Mambo tuliyodanganywa utotoni

NGULI

JF-Expert Member
Mar 31, 2008
4,805
1,225
1. Mtoto ananunuliwa hospitalini
2. Kufanya sex/ngono ni mambo ya ma balaa(ya kishetani)
3. Mtoto wa kiume hatakiwi jikoni atakuwa na tabia za kike
4. Mtoto wa Kiume haoti moto

NB: no. 3 & 4 nilisikia maeneo ya village kwetu nilikozaliwa.

no 4. Nilidadisi nikaambiwa na elders kuwa mwanaume sehemu ya kuzalisha/kiwanda mbegu za kiume iko nje ya mwili ambapo akiota moto hasa mkali itaadhiri uzao wake.

Tuendeleee mengine waliotudanganya ni nini?
 
Aine

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
1,604
0
7. Mama mjamzito hali yai akila yai anazaa mtoto mwenye kipara
8. Ukimaliza kula usinawe hadi wakubwa wamalize na wanawe
 
Aine

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
1,604
0
1. Mtoto ananunuliwa hospitalini
2. Kufanya sex/ngono ni mambo ya ma balaa(ya kishetani)
3. Mtoto wa kiume hatakiwi jikoni atakuwa na tabia za kike
4. Mtoto wa Kiume haoti moto

NB: no. 3 & 4 nilisikia maeneo ya village kwetu nilikozaliwa.
no 4. Nilidadisi nikaambiwa na elders kuwa mwanaume sehemu ya kuzalisha/kiwanda mbegu za kiume iko nje ya mwili ambapo akiota moto hasa mkali itaadhiri uzao wake.

Tuendeleee mengine waliotudanganya ni nini?

Nguli umenikumbusha mbali sana, thanx alot!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
Haaa haaaa haaaa haaaaaaaaaaaaaaaaa :teeth::teeth::teeth::teeth:
 
NATA

JF-Expert Member
May 10, 2007
4,510
1,195
1. Mtoto ananunuliwa hospitalini
2. Kufanya sex/ngono ni mambo ya ma balaa(ya kishetani)
3. Mtoto wa kiume hatakiwi jikoni atakuwa na tabia za kike
4. Mtoto wa kiume haoti moto

nb: No. 3 & 4 nilisikia maeneo ya village kwetu nilikozaliwa.

No 4. Nilidadisi nikaambiwa na elders kuwa mwanaume sehemu ya kuzalisha/kiwanda mbegu za kiume iko nje ya mwili ambapo akiota moto hasa mkali itaadhiri uzao wake.

Tuendeleee mengine waliotudanganya ni nini?
firgisi ya kuku ni ya baba
 
Utingo

JF-Expert Member
Dec 15, 2009
7,809
2,000
-dawa (kidonge) ikidondoka kinaishiwa nguvu, usikiokote ukameza - msisitizo wa kuwa msafi
-Mama asile mayai - msisitizo ili mtoto asiwe mkubwa sana mama akashindwa kujifungua na hakukuwa huduma za hosp kwa ajili ya operation ikitokea uhitaji huo
 
Pearl

JF-Expert Member
Nov 25, 2009
3,039
1,195
ukipita makaburini usiongee wala kugeuka nyuma
ukipewa muhindi unampa mkubwa akutengenezee njia ya kwenda kwenu(ukistuka umebaki mistari miwili tu)
 
Gaijin

JF-Expert Member
Aug 21, 2007
11,817
0
hee jamani mbona mie siku danganywa na vitu kaa hivi?

mtoto niliambiwa kuwa yumo tumboni na anakuwa mkubwa kila siku na hospitali unaenda kumtoa kwa mtindo wa kama kwenda haja kubwa :)
 
Nanren

JF-Expert Member
May 11, 2009
1,920
2,000
9. Kinyonga akitua kichwani kwako haondoki mpaka shangazi yako aje amtoe
10.Ukiona nyeti za wakubwa utapofuka macho
 
Sokomoko

JF-Expert Member
Mar 29, 2008
1,915
1,195
Naona watu hawajaelewa kitu gani kinahitajika hapa. Kuna vitu tulivyokuwa tukidanganywa kama watoto wanunuliwa, etc na kuna myth "Mvua ikinyesha huku jua linawaka ujue simba anazaaa." Hapo zawamani watoto wadogo ilikuwa ngumu kujua watoto wanapatikanaje ila sasa mambo yako wazi sana dogo wa miaka 7 anakuelezea kila kitu!
 
Mentor

JF-Expert Member
Oct 14, 2008
20,342
2,000
- Ati watu wakubwa hawanyi...ukimwona baba anaenda ******, ujue anaenda kutema mate tu.
- Kidudu chako ni cha kukojolea tu!!!!
- ukilia kwenye sufuria hutaoa (dat explains it eeh...maana nshachoka mimi kungoja mke mwema!lol)
- etc.
 
Rubi

JF-Expert Member
Oct 5, 2009
1,621
1,500
1. Kama ulikuwa mpenda nyama, ukila nyama halafu ukajifunga lile fupa shingoni ukalala nalo asubuhi ukiamka unakuta l imejaa nyama.

2. Ukipiga mluzi usiku unakaribisha nyoka nyumbani kwako
3. kama mnakula kwenye bakuli moja usitangulie kuchukua nyama kabla ya wakubwa matokeo yake unambulia patupu. halafu mwalimu wetu shule akatwambia vice versa kuwa kama manakula na wakubwa uwe wa kwanza kuchukua nyama tena kile kipande kikubwa na kizuri kwa sababu wewe ni mtoto unayehitaji kukua vizuri.

4. usinawe kabla ya wakubwa na usianze kula kabla ya wakubwa. afadhali siku hizi kila mtu na sahani yake.
 
Pearl

JF-Expert Member
Nov 25, 2009
3,039
1,195
ah ah ah sasa ww ur on ur way to heaven unataka mkeo aje kukaa eda?
- Ati watu wakubwa hawanyi...ukimwona baba anaenda ******, ujue anaenda kutema mate tu.
- Kidudu chako ni cha kukojolea tu!!!!
- ukilia kwenye sufuria hutaoa (dat explains it eeh...maana nshachoka mimi kungoja mke mwema!lol)
- etc.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom