Mama yake Zitto avamiwa

Mama yake Zitto avamiwa

Kukata hii longolongo Jeshi lichukue nchi kama miaka 15 hivi labda mtatia akili kwani siasa za kistaarabu hamziwezi
 
Kukata hii longolongo Jeshi lichukue nchi kama miaka 15 hivi labda mtatia akili kwani siasa za kistaarabu hamziwezi
Du, wewe nadhani unataka kuua watu kwa njaa. Hujui kuna watu wameajiriwa kupitia mitandao kukitetea chama chao
 
Hapa ninanusa deflection ya mambo fulani.....

Sasa mama yetu anakubali vipi kutoa msaada wa fedha kwa mtu so called mwanachama wa CDM kusaidia ujenzi bila yeye kutafuta undani wa huyo mwananchama?? Yaani Mama yetu pamoja na nafasi yake ndani ya chama anaweza vipi kukubali kutoa hela hata bila kuwasiliana na uongozi wa ofisi ambayo ilikuwa inakusudiwa kuwezeshwa? Kusaidia chama si kitu kibaya (Don't give me wrong), ila mtiririko wa utoaji msaada huo unajenga hisia fulani.

Aliyepiga simu alijitambulisha mwananchama wa CDM Tabata lakini mama pia anadai kuwa "alikubali kuwasaidia wale vijana" ukarabati wa ofisi ya TAWI. Hilo tawi halina uongozi au kamati ya ujenzi/maendeleo wa tawi? Yaani conversation(s) ya kwenye simu tu unamwamini mtu kuja nyumbani kwako bila verification yoyote kisa ni mwanachama wa CDM?? Usalama wenu viongozi mbona mnauachia uchi hivi?

Do viongozi need seminars jinsi ya ku-interact/pamoja na kujilinda na jamii especially wakati misaada ya ujenzi wa chama ikihitajika? Kwa mwendo huu mbona wengi wataibiwa kwa kutumia jina la chama pale watumiwapo hata text message kutoa misaada thru M-Pesa kusaidia kazi ya chama. Ingechukuwa muda gani kutafuta ukweli kuhusu huo msaada ulioombwa kwa niaba ya CDM Tabata?


Hata hivyo nampongeza kwa ushujaa wake kwa kuweza kukimbilia chumbani maana hawa watu si ajabu waliamini kuwa mama hasingepata ujasiri wa kuwaponyoka kutokana na disabilities.

Polisi na TCRA fanyeni kazi sasa, mama anayo namba ya simu na ninaamini kampuni ya simu mtakuwa na audio file(s) za maongezi hayo. Vile vile naamini jamii nzima (si viongozi pekee) nayo inapaswa kufundishwa jinsi ya kujilinda na matapeli wanaotumia njia yoyote especially digital devices kujinufaisha.
 
