Huu ni ushamba wa mapenzi au mimi ndiye siujui upendo?

Huu ni ushamba wa mapenzi au mimi ndiye siujui upendo?

Mjusi Sharobalo

JF-Expert Member
Joined
Sep 4, 2025
Posts
8,306
Reaction score
14,630
Wakuu salamu kwenu nyote.

Mwaka jana nikiwa eneo X jijini Dsm, nilipata Mshangazi umenizidi umri wa miaka kama 6 na watoto wawili. Ukweli ananipenda sana na pindi zingine kunipiga sapoti ya kifedha katika mishe zangu zinapokwama. Sasa mwaka huu tangu trh 6 Jan nilihama hilo eneo na kuhamia eneo Z mbali kidogo lakini ni hapahapa Dsm. Changamoto iliyopo ni kwamba, huku nimekuwa bize zaidi na harakati mchana kutwa.

Pia mawasiliano na watu nimepunguza sababu ya ugeni wa mazingira. Mara nyingi mkombozi wangu ni JF kuniondolea upweke. Sasa mshangazi amekuwa ni kero hasa mida ya usiku ambapo nahitaji kutulia na JF kuondoa uchovu. Yeye mida hiyo anataka apige simu tuongee hata kama hana jambo la maana la kuzungumza na mimi.

Kiukweli hii hali inanichukiza na ukimueleza uhalisia ni mgumu kuelewa na maneno kibao. Na mimi kumzingua sihitaji maana nipo kimkakati zaidi. Vocha, marupurupu na mazaga mengine kuna muda nasahau hadi bei yake, maana huwa nashitukia mzigo tu umetumwa. Wakuu kumtema sihitaji na pia kero nimechoka
 
Anakulipa, hivyo ni lazima uumpe huduma anayotaka. Kama hutaki kutoa huduma basi usichukue malipo anayo kulipa.

Kimsingi wewe umeolewa, hivyo timiza wajibu wako kwa mumeo. Kama hutaki achana naye.
 
Anakulipa, hivyo ni lazima uumpe huduma anayotaka. Kama hutaki kutoa huduma basi usichukue malipo anayo kulipa.

Kimsingi wewe umeolewa, hivyo timiza wajibu wako kwa mumeo. Kama hutaki achana naye.
Kwahiyo siku hizi sisi vijana wa hovyo tunaolewa na mishangazi si ndio maana yake au umenitusi mkuu?
 
Kwahiyo siku hizi sisi vijana wa hovyo tunaolewa na mishangazi si ndio maana yake au umenitusi mkuu?
Ndo maana yake. Wewe si unahudumiwa. Ukihudumiwa na wewe unatoa huduma.

Imagine wewe ndo ungekuwa una muhudumia mwanamke halafu anakuletea mapozi hata kuongea na wewe hataki eti yuko busy. Ungejisikiaje?
 
Mambo ni mengi muda mchache ajifunze uvumilivu, mimi sina muda wa kumchit ila siwezi kupoteza muda kuwasiliana nae masaa 24 nahitaji kujimwaya kwa uhuru JF.
 
Back
Top Bottom