Mambo Kumi yalomshinda Rais Magufuli

Mambo Kumi yalomshinda Rais Magufuli

Mambo yaliyoendeshwa kombo ndani ya miaka 30 iliyopita Zitto anataka yarekebishwe ndani ya siku 100! Magufuli aachwe afanye yale atakayoweza midhali keshaonyesha nia njema ya kuwatumikia wananchi.
Kuipa meno TAKUKURU unataka iwe baada ya miaka mingapi? Mbona ni rahisi kwa Magufuli kukata mishahara ya mawaziri kujengea vyoo vya shule lakini mzito kuipa meno Takukuru?
 
Kwa hesabu hizo basi mambo ambayo Magufuli hajagusa yanafika hata milioni
Unafurahi tunavyoagiza Sukari toka nje?? Tuna miwa inaoza huko Kilombero. Inahitaji miaka mingapi kufanya substution effect kwenye importation ya sukari? Mbona leo ana sign mkataba wa flyovers utakaoisha baada ya miaka 4? Usiwe mjinga wewe
 
Na Zitto alitaka hayo yote kumi yawe yamefanyika ndani ya siku 100?!

Talking is cheap, yeye Zitto amekuwa anapiga danadana ya kutaja majina ya watu walioweka fedha Swiss kwa muda gani?
Unadhani Serikali haina hayo majina? Kwa ujinga wako unaamini kabisa hakuna walioficha fedha nje ya nchi? Na kwa upumbavu wako unaamini serikali haimjui hata mmoja aliyeficha fedha offshore? Na kwa u-mbumbumbu wako unaamini kabisa serikali haiwezi kuwakamata hao wahuni? Basi kama unayowaza yatakuwa sahihi ni wazi hatuna serikali na kama nchi hatuko salama
 
Zitto kawaza kama mimi.Asante sana.
Simkubali Zitto na tabia zake za kipuuzi puuzi ila hapa kasema ya kweli tupu 1-8 yanatekelezeka na mchakato wa kuyatekeleza hautazidi ndani ya wiki 1 tu iwapo Magufuli atakuwa na nia ya dhati.
 
Sijui kama ni maneno ya Zitto au la; lakini sidhani kama hii inaweza kuwa ni hoja kwa sasa.
 
sasa zitto anataka magufuli aingilie posho za wabunge wakati huohuo wanadai bunge ni mhimili unaojitegemea? kwann asimshawishi spika au wabunge wenzie namna ya kuifuta hiyo posho ya vikao? harafu 2jiulize kitu, hv kwann wabunge we2 linapokuja swala la kufuta posho za vikao vya bunge huwa hanaweka pamba masikion?
 
Zitto Z Kabwe na MAMBO KUMI YALO MSHINDA MAGUFULI.

Siku 100 za Utawala wa Awamu ya 5 chini ya Rais Magufuli

Mambo 10 ya Msingi ambayo Rais Magufuli ameshindwa kuyafanya tangu aingie madarakani.

1 Mikataba yote ya Rasilimali za Nchi - PSAs Kwa Mafuta na Gesi Asilia na MDAs Kwa Madini bado ni Siri na sio Rais au Makamu wa Rais au Waziri Mkuu ambaye kaonyesha hata nia ya kutazama upya mikataba hii na kuiboresha Kwa maslahi ya watanzania. Mapato ya Nchi, makubwa kuliko ya utumbuaji majipu, yanaendelea kupotea. Mkataba wa IPTL bado unaendelea kunyonya Nchi na Serikali inatazama tshs 8 bilioni zinalipwa Kwa matapeli wa IPTL na PAP kila mwezi. Katika siku 100 tangu Rais Magufuli aingie madarakani, jumla ya tshs 30 bilioni zimeshalipwa Kwa IPTL/PAP ambazo zingeweza kununua CT scan Kwa hospitali zote za mikoa nchini. Fedha hii ni zaidi ya mkopo ambao Serikali imechukua kutoka Benki ya Dunia ili kujenga ' fly over ' ya Ubungo jijini Dar Es Salaam.

2) Posho za makalio katika mfumo mzima wa Serikali bado zinalipwa bila kufutwa kama Mpango wa Maendeleo 2011/2012 - 2015/2016 unavyotaka na kuagiza. Serikali imeongeza posho za kujikimu mpaka tshs 120,000 Kwa siku na Kwa wabunge bado wanalipwa posho ya makalio ya tshs 220,000 Kwa siku. Posho ambazo zimeshalipwa tangu Rais aingie madarakani ni sawa na kujenga barabara zote viporo za lami kuunganisha mkoa wa Tabora ( Kaliua - Urambo na Nyahua - Itigi ).

3) Serikali bado inatumia mashangingi na kila Waziri, Katibu Mkuu na wakuu wa idara wanatumia mashangingi ya gharama kubwa.

4) Tanzania bado inaagiza Sukari kutoka Nje na Serikali haina Mpango wowote ule wa kuondoa tatizo hilo. Hata katika Mpango wa Maendeleo Serikali haisemei sukari kabisa. Uagizaji wa Sukari ni jipu ambalo limeiva Lakini mkamuaji analilea. Hivyo hivyo Kwa sekta ya Nguo bado viwanda vya ndani vinapata ushindani usio halali kutoka Kwa nguo kutoka Nje zenye kuingia nchini bila kodi.

5 Taarifa ya Serikali kuhusu utoroshaji wa fedha Nje bado imefichwa na haijafikishwa bungeni. Hakuna hatua zozote zilizochukuliwa kudhibiti utoroshaji fedha na hakuna mashtaka yaliyofunguliwa Kwa wahusika.