1. Kama mweli walihitaji Laptop, hivi wasingeipata bila hata ya kutumia Bastora?2. Gaidi hata siku moja hakupi nafasi ya kumwita mtu mwingine, ni kimya kimya unawekewa mtutu na wewe mwenyewe pamoja nao unatangua chumbani kuonyesha na kutoa wananchokitaka.3. Kwa nini mlizi aache gate wazi? Tumia akili zaidi kutafakari sentensi moja moja1. Dereva ni shahidi kwa pili kwamba alimwona huyo kada wa chama alitoa bastora2. Tayari Kaimu Mkurungezi wa Usalama wa Taifa yumo kwenye kesi hii3. Mlinzi naye pia ni shahidi wa tatu katika gwalide la utambuzi4. Yule kada wa CDM aliyetambuliwa lazima atakuwa mwananchama kweli na atasema ukweli kwamba alitumwa na Kaimu Mkurungezi wa ulinzi na usalama.Kesi ni ya Ughaidi - inakituhumu chama cha demokrasia na maendeleo. inaweza kuunganihswa na ile ya kwanza ili kupata vitu kamili.Yetu macho -- Tanzania oyeeeeeeeeee!!!My Take: Kulikuwa hakuna haja ya kuanzisha vyama vingi kama kweli hatukuwa na nia ya dhati ya kushindana kwa hoja:
MKUU UNGANISHA HAYO YAKO NA YA MKUU BACELONA HAPA CHINI UONE, HIZO DOTS ZINAVYOENDANA.. YAANI SASA HIVI USALAMA WA TAIFA NI SISIEMU PURE (TENA WANAPOKEA MAELEKEZO YA NAPE, RAGE, MWIGURU NA WASIRA BILA KUMSAHAU NCHIMBI) By bacelona Kutokana na habari iliyoandikwa na gazeti la Mtanzania la leo kuhusumajambazi kumvamia Mama Shida Salum na maelezo yake ambayo ameyatoa ni kamaifuatavyo;i. Lengo kuu ni kuwa Polisi watamkamata Hemed Sabula, ambaye CHADEMA walimtumia kumrekodi Afisa usalama wa Taifa ambaye alikuwaanaanda ushahidi feki wa kumhusisha Lwakatare na ugaidi ……na tayari Polisiwameelekezwa kufanya hivyo kesho .ii. Usalama wa Taifa , wameamua kulipiza kisasi kwaCHADEMA baada ya kurekodiwa na wanataka kujua walirekodi nini na hichowalichorekodi kipo wapi, hivyo Sabula atateswa sana ili aseme aliwezajekuwarekodi iii. Zoka Jack , alifanya mawasiliano na ambaowalihusika katika kuandaa na kuandika habari hiyo na mwandishi alikuwaakielekezwa kila kitu, na ndio maana hajawahoji polisi kama suala hilo likokwenye uchungiuzi ama laa , na leo au kesho polisi watatoa tamko kuhusiana nasuala hilo na kuwa wanaendelea na uchunguzi na watamkamata Sabula, swaliatakaloulizwa ni kuwa mbona yeye aliuliza swali kama walivyofanya majambazi haowa kutungwa iv. Sabula mawasiliano yake ya simu yamefanyiwa kazina baahati mbaya ameonekana kuwa hakumuuliza mama Zitto swali hilo la kuwaanatoa wapi fedha za kuzunguka nchi nzima ,ila alimuuliza juu ya kamaanawafahamu watu hao ama kama alishawahi kuwaona naye akamwambia atarudi kwakebaadae na hakuna ushahidi wa kimawasiliano kama alirejea tena kwake na badalayake akaenda kuongea na vyobo vya habari.v. Kuhusu kwamba kijana mmoja ni mtu kutoka Tanga ,yupo kijana mmoja anaandaliwa anaitwa Khalid atakamatwa kwa hatua za baadae ,na huyu tayari ameshaandaliwa kimkakati.Nawashauri CHADEMA wafanye yafuatayo kwa hatua za sasa;a. Hakikisheni kuwa kuanzia leo mnaweka mawakili wenu kwaajili ya kuhakikisha kuwa Sabula haendi polisi peke yake ili asitesweb. Hakikishenikuwa mikanda mliyowarekodi watu wa usalama inawekwa mahali salama kwaniinatafutwa kwa gharama kubwa sana ili iweze kuandaliwa majibu.c. Wapo watuambao mpaka sasa wanaweza kupoteza kazi kutokana na sakata hili , jiandaenikuwatetea …..Naishia hapo kwa leo.
 
Mkuu hutayasikia tena baada ya 2015. Haya ni mateke ya mwisho ya CCM inayokufa na vibaraka wake ndani ya CDM.

nadhani umekosea ni mateke ya cdm kufa sasa kabla ya 2015 kama alivyo sema mzee wassira
 
