Mambo Kumi yalomshinda Rais Magufuli

Mambo Kumi yalomshinda Rais Magufuli

Me nadhani si rahisi kushughulikia yote hayo kwa siku 100, ingekuwa poa kama zitto angemkumbusha rais kuwa kuna mengine mengi ya kushughulikia, pia tunatakiwa tumpongeze kwa hapa alipofikia mi naona c pabaya sana. Maana haya maozo yalifanywa huku mkwere akinywa kahawa tu pale ikulu. Tumpe nafasi tuone
 
Zitto Kabwe na MAMBO KUMI YALIYO MSHINDA RAIS MAGUFULI.

Siku 100 za Utawala wa Awamu ya 5 chini ya Rais Magufuli

Mambo 10 ya Msingi ambayo Rais Magufuli ameshindwa kuyafanya tangu aingie madarakani.

1 Mikataba yote ya Rasilimali za Nchi - PSAs Kwa Mafuta na Gesi Asilia na MDAs Kwa Madini bado ni Siri na sio Rais au Makamu wa Rais au Waziri Mkuu ambaye kaonyesha hata nia ya kutazama upya mikataba hii na kuiboresha Kwa maslahi ya watanzania. Mapato ya Nchi, makubwa kuliko ya utumbuaji majipu, yanaendelea kupotea. Mkataba wa IPTL bado unaendelea kunyonya Nchi na Serikali inatazama tshs 8 bilioni zinalipwa Kwa matapeli wa IPTL na PAP kila mwezi. Katika siku 100 tangu Rais Magufuli aingie madarakani, jumla ya tshs 30 bilioni zimeshalipwa Kwa IPTL/PAP ambazo zingeweza kununua CT scan Kwa hospitali zote za mikoa nchini. Fedha hii ni zaidi ya mkopo ambao Serikali imechukua kutoka Benki ya Dunia ili kujenga ' fly over ' ya Ubungo jijini Dar Es Salaam.

2) Posho za makalio katika mfumo mzima wa Serikali bado zinalipwa bila kufutwa kama Mpango wa Maendeleo 2011/2012 - 2015/2016 unavyotaka na kuagiza. Serikali imeongeza posho za kujikimu mpaka tshs 120,000 Kwa siku na Kwa wabunge bado wanalipwa posho ya makalio ya tshs 220,000 Kwa siku. Posho ambazo zimeshalipwa tangu Rais aingie madarakani ni sawa na kujenga barabara zote viporo za lami kuunganisha mkoa wa Tabora ( Kaliua - Urambo na Nyahua - Itigi ).

3) Serikali bado inatumia mashangingi na kila Waziri, Katibu Mkuu na wakuu wa idara wanatumia mashangingi ya gharama kubwa.

4) Tanzania bado inaagiza Sukari kutoka Nje na Serikali haina Mpango wowote ule wa kuondoa tatizo hilo. Hata katika Mpango wa Maendeleo Serikali haisemei sukari kabisa. Uagizaji wa Sukari ni jipu ambalo limeiva Lakini mkamuaji analilea. Hivyo hivyo Kwa sekta ya Nguo bado viwanda vya ndani vinapata ushindani usio halali kutoka Kwa nguo kutoka Nje zenye kuingia nchini bila kodi.

5 Taarifa ya Serikali kuhusu utoroshaji wa fedha Nje bado imefichwa na haijafikishwa bungeni. Hakuna hatua zozote zilizochukuliwa kudhibiti utoroshaji fedha na hakuna mashtaka yaliyofunguliwa Kwa wahusika.

7 TAKUKURU bado haina mamlaka ya kukamata na kushtaki wenye makosa ya kifisadi. Vile vile mfumo wa kila mwenye Mali athibitishe yeye kaipataje ( reverse burden of proof ) haujaanzishwa nchini na matokeo yake ni kuzorota Kwa juhudi za kumaliza ufisadi Kwa kuboresha mifumo. Kinachoendelea ni kutumbua majipu kimkakati bila kuzuia majipu kuota tena.

8 Mali na Madeni ya Viongozi bado ni Siri. Wananchi hawajui Rais Wao anamiliki nini AMA anadaiwa nini. Hivyo hivyo Kwa viongozi waandamizi wote. Serikali ya Awamu ya Tano imeendeleza mfumo ule ule wa maadili ulio dhaifu na wenye kulea vitendo vya rushwa.

9 Serikali ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania imeshindwa kabisa kushughulikia suala la Zanzibar na matokeo yake ni kuiweka Nchi kwenye hatari kubwa ya kuvunjika Amani. Mshindi wa Uchaguzi Zanzibar hajatangazwa na Rais ametishia wananchi kuwa atatumia majeshi kukandamiza madai halali ya wananchi wa Zanzibar.

