Mambo Kumi yalomshinda Rais Magufuli

Mambo Kumi yalomshinda Rais Magufuli

Na Zitto alitaka hayo yote kumi yawe yamefanyika ndani ya siku 100?!

Talking is cheap, yeye Zitto amekuwa anapiga danadana ya kutaja majina ya watu walioweka fedha Swiss kwa muda gani?

...You missed the point dude!!

....Sio swala la hayo kufanyika ndani ya siku 100!!

....Ni at least kuweka misingi ya kukabiliana na hayo.

....Mlivyo wa ajabu watu wengine, utaniambia kuwa misingi ndiyo hiyo ya ziara za kushitukiza ktk ofisi na taasisi za umma mbalimbali kisha kusimamisha au kufukuza watu kazi ovyo ovyo kinyume cha sheria!!

.....Sisi wengine tulishakataa na tunasema kwa herufi kubwa kabisa HAPANA mara milioni moja, na tunasema huu ni usanii na unafiki wa kiwango cha juu kabisa kuliko hata wa Mkwere JK!!

....Kiukweli hatudanganyiki ng'o kwani kinachofanyika sasa ni majukumu ya kawaida yanayopaswa kufanyika siku kwa siku

.....Tulitengemea hadi sasa awe ameanza kuweka misingi ya mabadiliko ya kisheria na kimfumo.

...Hatutakuwa sustainable kama taifa kama tunategemea fikra, maagizo na makaripio ya mtu mmoja anayeitwa Magufuli kuwa yatatubeba tunakotaka kwenda!!

....Thanx to Zito Ruyagwa Kabwe kwani kaliweka hili katika lugha rahisi sana kueleweka, kwamba, kinachofanyika kwa lugha ya kwao ni utumbuaji majipu ya kimkakati ya kisiasa ambayo obviousily sio sustainable na itafika time wataishiwa mahali pa kutumbua, wanarudi kwenye bussiness as usual......si CCM ni ile ile bwana, au hii ni nyingine mkuu?

....Angeeleweka sana anakoelekea huyu bwana JPM kama ktk siku zake 100 in the office, angeshatumia mikutano miwili vya bunge iliyopita kupeleka miswaada kabambe hata miwili au mitatu ingalau inayoshadidia mageuzi makubwa ya kisiasa na kiuchumi anayotaka kuyafanya ili kutengeneza ROAD MAP na misingi ya kubadilisha au kuondoa kabisa mifumo iliyotengeneza matatizo na majipu haya na pengine hata sisi tungeanza kuiona nuru ya "Tanzania mpya ya Magufuli".

....Badala yake, katika hali na mazingira ya kushangaza na kujikanganya (contradictory circumstances) na falsafa yake ya KUTUMBUA MAJIBU na HAPA KAZI TU, tunaona analitumia bunge kama muhuri wa kupitishia maamuzi ya hovyo ya serikali yake ya kuzuia kituo cha television cha umma (TBC) kurusha matangazo ya moja kwa moja ya vikao vya bunge kwa kisingizio cha gharama na pia kufungia vyombo vya habari (gazeti la Mawio) kwa kutumia sheria za hovyo za kikoloni!!

...Huyu mtu ndiye tumwamini kuwa ana NIA na DHAMIRA ya kweli ya kupambana na uozo wa nchi hii uliotengenezwa na kulelewa na wao wenyewe ambao kiuhalisia wao wenyewe haohao miongoni mwao ndiyo MAJIPU???

....Aisee tutasubiri sana, maana bado MASIHA wa kweli wa kuitengeneza nchi hii hajaja na sembuse awe Magufuli huyu wa CCM hii hii!!??

...No sooner or later watu wataanza kulitambua tu hili
 
Zitto Z Kabwe na MAMBO KUMI YALO MSHINDA MAGUFULI.

Siku 100 za Utawala wa Awamu ya 5 chini ya Rais Magufuli

Mambo 10 ya Msingi ambayo Rais Magufuli ameshindwa kuyafanya tangu aingie madarakani.

