Mambo tuliyodanganywa utotoni

Mambo tuliyodanganywa utotoni

Ukiitwa usiku usiitike maana ni mashetani.

usitembee kinyumenyume utasababisha ndugu zako kufa.

ukiinamisha kichwa katikati ya miguu kama ni mtoto wa mwishokuzaliwa basi atazaliwa mwingine.

kuku wakigombana mnashikana vidole ili mpambano uendelee.

ugali ukiwa wa moto sana wakati wa kula basi alieupika ana wivu sana.

ukiwasha moto usipowaka haraka basi una tabia ya kujisaidia njiani

:teeth::teeth::teeth::teeth:
 
1. Mkiwa porini (e.g kuokota kuni) wingu kubwa likitanda kama mvua inataka kunyesha, atafutwe mtoto wa mwisho na mumfunge kamba kidole chake cha mwisho na mvua haitanyesha hadi mumfungue

2. Ukitwanga na mtwangio chini, mbingu Zitaanguka

3. Ukikalia kinu halafu ukajamba, utapata kifafa

4. Ukionyesha kidole kwenye makaburi lazima uking'ate, la sivyo hakitakunjika tena na kubaki kimenyoka hivohivo
 
Back
Top Bottom