Ni wale wale mtoto wa nyoka ni nyoka kaka hata akijivua gamba anabaki nyoka,niliwahi kumsikia Nape wakati wa kampeni za uchaguzi wa mbunge wa Kinondoni alikuwa na Tambwe Hiza ,katika kutoa hoja sikuona tofauti yoyote kati yake na Tambwe (ambaye huongea pumba wakati wote)mi nafikiri angekuwa yule kijana wa Arusha aliyesema inabidi tufikirie kwa kutumia kichwa badala ya tumbo,kwani ni kijana jasiri ,usipokuwa jasiri CCM unakuwa sawa na wale wale wa zidumu fikra za mwenyekiti wa CCMNawasalimu wanaJF.kuna taarifa isiyokuwa rasmi kuwa Nape nnauye anaweza kuwa katibu mwenezi wa ccm,kama taarifa hizi ni za kweli basi hizi zitakuwa jitihada maalum za ccm kuhakikisha wanarudisha hadhi ya chama mbele ya vijana(kujivua gamba) kwani vijana ndio wapiga kura wajao.
Je kwa maoni yako unadhani Nape ana mvuto kwa vijana kiasi cha kubadilisha sura ya ccm kwa jamii haswa vijana?
Yaa, Nape anafaa, he is good fighter! apewe nafasi aongoze.
wadau wa jf tuwe na utamaduni wa kupongezana pale mtu anapofanya jambo jema, nadhani jk anastahili pongezi kwangu ni mara ya kwanza kuona anatimiza ahadi zake anazozitoa, hivi karibuni mwezi februari alihaidi kuwa ccm itajivua gamba ili kurudisha taswira yake na mvuto kwa jamii na hili limetimia nadhani wansatahili bravoo
bravoo jk bravoooo,
bravo kwa ccm yenyewe kwa kukubali mabadiloko, daima wamekuwa watu wenye mawazo mgando na chama kushikiliwa na misimamo ya wachache lakini kwa sasa angalau wamekubaliana na kelele za magazeti na wananchi
bravoooooo ccm bravoooo
Cha kufurahia ni nafasi ya vijana katika siasa na kizazi hiki tufike wakati tusifungwe na itikadi za vyama bali tufungwe na malengo ya vijana kulikomboa taifa popote pale walipo pasipo kujali wewe ni wa chama gani.............Nape ni miongoni mwa wanaharakati safi katika vijana cha msingi nae asije akawa limbukeni wa sifa na vyeo anavyopatakwani vijana wengi ukiwapa cheo ndio unawamaliza kabisa
wa sura au kisiasa? kama ni sura Nape hamzidi Mnyika au Lema. Kama kisiasa Nape Hamzidi Mnyika, hata yeye mwenyewe (Nape) analijua hilo.
cdm ina vijana wengi ngazi ya uongozi wenye mvuto.mfano lema,mdee,wenje,sugu,mnyika n.k. isitoshe wazee walioko cdm wana maono ya ujana,kila mtu analijua hili hata JK pia.kwa ufupi naweza kusema kuna vita ya kugombea vijana na mshindi wa vita hiyo ndio atakayeongoza nchi hii miaka ijayo.
Hapo umsesma Kiloni, Makamba yawezekana ni hopeless lakini usisahau wameshughulikia mapaka sasa the 'official leadership' lakini siyo yenye shida, yenye shida ni defactor leadership - hiyo haijaguswa na huenda haitaguswa. Mara nyingi CCM wameshakaribia sana kuigusa ile 'point of pain' lakini ghafla kigugumizi huwapata na wakaamua kuingia mitini kila mtu na lwake.
Yetu Macho!
sasa mwataka ****** ajivue nae gamba si maandiko yatatimia ya kuwa kimekosa dira na mwelekeo....saratani bado inakitafuna kujivua gamba bado hakujasaidia kitu wanahitaji x-ray ya nguvu la sivo 2015 watakiona cha moto.wasiwasi wangu MUkama ana skendo kibao,Nape ndio kabisa zero, Zakhia mhhhhhh hata uwaziri ulimshinda nashangaa hadi leo hajapanda Kisutu kwa tuhuma za ufisadi wa majengo pacha na EPA, KInana sidhani kama ana jipya.Ni sawa na kuweka kiraka kilichozeeka kwenye nguo iliozeeka...
kama kuwasemea wananchi basi sugu ameanza kufanya hivyo zamani.mashairi ya nyimbo zake yalidhihirisha hivyo.ni kweli Nape aweza kuwa na C.V nzuri kuliko sugu lakini ujiulize mbele ya mtanzania kijana wa manzese,unga Ltd na ilemela nani atauteka umati?hili ndio jambo muhimu ambalo ccm wanatakiwa kujiuliza,pia ccm wakumbuke kuwa kwa vijana shati la kijani=ufisadi.kwa maoni yangu sitta,magufuli na mwakyembe wanaweza kuvutia vijana kuliko Nape na wenzake.Mkuu mie sikubaliani na wewe yaani unamfananisha Nape na Sugu? tuzungumze ku ukweli Nape ni miongoni wa vijana wenye CV kubwa kiutawala na jina la Nape tumeanza kulisikia kabla ya hayo majina ya mengine labda jina la Sugu ndio la kitambo tena sio kwenye siasa ni kwenye bongo fleva....