7 TAKUKURU bado haina mamlaka ya kukamata na kushtaki wenye makosa ya kifisadi. Vile vile mfumo wa kila mwenye Mali athibitishe yeye kaipataje ( reverse burden of proof ) haujaanzishwa nchini na matokeo yake ni kuzorota Kwa juhudi za kumaliza ufisadi Kwa kuboresha mifumo. Kinachoendelea ni kutumbua majipu kimkakati bila kuzuia majipu kuota tena.

8 Mali na Madeni ya Viongozi bado ni Siri. Wananchi hawajui Rais Wao anamiliki nini AMA anadaiwa nini. Hivyo hivyo Kwa viongozi waandamizi wote. Serikali ya Awamu ya Tano imeendeleza mfumo ule ule wa maadili ulio dhaifu na wenye kulea vitendo vya rushwa.

9 Serikali ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania imeshindwa kabisa kushughulikia suala la Zanzibar na matokeo yake ni kuiweka Nchi kwenye hatari kubwa ya kuvunjika Amani. Mshindi wa Uchaguzi Zanzibar hajatangazwa na Rais ametishia wananchi kuwa atatumia majeshi kukandamiza madai halali ya wananchi wa Zanzibar.

10 Hakuna hatua zozote zimechukuliwa kuanza mchakato wa Katiba. Inaonyesha Serikali haina mpango kabisa na Katiba mpya.
jpm hana ubavu wakugusa kwani hajipendi ataishia miaka mitano
 
Mambo yaliyoendeshwa kombo ndani ya miaka 30 iliyopita Zitto anataka yarekebishwe ndani ya siku 100! Magufuli aachwe afanye yale atakayoweza midhali keshaonyesha nia njema ya kuwatumikia wananchi.
Hata kutuambia ana mali gani na ana madeni gani rais inatakiwa tusubiri?akili itumike kidogo taasisi ya urais siyo sehemu ya mafunzo unatakiwa uwe na utayari wa kuwa rais kweli,ila jamaa kiatu hakimtishi.
 
hata Rumi haikujengwa kwa siku 100, nakubaliana na namba tatu tu kati ya hayo yote mengine ni ya kisera na kimfumo ambayo hata kikwete aliyekaa kwa siku zaidi ya 1500 hakuweza
 
Kuna vitu Magu hatagusa navyo ni mambo aloyofanya JK
 
Mh zitto ametoa eti mambo kumi ambayo yeye anayaona hayajafanyiwa kazi, na anahisi yamesahaurika katika agenda za Mh Rais. Zitto amesahau kuwa ni siku 100 tu zimepita na zimebaki siku 1725.

Lakini zito nikukumbushe, mbona miaka imepita na wewe umeshindwa kuwafanyia watanzania yafuatayo, ambayo alutoa ahadi kututimizia.
  1. Kutaja majina ya Watanzania wenye account nje ya nchi?watoroshaji pesa
  2. Kutuletea ushahidi wa transactions za mbowe kuhongwa pesa na Nimrod Mkono
  3. Kutuletea ushahidi wa rushwa iliyotolewa na Mgodi wa buzwagi kwa waziri karamagi ili takukuru wamshughulikie (kama ulivyoombwa wakati huo)??
Zitto acha unafiki, Mh Rais ana siku 100 tu, wewe hayo matatu yamekushinda zaidi ya miaka sasa, acha kubwabwaja, majipu yatumbuliwe, kila jipu lina muda wake,
 
Kati ya Zito na Magufuli nani mwenye power na Mamlaka zaidi.wewe mwenyewe mleta mada mnafiki tu.
 
Kati ya Zito na Magufuli nani mwenye power na Mamlaka zaidi.wewe mwenyewe mleta mada mnafiki tu.
wewe ndo mnafiki, zitto alisema ataleta ushahidi wa hayo yote, inamaanisha alikuwa na uwezo nayo, mbona hajaleta mpaka sasa, anapata wapi moral authority ya kum challenge Dr. Magu
 
Msome tena Zitto. Kwani kuanza review ya mikataba ya gesi kunahitaji nguvu ipi inayomshinda Magufuli? Kwani ni dhambi kuanza review ya mikataba ya Madini na gesi hata ndani ya siku 2 baada ya kuapishwa? Kupitia upya mikataba hiyo kunamzuia nini kuendelea kutumbua majipu?
Siku 2 kujadili mikataba? Hauko serious! Mikataba sio page mbili, ni kitabu na unatakiwa kupitia neno moja baada ya lingine na kuelewa lina maana gani. Hata siku 100 hazitoshi, labda aamue kujilipua na kuivunja kwa mabavu ila sheria za kimataifa zitatushika endapo atafanya hicyo!
 
Bado mapema sana, huwezikurupuka kwa kila kitu nchi ilishauzwa ck mingi kuirudisha ktk mstar kwa ck mia cio raic kivile
 
Usiwe mjinga wewe... Wabunge wako wa CCM na wa Ukawa wanalipwa Tsh 220,000/- kwa KUJAMBIA VITI VYA BUNGENI kila siku. Magu anaogopa nini kufyeka hiyo hela ya mashuzi bungeni? Na penyewe unataka hadi siku ngapi zipite?
Nimecheka sana jamaa yangu!
 
Je hayo yote yamo kwenye ilani ya chama chake?
 
Zito Acha Ushabiki na Kupotosha. Mbona wewe hujataja majina ya walioweka fedha kwenye mabenki ya nje licha ya kuahidi?
 
Back
Top Bottom