Usipoishi nao kwa akili nyingi watu hawa utajikuta matatizoni muda mwingi

Feb 4, 2024
67
206
1. Wanaojiona sahihi muda wote hawa hawachelewi kukubebesha makosa yasiyo kuhusu.

2. Wajuaji kupitiliza hawa muda wote watakulaumu tu kwani kila jambo watakuona unakosea hata kama wao ndio wamekosea.

3. Wanaokutafuta kwenye shida tu hawa utawaona marafiki ukiwa na kitu cha kuwapa ila siku ukiwa kwenye uhitaji watakuacha mtaroni.

4. Waropokaji hawa muda wowote watamwaga siri zako mbele ya wasiotakiwa kuzijua hivyo hakikisha hawajui mambo yako ambayo hayatakiwi kujulikana na wengi.

5. Wenye imani za kishirikina kupitiliza hawa hata kwenye jambo la kawaida wao watakushauri uende kwa mganga wa kienyeji kwa sababu wao hawaamini tena kwenye ukawaida.

6. Wenye imani za dini kupitiliza, hawa pia kwenye sehemu unayotakiwa utumie akili zako wao watakushauri ufunge na kuomba ili upate majibu sasa ikiwa zaidi hii inakuwa kupoteza muda. Pia watakushauri uvumilie hata sehemu unayotakiwa kuondoka.

7. Wenye wivu wa mapenzi kupitiliza, hawa kwa muda mfupi watakufanya ufurahie mapenzi ila kwa undani zaidi watafanya ufeli mambo ya msingi kwa mfano unaweza kupata dili la maana la pesa ila watakukataza usiende kalifanya wakihofia kuibiwa kimapenzi.

8. Wenye mitizamo ya kimaskini, hawa muda wote wanaamini utajiri ni dhambi hivyo ukiwa nao na wakakumudu basi watakushauri uwe sawa nao.

9. Waliokata tamaa na kuridhika, hawa muda wote watakwambia maisha ndio haya haya.

10. Wenye utoto ilihali ni wakubwa, hawa watalia kwa kila changamoto yaani kwao hawana changamoto ya kuvumilia bali kulia na kukata tamaa, ukiwa nao na wakakumudu utafanana nao.

Mwanasayansi Saul kalivubha.
 
Back
Top Bottom