Baada ya kutoka hapo polisi , Shida alimpigia simu katibu mkuu wa CHADEMA DR. WILIBROD SLAA na kumueleza juu ya tukio hilo, DR Slaa alimwambia kwamba aende kuripoti katika ofisi yao ya ulinzi na usalama makao makuu ya CHADEMA. Alipoenda ofisi ya ulinzi na usalama alimkuta Naibu mkurugenzi wa ulinzi na usalama aitwaye AHMED SABULA ambaye alimwambia Shida kwamba, wamepata habari juu ya tukio hilo na pia wanazo habari za yeye kupita mikoani kumnadi mwane Zitto Kabwe ili apate uenyekiti wa CHADEMA. Maneno hayo yalimkatisha tamaa, Akaamua kuondoka, lakini alipofika njiani alipigiwa simu na Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe ambaye alimfokea kwanini alikwenda kueleza tukio la kuvamiwa na vijana hapo makao makuu ya CHADEMA. Mama SHIDA shida alikosa la kusema na hatimaye akaanza kuamini kuwa vijana wale walitumwa na Mbowe ili kumtisha au kumdhuru.
Khaa!! hivi story kama hizi huwa mnaprove vipi?? Maneno maneno maneno tuuuuu bila ushahidi
 
Sijui Mh. Zitto amewakosea nini viongozi wenzake wa CHADEMA.

SUMU huua na huharibu, thread yako inaonyesha ni jinsi gani unafikiri kwa kutumia vidole. Mh.ZZK ameshariweka wazi kuwa tukio la mama yake kunusurika kuibiwa lichukuliwe kama tukio la kawaida linaloweza kumkuta mtanzania yoyote wa kawaida.

Nichukue nafasi hii kumpongeza mh.ZZK kwa hakika ana majibu yanayoonyesha ukomavu wa kisiasa wa hali ya juu kabisa. huyu ndiyo aina ya wanasiasa ambao TZ inawahitaji kuja kuingoza Tanzania yenye conflicting interests. hakika zzk umeonyesha kuwa uko tayali kuchukua mamlaka ya juu na kati na una uwezo wa kuyasimamia majukumu hayo na kuipeperusha vyema bendere ya TZ.

Tukio lolote la jinai halipaswi kuchukuliwa kiwepesi wepesi tu na kutoa judgement, taratibu zifuatwe na hatua zichukuliwe na hata zikibainisha kuwa watuhumiwa ni wanachama wa CDM bado hakuifanyi CDM iwe ndio mastermind wa tukio hilo. ni ukweli ulio wazi kuwa ndani ya CCM wapo vibaka,wezi,majambazi miongoni mwa wanachama wao kama ilivyo kwa CDM na vyama vingine vya siasa.Hivyo hili la mwanachama mmoja mmoja kuwa mtuhumiwa wa tukio fulani halina nafasi ktk kukihusisha chama fulani kwenye tukio husika.
 
Mama mzazi wa Naibu katibu mkuu wa CHADEMA Zitto Kabwe, amenusurika kutekwa. Waliomvamia wamemtishia kumuua huku wakimtaka awape laptop,simu na mawasiliano yake mengine...
Ngoja nilale upande upande nisome gazeti lako.
 
