Mambo Kumi yalomshinda Rais Magufuli

Mambo Kumi yalomshinda Rais Magufuli

Kama hata hatujui hao wanaojiita 'watumishi' wetu tunawalipa kiasi gani seuze mali zao?
Mishahara ya watumishi wa umma bado ina tofauti kubwa kabisa hadi kupelekea wengine wenye sifa za kufanana kulipwa milioni 35 kwa mwezi na wengine laki 8. Nalo hilo ni jipu litumbuliwe nchi hii ni yetu wote!
 
Zitto kaongea Madini hapo, bila JPM kuyatatua hayo tutakuwa tunatwanga maji kwenye kinu!
 
Bado mapema sana, huwezikurupuka kwa kila kitu nchi ilishauzwa ck mingi kuirudisha ktk mstar kwa ck mia cio raic kivile
Mapema ni lini? na kukurupuka ni kufanyaje? Kutuma Waziri mkuu kufunga koki za mafuta sio mapema? Kuanza kupitia upya mikataba ya mafuta, madini na gesi ndio mapema?! Kumkataza Nape na wizara yake isiyo na tija kwa taifa asitumie VX V8 napo unasema ni mapema?
 
Siku 2 kujadili mikataba? Hauko serious! Mikataba sio page mbili, ni kitabu na unatakiwa kupitia neno moja baada ya lingine na kuelewa lina maana gani. Hata siku 100 hazitoshi, labda aamue kujilipua na kuivunja kwa mabavu ila sheria za kimataifa zitatushika endapo atafanya hicyo!
Rudi tena unisome, tatizo lako umekurupuka sana, nimesema hata siku ya pili baada ya kuapishwa kwake angeanza kupitia mikataba......nani kasema mikataba ina page 2?
 
Hivi kweli siku 100 unaweza kutengeneza mfumo kutengeneza sukari na nchi ikaacha kuagiza toka nje!? Kweli nyani haoni kundule, yeye miaka kumi ya kuwatumikia watu wa Kigoma kaskazini kawaacha maskini akakimbilia Kigoma mjini huku kaskazini akimuachia Serukamba na shida ziko pale pale. Leo anamnyooshe kidole kiongozi ambaye hata bajeti ya kwake mwenyewe haja implement. Zitto na laghai mkubwa
 
Zitto Z Kabwe na MAMBO KUMI YALO MSHINDA MAGUFULI.

Siku 100 za Utawala wa Awamu ya 5 chini ya Rais Magufuli

Mambo 10 ya Msingi ambayo Rais Magufuli ameshindwa kuyafanya tangu aingie madarakani.

1 Mikataba yote ya Rasilimali za Nchi - PSAs Kwa Mafuta na Gesi Asilia na MDAs Kwa Madini bado ni Siri na sio Rais au Makamu wa Rais au Waziri Mkuu ambaye kaonyesha hata nia ya kutazama upya mikataba hii na kuiboresha Kwa maslahi ya watanzania. Mapato ya Nchi, makubwa kuliko ya utumbuaji majipu, yanaendelea kupotea. Mkataba wa IPTL bado unaendelea kunyonya Nchi na Serikali inatazama tshs 8 bilioni zinalipwa Kwa matapeli wa IPTL na PAP kila mwezi. Katika siku 100 tangu Rais Magufuli aingie madarakani, jumla ya tshs 30 bilioni zimeshalipwa Kwa IPTL/PAP ambazo zingeweza kununua CT scan Kwa hospitali zote za mikoa nchini. Fedha hii ni zaidi ya mkopo ambao Serikali imechukua kutoka Benki ya Dunia ili kujenga ' fly over ' ya Ubungo jijini Dar Es Salaam.CCM Hawana SERA ya UWAZI na haipo kwenye ILANI YAO na HAIKUAHIDIWA popote na kiongozi wa CCM kwenye uchaguzi kwa njia za kidemokrasia kabisa wakaaminiwa wakachaguliwa.Kwanini wewe unajihisihisi kwamba mikataba hiyo ina mapungufu?????????????????????

2) Posho za makalio katika mfumo mzima wa Serikali bado zinalipwa bila kufutwa kama Mpango wa Maendeleo 2011/2012 - 2015/2016 unavyotaka na kuagiza. Serikali imeongeza posho za kujikimu mpaka tshs 120,000 Kwa siku na Kwa wabunge bado wanalipwa posho ya makalio ya tshs 220,000 Kwa siku. Posho ambazo zimeshalipwa tangu Rais aingie madarakani ni sawa na kujenga barabara zote viporo za lami kuunganisha mkoa wa Tabora ( Kaliua - Urambo na Nyahua - Itigi ).Mnataka aingilie tena mseme BUNGE ni MHIMILI HURU NA hauingiliwi na serikali na muda huohuo mnataka aingilie kati tena????????????????