1 Mikataba yote ya Rasilimali za Nchi - PSAs Kwa Mafuta na Gesi Asilia na MDAs Kwa Madini bado ni Siri na sio Rais au Makamu wa Rais au Waziri Mkuu ambaye kaonyesha hata nia ya kutazama upya mikataba hii na kuiboresha Kwa maslahi ya watanzania. Mapato ya Nchi, makubwa kuliko ya utumbuaji majipu, yanaendelea kupotea. Mkataba wa IPTL bado unaendelea kunyonya Nchi na Serikali inatazama tshs 8 bilioni zinalipwa Kwa matapeli wa IPTL na PAP kila mwezi. Katika siku 100 tangu Rais Magufuli aingie madarakani, jumla ya tshs 30 bilioni zimeshalipwa Kwa IPTL/PAP ambazo zingeweza kununua CT scan Kwa hospitali zote za mikoa nchini. Fedha hii ni zaidi ya mkopo ambao Serikali imechukua kutoka Benki ya Dunia ili kujenga ' fly over ' ya Ubungo jijini Dar Es Salaam.

2) Posho za makalio katika mfumo mzima wa Serikali bado zinalipwa bila kufutwa kama Mpango wa Maendeleo 2011/2012 - 2015/2016 unavyotaka na kuagiza. Serikali imeongeza posho za kujikimu mpaka tshs 120,000 Kwa siku na Kwa wabunge bado wanalipwa posho ya makalio ya tshs 220,000 Kwa siku. Posho ambazo zimeshalipwa tangu Rais aingie madarakani ni sawa na kujenga barabara zote viporo za lami kuunganisha mkoa wa Tabora ( Kaliua - Urambo na Nyahua - Itigi ).

3) Serikali bado inatumia mashangingi na kila Waziri, Katibu Mkuu na wakuu wa idara wanatumia mashangingi ya gharama kubwa.

4) Tanzania bado inaagiza Sukari kutoka Nje na Serikali haina Mpango wowote ule wa kuondoa tatizo hilo. Hata katika Mpango wa Maendeleo Serikali haisemei sukari kabisa. Uagizaji wa Sukari ni jipu ambalo limeiva Lakini mkamuaji analilea. Hivyo hivyo Kwa sekta ya Nguo bado viwanda vya ndani vinapata ushindani usio halali kutoka Kwa nguo kutoka Nje zenye kuingia nchini bila kodi.

5 Taarifa ya Serikali kuhusu utoroshaji wa fedha Nje bado imefichwa na haijafikishwa bungeni. Hakuna hatua zozote zilizochukuliwa kudhibiti utoroshaji fedha na hakuna mashtaka yaliyofunguliwa Kwa wahusika.

7 TAKUKURU bado haina mamlaka ya kukamata na kushtaki wenye makosa ya kifisadi. Vile vile mfumo wa kila mwenye Mali athibitishe yeye kaipataje ( reverse burden of proof ) haujaanzishwa nchini na matokeo yake ni kuzorota Kwa juhudi za kumaliza ufisadi Kwa kuboresha mifumo. Kinachoendelea ni kutumbua majipu kimkakati bila kuzuia majipu kuota tena.

8 Mali na Madeni ya Viongozi bado ni Siri. Wananchi hawajui Rais Wao anamiliki nini AMA anadaiwa nini. Hivyo hivyo Kwa viongozi waandamizi wote. Serikali ya Awamu ya Tano imeendeleza mfumo ule ule wa maadili ulio dhaifu na wenye kulea vitendo vya rushwa.

9 Serikali ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania imeshindwa kabisa kushughulikia suala la Zanzibar na matokeo yake ni kuiweka Nchi kwenye hatari kubwa ya kuvunjika Amani. Mshindi wa Uchaguzi Zanzibar hajatangazwa na Rais ametishia wananchi kuwa atatumia majeshi kukandamiza madai halali ya wananchi wa Zanzibar.

10 Hakuna hatua zozote zimechukuliwa kuanza mchakato wa Katiba. Inaonyesha Serikali haina mpango kabisa na Katiba mpya.

Here is what President Magufuli did after just three months as president of Tanzania:

1. Soon after his election, Magufuli declared there would be no celebration of Independence Day on 9 December because it would be shameful to spend huge sums of money on the celebrations when people were dying of cholera. Instead, the day has been set as a national day of cleanliness and the money will go toward street¬cleaning services. He has said everybody should pick up their tools and clean their backyards.

