Kutokana na habari iliyoandikwa na gazeti la Mtanzania la leo kuhusumajambazi kumvamia Mama Shida Salum na maelezo yake ambayo ameyatoa ni kamaifuatavyo;
i. Lengo kuu ni kuwa Polisi watamkamata Hemed Sabula, ambaye CHADEMA walimtumia kumrekodi Afisa usalama wa Taifa ambaye alikuwaanaanda ushahidi feki wa kumhusisha Lwakatare na ugaidi ……na tayari Polisiwameelekezwa kufanya hivyo kesho .
ii. Usalama wa Taifa , wameamua kulipiza kisasi kwaCHADEMA baada ya kurekodiwa na wanataka kujua walirekodi nini na hichowalichorekodi kipo wapi, hivyo Sabula atateswa sana ili aseme aliwezajekuwarekodi
iii. Zoka Jack , alifanya mawasiliano na ambaowalihusika katika kuandaa na kuandika habari hiyo na mwandishi alikuwaakielekezwa kila kitu, na ndio maana hajawahoji polisi kama suala hilo likokwenye uchungiuzi ama laa , na leo au kesho polisi watatoa tamko kuhusiana nasuala hilo na kuwa wanaendelea na uchunguzi na watamkamata Sabula, swaliatakaloulizwa ni kuwa mbona yeye aliuliza swali kama walivyofanya majambazi haowa kutungwa
iv. Sabula mawasiliano yake ya simu yamefanyiwa kazina baahati mbaya ameonekana kuwa hakumuuliza mama Zitto swali hilo la kuwaanatoa wapi fedha za kuzunguka nchi nzima ,ila alimuuliza juu ya kamaanawafahamu watu hao ama kama alishawahi kuwaona naye akamwambia atarudi kwakebaadae na hakuna ushahidi wa kimawasiliano kama alirejea tena kwake na badalayake akaenda kuongea na vyobo vya habari.
v. Kuhusu kwamba kijana mmoja ni mtu kutoka Tanga ,yupo kijana mmoja anaandaliwa anaitwa Khalid atakamatwa kwa hatua za baadae ,na huyu tayari ameshaandaliwa kimkakati.
Nawashauri CHADEMA wafanye yafuatayo kwa hatua za sasa;
a. Hakikisheni kuwa kuanzia leo mnaweka mawakili wenu kwaajili ya kuhakikisha kuwa Sabula haendi polisi peke yake ili asiteswe
b. Hakikishenikuwa mikanda mliyowarekodi watu wa usalama inawekwa mahali salama kwaniinatafutwa kwa gharama kubwa sana ili iweze kuandaliwa majibu.
c. Wapo watuambao mpaka sasa wanaweza kupoteza kazi kutokana na sakata hili , jiandaenikuwatetea …..
Naishia hapo kwa leo.