3) Serikali bado inatumia mashangingi na kila Waziri, Katibu Mkuu na wakuu wa idara wanatumia mashangingi ya gharama kubwa.

4) Tanzania bado inaagiza Sukari kutoka Nje na Serikali haina Mpango wowote ule wa kuondoa tatizo hilo. Hata katika Mpango wa Maendeleo Serikali haisemei sukari kabisa. Uagizaji wa Sukari ni jipu ambalo limeiva Lakini mkamuaji analilea. Hivyo hivyo Kwa sekta ya Nguo bado viwanda vya ndani vinapata ushindani usio halali kutoka Kwa nguo kutoka Nje zenye kuingia nchini bila kodi.Ulitaka iache ghafla ndani ya hizi siku 100?

5 Taarifa ya Serikali kuhusu utoroshaji wa fedha Nje bado imefichwa na haijafikishwa bungeni. Hakuna hatua zozote zilizochukuliwa kudhibiti utoroshaji fedha na hakuna mashtaka yaliyofunguliwa Kwa wahusika.

7 TAKUKURU bado haina mamlaka ya kukamata na kushtaki wenye makosa ya kifisadi. Vile vile mfumo wa kila mwenye Mali athibitishe yeye kaipataje ( reverse burden of proof ) haujaanzishwa nchini na matokeo yake ni kuzorota Kwa juhudi za kumaliza ufisadi Kwa kuboresha mifumo. Kinachoendelea ni kutumbua majipu kimkakati bila kuzuia majipu kuota tena.

8 Mali na Madeni ya Viongozi bado ni Siri. Wananchi hawajui Rais Wao anamiliki nini AMA anadaiwa nini. Hivyo hivyo Kwa viongozi waandamizi wote. Serikali ya Awamu ya Tano imeendeleza mfumo ule ule wa maadili ulio dhaifu na wenye kulea vitendo vya rushwa.

9 Serikali ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania imeshindwa kabisa kushughulikia suala la Zanzibar na matokeo yake ni kuiweka Nchi kwenye hatari kubwa ya kuvunjika Amani. Mshindi wa Uchaguzi Zanzibar hajatangazwa na Rais ametishia wananchi kuwa atatumia majeshi kukandamiza madai halali ya wananchi wa Zanzibar.

10 Hakuna hatua zozote zimechukuliwa kuanza mchakato wa Katiba. Inaonyesha Serikali haina mpango kabisa na Katiba mpya.
Tutajie na wew ndani ya hizi siku 100 umefanya nini????????
 
Tatizo la Zitto anataka priority zake ziwe za Magufuli, anataka Magufuli akurupuke kama yeye. Hatuendi hivyo, raisi bado anaunda timu, hajafikia hata kuteua wakuu wa mikoa na wilaya.
Huyu Zitto alijua kuwa mafuta yanapigwa bypass bandarini miaka mingi akaishia kwenye kabrasha tu za kamati ya PAC hakuwahi kuwasilisha hoja binafsi, leo hii anataka Magufuli alime miwa, avune, atengeneze sukari ndani ya siku mia moja. Insanity
 
Unafurahi tunavyoagiza Sukari toka nje?? Tuna miwa inaoza huko Kilombero. Inahitaji miaka mingapi kufanya substution effect kwenye importation ya sukari? Mbona leo ana sign mkataba wa flyovers utakaoisha baada ya miaka 4? Usiwe mjinga wewe
Kwa akili yako hata kama angefanya hiyo substitution ya sukari ungelalamika mbona mchele au unga mbona haujashuka bei.Hizo unazosema ni priority zako ungekuwa Raisi ungeanza nazo ,JPM ana priority zake na ameanza uzifanyia kazi cha msingi ni kuijenga Tanzania mpya
 
Tutajie na wew ndani ya hizi siku 100 umefanya nini????????
(Dotto sio mtawala,,hakupewa siku 100,,aliepewa ni raisi Jpm,,na siku 100 ndio znaweza Pima utendaji na utekelezaji wa aliyoyaahidi,,sasa alieahidi ni jpm na si mwananchi wa kawaida,,hivyo mwananchi wa kawaida anavyojaribu kuhoji si kosa,,asante
 
Maslahi ya nchi kwanza, ilani baadae. Mbona mlinyimwa Kadhi na kwenye ilani alikuwepo?

Kwani yaliyomo kwenye ilani yanahusu maslahi ya nani?

Huwezi kusema rais kashindwa kufanya hivi ama vile ilhali unajua hivyo vitu hakuviahidi kuvifanya.

BTW:Case ya kusingiziwa hujatimiza kitu ambacho hukuahidi wala haishabihiani na hiyo ya kutokutizimiza ulichoahidi.
 