2. After his first official visit to the Muhimbili Hospital, and seeing the horrible state it was in, he ordered over 200 million shillings marked for parliament parties be used to pay for beds for people lying on the floor and sharing beds.

A few days later 300 beds were delivered. He dismissed the governing board and got a new team in place, and within days the broken MRI was fixed. He also pared down his inauguration party from $100,000 to $7,000 and sent the extra money to the hospital.

3. Three days into his term, Magufuli announced a ban on all foreign travel by government officials. They have been instructed to instead make regular visits to rural areas to learn and help solve problems facing everyday Tanzanians. All tasks that required officials to travel abroad would instead be done by High Commissioners and Ambassadors who are already in place.

4. He has restricted all first and business class travel to government officials, except the President, Vice President and Prime Minister.

5. There will be no more workshops and seminars in expensive hotels when there are so many ministry board rooms available.

6. He suspended the Tanzania Revenue Authority’s chief and other officials pending investigations after a visit by Prime Minister Kassim Majaliwa to the port of Dar es Salaam found 350 containers listed in its books were missing.

7. When he had to travel 600km to Dodoma, from Dar, to officially open parliament last week, he didn’t order a private jet; instead, he chose to drive.

8. At the National Assembly in Dodoma last week he clearly sent out the message that it will not be business as usual under his leadership.

9. He promised to cut public spending, fight corruption and enhance accountability in public service. He said it is time for Tanzanians to walk the talk.

10. Magufuli reportedly told parliamentary leaders that the people of Tanzania want him to solve their problems and not make speeches.
Source: New Tanzania President stuns social media activists
 
Rudi tena unisome, tatizo lako umekurupuka sana, nimesema hata siku ya pili baada ya kuapishwa kwake angeanza kupitia mikataba......nani kasema mikataba ina page 2?

Msome tena Zitto. Kwani kuanza review ya mikataba ya gesi kunahitaji nguvu ipi inayomshinda Magufuli? Kwani ni dhambi kuanza review ya mikataba ya Madini na gesi hata ndani ya siku 2 baada ya kuapishwa? Kupitia upya mikataba hiyo kunamzuia nini kuendelea kutumbua majipu?
Bavicha bhana, sasa hujanielewa nini hapo kwenye page 2 au mkataba ni kama 'kitabu'?
Zitto kaamua tu kuwa mpinzani hapo ila akili hapo kaiacha kigoma kijijini.
 
Wene ni Mjinga,mikataba ya gesi ilipitishwa bungeni ndani ya siku ngapi?.

Wapinzani siwalidai siku hazitoshi lakini nyie mkasema ni nyingi?.

Iweje leo kwa Magufuli uzione siku 100 ni chache?.
 
JAMII -ASM;

Hakuna anayekataa kuwa hajachukua hatua hizo, na basically ni hatua na maamuzi mazuri tu!

My simple questions to you are these;

1. Are those measures and decisions sustainable?

2. What will happen if Magufuli goes today?

3. Is it guaranteed that no one else will come up with his/her own other decisions as the way he/she sees things by him/herself?

I hope you have got my point......
 
Zitto Z Kabwe na MAMBO KUMI YALO MSHINDA MAGUFULI.

Siku 100 za Utawala wa Awamu ya 5 chini ya Rais Magufuli

Mambo 10 ya Msingi ambayo Rais Magufuli ameshindwa kuyafanya tangu aingie madarakani.

1 Mikataba yote ya Rasilimali za Nchi - PSAs Kwa Mafuta na Gesi Asilia na MDAs Kwa Madini bado ni Siri na sio Rais au Makamu wa Rais au Waziri Mkuu ambaye kaonyesha hata nia ya kutazama upya mikataba hii na kuiboresha Kwa maslahi ya watanzania. Mapato ya Nchi, makubwa kuliko ya utumbuaji majipu, yanaendelea kupotea. Mkataba wa IPTL bado unaendelea kunyonya Nchi na Serikali inatazama tshs 8 bilioni zinalipwa Kwa matapeli wa IPTL na PAP kila mwezi. Katika siku 100 tangu Rais Magufuli aingie madarakani, jumla ya tshs 30 bilioni zimeshalipwa Kwa IPTL/PAP ambazo zingeweza kununua CT scan Kwa hospitali zote za mikoa nchini. Fedha hii ni zaidi ya mkopo ambao Serikali imechukua kutoka Benki ya Dunia ili kujenga ' fly over ' ya Ubungo jijini Dar Es Salaam.

