Mambo tata kuhusu NASA na safari ya mwezini: Ni kweli Neil Armstrong alisilimu baada ya kusikia Adhana mwezini?

US hawawezi kudanganya kuhusu kutua Mars au popote angani bila kubainiwa na Russia na China. Labda kama unaamini US wana pesa ya kuzihonga nchi hizo.
Je ikiwa ni syndicate ya watu wachache kuwajengea hofu wengi!? Kujidhihirisha ukubwa na ubora kwa kuonekana kufanikisha yale yasiyowezekana!?

Huwa naupenda mfano wa Nuclear Tech.. jinsi inavyokuwa ya kikundi fulani tuu... Ukijaribu lazima usongwesongwe na madhila mpk ukome. Ukiwa mbishi kama Uchina unatoboa na ww unakaa mezani unaanza kucheza karata za kikubwa
 
Huyu jamaa hata angesilimu basi asingeunufaisha chochote uislamu.

Kusilimu ingekuwa ni faida kwake na wala sio kwa dini ya uislamu.sijui kwa nini watu wanazusha sana hizi habari ambazo uhakika wake ni utata.

Akisia adhana ama asisikie huko mwezini kama alienda kweli hiyo bado sio hoja ya kuwa sasa uislamu ndiyo dini imebainika ya kweli

Uislamu utabaki kuwa uislamu tokea hapo.
Sahihi🤝
 
Anyway mambo ya dini hayajawahi kufikia kikomo cha mjadala. Na u apozungumzia imani ni ngumu sana akili kutumika kwenye majadiliano.

Waislamu wanapenda sana kutumia watu maarufu kujitangaza, ndio maana hata Loon ( Yule rapper ) alipewa airtime sana baada ya kusilimu.

Hata hapa kwetu, check ilivyotokea kwa Ben po.
Sidhani kama , uko sahihi
 
Kuna sehemu nitakuuliza kama hewa hakuna sauti itafikaje na wote wanatumia redio maalumu.
Kwa kuwa teknolojia kipindi hicho iliyokuwa inaweza kufika anga ya juu zaidi SW(short wave) kimawasiliano
View attachment 1707298
View attachment 1707299

Na kumbuka SW ilikuwa inamuingiliano wa redio zilizokuwa zinatumika kwa wale mnao kumbuka SW labda kidogo AM.inawezekana katika mawasiliano signal zikaingilia za redio iliyopo nchi ambazo mda fulani kupiga adhana na kumfanya kuuliza labda wakati akitafuta muelekeo wa mawasiliano
Hapa umenifungua kitu kingine inawezekana pia ulikuwa muingiliano wa soundwaves za Adhana huku duniani

Lakini je muingiliano wa sauti huwa na sauti thabiti isiyoyumba yumba?? rejelea kwenye makala hapo jibu alilojibu Neil...(kama ni kweli) ya kwamba sauti ile ilikuwa kali zaidi na Thabiti tofauti ya za miskiti aliyoziskia huku

Miingiliano ya Sauti haiwezi kuwa pure perfect rejelea Experiment ya nikola Tesla na muingiliano wa soundwaves kati ya watu nchi tofauti
 
1.Neil Armstrong hakuwahi kuwa Muislamu, hivyo vyanzo vyako taarifa ni kutoka vyombo vya udaku,kwa hapa bongo ungeweza kulinganisha na magazeti ya Shigongo.
2.UFO ni Unidentified Flying Object sio vyombo vya kigeni kutoka sayari nyingine. Ni vitu ambavyo huwa vinaonekana vikizunguka karibu na sayari ya dunia lakini lakini haviwezi kutambulika au kueleweka ni nini hasa, kuongelea kuna UFO nje huko mbali na dunia haina mashiko.
 
Huyu jamaa hata angesilimu basi asingeunufaisha chochote uislamu.

Kusilimu ingekuwa ni faida kwake na wala sio kwa dini ya uislamu.sijui kwa nini watu wanazusha sana hizi habari ambazo uhakika wake ni utata.