10 Hakuna hatua zozote zimechukuliwa kuanza mchakato wa Katiba. Inaonyesha Serikali haina mpango kabisa na Katiba mpya.
 
Hilo la Zanzibar!

Naomba magufuli aendelee kujiweka pembeni hivyo hivyo !

Kina jecha walishasema watafanya uchaguzi....

Wenye kuongozwa na rais Wa Zanzibar ni wazanzibar wenyewe....waachie waamue wenyewe...
 
hongera zitto ni kweli huwez kutumbua majipu huku unashindwa kuzuia majipu yasiumuke
 
watu mnakurupuka kubeza maoni yake wakati ameeleza suala la kugusia ama kupitia upya masuala hayo 10 na si kama fikra zenu zilizokurupuka kwamba amesema yatimizwe ndani ya siku 100
 
Huo ndiyo uwezo wa Magu jamani.
Vision yake ndipo ilipoishia hapo

Mambo mengine mnamchosha mzee wa watu buree.
 
Zito ni mwana siasa anayejua siku zones
CCM haina mpango wa kuzuia ufisad mkubwa
Nashukuru zito yupo sahihi sana
 
Hayo yote hayawezi fanyika kama hujatumbua majipu kwanza. Zitto naye atulie, ila akitulia chama chake kinapotea inabidi aseme tu. Ni sawa sawa na kupeleka mambo ya utalii ndani ya alshababu, si watawateka watalii na kudai ransom
 
Nashaka ACT wazalendo wanatry too hard kujionesha wao ni zaidi ya chadema. wanakitu inferior so wanataka waonekane walisema wao kabla so that ionekane ni agenda yao....... huu sio mwanzo mzuri.
 
Zitto Z Kabwe na MAMBO KUMI YALO MSHINDA MAGUFULI.

Siku 100 za Utawala wa Awamu ya 5 chini ya Rais Magufuli

Mambo 10 ya Msingi ambayo Rais Magufuli ameshindwa kuyafanya tangu aingie madarakani.

1 Mikataba yote ya Rasilimali za Nchi - PSAs Kwa Mafuta na Gesi Asilia na MDAs Kwa Madini bado ni Siri na sio Rais au Makamu wa Rais au Waziri Mkuu ambaye kaonyesha hata nia ya kutazama upya mikataba hii na kuiboresha Kwa maslahi ya watanzania. Mapato ya Nchi, makubwa kuliko ya utumbuaji majipu, yanaendelea kupotea. Mkataba wa IPTL bado unaendelea kunyonya Nchi na Serikali inatazama tshs 8 bilioni zinalipwa Kwa matapeli wa IPTL na PAP kila mwezi. Katika siku 100 tangu Rais Magufuli aingie madarakani, jumla ya tshs 30 bilioni zimeshalipwa Kwa IPTL/PAP ambazo zingeweza kununua CT scan Kwa hospitali zote za mikoa nchini. Fedha hii ni zaidi ya mkopo ambao Serikali imechukua kutoka Benki ya Dunia ili kujenga ' fly over ' ya Ubungo jijini Dar Es Salaam.

2) Posho za makalio katika mfumo mzima wa Serikali bado zinalipwa bila kufutwa kama Mpango wa Maendeleo 2011/2012 - 2015/2016 unavyotaka na kuagiza. Serikali imeongeza posho za kujikimu mpaka tshs 120,000 Kwa siku na Kwa wabunge bado wanalipwa posho ya makalio ya tshs 220,000 Kwa siku. Posho ambazo zimeshalipwa tangu Rais aingie madarakani ni sawa na kujenga barabara zote viporo za lami kuunganisha mkoa wa Tabora ( Kaliua - Urambo na Nyahua - Itigi ).

3) Serikali bado inatumia mashangingi na kila Waziri, Katibu Mkuu na wakuu wa idara wanatumia mashangingi ya gharama kubwa.

4) Tanzania bado inaagiza Sukari kutoka Nje na Serikali haina Mpango wowote ule wa kuondoa tatizo hilo. Hata katika Mpango wa Maendeleo Serikali haisemei sukari kabisa. Uagizaji wa Sukari ni jipu ambalo limeiva Lakini mkamuaji analilea. Hivyo hivyo Kwa sekta ya Nguo bado viwanda vya ndani vinapata ushindani usio halali kutoka Kwa nguo kutoka Nje zenye kuingia nchini bila kodi.

5 Taarifa ya Serikali kuhusu utoroshaji wa fedha Nje bado imefichwa na haijafikishwa bungeni. Hakuna hatua zozote zilizochukuliwa kudhibiti utoroshaji fedha na hakuna mashtaka yaliyofunguliwa Kwa wahusika.

7 TAKUKURU bado haina mamlaka ya kukamata na kushtaki wenye makosa ya kifisadi. Vile vile mfumo wa kila mwenye Mali athibitishe yeye kaipataje ( reverse burden of proof ) haujaanzishwa nchini na matokeo yake ni kuzorota Kwa juhudi za kumaliza ufisadi Kwa kuboresha mifumo. Kinachoendelea ni kutumbua majipu kimkakati bila kuzuia majipu kuota tena.

