Mama yake Zitto avamiwa

Join Date : 22nd February 2013
Posts : 1,039
Rep Power : 516
Likes Received81
Likes Given10

Unatisha muda mfupi Post kibao, naona mnalipwa kwa wingi wa posts, poleni sana magamba
Mkuu umeingia shifti ya mchana nini make naona una mori na ari ya juu poa pambana kamanda chama kinatambua uwepo wako mkuu.
 
Du, wewe nadhani unataka kuua watu kwa njaa. Hujui kuna watu wameajiriwa kupitia mitandao kukitetea chama chao
Sijali ni chama gani, lakini politicians wameshindwa siasa za kiungwana. Cha msingi hapa nchi kuendeshwa kwa mtutu hadi watie akili
 
Kweli ukishakula nyama ya mtu utaendelea tu...

Yani pamoja ya kwamba Kubwa la Magaidi limekamatwa bado vijana wake wanaendeleza kazi ?

CHADEMA mtatumaliza...
Muwe mnatumia ganzi siku moja moja
 

Baada ya kutoka hapo polisi , Shida alimpigia simu katibu mkuu wa CHADEMA DR. WILIBROD SLAA na kumueleza juu ya tukio hilo, DR Slaa alimwambia kwamba aende kuripoti katika ofisi yao ya ulinzi na usalama makao makuu ya CHADEMA. Alipoenda ofisi ya ulinzi na usalama alimkuta Naibu mkurugenzi wa ulinzi na usalama aitwaye AHMED SABULA ambaye alimwambia Shida kwamba, wamepata habari juu ya tukio hilo na pia wanazo habari za yeye kupita mikoani kumnadi mwane Zitto Kabwe ili apate uenyekiti wa CHADEMA. Maneno hayo yalimkatisha tamaa, Akaamua kuondoka, lakini alipofika njiani alipigiwa simu na Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe ambaye alimfokea kwanini alikwenda kueleza tukio la kuvamiwa na vijana hapo makao makuu ya CHADEMA. Mama SHIDA shida alikosa la kusema na hatimaye akaanza kuamini kuwa vijana wale walitumwa na Mbowe ili kumtisha au kumdhuru.
 

Toka asubuhi nimekuwa niikisoma uzi huu nikijiuliza itakuwaje tukio litokee ijumaa na gazeti moja tuu la Mtanzania liandike
Lakini huyu Shida Binti Salum mama yake Zitto ameingia rasmi sasa kwenye uzandiki wa kuchafua chama, anasema kada wa chadema likuwa kati ya majambazi, hamtaji kwa jina, mara anachanganya story kuwa eti ni vijana wa tabata walimuomba fedha za kukarabati ofisi yao mara anasema alimuona Tanga hadithi haileti maana hii, lakini pia anasema aliongea na Dr Slaa , hapo mwenye akili unajua anaunganisha story loo,aliyemuelekeza aongee na Sabula ambaye alimuuliza kwa nini anazunguka nchi nzima kumnadi mwanawe uraisi na uenyekiti hapo tayari kachachua mchuuzi yaani ndio maana tuna uliza huko TISS tuna watu wenye vichwa vya panzi hawawezi kutunga mtungo wa propaganda ambazo wananchi hawawezi kuhisi kitu na kuwaunganisha
Sasa Mama yake zitto anataka kusema Sabula ndio alikuwa jambazi
huyo kijana Ahmed anashughuli gani za chama ambazo zitawaaminisha wananchi kuwa kweli ni kada wa chadema aliyetumwa
Manake TISS wameshindwa flat kabisa kuunganisha Lwakatare na Ludovick ili jamii iwaamini matokeo imekuwa aibu kwa TISS
Nyie TISS ,Zitto na Mama yako sikilizeni wananchi tutalinda chadema kwa nguvu zetu zote ,hizi propaganda zenu zitakula kwenu ,sasa hivi nikuwaeleza wananchi jinsi TISS walivyo wazembe na wanavyowabeba MACCM
 
Kweli ukishakula nyama ya mtu utaendelea tu...

Yani pamoja ya kwamba Kubwa la Magaidi limekamatwa bado vijana wake wanaendeleza kazi ?

CHADEMA mtatumaliza...
Muwe mnatumia ganzi siku moja moja
Kaka nchi hii tuna Gaidi kigagula mmoja tuu Jakaya Kikwete na mwanawe Ridhiwani unajua Dola bilioni moja na nusu za wachina zimeshatoka, mama yako atafufuka kuja kuzilipa
 
Siku akitekwa mama yako ndo utajia CDM ni Mafia , wewe si ulikuwa unajidai kuwatetea?

mimi husema kile ninachokiamini ni sahihi pasipo kufungwa na itikadi za chama chochote cha siasa.
atakayefanya vizuri nitasema bila woga na atakayefanya vibaya pia nitasema bila woga.
sijui wewe ulitaka nifanye nini.
 
Shida Binti Salum Mama yake Zitto ni mwanamke ambaye mimi nilimuheshimu sana kama wanawake majasiri wenye utashi wa kupenda nchi yao lakini Shida na mwanawe Zitto looh kumbe ni magaidi wa kidemokrasia,kitu gani wanacholingia ni hao TISS hata kama Shida umenunuliwa nyumba dubai kama watu mitaani wanavyosema lakini usijivue nguo tafadhali hili dili limekuchafua forever dear
 

ingekuwa mama yako amefanyiwa haya ungeandika huu ujinga wako hapa???? tuwe na huruma ya kibinadamu hata kama tuna uroho wa madaraka kama mbwa mwenye njaa
 

asiyekujua hawezi kukuthamini.. natamani zitto ayaone haya maneno yako ya kigaidi, kinyama na yaliyojaa uroho...
 
Huyu mama anasema aliwahi kuvamiwa akiwa mwanza,halafu swali lingine linalonifanya nifikkri ni kwa nini mwenyekiti alimfokea yule mama alipokwenda kupeleka malalamiko ya kuvamiwa makao makuu ya chma.
Hadithi upande moja unaiamini baada ya gazeti la Uhuru,Habari leo,Jambo leo kudharaulika na wananchi ,baada ya kuona habari haziuziki,leo Mtanzania Jumatano ndio umekuwa mdomo wa Zitto kabwe,Zitto kabwe mission gani alifanya akashinda,sasa anamwingiza na mama yake sawa tutaona mwisho wake
 
Kaka nchi hii tuna Gaidi kigagula mmoja tuu Jakaya Kikwete na mwanawe Ridhiwani unajua Dola bilioni moja na nusu za wachina zimeshatoka, mama yako atafufuka kuja kuzilipa

hivi wewe ni binadamu wa kawaida au ni shetani.....gaidi ni lwakatare na ludovick nadhani na wewe ni miongoni mwao kutokana na maneno yako haya
 
Mama Zitto mweleka kaanguka chini puu nimdharau sana huyu mama unajua kama ulikuwa na heshima na mtu alafu akageuka kiroboto unababua tuu
 
Habari yenyewe imekaa kiudaku mno! Mtanzania ni bora wautumie muda huu kumjenga mgombea wao Lowasa kuliko kuandika habari za kiudaku!
 
Duh Zitto tena kuna kitu kinaelekea kuwa wazi hapa wataumbuka watu hapa
 
Huyu mama na mwanae wote Chama Cha Mafisadi tu, sijui wanangoja nini huku?! hawa chokochoko hawakuanza leo!! timua tu!!

Enzi zao zilishaisha walitikisa bwana enzi hizoooo sasa hivi propaganda zao wapelekee kuleeeeeeeeeeeeeeeeeeeee ,wameishiwa hao wanatumika kama manamba
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…