Akisia adhana ama asisikie huko mwezini kama alienda kweli hiyo bado sio hoja ya kuwa sasa uislamu ndiyo dini imebainika ya kweli

Uislamu utabaki kuwa uislamu tokea hapo.
Watu wanatengeneza rumors hizi kwa ma celebreties au watu wakubwa wenye ushawishi kwa lengo la kuwa convince watu waifuate imani hiyo

Na kweli kwa kiasi flani wanafanikiwa, mfano jamaa yako Jurjani anaamini kuwa Jacques Cousteau alisilimu baada ya kushuhudia bahari mbili zilizokutana bila maji kuchangamana kwa dhana ya kwamba kuran ni kitabu cha mungu kweli kwasababu kimeandika habari hiyo

Licha ya kwamba jamaa alijitokeza kupinga hayo madai ya uzushi na mpaka anakufa alifanyiwa ibada za kikatoliki lakini Jurjan anabisha
 
Watu wanatengeneza rumors hizi kwa ma celebreties au watu wakubwa wenye ushawishi kwa lengo la kuwa convince watu waifuate imani hiyo

Na kweli kwa kiasi flani wanafanikiwa, mfano jamaa yako Jurjani anaamini kuwa Jacques Cousteau alisilimu baada ya kushuhudia bahari mbili zilizokutana bila maji kuchangamana kwa dhana ya kwamba kuran ni kitabu cha mungu kweli kwasababu kimeandika habari hiyo

Licha ya kwamba jamaa alijitokeza kupinga hayo madai ya uzushi na mpaka anakufa alifanyiwa ibada za kikatoliki lakini Jurjan anabisha
Ndio hulka ya wana dini.
 
HAYA NDIYO MAMBO TATA KUHUSU NEIL ARMSTRONG NA SAFARI YA MWEZINI


Jana nlifanikiwa kuangalia video , baada ya shirika la anga la MAREKANI, NASA kufanikisha kupeleka chombo cha utafiti katika sayari nyekundu (MARS)

Chombo hicho kilichopewa jina la Perseverance Rover ambapo kiliondoka Duniani July 2020 na kusafiri kwa miezi 7 na Chombo hicho ndicho Chombo kikubwa katika vilivyowahi kukanyaga sayari ya MARS.

View attachment 1706996

Kongole kwa NASA , kwa kufanikisha ilo tukipata jambo hilo ambalo pia linaitaji UZI wake ....baada ya kutoka kuwaangalia ndipo nikapata msukumo wa kuangalia mission nyingine tofauti tofauti za Space, ambazo baadhi ya hizo,zikanisukuma kuandika nlichoandika..ilhali kinajulikana na Wengi.


Wasalaam


Pamoja na kumbukumbu ya miaka mingi kupita na mmoja wa watu mashuhuri katika mpango wa utafutaji nafasi za wanadamu kuwa mashuhurii, inatupa kigezo cha kuchunguza tena mafumbo haya mapana kwa kadri nafasi zetu zinavyoruhusu ,baada ya kupitia historia ambayo sisi wote tunaijua leo kama Tukio Apollo 11.


Matukio ya kihistoria katika uchunguzi wa binadamu na ugunduzi wa kisayansi mara nyingi unaweza kunasa mawazo ya mwanadamu kwa namna tofauti, ya kwamba mambo kadhaa hufunikwa katika wingu la fumbo ambalo tafsiri za kushangaza hatimaye huibuka.

Safari ya mwezini ya Neil Armstrong ya Julai 1969 haikucha kuwa na mafumbo Mengi

View attachment 1706997

Tangu mchakato wa Apollo 11 na wanaanga watatu kwenda mwezini na kufanikiwa kurudi tena kwenye jamii baada ya safari yao , baada ya utulivu ikaonekana kuwa imetoa dimbwi lenye rutuba kwa kueneza hadithi nyingi juu ya jumbe tofauti za watu ,kutoka kuwa wajinga hadi kuwa wajanja wa kudadavua mambo

Kuna waliodokeza kuwa SAFARI ilitengenezwa hapa hapa duniani na NASA hawakufanikiwa kutua mwezini miaka ile
ili kuitisha Urusi na kuishtua Dunia ikatengenezwa Igizo la mission ya mwezini...kifupi yako mengi sana

Kutokana na wigo huu wacha tuchunguze Fununu zingine za kuvutia zaidi.


Je! Neil Armstrong alisilimu?



Kwanza kulikuwa na hadithi ya Neil kuwa muislamu. Muda mfupi baada ya wanaanga wa kwanza wa Safari wa mwezi kurudi Duniani ndipo hadithi ikaibuka kwamba Neil Armstrong alikuwa Mwislamu.