MKUU UNGANISHA HAYO YAKO NA YA MKUU BACELONA HAPA CHINI UONE, HIZO DOTS ZINAVYOENDANA.. YAANI SASA HIVI USALAMA WA TAIFA NI SISIEMU PURE (TENA WANAPOKEA MAELEKEZO YA NAPE, RAGE, MWIGURU NA WASIRA BILA KUMSAHAU NCHIMBI) By bacelona Kutokana na habari iliyoandikwa na gazeti la Mtanzania la leo kuhusumajambazi kumvamia Mama Shida Salum na maelezo yake ambayo ameyatoa ni kamaifuatavyo;i. Lengo kuu ni kuwa Polisi watamkamata Hemed Sabula, ambaye CHADEMA walimtumia kumrekodi Afisa usalama wa Taifa ambaye alikuwaanaanda ushahidi feki wa kumhusisha Lwakatare na ugaidi ……na tayari Polisiwameelekezwa kufanya hivyo kesho .ii. Usalama wa Taifa , wameamua kulipiza kisasi kwaCHADEMA baada ya kurekodiwa na wanataka kujua walirekodi nini na hichowalichorekodi kipo wapi, hivyo Sabula atateswa sana ili aseme aliwezajekuwarekodi iii. Zoka Jack , alifanya mawasiliano na ambaowalihusika katika kuandaa na kuandika habari hiyo na mwandishi alikuwaakielekezwa kila kitu, na ndio maana hajawahoji polisi kama suala hilo likokwenye uchungiuzi ama laa , na leo au kesho polisi watatoa tamko kuhusiana nasuala hilo na kuwa wanaendelea na uchunguzi na watamkamata Sabula, swaliatakaloulizwa ni kuwa mbona yeye aliuliza swali kama walivyofanya majambazi haowa kutungwa iv. Sabula mawasiliano yake ya simu yamefanyiwa kazina baahati mbaya ameonekana kuwa hakumuuliza mama Zitto swali hilo la kuwaanatoa wapi fedha za kuzunguka nchi nzima ,ila alimuuliza juu ya kamaanawafahamu watu hao ama kama alishawahi kuwaona naye akamwambia atarudi kwakebaadae na hakuna ushahidi wa kimawasiliano kama alirejea tena kwake na badalayake akaenda kuongea na vyobo vya habari.v. Kuhusu kwamba kijana mmoja ni mtu kutoka Tanga ,yupo kijana mmoja anaandaliwa anaitwa Khalid atakamatwa kwa hatua za baadae ,na huyu tayari ameshaandaliwa kimkakati.Nawashauri CHADEMA wafanye yafuatayo kwa hatua za sasa;a. Hakikisheni kuwa kuanzia leo mnaweka mawakili wenu kwaajili ya kuhakikisha kuwa Sabula haendi polisi peke yake ili asitesweb. Hakikishenikuwa mikanda mliyowarekodi watu wa usalama inawekwa mahali salama kwaniinatafutwa kwa gharama kubwa sana ili iweze kuandaliwa majibu.c. Wapo watuambao mpaka sasa wanaweza kupoteza kazi kutokana na sakata hili , jiandaenikuwatetea …..Naishia hapo kwa leo.
Usalama wa taifa inakuwaje na suala la kutekwa na mama yake zito
 
mungu wa ugaidi


hahaaaa binti leo umetokelezea, naona utakula kama laki hivi kwa kuchangia naona kila page unachangia kama mara kumi hivi yaaani wewe ni kurefresh tu page, maana unabadilisha tu pc hapo lumumba na kucheng ID, mara uwe wingu, mara taswira, mara majebere, mara sumu, mara ujiite m23.... hongera binti, tumika tumika mara ya mwisho hivyo si unajua hakuna marefu yasiyo na mwisho, na hauwezi kuifikia 3 bila moja na mbili kuzipita..... serukamba wewe

EBU BINTI NIJIBU,
1. ILE SINGO YA MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA ILIKU NA MAANA GANI HIVI BADO MNAKUMBUSHANA HPO LUMUMBA KUHUSU KUITIMIZA??
2. KWA AKILI ZAKO UNADHANI CDM IKIWA KAMA CUF NDIYO ZILE AHADI 68 ZA 2010 ZITATIMIA AU NDIO WATZ WATAZIDI KUWAPENDA??

3. HIVI KOLIMBA, NYERERE, NA KUWEKEWA SUMU KWA MWAKYEMBE NA MWANDOSYA, KUTESWA KWA ULIMBOKA NI CDM NA KUUWA KWA YULE PROF WA UDSM NI CHADEMA SIYO???
4. SO CHADEMA IKIFA NDIO MTALETA MABILIONI YA USWIS TZ, YASAIDIE KUFUFUA VIWANDA MLIVYOUA NCHI NZIMA NA RELI YETU


STARABIKA BINTI, TUMIA AKILI YAKO JAPO 0.000005%...

NIKUSAIDIE TU, ADUI YENU SI UPINZANI, BALI ADUI YENU NI AHADI HEWA MANAZOTOA KWA WATZ, ZITEKELEZENI MUONE KAMA KUNA MATITIZO

ENDELEA KUTUMIKA....
 
Haya yote yatafahamika tu. Solidarity Forever wana-Chadema. Pole mama Zitto na hongera kamanda Zitto kwa kauli mujarabu.
 
