Mama yake Zitto avamiwa

mbona CHAMVIGA una jichanganya? kweli ni mtu makini kweli? tukio limetokea dar(tabata) au kigoma? hizi chuki binafsi na uongo vina kusaidia nini? sentesi yako imeonesha wewe ni muongo na ujui chochote! pumzika

Utaelewa tu hii tabia yenu kujifanya kugeuza mambo ili muendelee kuuhadaa uma una mwisho.
 
Last edited by a moderator:
CCM kupitia media zao na hao wahuni wao wanahangaika sana kuipaka matope CHADEMA isipate kura za waislam kupitia jina la ZITTO.mtahangaika sana lakini TUMEWACHOKA!Hatutaichagua Chadema kwa kuwa ni "watakatifu saana" ila tu kwa kuwa tumeichoka CCM!
 


Mkuu Dr. W. Slaa, with all due respect, kwanza asante kulitolea hili ufafanuzi wa kina ambao angalau, it makes sense!, kama na lile tukio la video, ungelitolea ufafanuzi kama huu, Chadema kingekuwa a bit safer than hapa kilipo sasa katika lile!. Mimi kama mwananchi tuu wa kawaida, najaribu kuvaa viatu vya Victim.
  1. Kitendo cha kiongozi wa juu wa Chadema kwa level hiyo, kukutwa na maswahibu hayo, bila kuwaarifu viongozi wake wowote wa juu, kisha nyinyi mnakuja kuisoma kwenye magazeti na mitandao, ni uthibitisho tosha kuna tatizo inside the core!. Tatizo linaweza kuwa ni la chama as an institution au ni la viongozi wa chama as individuals, the botom line ni kuna tatizo na lipo, na linahitaji kuwa addressed!, ikumbuke hata video ya Mwigulu, alipewa na kiongozi wa Chadema!, aliyeileta ile video humu jf ndie huyo huyo aliyeileta humu ile karatasi yenye mwandiko wa Rwakatare, na ndiye aliyeileta humu jf ile barua ya Zitto!. Mimi nilipandisha uzi humu jf nikisema Chadema kuna kirusi!, nilibezwa, ila nikasisitiza ukweli utasimama!.
  2. Suala la tuhuma za kutaka kudhuru ni tuhuma tuu, kwa vile alikuwepo aliyeshikwa na sumu ya panya, hata kama hakuna mlalamika, wala hakuna aliyeshitaki, wala mdhurika mwenyewe kusema haamini kama kuna kitu kama hicho, hakuondoi uwezekano wa uwepo mpango huo, hivyo kanuni ya thuma still applies subject to verification.
  3. Hili la Mama Salum, kwanza naomba nikurekebishe kidogo, hakusema kuwa aliwahi kumuona Mwanza, bali ni Tanga. Naomba ninukuu gazeti "Alisema anaweza kuwatambua watu hao akiwaona na kwamba mmoja wao si mgeni machoni mwake, kwa sababu aliwahi kumuona mkoani Tanga katika moja shughuli za chama hicho".Kauli hii inaashiria hajathibitisha kuwa ni kada, bali sii mgeni machoni pake!. Kwenye event ya watu wengi, mtu unaweza tuu kuwatambua baadhi kwa sura, hili lakutakiwa kumtambua kwa sura, sii kumtendea haki!. Kwa mtu wa kawaida, unaweza kukumbuka sura sio ngeni, bila kukumbuka kitu kingine chochote kama uliiona wapi, lini na katika mazingira gani!, hivyo kwa hili, lets give her benefits of doubt!.
  4. Kwa vile victim ni kiongozi wa Chadema, shughuli zake nyingi zitakuwa ni za chama, hivyo ile kumbukumbu ya familiar face, ita point moja kwa moja kwa mwanachama, mshabiki, au mfuasi tuu wa chama, hivyo kumuita ni kada is right!. Anaweza kuwa ni imposter aliyeenda kuomba msaada kwa kiongozi wa Chadema ili kuikarabati phanton office ya Chadema hapo tabata relini, lazima atakuwa ni mfuasi!. Mtaani, mwanachama, mfuasi na mshabiki, wote ni makada tuu!.
  5. Kama uchunguzi wa ndani umefanyika na kugundua kuwa ni hila chafu ya kuichafua Chadema, then ile hoja uyangu ya kirusi/virusi ndani ya inner core ya Chadema inazidi kupata nguvu, uchunguzi kama huu ungefanyika kwenye ile video, ungedua kuwa sio fake bali ni bonafide genuine, hivyo uchunguzi huu uendelee ili kuvibaini virusi, msafishe nyumba yenu ahead of 2015.
  6. Kumbe ndio maana umeingia na ID bila kificho. Asante kwa kuingia na ID yako bila kificho!.
  7. Nakushukuru kwa kutohukumu, kauli kama hii pia ulipaswa kuitoa wakati wa video kwa kusema huwezi kudhibitisha kiongozi wako alisema yale maneno au hakusema, na kueleza kuwa Chadema haihusiki na yaliyomo, ili ikitokea ikakutikana ni kweli, then maneno yale yanakuwa ni ya mhusika tuu na sio ya chama.
  8. Umeeleweka.
  9. Hili la umakini wa Chadema nalo ni relative na subjective, na umakini huu sasa utaonekana katika namna ya ku apply anti virus yake ili kukisafisha na hizi kadhia zinazokinyemelea, ikiwemo kukisafisha na hao virusi kwenye inner core yake!.
  10. Amen.
Pasco.
 
ZITTO YUKO KWENYE SHINIKIZO KUBWA KUTAKIWA KUKIHAMA CHADEMA ILI MPANGO WA KUKIOKOA CCM KWA MPANGO KAMA ULE WA KENYA UWEZE KUANZA KTI YAKE NA NCHIMBI MUDA KABLA YA 2015

CHADEMA Mako Makuu tayari wanazo taarifa zote muhimu kuhusu Zitto na jinsi gani alivyo kwenye shinikizo kubwa mno kutakiwa na CCM kuhamia NCCR-Mageuzi wakati wowote. Yote haya yanafahamika tena kiundani zaidi na njia mbadala nazo ziko tayari kuyashinda yote haya.

Ni imani yao kwamba bila Zitto eti hakutoku na CHADEMA chenye nguvu tena. Imani hiyo ni potofu kwa kuwa kuna jembe kibao ndani ya CHADEMA na wanajiendesha kama taasisi zaidi kuliko nafsi mmoja mmoja.

Kimsingi Zitto alikua atumie kisingizio cha Lwakatare kukihama CDM lakini mpango ukabuma. Hivi sasa tunazo taarifa za kutafutwa mianya na visingizio vya kila aina kusaidia kutimiza lengo hilo. Mara baada ya hapo Zitto's political platform shall massively be oiled by CCM huku vijana wale waliotangulia wakijumuika naye na kuanza kazi moja ya kukisaidia CCM kukishambulia CDM.

Kwa kifupi, template wanayoifanyia kazi CCM hivi sasa ni ile ya akina Uhuru Kenyatta bila kujua ya kwamba mazingira ni tofauti aja na kwamba kamwe mpango wao huo hauwezi ukafika mbali.

CCM hivi sasa kinapigia ramli eti kurudi madarakani kwa staili ya KANU hivi sasa kule Kenya lakini kwa kupitia kufadhili vyama vingine vidogo vidogo kama vile NCCR-Mageuzi, TLP na UDP kisha kukusanya hizo CCM 'A', 'B', 'C' na 'D' kuunda serikali dhaifu iliyo na wabunge kiduchu bungeni.

Mpango mzima unafikiriwa kutekelezwa kwa kutumia ile Computer Software toka Ghana (endapo CHADEMA kitaingia mtego wa kukubali upigaji kura kwa njia ya kompyuta) kuibia kura bila ya wananchi wakawaida kuelewa kitakachokua kimetendeka.

Hadi hivi sasa vyama tawala tayari vimeingia agano la kusaidia wenzao kubakia madarakani kwa namna yoyote ile na kwamba kukitokea fujo za kupinga matokeo basi wataleta nchini majeshi kusaidia kulinda azma hiyo.

Hili ni jambo la kutambuliwa mapema na CHADEMA kukiwekea mkakati huku wakijua ya kwamba karibia vyama vyote vya upinzani nchini hadi hivi sasa hawako upande wetu bali ni wasaidizi wa mpango huo.


 

We CHAMVIGA bila shaka utakuwa le umevuta bangi au ndo umetafuna pilipili kichaa kwan sio bure,
unaandika uchochezi thread nzima gaid w. Na hii thread umeishobokea sana utadhan una hati miliki nayo.
 
Last edited by a moderator:

Unauliza maswali kisha unajijibu mwenyewe, unaandika predictions zako huku ukituaminisha unajua kinachokuja kifupi wewe huna lolote unachofanya hapa ni kuwachezea wenye kufikiri na kutoa conclusion kirahisi.
Zitto ni chadema na chadema ni zitto nadhani kayazungumza mwenyewe mh Zitto.
Unaonyesha kwamba zitto si chochote cdm na hata akiondoka hakuna madhara makubwa hapa unaandika huku roho yako unakusuta ni nani asiejua kuondoka chadema zitto ni sawa na kumrudisha mtoto alieko la 7 kumrudisha la 1? Acha unafiki na kuweni wise people huenda mkashindana somehow na Ccm ila kwa umbea huu hamna mtakapofika.
 
Hebu punguza kidogo munkari, pengine umetoneshwa penyewe penye kidonda ila lengo ilikua ni tofauti na hapo.

Cha msingi, usisahau kurudi hapa hapa ubaoni, ndani ya kipindi cha miezi 18 tangu hivi sasa, na tupate kuulizana juu ya swala hili hili hapa. Kumbuka, endapo utasahau agano hili hapa basi mimi ni mzuri sana katika kuhifadhi ahadi; nitakukumbusha juu ya hilo.

Karibu sana katika darasa la siasa, na wala si SIHASA, ili upate kuimarika zaidi kupita picha unayopata kutokana tu na ule ujumbe amba milango yote ya fahamu yanakuzawadia sawa tu na wengine hapo nje - hapo ndipo utakapobahatika kupata japo kipenyo cha kuweza kusimama walau hatua moja mbele ya umati.

Tofauti za maoni ulizonyambua humu zinaheshimika sana na haki yako ya kufanya hivo pia ni sehemu kuu ya wajibu wangu kutetea hata iweje.


 

ina maana wewe kwa kuwa ni mtumwa wa Mama Slaa na wazandiki wengine ndio mwenye haki na ni sawa kwako kushambulia rafiki yangu kila kukicha!

By the way, kwa kadri ninavyokujua siamini kama kuna kitu chochote tunachoshabihiana. U r just a wannabe myopic rebel with no ideological or principles of political life. Misimamo yako mingi ni ya kujikweza kuliko imani ama upeo wa masuala.

By tha way u need kujielimisha zaidi historia ya mapambano ya huyo unayependa kumuingiza katika majadiliano nami na usishangai kuwa wakati wake akiwa kama mimi alikuwa akipambana na siasa za hatari na maadui waliopevuka kuliko hizi siasa za matumbo mnazoziendesha.

Na kuhusu hili la uhusika wa Dr Slaa na masuala ya Morogoro na Igunga kwa kuwatumia kina Sabula na Mtemelwa ninayajua na wengi tu wanayajua na baadhi yao wameshaungama kama wengine wengi wanaotumiwa kama wewe katika "shughuli maalum"... Sasa kama mnajiona ninyi ndio mnajua siasa chafu endeleeni kupayuka hapa na sisi turopoke zaidi.

kwa taarifa yako hili tukio la Mama Zitto ambalo kwa kiasi fulani limepotoshwa na habari ya Mtanzania lilipotokea kitu cha kwanza alichokifanya Zitto ni kuhakikisha kuwa taarifa zake hazivuji kwa imani yake kwamba bado anapaswa kukilinda chama kwa kuwalinda maadui zake wanaomuwinda, kumfitini na kuendeleza uzandiki dhidi yake kila kukicha. Sasa kama ninyi mbataka aanze kuongea anaoyajua na yanayomkuta kila siku endeleeni na huu upuuzi wenu mnaoundeleza hapa!
 

-Actuall you are not my peer intellectually by any description.

You are just another desperate attention seeker in town.What do you know about Ideologies?

Umri ulio nao unakutosha kurudi shule mbona kuna wenzako wameamua kurudi shule?Hizo personal grudges usizilete kwenye mjadala maana si kawaida yangu kurithi maadui za watu.

Najua kinachokuumiza wewe na wenzio ni kuona nasimama kwa ajili ya Taasisi tofauti na mlivyotaka mimi nisimame kwa ajili yenu.It suits you,not me.

Wakati mwingine mtu mwenye akili timamu akikaa karibu na mzee mwenye buasara anastahili angalao kunufaika na Busara hizo.Tumia fursa uliyo nayo muda huu ukiwa karibu na Dr.Salim.Jiangalie sana kaka na pia washauri wenzio ambao sitaki kuwataja hapa.Mtawadanganya vijana wengine ila sio mimi kwa kuwa nawajua na malengo yote ninayajua.

Siasa zako za kibaguzi na kinafiki haziwezi kutufunza lolote sisi wadogo zako.

Hayo matusi uliyotukana hapo juu ujue pia hata mimi nina uwezo wa kurudisha and i always overdo.

Be warned!
 

Jamaa unavichekesho ile mbaya, kila kitu una act unakijua. We are watching you avanchar.
 
Ben Saanane

CHADEMA ni mpango wa Mungu na yeyote atakayesaliti na kuhujumu kamwe hatobaki salama.

Shard Kole@Tabora1

Fikra kama hizi ambazo zinaelekea kuhodhi mitizamo ya wana CHADEMA siku hizi ndio msingi mkuu wa ujinga mwingi unaoendelea katika chama hichi. Fikra kama hizi zimekigeuza CHADEMA kuwa chama cha kihafidhina kabisa with all the hate, bigotry and absurd characters that are found with RIGHT WING parties duniani. Wanajidanganya kama vile Mungu huyu ni wao pekee. Mungu huyu ni wa wengi na anayaona mabaya yote mnayowafanyia wenzenu. Akiwarudi mnaanza kutafuta mhawi!

Okoa demokrasia ya Tanzania, ondoa CHADEMA fromthis absurd path!
 

You must be out of you mind.do credibility a favor by proving beyound doubt your assertion above.You can do better than this Mr.Jack of all trades, master of none.

Sijui unamsaidia na kumshauri nini Mzee Salim kwa fikra hizi ulizoonyesha hapa zinazoegemea fikra za mitaani.Tell those rumor-mongering friends of yours to stop this nonsense.
 
 
Utaelewa tu hii tabia yenu kujifanya kugeuza mambo ili muendelee kuuhadaa uma una mwisho.

Uongo wako na wa mama yako umekuwa taken by event mulifikiri dili litalipa wapi bwana, mara wabunge wamefukuzwa wakawa front page TV na radio ndio ikawa hadithi mara limekuja la mulongo na Lema huko Arusha nalo wiki nzaima mara la Bajeti ya maji kutpwa njia ya mwongo fupi mrejeeni mumba mukiri dhambi mbaya hiyo mufanyayo
 


Kaka sasa kama anti virus yenyewe nayo imekuwa kirusi shughuli itafanyikaje? Zitto aliomba iundwe tume ya kuchunguza haya yote na yeye alikuwa tayari kukaapembeni aruhusu uchunguzi huo kufanyika kwa uwazi lakini hadi leo hakuna kitu. WHY?

kuhus hilo tukio hata mimi nilidhangaa ilipodaiea kuwa Mama Shida amesema kuwa ni kada wa Chadema. Nikadhani kuwa gazeti wamespin lakini kumbe kulikuwa hata na qoute inayosema vile ambavyo nilisikia mimi... Kuwa mmoja wa vijana hao sura yake kama amewahi kuiona katika shughuli za chama.

kingine kinachotia kinyaa ni hili suala la kudai kuwa Mama Zitto hakuwasiliana na Dr Slaa na Freeman... Hapa napata maswali mengi sana. Mimi nilipopata taarifa kanza nilidhani yqweza kuwa oppurtunists ambao Zitto amewatambua kama agent provocateurs, lakini sasa naanza kufikiria vingine!
 
Naendelea kusikilizia na kusubiria kama baadhi ya hizi hoja zangu humu zitapata majibu!.
Pasco.
 
Mkuu Omar, kwa hili, naziona kila dalili za "low state of mind incapacitation at an earl age!", sijui kama hata hiyo 2015 tutafika tukiwa salama!, kwa sababu, kadri miaka inavyokwenda, this low state of mind incapacitation, will turn into high state of mind incapacitation and finally will reach the state of highest state of mind incapacitation!, halafu ndio baadhi yetu sisi ambao ni wanahabari, tunatakiwa kuwaaminisha Watanzania kuwa "this is the man we need" for the next ten years from 2015!.

Mungu Ibariki Tanzania!.
Pasco.
 

Hoja zako wakati mwingine ni nzuri sana, lakini unapozichanganya na kujiamini kiasi cha juu kabisa kwamba lolote unalofikiri ndiyo ukweli wenyewe zinatia mashaka. Ukiwa mwanahabari unaweza kuchagua kuwa huru au kujifunga na kikundi fulani cha watu unaoweza kuwaripot wapendavyo wao. Hata hivyo sidhani kama jukumu la kuwaaminisha Watanzania (hapo kwenye red) ni la wanahabari peke yao. Kwani:

  1. Kuna wanahabari walioshindwa kuwaaminisha Watanzania,
  2. Kuna wanasiasa walioamua kuwaajiri wanahabari ili wafanye propaganda
  3. Kuna wanasiasa walioamua kufanya kazi ya wanahabari
Kwa hali hiyo, 'habari' nyingi za kisiasa zimekuwa zikiishia kuegemea upande fulani kwa nia ya kusafisha kambi na wakati huo huo 'kumwaga sumu' kwa kambi nyingine hata ndani ya chama kimoja.

Je, Watanzania wategemee nini kwa mwandishi mwenye personal/ideological bias?
 
Mkuu Omar, naziona kila dalili za "mind incapacitation at an earl age!",
God forbid...are you sure you are okay Pasco?
sijui kama hata hiyo 2015 tutafika tukiwa salama!,
True, there are those who wish that day never comes...aren't the guilty are always afraid?
halafu ndio baadhi yetu ambao ni wanahabari, tunatakiwa kuwaaminisha Watanzania
Mnatakiwa kuwaaminisha Watanzania!...Kwani hao Watanzania hawana macho wala masikio?
kuwa "this is the man wee need" for the next ten years from 2015!.
Change is inevitable Pasco ila hiyo ten years inatoka wapi? Oops...samahani sana, ni mazoea!
Mungu Ibariki Tanzania!.
Why now...what about the last 50 years.
Yeah, I thought so...have a nice day Pasco!
 
Mkuu Mag3, hata mimi ni binadamu, inawekana na mimi pia tayari niko kwenye the same state at an early age!.
We are all humans, no body is perfect!.
Pasco.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…