demigod
JF-Expert Member
- Jan 2, 2015
- 8,250
- 15,116
Kwanza, ni muhimu kuelewa kuwa kila timu ina changamoto zake na hakuna njia moja ya kufikia mafanikio. Hata hivyo, hapa kuna mambo kumi ambayo Simba SC wanaweza kuyafanya ili kufikia kiwango na ubora wa Yanga SC hivi sasa:-
1. Kuwa na uongozi thabiti na waaminifu ambao unaweza kuendesha timu kwa ufanisi na uwazi.
Uongozi ni pamoja na wabeba maono na malengo yenye uhalisia. Mfano:- Murtaza Mangungu aliwapa ahadi kuwa kama akiingia madarakani basi atahakikisha Klabu ya simba inaifunga Yanga. Huyu sio aina bora ya kiongozi.
2. Kuwekeza katika vifaa bora vya mafunzo na ujenzi wa miundombinu ya kisasa kwa ajili ya timu.
Aina ya vifaa ambavyo Yanga wanatumia mazoezini ni mfano wa kuigwa kwa kuwa sijawahi kuviona ktk viwanja vya mazozi vya Simba. Vile vile wanapaswa kutafuta kambi nzuri ambayo inafanana na Avic Town. Kule mbweni hakuna utulivu wa kutosha maana kila wakati vigoma vya urigwai vinapita.
3. Kuajiri makocha bora na wenye uzoefu ambao wanaweza kuendesha mafunzo ya kiwango cha juu na kuendeleza vipaji vya wachezaji.
Kocha bora ni yule mwenye CV ambayo inaonyesha kuwa aliwahi kufanya jambo fulani huko nyuma. CV ya Robertinho haionyeshi kuwa kama amewahi kishinda kombe lolote lile barani afrika. Simba wanapaswa kutafuta kocha mpya ambaye aliwahi kushinda hata kombe lolote la CAF.
4. Kuimarisha mfumo wa usajili wa wachezaji kwa kufanya tathmini ya kina na kuchagua wachezaji wenye ujuzi na talanta za kipekee.
Kama kuna klabu inaongoza upigani basi, Simba ni namba moja nchini. Jamaa wameajiri Scout ambaye hapo awali alihusika kumleta SAWADOGO klabuni kwao. Inashangaza mno.
Inafaa waige kutoka Yanga, ukiona mchezaji mzuri unamfuata hadi kwa mama yake na wala sio kutuma watu. Mfano Eng Hersi alimfuata mama yake Aziz Ki.
5. Kuhakikisha kuwa wachezaji wanapata mafunzo ya kutosha kuhusu mbinu na uwezo wa kucheza kwa pamoja kama timu.
Mafunzo na mbinu yanatokana na kocha mzuri ambaye anayeweza kuongoza kwa mfano ili wachezaji waweze kuelewa vyema. Sasa mginda kwa unene ule anawezaje kumuonyesha Kibu Denia namna ya kuwa na Pace? Simba inabidi ijitafakari ktk eneo hili
6. Kutoa motisha kwa wachezaji kwa njia ya malipo mazuri, mikataba mizuri na fursa za kujitokeza katika mechi za kimataifa.
Inasemekana kuwa Mo Dewji ni tajiri bahiri kuwahi kutokea ktk historia ya soka hapa Tanzania. Jamaa anapaswa kujifunza kutoka kwa Mr Ghalib. Uwezi kushindwa kuwalipa bonus wachezaji ili hali kila siku wanabeba ndoo za sabuni na matangazo ya juisi. Kama hawezi aiache timu ili waje wengine wenye nia njema.
7. Kujenga uhusiano mzuri na mashabiki na kuhakikisha kuwa wanahisi sehemu ya timu na wanapewa huduma bora.
Mashabiki wa simba wanaipenda timu yao lkn timu haiwapendi, haiwezekani mpaka sasa hakuna shabiki wa simba mwenye kadi ya kielektroniki kama mashabiki wenzao wa Yanga. Kadi za uanachama zinajenga mahusiano baina ta Klabu na mashabiki.
Yaani sasa hivi mashabiki wa simba wanaishabikia simba kwasababu tu waliipenda wao wenyewe na hawana uwezo wa kuhamia timu nyingine kwasababu soka sio kama dini. Vinginevyo wengi wangekuwa wamehamia Namungo na Singida BS.
8. Kuwa na mkakati wa masoko ambao unaweza kufikia watazamaji wengi na kushiriki katika matukio mbalimbali ya kijamii.
Matukio mbalimbali ni kama kushiriki kutoa misaada mbalimbali kwa wale wasio jiweza. Yanga wamekuwa wakifanya hivi tangu mwaka 2021. Simba walifanya mara moja tu tena walitoa zawadi zisizo zidi elfu 50.
9. Kujenga uhusiano mzuri na vyombo vya habari na kutoa taarifa za kina kuhusu timu, wachezaji na matukio mbalimbali.
Habari zao mara nyingi hawataki kuzivujisha mitandaoni, mara nyingi wanazificha kwenye APP yao. Hii inalwapa shida wachambuzi & waandishi wa habari kupata habari za michezo.
10. Kuendeleza maadili mema kama vile nidhamu, uwajibikaji, uaminifu na umoja kati ya wachezaji, viongozi na mashabiki.
Nidhamu imekuwa tatizo kubwa sana kwao. Hawajipi nafasi ya kujifunza kutoka kwa wenzao Yanga. Wanatabia yakuchukua wachezaji waliochwa na vilabu vingine kwa makosa ya kinidhamu mfano Saido Ntibanzokinza. Vile vile hawana uwezo wa kuwaadhibu wachezaji wanao vuta bangi klabuni mfano Jonas Mkude. We mchezaji anawezaje kumtongoza CEO? Basi Mkude aliweza kufanya hivyo mara kwa mara pale atokapo kuvuta Shisha.
Hayo ni machache wakuu, ila tusichukiane pale tunapo kosoa ili kufanyike mabadiliko.