Hivi wewe Slaa mbona unaroho ya namna hii? Zitto amekukosea nini mpaka kufikia kutaka kumteka mama yake? Acha ubaya mzee, hata kama ni kutaka madaraka lakini hatujafika huko.

Pole sana mama, mungu atakulinda.

Hayo maswali muulize mwigulu nchemba.
 
Usalama wa taifa inakuwaje na suala la kutekwa na mama yake zito

usalama wa taifa inakuwaje na kuwekewa sumu kwa mwakyembe na Mwandosya, au Rama & Jack Zoka kumteka Dr. Ulimboka kwani wana maslahi gani na hawa watu... USIKIMBIE NIJIBU

Note: Usisahu kutupa mrejesho ahadi 69 za 2010 mlizo ahidi mmetimiza ngapi mpaka sasa tunakumbuka ujue
AHADI - ALIITOA AKIWA WAPI...




1. Kujenga reli mpya kutoka Dar es Salaam mpaka mikoa ya Kanda ya ziwa - Nzega, Tabora
2. Mkoa wa Tanga kuwa Jiji la Viwanda - Tanga mjini
3. Tabora kutumia maji ya Ziwa Victoria - Igunga
4. Kulipa madeni ya chama cha Ushirika mkoa wa Shinyanga (SHIRECU) - Shinyanga
5. Kumaliza migogoro ya Ardhi nchini - Dodoma
6. Wakulima kuacha kutumia jembe la mkono - Dodoma mjini
7. Kuwapatia trekta wakulima - Kata ya Mrijo, Dodoma
8. Wananchi kutoondolewa kwenye Ranchi ya Misenyi - Kagera
9. Kujenga Uwanja wa Ndege Misenyi - Kagera
10. Kupanua Uwanja wa Ndege Bukoba - Bukoba Mjini
11. Kujenga uwanja wa ndege mkubwa Kigoma - Kigoma Mjini
12. Mtukula kupatiwa umeme kutoka Uganda - Kagera
13. Mikoa ya Kagera, Kigoma, Lindi, Rukwa na Ruvuma kuunganishwa katika gridi ya taifa ya umeme - Kagera
14. Kuimarisha Takukuru kwa miaka mitatu - Kagera
15. Hukumu kwa waliopatikana na hati ya kuua albino - Mbeya
16. Kununua meli kubwa kuliko MV Bukoba - Kagera
17. Kuanzisha benki ndogondogo kwa ajili ya wajasiriamali
18. Serikali kuvisaidia vyama vya ushirika - Mwanza
19. Kuimarisha usalama Ziwa Victoria na Ziwa Tanganyika kwa kupeleka kikosi maalum chenye vifaa kupambana na wahalifu - Mwanza
20. Wilaya ya Geita kuwa hadhi ya mkoa Januari mwakani - Geita
21. Kulinda muungano kwa nguvu zote - Pemba
22. Kuwajengea nyumba waathirika wa mafuriko Kilosa - Morogoro
23. Kununua meli mpya kubwa Ziwa Nyasa - Mbeya mjini
24. Kujenga bandari Kasanga – Rukwa
25. Kumaliza tatizo la walimu miaka mitano ijayo - Songea
26. Kufufua mgodi wa makaa ya mawe Kiwira - Mbeya
27. Kuzuia hatari ya kisiwa cha Pangani kuzama - Tanga
28. Kununua bajaji 400 kwa ajili ya kubeba wajawazito hasa vijijini - Iringa
29. Kujenga barabara yenye kiwango cha lami kutoka Same mpaka Kisiwani – Kihurio na kuiunganisha na barabara kuu ya Moshi - Dar es salaam - Same mkoani Kilimanjaro
30. Kumaliza tatizo la maji katika wilaya ya Same - Same Mjini
31. Kuboresha barabara za Igunga - Tabora
32. Kusambaza walimu 16,000 katika shule za sekondari zenye upungufu makubwa wa walimu - Kisesa Magu
33. Kununua vyandarua viwili kwa kila kaya - Mbeya Mjini
34. Kuzipandisha hadhi hospitali maalumu saba nchini kuwa za rufaa ili kuipunguzia mzigo Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MHN) - Hydom Manyara