Nadhani Magufuli anasuburi kwanza kuandaa miswaada ya kuwakabili mafisadi. Bunge likishapitisha miswaada hiyo kisha kuwa sheria, ndipo Muheshimiwa raisi atapata legal base ya kuanzisha mahakama ya mafisadi. Ligi itaanzia hapo. Sidhani kwamba ZITO atakuwa na cha kusema!

Zitto Z Kabwe na MAMBO KUMI YALO MSHINDA MAGUFULI.

Siku 100 za Utawala wa Awamu ya 5 chini ya Rais Magufuli

Mambo 10 ya Msingi ambayo Rais Magufuli ameshindwa kuyafanya tangu aingie madarakani.

1 Mikataba yote ya Rasilimali za Nchi - PSAs Kwa Mafuta na Gesi Asilia na MDAs Kwa Madini bado ni Siri na sio Rais au Makamu wa Rais au Waziri Mkuu ambaye kaonyesha hata nia ya kutazama upya mikataba hii na kuiboresha Kwa maslahi ya watanzania. Mapato ya Nchi, makubwa kuliko ya utumbuaji majipu, yanaendelea kupotea. Mkataba wa IPTL bado unaendelea kunyonya Nchi na Serikali inatazama tshs 8 bilioni zinalipwa Kwa matapeli wa IPTL na PAP kila mwezi. Katika siku 100 tangu Rais Magufuli aingie madarakani, jumla ya tshs 30 bilioni zimeshalipwa Kwa IPTL/PAP ambazo zingeweza kununua CT scan Kwa hospitali zote za mikoa nchini. Fedha hii ni zaidi ya mkopo ambao Serikali imechukua kutoka Benki ya Dunia ili kujenga ' fly over ' ya Ubungo jijini Dar Es Salaam.

2) Posho za makalio katika mfumo mzima wa Serikali bado zinalipwa bila kufutwa kama Mpango wa Maendeleo 2011/2012 - 2015/2016 unavyotaka na kuagiza. Serikali imeongeza posho za kujikimu mpaka tshs 120,000 Kwa siku na Kwa wabunge bado wanalipwa posho ya makalio ya tshs 220,000 Kwa siku. Posho ambazo zimeshalipwa tangu Rais aingie madarakani ni sawa na kujenga barabara zote viporo za lami kuunganisha mkoa wa Tabora ( Kaliua - Urambo na Nyahua - Itigi ).

3) Serikali bado inatumia mashangingi na kila Waziri, Katibu Mkuu na wakuu wa idara wanatumia mashangingi ya gharama kubwa.

4) Tanzania bado inaagiza Sukari kutoka Nje na Serikali haina Mpango wowote ule wa kuondoa tatizo hilo. Hata katika Mpango wa Maendeleo Serikali haisemei sukari kabisa. Uagizaji wa Sukari ni jipu ambalo limeiva Lakini mkamuaji analilea. Hivyo hivyo Kwa sekta ya Nguo bado viwanda vya ndani vinapata ushindani usio halali kutoka Kwa nguo kutoka Nje zenye kuingia nchini bila kodi.

5 Taarifa ya Serikali kuhusu utoroshaji wa fedha Nje bado imefichwa na haijafikishwa bungeni. Hakuna hatua zozote zilizochukuliwa kudhibiti utoroshaji fedha na hakuna mashtaka yaliyofunguliwa Kwa wahusika.

7 TAKUKURU bado haina mamlaka ya kukamata na kushtaki wenye makosa ya kifisadi. Vile vile mfumo wa kila mwenye Mali athibitishe yeye kaipataje ( reverse burden of proof ) haujaanzishwa nchini na matokeo yake ni kuzorota Kwa juhudi za kumaliza ufisadi Kwa kuboresha mifumo. Kinachoendelea ni kutumbua majipu kimkakati bila kuzuia majipu kuota tena.

8 Mali na Madeni ya Viongozi bado ni Siri. Wananchi hawajui Rais Wao anamiliki nini AMA anadaiwa nini. Hivyo hivyo Kwa viongozi waandamizi wote. Serikali ya Awamu ya Tano imeendeleza mfumo ule ule wa maadili ulio dhaifu na wenye kulea vitendo vya rushwa.

9 Serikali ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania imeshindwa kabisa kushughulikia suala la Zanzibar na matokeo yake ni kuiweka Nchi kwenye hatari kubwa ya kuvunjika Amani. Mshindi wa Uchaguzi Zanzibar hajatangazwa na Rais ametishia wananchi kuwa atatumia majeshi kukandamiza madai halali ya wananchi wa Zanzibar.

10 Hakuna hatua zozote zimechukuliwa kuanza mchakato wa Katiba. Inaonyesha Serikali haina mpango kabisa na Katiba mpya.
 
Zitto Z Kabwe na MAMBO KUMI YALO MSHINDA MAGUFULI.