2) Posho za makalio katika mfumo mzima wa Serikali bado zinalipwa bila kufutwa kama Mpango wa Maendeleo 2011/2012 - 2015/2016 unavyotaka na kuagiza. Serikali imeongeza posho za kujikimu mpaka tshs 120,000 Kwa siku na Kwa wabunge bado wanalipwa posho ya makalio ya tshs 220,000 Kwa siku. Posho ambazo zimeshalipwa tangu Rais aingie madarakani ni sawa na kujenga barabara zote viporo za lami kuunganisha mkoa wa Tabora ( Kaliua - Urambo na Nyahua - Itigi ).

3) Serikali bado inatumia mashangingi na kila Waziri, Katibu Mkuu na wakuu wa idara wanatumia mashangingi ya gharama kubwa.

4) Tanzania bado inaagiza Sukari kutoka Nje na Serikali haina Mpango wowote ule wa kuondoa tatizo hilo. Hata katika Mpango wa Maendeleo Serikali haisemei sukari kabisa. Uagizaji wa Sukari ni jipu ambalo limeiva Lakini mkamuaji analilea. Hivyo hivyo Kwa sekta ya Nguo bado viwanda vya ndani vinapata ushindani usio halali kutoka Kwa nguo kutoka Nje zenye kuingia nchini bila kodi.

5 Taarifa ya Serikali kuhusu utoroshaji wa fedha Nje bado imefichwa na haijafikishwa bungeni. Hakuna hatua zozote zilizochukuliwa kudhibiti utoroshaji fedha na hakuna mashtaka yaliyofunguliwa Kwa wahusika.

7 TAKUKURU bado haina mamlaka ya kukamata na kushtaki wenye makosa ya kifisadi. Vile vile mfumo wa kila mwenye Mali athibitishe yeye kaipataje ( reverse burden of proof ) haujaanzishwa nchini na matokeo yake ni kuzorota Kwa juhudi za kumaliza ufisadi Kwa kuboresha mifumo. Kinachoendelea ni kutumbua majipu kimkakati bila kuzuia majipu kuota tena.

8 Mali na Madeni ya Viongozi bado ni Siri. Wananchi hawajui Rais Wao anamiliki nini AMA anadaiwa nini. Hivyo hivyo Kwa viongozi waandamizi wote. Serikali ya Awamu ya Tano imeendeleza mfumo ule ule wa maadili ulio dhaifu na wenye kulea vitendo vya rushwa.

9 Serikali ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania imeshindwa kabisa kushughulikia suala la Zanzibar na matokeo yake ni kuiweka Nchi kwenye hatari kubwa ya kuvunjika Amani. Mshindi wa Uchaguzi Zanzibar hajatangazwa na Rais ametishia wananchi kuwa atatumia majeshi kukandamiza madai halali ya wananchi wa Zanzibar.

10 Hakuna hatua zozote zimechukuliwa kuanza mchakato wa Katiba. Inaonyesha Serikali haina mpango kabisa na Katiba mpya.
Kumbuka Rais ana 100 dys hebu tumpe muda zaidi sawa sawa?
 
Kumbe Zitto ni mtupu kiasi fulani? Haya yote alitegemea yafanyike ndani ya siku 100? Yeye na majina ya Uswiss mbona hajasema? Ana kinga ya kibunge ila bungeni hajayasema!
Hayakusemwa katika siku 100. Je yanafikiriwa?
 
By the way " who's Zitto Kabwe"??? huyu si ndio mchumia tumbo tu hana hata chembe ya uongozi, hebu atulie au ikibidi akojoe alale sisi tunapiga kazi na ngosha.Hii ni awamu ya 5 apishe pembeni yeye ajikite katika kujenga NGO yake ya ACT....Hapa kazi tuu!!
 
Angetaja na matatu tu yaliyomshinda yeye ndani ya siku 100
 
Back
Top Bottom