Mambo tuliyodanganywa utotoni

1.Usitembee juu ya kaburi, utatoka madonda mwili mzima
2.Usikae juu ya figa mama yako atakufa siku ya tatu
3.Usiwachungulie wakubwa wakioga maji yake yaweza kukurukia jichoni maana huwa yanapofua watu.
 
1. Mtoto ananunuliwa hospitalini
2. Kufanya sex/ngono ni mambo ya ma balaa(ya kishetani)
3. Mtoto wa kiume hatakiwi jikoni atakuwa na tabia za kike
4. Mtoto wa Kiume haoti moto

NB: no. 3 & 4 nilisikia maeneo ya village kwetu nilikozaliwa.

no 4. Nilidadisi nikaambiwa na elders kuwa mwanaume sehemu ya kuzalisha/kiwanda mbegu za kiume iko nje ya mwili ambapo akiota moto hasa mkali itaadhiri uzao wake.

Tuendeleee mengine waliotudanganya ni nini?

Labda wewe Ndio Ulidanganywa Mimi/Sisi hatukuambiwa ujinga UO na Pili sikuwahi Kuuliza swali lolote na wala sikukaa Jikoni NImezaliwa House geli wapo tena watatu sasa sijui wewe Ulidangwa na nani Muweke wazi Mkuu Nafikiri hayo umeyasikia
 
kuna mfalme anaishi angani ni mwema sana na tusipotenda wema siku moja atashuka atatuchoma moto
 
  • Ukisimama mwenzako/wenzako wote wakiwa wamekaa unamnyonya damu
  • Ukiona jicho la kushoto linacheza kuna mgeni anakuja
  • Uki -imba wakati unakula utaoa mke toka mbali
  • Msichana akiwa na tabia ya kucheka cheka atakuwa changu
 
jamani utt raha sana nikikumbuka uongo wa utt na ninayoyaona ss najisikia raha ila roho inaniumaga pale ninapomdanganya mtt wangu uongo huo ananiambia bb uongo sikweli
 
Labda wewe Ndio Ulidanganywa Mimi/Sisi hatukuambiwa ujinga UO na Pili sikuwahi Kuuliza swali lolote na wala sikukaa Jikoni NImezaliwa House geli wapo tena watatu sasa sijui wewe Ulidangwa na nani Muweke wazi Mkuu Nafikiri hayo umeyasikia

Utakuwa wewe umezaliwa uswahilini/mijini ambapo ukweli daima hata kwa vitendo watoto wanaona sisi ni wa village. Unasema hukuwahi kuuliza swali mm navyojua watoto siku zote ni wadadisi wa mambo na wanapenda kujua vitu kutokuuliza swali kunaonyesha wewe zombie wa kifa mtu.
 
nakumbuka bibi yangu kuna ndege fulani akilia tu asubui bibi anakuambia nendeni stendi lazima kuna mgeni anakuja leo tena anaweza kutaja na jina kabisa yani alikuwa anamjulia sana yy anaangalia location yule ndege alolilia na alilia mara ngapi mara nyingi inakuwa kweli kabisa mara chache sana ikikwama acje mgeni
 
Utakuwa wewe umezaliwa uswahilini/mijini ambapo ukweli daima hata kwa vitendo watoto wanaona sisi ni wa village. Unasema hukuwahi kuuliza swali mm navyojua watoto siku zote ni wadadisi wa mambo na wanapenda kujua vitu kutokuuliza swali kunaonyesha wewe zombie wa kifa mtu.

alishasema alilelewa na hg so lazima alidumaa uttni huyo
 
Dada zangu wakati wananyonyoa kuku hawakutakiwa kuongea hata neno moja, kwani ukiongea manyoya ya kuku yanaota tena.
 
1. Ukitaka kupiga simu unakwenda kwenye mlingoti wa nyaya za TTCL na kuanza kuongea, hallooo!!!
2. Ukipita makaburini usinyooshee kidole kabuli, kitabaki hivyo hivyo
3. Usishone nguo na sindano ya mkono usiku
4. Ukikojoa ni lazima utemee mate pale ulipokojoa kabla hujaondoka
5. Marufuku kula na kuongea
6. Mtoto wa kiume ukipigwa na mwiko au fagio utakuwa ******* (husimamishi mdudu)
7. Usile gizani kwa sababu utakula na shetani
8. Marufuku kusema mkubwa ni mwongo mana huwa hadanganyi
9. Marufuku kubishana na wakubwa, wewe kila kitu ukiiambiwa ni sawa tu (hebu niambie watoto wa siku hizi)
 
1.Umenoa, kama unapiga Penati wakati mpinzani wako ameminya koro..... zake.
2. Weka kijiti mfano wa kiberiti kichwani, kupunguza hasira ya wazazi wakati wa mahojiano juu ya ulichokosea.
3. Ukijikwaa njiani (zaidi ya mara moja) kuna watu wanakusema mahala
4. Ukimwota amekufa huwa amekula sana na kushiba vizuri
 
Wakati wa kula kama ni wali/ugali kwa nyama,niliambiwa nisile nyama mpaka wali/ugali uishe! Duh! Kumbe nilikua nadanganywa aisee maana ukija kuzinduka nyama kwishnei! Ila hii tabia ya kula wali/ugali kisha nyama hadi leo naiona sana. Hata wewe ukiwa kwenye mgahawa jaribu kuchunguza utaona.
 
Ukiitwa usiku usiitike maana ni mashetani.

usitembee kinyumenyume utasababisha ndugu zako kufa.

ukiinamisha kichwa katikati ya miguu kama ni mtoto wa mwishokuzaliwa basi atazaliwa mwingine.

kuku wakigombana mnashikana vidole ili mpambano uendelee.

ugali ukiwa wa moto sana wakati wa kula basi alieupika ana wivu sana.

ukiwasha moto usipowaka haraka basi una tabia ya kujisaidia njiani
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom