Ukweli kuhusu Israel, Waarabu, na Ibrahim

Mhaya

JF-Expert Member
Aug 20, 2023
1,658
4,866
Tupeane elimu kidogo, kuna watu wanachanganya mambo. Hapa tufundishane jambo moja. Kitu cha kwanza kabisa watu wanachokichanganya ni kuhusu Ibrahim, wengi wanasema Ibrahim alikuwa Mwarabu, ndugu yangu, nikwambie tu kwamba jamaa hakuwa Mwarabu.

Ibrahim baada ya kuzaa na kijakazi ambaye alikuwa Mwarabu, inamaanisha damu yake ilichanganyika na ya Kiarabu na ndiyo maana tunasema Ishmael ni baba wa Waarabu kwa sababu mama yake alikuwa Mwarabu.

Nchi za Kiarabu ambazo zipo kwenye umoja ni hizi, Algeria, Bahrain, Iraq, Jordan, Kuwait, Djibout, Saudi Arabia, Tunisia, United Arab Emirates, Yemen, Somalia, Sudan, Syria, Comoros, Misri, Maurtania, Qatar na Palestina.

Kwa nini Waarabu wanamchukia Israel? Ni kwa sababu si Mwarabu mwenzao. Na hao ndiyo wa kizazi cha Ibrahim. Kwa hiyo kama ulikuwa unahisi Ibrahim alikuwa Mwarabu, futa hiyo akilini mwako.

Hata Iran sio Waarabu, najua wengine mtakuwa hamlijui hili kwa undani. Miongoni mwa nchi za Kiarabu, Iran hayupo kwa sababu yeye si Mwarabu.

So Israel na Waarabu ni baba mmoja ila mama tofauti. Ibrahim alizaa na Muisrael mwenzake kwa kipindi hicho ilikuwa bado haijaitwa Israel na mtoto wake kuitwa Isaka ila yule aliyezaa na kijakazi ambaye ni Mwarabu anaitwa Ishmael. Tatizo kubwa la vita baina ya Mwarabu na Israel ni hapa.

Kama Israel angekuwa Mwarabu, leo usingesikia vita vinavyoendelea huko. Na mara zote Israel anawaambiaga kwamba nchi zote za Uarabuni ni mali ya Israel na ndiyo maana kila anapokwenda kupiga, anachukua ardhi na kutanua nchi yake.

Israel walipewa nchi ndogo sana wakae baada ya kutawanywa na Adolf Hitler, baada ya kuanza kurudi, wakaitaka nchi yao, lakini kwa bahati mbaya waliwaona Waarabu washajigawia ardhi yao. Walichokifanya ni kuanza kupigana nao.

Kama unakumbuka Umoja wa Mataifa uliingilia kati, ulichukizwa na kitendo cha Israel kuwapiga Waarabu, walichokifanya, wakawapelekea Biblia ambayo kwa nyuma kuna ramani ya Israel tangu enzi za Musa. Wakawaonyesha na kuwaambia kwamba nchi zote za Uarabuni ni Israel, tutakapokuwa wengi, tutaendelea kupiga na kuirudisha nchi yetu.

So jua hili. Ibrahim hakuwa Mwarabu. Musa hakuwa Mwarabu. Suleimani mtoto wa Daudi na baba yake huyo hawakuwa Waarabu. Ni Waisrael ambao bado wanaendelea kupigana na Waarabu ili wachukue nchi yao iliyowafanya waondoke Misri.

Uzao wa Ibrahim ndiyo uliomleta Yusufu ambaye akawachukua Waisrael kwenda kuishi Misri. Maisha yalikuwa ya raha sana, watu waliionjoi maisha lakini baada ya mfalme huyo kufa, ndipo akaja mfalme mwingine ambaye sasa hakuwataka Waisrael, akawafanya watumwa wake.

Wakafanyishwa kazi. Baadaye ndipo Musa akazaliwa ndani ya ardhi ya Kiarabu. Akapewa jukumu la kuwatoa Israel kutoka hapo Misri kwenda kwao. Wakati huo ndio ambao nao Waarabu walikuwa wamejinyakulia nchi, tena walikuwa ni watu wakubwa kimuonekano.

Musa akaanza mchakato wa kuwatoa Israel Uarabuni na kuwapelekea Israel. Waliishi Misri kwa miaka 400. Wakaondoka na kwenda Misri, na walitumia miaka 40.

Musa hakuingia Israel, alikufa jangwani na Mungu kumzika. Wale waliofanikiwa kuingia huko Israel ndio walioendelea kuipambania ardhi yao mpaka leo hii.

Hapa kuna jambo moja.

Vita ya Israel na Waarabu itapamba moto hapo baadaye. Itapigwa vita kali sana. Sasa kwa kuwa Israel ataonekana kuwa kiburi na mwenye nguvu sana, dunia nzima itaanza kumcharaza. Huyu Marekani anayeonekana kuwa karibu na Israel naye atamgeuka, kila nchi duniani itamgeuka na kumpiga.

Mwisho wa siku baada ya kuona wanapigwa sana, watakimbilia mpaka kwenye mlima ule aliopaa Yesu, wataomboleza na kulia, hapo ndipo Yesu atashuka kuimaliza vita hiyo, na huo ndiyo utakuwa mwisho wa kila kitu.
 
