Nyumba na gari vitamsaidia nini wakati atakua keshabeba laana, dhambi na mikosi ya kutosha kwa kulala na huyo mwanamke?
Riyan usimuangalie huyo mama kama yeye angalia msukumo wa hiyo roho ya kukutumikisha ulio ndani yake unaenda kutengeneza nini kwenye maisha yako
UFUNUO 2: 13; 19-22
Napajua ukaapo, ndipo penye kiti cha enzi cha Shetani; nawe walishika sana jina langu, wala hukuikana imani yangu, hata katika siku za Antipa shahidi wangu, mwaminifu wangu, aliyeuawa kati yenu, hapo akaapo Shetani.
Nayajua matendo yako na upendo na imani na huduma na subira yako; tena kwamba matendo yako ya mwisho yamezidi yale ya kwanza.
Lakini nina neno juu yako, ya kwamba wamridhia yule mwanamke Yezebeli, yeye ajiitaye nabii na kuwafundisha watumishi wangu na kuwapoteza, ili wazini na kula vitu vilivyotolewa sadaka kwa sanamu.
Nami nimempa muda ili atubu, wala hataki kuutubia uzinzi wake.
Tazama, nitamtupa juu ya kitanda, na hao wazinio pamoja naye, wapate dhiki kubwa wasipotubia matendo yake;