35. Kulinda amani nchini kwa kuzuia chokochoko za kidini, kikabila na kisiasa - Musoma
36. Kulinda haki za walemavu - Makete
37. Kujenga baabara ya Njombe - Makete kwa kiwango cha lami,urefu wa kilomita 109 - Iringa mjini
38. Kujenga barabara Musoma – Mto wa Mbu Arusha - Arusha
39. Kuanzisha jimbo la Ulyankulu- Shinyanga Mjini
40. Kujenga barabara ya lami Manyoni-Kigoma – Kaliua,Tabora
41. Kukarabati barabara ya Arusha Moshi - Arusha Mjini
42. Kuboresha barabara ya Handeni, Kondoa, mpaka Singida - Dodoma
43. Kuwafidia wanakijiji ng'ombe waliopotea wakati wa ukame mwaka 2009 - Longido
44. Vijiji vyote vilivyoko kilomita 15 kutoka kwenye bomba kuu la mradi mkuu wa maji wa Ziwa Victoria - Shinyanga-Kahama kuunganishiwa maji - Shinyanga
45. Tatizo la umeme kufikia kikomo Novemba mwaka huu mkoani Arusha – Arusha mjini
46. Kukopesha wavuvi zana za kilimo - Busekera, Wilaya ya Musoma
47. Kuwapatia maji wakazi wa Wilaya ya Longido - Longido
48. Kujenga barabara ya lami kupitia pembezoni mwa Hifadhi ya Taifa ya Seregenti – Ngorongoro
49. Utekelezaji wa mpango wa maendeleo ya kilimo kuwasaidia wafugaji kuweza kupata na kutunza mifugo yao vizuri - Mbulu mkoani Manyara
50. Kusambaza maji nchi nzima - Babati vijijini
51. Kusambaza umeme, utoaji wa huduma za afya, na uboreshaji wa kilimo cha umwagiliaji na utoaji ruzuku kwa wakulima. mwaka 2010-2015 - Babati vijijini
52. Kuongeza mara tatu idadi ya wananchi wanaonufaika na ruzuku ya pembejeo za kilimo kwa mfumo wa vocha - Iringa
53. Kuhakikisha Isimani inapata maji ya uhakika - Iringa
54. Kuiwekea lami barabara inayokwenda katika Hifadhi ya Taifa ya Ruaha, ambayo ndiyo hifadhi kubwa kuliko zote Tanzania - Iringa
55. Kulinda usalama wa wananchi kwa ujumla ili kudumisha amani na sifa ya nchi -Ifunda
56. Kutokomeza malaria 2015 - Bunda, mkoa wa Mara
57. Kuwapa wanawake nafasi zaidi - Kilolo, Iringa
58. Ahadi kuisadia Zanzibar kuendeleza miradi mbalimbali ya kijamii - Kibandamaiti Mjini Zanzibar
59. Kuipandisha hadhi hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar kuwa ya rufaa - Kibandamaiti mjini Zanzibar
60. Kuisaidia Zanzibar kila panapohitajika msaada - Kibandamaiti
61. Serikali kujenga upya bandari ya Mbambabay - Ruvuma
62. Ununuzi wa Meli mpya yenye uwezo wa kubeba tani 400 - Mbambabay Ruvuma
63. kufufua chama kikuu cha ushirika cha wakulima wa Mbinga (MBICU) – Ruvuma
64. Ahadi Rais wa Marekani Barack Obama kuimwagia misaada Tanzania – Ruvuma
65. Ahadi hakutakuwa na umwagaji wa damu baada ya uchaguzi-Dar es Salaam
66. Mtwara kuwa mji wa Viwanda – Mtwara
67. Ahadi ujenzi wa kwanda cha dawa ya kuua viluilui vya mbu - Kibaha
68. Hospitali ya Tumbi kuwa ya mkoa - Kibaha
69. Halmashauri ya manispaa ya Kibaha kutenga eneo maalumu la viwanda - Kibaha
 
Back
Top Bottom