8 Mali na Madeni ya Viongozi bado ni Siri. Wananchi hawajui Rais Wao anamiliki nini AMA anadaiwa nini. Hivyo hivyo Kwa viongozi waandamizi wote. Serikali ya Awamu ya Tano imeendeleza mfumo ule ule wa maadili ulio dhaifu na wenye kulea vitendo vya rushwa.

9 Serikali ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania imeshindwa kabisa kushughulikia suala la Zanzibar na matokeo yake ni kuiweka Nchi kwenye hatari kubwa ya kuvunjika Amani. Mshindi wa Uchaguzi Zanzibar hajatangazwa na Rais ametishia wananchi kuwa atatumia majeshi kukandamiza madai halali ya wananchi wa Zanzibar.

10 Hakuna hatua zozote zimechukuliwa kuanza mchakato wa Katiba. Inaonyesha Serikali haina mpango kabisa na Katiba mpya.
Naona Zitto kafuta hii post fasta dah
 
Tusimpuuze ZZK ana kitu cha kutukumbusha na kutushauri kama taifa na kama kweli tunalenga kuwa taifa lenye uchumi wa kati ifikapo 2015. Tukiendelea kulipa pesa kwenda IPTL kwa makusanyo ya 1.3 trilioni tunakuwa kimsingi tumekusanya bilioni miatano tu maana 8 zinakuwa zimetoka na kwa mtindo huo mapato hayawezi ongezeka wala kupunguza deni la taifa itakuwa ndoto. Walioingia mkataba huo si mali zao tunazijua...tutimize lengo la mkataba ila kila wanachokipata tuwafilisi maana hawa ni watanzania wenzetu tu...tuwafillisi wataachia wenyewe IPTL na kuirudisha huko ilikotoka bila matatizo ya kushitakiwa huko Uingereza kulikowekwa kwenye mkataba huo wa IPTL...filisi Karasinga hata kama mali ziko Uswisi zichukuliwe tu mbona za waziri yule wa fedha na jitihada za vyama vingi zilichukuliwa tena zikiwa huko huko ulaya?
 
Zito hajazungumzia kuwa yawe yametekelezwa kuna mambo kasema hata kuzungumziwa hayajazungumziwa. someni muelewe sio mnaleta ya Braza K.

Mi naona ni vizuri zaidi asigusie, maana ukigusa watajipanga. Hapa yenyewe watu washaanza kuhamisha mali na kupeleka nchi za nje. Ameonyesha nia ya kufanya mabadiliko, tumpe support na kila mwananchi anaweza kuwa "mmbeya" kwa ajili ya manufaa ya taifa hili ambalo lilishakosa mwelekeo. UZALENDO KITU MUHIMU.
 
Kuna siri gani na IPTL, Mbona jaguswi, hashikwi?? Mbona Magufuli hapo anakuwa bubu? b30?? Maweeee
 
Kumbe Zitto ni mtupu kiasi fulani? Haya yote alitegemea yafanyike ndani ya siku 100? Yeye na majina ya Uswiss mbona hajasema? Ana kinga ya kibunge ila bungeni hajayasema!
Msome tena Zitto. Kwani kuanza review ya mikataba ya gesi kunahitaji nguvu ipi inayomshinda Magufuli? Kwani ni dhambi kuanza review ya mikataba ya Madini na gesi hata ndani ya siku 2 baada ya kuapishwa? Kupitia upya mikataba hiyo kunamzuia nini kuendelea kutumbua majipu?
 
"Kashindwa kabisa" Really????
Mi nasema hajagusa huko kiasi cha kwenda public.
Natumaini ataingia huko panapo Muda mwafaka
Na wakati utakapofika Zitto atasema nilisemam mimi, sio mbaya! Thanks for the reminder, itz only about time!!
Matumizi ya Mashangingi yanahitaji miaka mingapi kuyafutilia mbali? Mbona kama hamjielewi mnakotaka kwenda? Siku 100 kama kaweza kununua koki za mafuta bandarini anashindwa nini kumwambia Nape aachane na Shangingi apande Stalet? Hivi wizara kama ya Nape ina faida gani kwa jamii hadi itumie VX V8?
 
hv wakuu kuna ukwl kuwa huyu mheshmiwa ztto hachukui posho ya vikao bungen,?
Ishu ya Posho ya Kujambia viti bungeni ipo kisheria/kitaratibu ndio maana mimi simlaumu mbunge wangu Mnyika kuitafuna. Ifutwe hiyo Sheria au ufutwe huo utaratibu. Kwanza ni rushwa kwa wabunge maana hawastahili kuwa nayo lakini wanapewa.
 
Back
Top Bottom