidii. Jitahidi uweze assess situation uliyomo mara kwa mara huku ukijaribu unda strategy nzuri ya kukabiliana nayo

Mantain your calm.

Go on with your daily routine .

Worry less.

Kama upo uwezekano wa kuipata, utaipata. Kama haupo, hata ukiacha kula, ukajikunyata, ukachanganyikiwa, hutoipata. So, jaribu kuwa mtulivu hata situation iwe mbaya kivipi.


7. Kukata Mawasiliano

You'll be surprised, kujua idadi ya matatizo unayoweza ku solve kwa kuamua kuwa muwazi na kuongea, na mtu sahihi.

Isolation, n kitu kibaya sana ambacho unapaswa ukiwepe. Haswa ukiwa kwenye situation mbovu inayohitaji pesa kwa haraka.

Liwe n deni, iwe n dharua, marejesho, any of that, usikate mawasiliano na mhusika wa upande wa pili kwenye huo muamala.

Update them about your status, efforts, progress, plans, whatever. Ila usitoke hewani.



Yangu ni hayo, karibu.
Nawe ongeza ya kwako...

Kainetics
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom