Mama yake Zitto avamiwa

Mama yake Zitto avamiwa

-Kwanza huyo mtu anayeitwa Sagula yupo Chadema?

-Pili;Mbona umeshatoa hukumu ya ulichoita 'kesi hizi'.Be rattional,argue objectively.

Nawatahadharisha wanaJF wasiokuelewa tu.

Umepanda cheo siku hizi unatumia ka mguu ka kuku badala ya kale ka unga kekundu!!
 
This is just sad. Nimemsoma Dr. Slaa na nimemuelewa. Ni muhimu watu wanaposoma habari zinazohusiana na CDM kusoma kwa umakini mno. Ikumbukwe kuwa CDM ni tishio kubwa zaidi kwa watawala kuelekea 2015 kuliko wakati mwingine wowote. NI kwa sababu hiyo hakuna jambo litakaloachwa kufanyika kama kwa kulifanya kutasaidia kuchafua jina la CDM, kuwagonganisha watu na kwa hakika kupunguza imani ya wananchi.

Viongozi na wanachama wa CDM wanapaswa kuelewa hilo na should never take anything for granted.

It's serious Brother.Keshokutwa utasikia CHADEMA yamtuma Mzee Mwanakijiji kuua viongozi wa CCM ughaibuni.
 
Last edited by a moderator:
Msaky alitaka kuuwawa eti yuko very very close to zitto. Verry very very very close to zito. Mama yake zito naye hivyo sasa zito atapona kweli. Hivi vichaadema viuaji kweli
 
Amekurupushwa kigoma kakimbilia huku jf kuendeleza mashambulizi kwenye familia ya Zitto.
Mkuu lwesye pumzika kama Ben saa8 alivyotulia attempt mbovu za kutoa uhai wa watu utawasakama sana.

Sceptic tank contents....!
 
ukichukulia maungamo ya Sagula katika mambo ya Morogoro na Igunga ambayo Dr Slaa naye anahusika naelekea kukubaliana nawe katika hili... Wanatapatapa!
This is too low and uncalled for.Nilikuambia Rangi zako halisi zinajulikanq

Unamuaibisha sana Dr.Salim Ahmed Salim kama msaidizi wake wa karibu.

Huyo ni Mwanadiplomasia nguli ninayemuheshimu sana ila tabia yako hii unayoionyesha kwenye social networks haiendani na weledi,taaluma ,Umri na heshima ya waliokuzunguka.

My brother,nakushauri uchukue likizo kidogo utoke humu kwenye social networks na unajua jinsi ninavyokuheshimu kwa kiasi flani.

Mimi na wewe tunakubaliana katika UMAJUMUI wa Afrika ambao utajengwa juu ya misingi ya haki na usawa.Human dignity inapewa kipaumbele.Hayo uliyoandika hapo juu ni mzaha kwenye maisha ya mwanadamu na umeingia mtegoni kirahisi.Kuna aliyesema kuna mahakama kubwa kuliko zote ambayo ni court of conscience.

Jifikirie sana na ujipime kulingana na uliyoandika hapo juu kaka Omar.
 

Samahani Dr Slaa, leo ulimtuma Sabula kwenda kwa Mama Shida Salum?[/QUOTE]

Mkuu mbona amejibu hili kuwa hata kuongea hakuongea nae mpaka Dr Slaa alipoona habari gazetini na kumpigia Mama Zitto kujua ukweli wa ile habari?

Mkuu wewe mkongwe humu JF nategemea utakuwa objective kwenye hili!
 
Wanabodi,

Mkisoma majibu ya Dr Slaa huu mjadala ambao binafsi nimeufatilia toka jana maudhui yote na muelekeo wa huu mjadala wote utabadilika!!

Msiseme zaidi tusubiri mama Zitto aikane hii habari au vinginevyo.

Nashangaa malengo ya Bashe na hili gazeti lake, hii habari itatufanya wengine tushangae hawa watu wanafanya siasa kwa propaganda za kijinga kupitiliza!
 
Last edited by a moderator:
Apa kuna kitu kinatengenezwa na ccm cha kuwagombanisha zito na uongozi wa juu wa chadema. Mwigilu mtu mbaya sana tangu nilisikie jina hili mashikioni kwangu Tanzania hapakaliki.
 
Hawa watu walikua sio majambazi wala chochote ispokua walikua wanataka wafikishe ujumbe kwa uyu mama kama walivoagizwa kuwa mtoto wake ana maadui ndani ya chama chake. Hizi ni mbinu za aina nyengine anazozitumia mwigilu kuimaliza chadema kisiasa.
 
It's serious Brother.Keshokutwa utasikia CHADEMA yamtuma Mzee Mwanakijiji kuua viongozi wa CCM ughaibuni.
mi nimesikia lema ana mkono katika mauaji ya mwanafunzi arusha.kwamba ametuma vibaka wafanye mauaji ili alitumie tukio hilo kisiasa,ndo maana aliacha mkutano mbeya ili awe arusha kwa sababu hiyo.je kuna ukweli hapo?
 
Last edited by a moderator:
Kinder,

1) Nadhani, kama umesoma post yangu vizuri, nimesema nimeisikia habari hii Jana baada ya kuisoma kwenye Mtanzania na kwenye Mtandao wa Jamii Forum. Ni logic ya kawaida tu huwezi kuitolea Taarifa jambo usilofahamu. Nimesema Mama Zitto hakumjulisha hata Mwenyekiti wa Chama, sasa Chama kingelifanya muujiza gani?

2) Suala la Dr. Slaa kutaka kumdhuru Zitto, unataka nieleze nini wakati Zitto, mwenyewe ameisha sema na kunukuliwa na vyombo vya habari kuwa "haamini" habari hizo? Akili ya kawaida tu inatosha kukuonyesha kuwa ni upuuzi kungangania tamthilia iliyotokea miezi takriban 8, haijawahi kuripotiwa polisi wala na anayedhaniwa kutaka kuuwa, au na hao wanaojidai ni mashahidi wa kuiona kwa macho yao. Jiulize, kwanini walianza kuitoa stori hiyo kwa nguvu zote baada ya kuingia chama hasimu na Chadema. Ungelisoma filosophia ningelikuambia fanny conclusion by "inference",

3) Habari ya Mama Zitto kusema wahusika aliwaona Mwanza... Si la Chama. Nadhani ustaarabu wa kawaida ni kumwomba Mama Zitto amtaje huyo mtu wa Mwanza kwa jina, aeleze walikutana mahali na katika Mazingira gani. Si swala la Chama wala la Katibu Mkuu. Aidha, Kama alisema ni kada wa Chama, ni jukumu la Mama Zitto kuombwa kuweka hadharani viashiria vilivyomfanya "ahisi" kuwa ni "kada wa Chadema".

Mama Zitto ni mjumbe wa Kamati Kuu, kwa nafasi yake Nina hakika anafahamu au anapaswa kuwafahamu macadam wengi wa Chadema kwa kuwa anashiriki shughuli nyingi za Chadema. Nilivyosema ni kuwa kwa majukumu yangu ya Katibu Mkuu nimefanya uchunguzi wetu wa ndani, na kugundua kuwa hakuna kijiwe kinachojengwa na katika eneo la Tabata. Nimepata mawasiliano yote yaliyokuwa yanafanyika, na baada ya kuzungumza na Mama Zitto na Sabula na viongozi wetu wa Tabata ni dhahiri kulikuwa na hill Chafu ya kuichafua Chadema. Ndio maana nimeingia kwa ID yangu bila maficho kwa kuwa ni jukumu langu la Kikatiba kuwaeleza wanachama wetu, wapenzi wetu na wananchi kwa ujumla.

Mimi sijasema Mama Zitto kavamiwa au hakuvamiwa, ila nilichosema, Chadema Kama Chama haikuhusika kama ilivyotaka kuonyeshwa na baadhi ya watu kwa malengo Yao binafsi. Mwenye macho huambiwi tazama, wairaq tunasema mwenye "busara humtambua mwewe mwenye mimba angali angani..." sina hakika Kama nimetafsiri sahihi, lakini nadhani inaeleweka.

Chadema ni chama makini hakiwezi kuingizwa tu kwenye mitego ya hovyo hovyo. Tunaanza na Mungu, Tunabaki na Mungu na Tutamaliza na Mungu.
 
Tujiulize hizi ID mpya zinazoleta mashambulizi na kukichafua CHADEMA na viongozi wake kwenye thread hii zina malengo gani hasa?
 
Me ninashaka sana na katibu mkUu na mwenyekiti maana hawa hawapendi kukosolewa na pia wao ni miungu watu so kila mmoja wawafuate wao sina imani na chama cha kikanda chama cha ki gaidi juzi wametaja list yao eti ya mawaziri duh 99 percent wakristo alafu wanasema sio wadini nyamayao hawa
 
Tujiulize hizi ID mpya zinazoleta mashambulizi na kukichafua CHADEMA na viongozi wake kwenye thread hii zina malengo gani hasa?

Mkuu Ben, Mafuso na mabasi ya Abood na Bunda yamemwaga watu JF kwa hiyo usishangae.
 
Tujiulize hizi ID mpya zinazoleta mashambulizi na kukichafua CHADEMA na viongozi wake kwenye thread hii zina malengo gani hasa?
Naona boss wako Slaa anajaribu kukusafisha kiaina, wewe ulikuwa wapi wakati wa tukio?
 
Sijui Mh. Zitto amewakosea nini viongozi wenzake wa CHADEMA.

Kumbe kweli CHadema ni magaidi!!!!!!.alafu eti wanasema usalama wa taifa wanatoa watu kucha waongo wakubwa.Tatizo Mfumo kristo haumtaki Zitto japokua Zito ni jembe zuri la chadema.Mchungaji wao wanae mng'ang'ania atakua hatari ktk huo mfumo kuliko ulivyo sasa kwa GAMBA.Pole bro Zito, lakini jua kazi unayo.
 
(Kwa mujibu wa taarifa hizo, tukio hilo lilitokea Ijumaa ya Aprili 19, majira ya saa moja na nusu asubuhi.) Tukio limetokea tangu Tarehe 19 linakuja ripotiwa kwenye vyombo vya habari tarehe 23, Swali la kujiuliza tukio hili ni kubwa kwa nini halikuripotiwa mapema? je ili kuliingiza kisiasa Polisi wametumia nafasi hii kupanga na muhusika aliyevamiwa ili kulibadirisha liwe kisiasa na ndo maana wametumia siku kadhaa kuliandaa hili?
("Nilijua kuwa ninakufa, sikuona haja ya kubishana nao sana, nikamwita dereva wangu, Mtana, alete simu yangu niliyokuwa nikiichaji chumbani na flash ili niwapatie, wakati akielekea kuvichukua aliwaona walivyokuwa wameniwekea bastola, akakimbia moja kwa moja chumbani akajifungia na kuanza kupiga kelele, wakatoka haraka wakakimbia," alisema.)
Kipengere hiki kinanitia shaka kidogo Utendaji kazi wa majambazi hawawezi kumwachia mtu eti aende pekeyake chumbani kuleta simu huku wakimwangalia tu, Halafu anapiga kelele huku Bosi wake akiwa kaelekezewa Bastora wakati kufanya hivyo ni kuhatarisha maisha ya aliyeelekezewa bastora na kwa nini asitumie nafasi hiyo kupiga simu Polisi?.

** Inawezekana tukio limetokea kweli lakini lilivyowasilishwa kwenye vyombo vya habari(MTANZANIA) limeandikwa kwa lengo la kisiasa na ndo maana kuna vipengere vyenye utata ambavyo si raisi kuaminika**
 
Tatizo kubwa la hii habati la mama wa kamanda wetu ni kuhusishwa na siasa na gazeti la mafisadi. Na jinsi ZZK alivyotoa maelezo yake , kwa watu wenye akili maelezo ya ZZK yamezua maswali mengi kuliko majibu.

Naomba kanusho la mama ZZK kupitia kwa ZZK kuwa maelezo ya gazeti la Mtanzania sio yake.

Ila kama ni ya mama ZZK basi kuna matatizo makubwa sana kati ya familia ya ZZK na chama. Na kama sio ya kwake kwa mujibu wa Dr wote tukubali kuwa CCM imetumia mbinu zake tena kutuchanganya. Ila mpaka ZZK au mama yake atakapokuja kuyakataa maelezo yale.

Asante Dr P Slaa kwa maelezo mazuri na yanoyojitosheleza, tutakukumbuka daima kwa utumishi unaotukuka na heshima uliyoipatia chadema kwa kufanya kazi bila tamaa ya cheo.
 
Back
Top Bottom