Sijakuelewa hapo unaposema ismail ni baba wa waarabu kwa kuwa mama yake alikua mwarabu .inamaana waarabu wanafata koo zao kupitia kwa mama na si baba?? Kwanini ismael aendeleze ukoo wa waarabu wakati baba yake hakua mwarabu?? Kwanini asiendeleze ukoo wa kizazi chake cha babaake??

Sent from my Infinix X6517 using JamiiForums mobile app
 
Kwa sababu chimbuko la uislamu linaanzia kwake
 
Ndio maana akapachikwa ukoo wa kiarabu ambao haumuhusu?? Au zamani walikua wanafata koo za mama

Sent from my Infinix X6517 using JamiiForums mobile app
Ismail anachukuliwa kuwa baba waarabu kulingana na mila ya Kiislamu. Imani hii imejikita katika Quran na Hadith za Mtume Mohammad, ambazo ni maandiko ya msingi katika Uislamu.

Kwa mujibu wa vyanzo hivi, Ismail alikuwa mtoto wa kwanza wa Nabii Ibrahimu na mkewe Hajiri (Hajar). Ibrahim ni mtu muhimu katika mila za Kiislamu na Kiyahudi-Kikristo.

Katika mapokeo ya Kiislamu, inaaminika kuwa Ismail aliishi katika maeneo ya Uarabuni, hasa katika eneo ambalo lingekuwa Makka. Uzao wake uliofata unaonekana ni wa Kiarabu ambao ni mababu wa waarabu wa hivi leo, na Quran inamtaja yeye na baba yake Ibrahim kama watu muhimu katika historia ya Uislamu.

Ni muhimu kutambua kwamba imani hii kimsingi inategemea maandiko ya kidini na ni suala la imani ndani ya mapokeo ya Kiislamu. Nje ya miktadha ya kidini, dhana ya Ismail kama baba wa Waarabu inaweza isiwe na maana sawa.

Ni kama Ibrahim anavyoitwa Baba wa mataifa, wakati yeye ni myahudi na mbona kuna wachina, waafrika, wa-mexico, walatini
 
Mada zako Zina mix.

Waarabu mpaka Leo farao Wana muita firauni.

Tambua muafrika ndio aliyewatesa waarabu na wazungu.

Ndio maana hasira zao zipo kwa ajili ya waafrika tokea historia.

Waafrika mungu ndio aliwapa Kila kitu ambao ni weusi.

Ndio maana adamu ni mweusi.

Ni kianza kushusha utaleta mada za CCM.

Ukichangia maendeleo sio mwana siasa ila ukiuliza maendeleo ni mwana siasa tena mpinzani
 
Lazima kwanza ujiulize,Israel ni nani? Israel ni Yakobo na si Ibrahim wala mwanae Isaka. Unaposema Ibrahim hakuwa Mwarabu,umejiuliza asili yake? Jibu ni kwamba Ibrahim alitoka Uru ya Wakaldayo ambayo baadaye ikaitwa Iraq.Je,Iraq ni Waarabu au siyo Waarabu? Yote Kwa yote hawa watu wote si ndugu zangu wala Nini ila wote sisi tunamuabudu Mungu.
 
Bado haupo sahihi kwasababu mjakazi ambaye Ibrahim alizaa nae alikuwa Mmisri na wamisri wa nyakati hizo walikuwa ni weusi kwahiyo hawakuwa Waarabu Historia hii tuliyo nayo imepikwa kuficha jambo.
Wazungu walikaa wee,wakatengeneza nadharia za kututawala.Dini za kiyahudi,kikristo na kiislamu zilitengenezwa Kwa mpango maalumu.Zitaendelea kuwa pigo mujarabu kwetu sisi na tunaofanana nao.Wenye dini zao sasa hivi hawana mpango nazo hadi wameamua kufirana na upumbavu mwingine.Ukienda Israel ,USA,Uk Dubai nk. Mashoga wamejaa hadi wanapata vyeo vya juu serikali na wanaheshimika.Huku kwetu tunajikita kuabudu dini zisizo zetu.Pumbaf thana Afrika.
 
Ismail anachukuliwa kuwa baba waarabu kulingana na mila ya Kiislamu. Imani hii imejikita katika Quran na Hadith za Mtume Mohammad, ambazo ni maandiko ya msingi katika Uislamu.

Kwa mujibu wa vyanzo hivi, Ismail alikuwa mtoto wa kwanza wa Nabii Ibrahimu na mkewe Hajiri (Hajar). Ibrahim ni mtu muhimu katika mila za Kiislamu na Kiyahudi-Kikristo.

Katika mapokeo ya Kiislamu, inaaminika kuwa Ismail aliishi katika maeneo ya Uarabuni, hasa katika eneo ambalo lingekuwa Makka. Uzao wake uliofata unaonekana ni wa Kiarabu ambao ni mababu wa waarabu wa hivi leo, na Quran inamtaja yeye na baba yake Ibrahim kama watu muhimu katika historia ya Uislamu.

Ni muhimu kutambua kwamba imani hii kimsingi inategemea maandiko ya kidini na ni suala la imani ndani ya mapokeo ya Kiislamu. Nje ya miktadha ya kidini, dhana ya Ismail kama baba wa Waarabu inaweza isiwe na maana sawa.

Ni kama Ibrahim anavyoitwa Baba wa mataifa, wakati yeye ni myahudi na mbona kuna wachina, waafrika, wa-mexico, walatini
Kwa mantiki hiyo ismail hakuwa mwarabu kwa maana babaake sio mwarabu lakini waarabu waliamua kumpachika uarabu ili awe baba wa waarabu.ok
 
Back
Top Bottom