Kulingana na hadithi hiyo, wakati wote wakiwa angani Aldrin na Armstrong walikuwa wamesikia sauti ambayo baadaye Armstrong aligundua ilikuwa ni 'Adhana' (wito wa Waislam kwajili ya Swala). Baada ya kufika Duniani na kufanya Tour mbalimbali , miongoni mwa nchi hizo misri nayo ilikuwepo huko ndiko alikopata kusikia sauti hiyo kwa mara nyingine tena na kufuatilia zaidi kwa undani kuihusu

Uvumi huo uliendelea kuwa juu na inasemwa baada ya kujua ni nini maana ya maneno hayo, Armstrong alisilimu. Ingawa chanzo cha hadithi hii hakijulikani habari hiyo ilipatikana zaidi kwenye kurasa za magazeti huko Misri, Indonesia, na Malaysia.


Lakini vipi kulikuwa na ukweli katika hadithi hiyo??


Baadhi ya taarifa zinasema

Nanukuu

When Armstrong and company walked on the moon, they heard sounds in a strange language they did not understand. Only later, after returning to earth, did they realize that it was actually the Adhan"

Majibu ya neil ndiyo yaliyoleta utata zaidi

Armstrong was heard to remark: "I have seen a few mosques with powerful speaker systems, but wow, somebody down here certainly turned on the power on that day!’”


Haya majibu yalifunga mijadala Mingi , Sana kuwaacha watu katika mshangao zaidi aliwaza nini kujibu hivyo hakuna Ajuaye


Vyema tunaweza kupata kidokezo katika majibu ya Armstrong katika sehemu ya pili ya habari hii , Kwa kipindi cha muda mwanadamu huyu wa kwanza kukanyaga Mwezini aliwasiliana na mashirika fulani ya kidini, serikali, na watu binafsi wakimwalika kushiriki katika shughuli za Kiislamu.


Ingawa alisisitiza hamu yake ya kutomkosea mtu yeyote au kudharau dini yoyote alishauri kwamba habari za yeye kuwa muislamu hazikuwa sahihi na kwamba mtu yeyote anayeuliza maswali zaidi kuwa adabu lakini kwa uthabiti aliwaambia kwamba hakuwa na uzoefu wa kubadilika wala haikuwa kapanga kushiriki katika shughuli zozote za kidini.

Wakati Neil Armstrong alipoendelea kujikuta akipata taarifaa za uvumi wake kuenea zaidi ,katika mielekeo kama hiyo asiyoitaka, akahisi ni muhimu kuwa na mkutano wa simu na waandishi wa habari huko Cairo ambao walimsikia akisema kwamba yeye sio Mwislamu. Hadi leo wengine wanasemekana kuamini kwamba kukana kwake hadharani juu ya suala hilo kulikuwa chini ya shinikizo kali kutoka kwa serikali ya MAREKANI.

View attachment 1707000

Lakini je katika hali ya kawaida

TUNAWEZA KUSIKIA SAUTI MWEZINI??

Hapana, haiwezekani kwenye mwezi kwa mawimbi ya sauti kusafiri.


Kwa kuwa hakuna hewa kwenye mwezi, haiwezekani mawimbi ya sauti kusafiri.

Lazima utumie redio au kitu kama hicho kwa mawimbi ya sauti yaweze kwenda kwenda

HATUWEZI JUA PIA MAANA MUNGU SIO KAWAIDA LOLOTE ANAWEZA FANYA PIA

View attachment 1706999

Je! Neil Armstrong na wanaanga wa Apollo 11 waliona chombo cha anga cha sayari ya kigeni??



Kana kwamba safari ya kwanza ya kutua binadamu kwenda kwa kitu kingine cha nje katika Mfumo wa Jua haikuwa ya kufurahisha vya kutosha, habari zingine baadaye iligundulika kuwa wanaanga wa Apollo 11 walikuwa wameshuhudia UFOs zingine angani.

View attachment 1707001

Ilisemekana kwamba waliona kitu kimoja kisichojulikana kilichoruka sambamba nao na kililingana na kasi ya chombo cha angani cha Columbia, Wanaanga wale walijaribu kukizingatia wakati wa safari ya Trans-lunar, lakini kilipotea kabla ya picha yoyote kupigwa.

Ili kuthibitisha labda inawezekana ilikuwa sehemu ya roketi nyingine ambayo ilikuwa kwenye uzinduzi rocket ya Saturn V ambayo nayo ilikuwa inasapport misheni hiyo, wanaanga walituma Ujumbe kujaribu kujua umbali unaokadiriwa kati ya roketi hiyo na Chombo chao

Jibu kutoka Houston lilithibitisha kwa wanaanga kwamba baada ya kutengana nacho njiani,isingewezekana kwao kuona sehemu yoyote ya roketi hiyo ya Columbia iliyokuwa kwenye uzinduzi wakati huo.