Siku 100 za Utawala wa Awamu ya 5 chini ya Rais Magufuli

Mambo 10 ya Msingi ambayo Rais Magufuli ameshindwa kuyafanya tangu aingie madarakani.

1 Mikataba yote ya Rasilimali za Nchi - PSAs Kwa Mafuta na Gesi Asilia na MDAs Kwa Madini bado ni Siri na sio Rais au Makamu wa Rais au Waziri Mkuu ambaye kaonyesha hata nia ya kutazama upya mikataba hii na kuiboresha Kwa maslahi ya watanzania. Mapato ya Nchi, makubwa kuliko ya utumbuaji majipu, yanaendelea kupotea. Mkataba wa IPTL bado unaendelea kunyonya Nchi na Serikali inatazama tshs 8 bilioni zinalipwa Kwa matapeli wa IPTL na PAP kila mwezi. Katika siku 100 tangu Rais Magufuli aingie madarakani, jumla ya tshs 30 bilioni zimeshalipwa Kwa IPTL/PAP ambazo zingeweza kununua CT scan Kwa hospitali zote za mikoa nchini. Fedha hii ni zaidi ya mkopo ambao Serikali imechukua kutoka Benki ya Dunia ili kujenga ' fly over ' ya Ubungo jijini Dar Es Salaam.

2) Posho za makalio katika mfumo mzima wa Serikali bado zinalipwa bila kufutwa kama Mpango wa Maendeleo 2011/2012 - 2015/2016 unavyotaka na kuagiza. Serikali imeongeza posho za kujikimu mpaka tshs 120,000 Kwa siku na Kwa wabunge bado wanalipwa posho ya makalio ya tshs 220,000 Kwa siku. Posho ambazo zimeshalipwa tangu Rais aingie madarakani ni sawa na kujenga barabara zote viporo za lami kuunganisha mkoa wa Tabora ( Kaliua - Urambo na Nyahua - Itigi ).

3) Serikali bado inatumia mashangingi na kila Waziri, Katibu Mkuu na wakuu wa idara wanatumia mashangingi ya gharama kubwa.

4) Tanzania bado inaagiza Sukari kutoka Nje na Serikali haina Mpango wowote ule wa kuondoa tatizo hilo. Hata katika Mpango wa Maendeleo Serikali haisemei sukari kabisa. Uagizaji wa Sukari ni jipu ambalo limeiva Lakini mkamuaji analilea. Hivyo hivyo Kwa sekta ya Nguo bado viwanda vya ndani vinapata ushindani usio halali kutoka Kwa nguo kutoka Nje zenye kuingia nchini bila kodi.

5 Taarifa ya Serikali kuhusu utoroshaji wa fedha Nje bado imefichwa na haijafikishwa bungeni. Hakuna hatua zozote zilizochukuliwa kudhibiti utoroshaji fedha na hakuna mashtaka yaliyofunguliwa Kwa wahusika.

7 TAKUKURU bado haina mamlaka ya kukamata na kushtaki wenye makosa ya kifisadi. Vile vile mfumo wa kila mwenye Mali athibitishe yeye kaipataje ( reverse burden of proof ) haujaanzishwa nchini na matokeo yake ni kuzorota Kwa juhudi za kumaliza ufisadi Kwa kuboresha mifumo. Kinachoendelea ni kutumbua majipu kimkakati bila kuzuia majipu kuota tena.

8 Mali na Madeni ya Viongozi bado ni Siri. Wananchi hawajui Rais Wao anamiliki nini AMA anadaiwa nini. Hivyo hivyo Kwa viongozi waandamizi wote. Serikali ya Awamu ya Tano imeendeleza mfumo ule ule wa maadili ulio dhaifu na wenye kulea vitendo vya rushwa.

9 Serikali ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania imeshindwa kabisa kushughulikia suala la Zanzibar na matokeo yake ni kuiweka Nchi kwenye hatari kubwa ya kuvunjika Amani. Mshindi wa Uchaguzi Zanzibar hajatangazwa na Rais ametishia wananchi kuwa atatumia majeshi kukandamiza madai halali ya wananchi wa Zanzibar.

10 Hakuna hatua zozote zimechukuliwa kuanza mchakato wa Katiba. Inaonyesha Serikali haina mpango kabisa na Katiba mpya.
Huyu jamaa huwa anaonaga kwa jicho la tatu. Namuelewa sana zitto
 
"Kashindwa kabisa" Really????
Mi nasema hajagusa huko kiasi cha kwenda public.
Natumaini ataingia huko panapo Muda mwafaka
Na wakati utakapofika Zitto atasema nilisemam mimi, sio mbaya! Thanks for the reminder, itz only about time!!

Kwani akisema "nilisema mimi" we inakuuma nini? Ulitegemea mbowe form six failure aongee hayo?
 
Back
Top Bottom