Baada ya kuruka sambamba na chombo hicho cha kigeni angani kwa dakika chache chombo kile chenye kung'aa mwishowe kiliwapotea nyuma, na wanaanga kamaliza safari yao yote kuelekea Mwezini bila kukiona tena

View attachment 1707002

Ingawa hakuna mtu atakayeweza kusema kwa uhakika wa asilimia mia moja kile kitu kilichoongozana kwa muda mfupi na ndege ya Wanaanga kilikuwa ni nini??, wanaanga wa Apollo 11 walifikia hitimisho kwamba kitu hicho ni moja ya kontena chombo chao ambayo kasi ya kukimbia hapo awali ilikuwa imeiwezesha kwenda sawa na chombo



Swali ni Kweli Habari hizi chache zinaweza kuwa na Ukweli ndani????

Kama ni Uongo Kwanini zililetwa kwa manufaa gani???





DaVinci XV
Swali linalo niumiza kichwa ni Hio flag kupepea wakati hapo hakuna hewa wala upepo je! iliwezekana vipi kupepea?
 
Capture1.PNG
 
Anyway mambo ya dini hayajawahi kufikia kikomo cha mjadala. Na u apozungumzia imani ni ngumu sana akili kutumika kwenye majadiliano.

Waislamu wanapenda sana kutumia watu maarufu kujitangaza, ndio maana hata Loon ( Yule rapper ) alipewa airtime sana baada ya kusilimu.

Hata hapa kwetu, check ilivyotokea kwa Ben pol.
Dini yao ndivyo ilivyo bila kiki na u-al qaida haiendi mbele
 
Iyo safari ya mwezin pia ina utata mwing ikiwemo bendera kuonekana inapepea na huko hamna upepo na mengine kafhaa
 
HAKUNA KITU KINAWAUMIZA MAAMUMA KAMA MWANADAMU KUTUA KATIKA MWEZI TENA BILA KUVUA VIATU.MAAMUMA WAAAMINI MWENZI NI SEHEMU TAKATIFU.

NDIO MAANA HUWA WANAIBUKA NA CONSPIRACY THEORIES ZA AJABU AJABU
Nani kasema mwezi ni mtakatifu ,ukishindwa kutoa uthibitisho wapi imehubiriwa hii jua Wewe ni kilaza tuu
Labda unadhani kuna wanao tafuta mbadala wa Mungu Jua wa Sunday yule waMisri wa kale wakimwita Ra amabapo ni upuuzi
 
1.Neil Armstrong hakuwahi kuwa Muislamu, hivyo vyanzo vyako taarifa ni kutoka vyombo vya udaku,kwa hapa bongo ungeweza kulinganisha na magazeti ya Shigongo.
2.UFO ni Unidentified Flying Object sio vyombo vya kigeni kutoka sayari nyingine. Ni vitu ambavyo huwa vinaonekana vikizunguka karibu na sayari ya dunia lakini lakini haviwezi kutambulika au kueleweka ni nini hasa, kuongelea kuna UFO nje huko mbali na dunia haina mashiko.
shukraani mkuu
 
Nani kasema mwezi ni mtakatifu ,ukishindwa kutoa uthibitisho wapi imehubiriwa hii jua Wewe ni kilaza tuu
Labda unadhani kuna wanao tafuta mbadala wa Mungu Jua wa Sunday yule waMisri wa kale wakimwita Ra amabapo ni upuuzi
Naunga mkono hoja ...hakuna mafunzo kwenye uislam yalioupa utukufu mwezi ...mafunzo ya uislam yako perfect sana
 
Iyo safari ya mwezin pia ina utata mwing ikiwemo bendera kuonekana inapepea na huko hamna upepo na mengine kafhaa
yapo mengine mengi yamefichuliwa

Hata kwamba Neil hakuwa wa mwanzo bali warusi ndyo walianza lakini mission ilifeli
 
Unaweza kujua ni Kwanini Mohammed Ali anaonekana kuwa celebrated sana miongoni mwa waislamu ???
wale ni katika watu wachache ambao wanabadilika na kushare visa vyao

Kwa asilimia mia na umaarufu wake lazima watu wamtilie maanani

Rejelea malcom X ...akatoa na Article kabisa baada ya kusilimu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom