Mama Uwoya amkana Dogo Janja, asema haitambui ndoa yao na mwanae ni mjane

real G

JF-Expert Member
Feb 7, 2013
5,227
5,287
Mama mzazi wa muigizaji wa filamu hapa nchini, Irene Uwoya amefunguka na kueleza kuwa hamtambui mume wa sasa wa mwanaye, Dogo Janja na anachokijua yeye ni kuwa mume wa ndoa wa mwanaye amefariki mwaka jana.

Mama Uwoya ameongeza kuwa anachokifahamu yeye mpaka sasa mwanaye ni mjane, kwani aliyekuwa mume wake, Ndikumana amefariki dunia, na kabla ya hapo walikuwa wana ugomvi tu ila hawakuwahi kuachana.

Mama huyo aliendelea kueleza kuwa mwanaye, Irene uwoya, alifunga ndoa ya kanisani na aliyekuwa muewe, marehemu Ndikumana, ambaye walijaliwa kupata mtoto mmoja wa kiume na walikuwa hawajaachana lakini walikuwa katika mgogoro ambao walishindwa kuutatua mpaka mwanasoka huyo alipopatwa na umauti.

“Ngoja nikwambie hakuna ndoa ambayo wazazi hawashirikishwi, ndoa yoyote lazima wazazi wajue na washiriki. Ninachojua kuwa irene ni mjane, mumewe ambae sisi tunamjua ndo huyo ameshafariki. Ninachojua mimi ni kuwa swala la ndoa lazima watu wazazi washirikishwe kuanzia mwanzo hadi mwisho,” alisema mama Uwoya.

Hata hivyo mama huyo anasema kwa kuwa kama Irene ni mtu mzima, basi anajua kitu anachofanya, hivyo hawawezi kumzuia na kumkataza. Lakini kitu cha kujua ni kwamba wazazi hawakuwahi kuapata taarifa kuwa mtoto wao alipewa talaka na mwanaume aliyefunga nae ndoa; na kwa sababu wao sio watu wa kufatilia vyombo vya habari hawakutaka kufatilia maswala ya media, ila walitaka kusikia kutoka kwa mtoto wao.

“Tunachojua mwanetu ni mjane, kama ana ndoa anaijua yeye. Lakini sisi hatuitambui na wala hatuaamini. Wala hatumjui huyo mtu anaitwa Dogo Janja labda wanaigiza,” alisema mama Uwoya.

Chanzo: Muungwana blog
 
JANJA.png
 
Si kweli kuwa mzazi lazima ashirikishwe kwenye ndoa. Sheria haisemi hivyo, labda kwa mtoto. Kumshirikisha mzazi, mlezi, ndugu au jamaa kwenye ndoa ni utaratibu wa binafsi tu. Ndoa ni suala na mtu binafsi.
Amesema kuwa anazungumza Kwa minajili Ya kisheria? Anawakilisha tamaduni zetu za kiafrika ,ndio maana mzazi anapomkataa mchumba ni tatizo harusi inakua ngumu kufanyika unless Ulazimishe Kwa nguvu, pia uwoya ameingia mkataba Mpya huku ule alioingia mwanzo na ndikumana haujavunjwa , uwoya amefunga ndoa Kabla ndikumana hajafa, sijui sheria inasemaje hapo
 
Amesema kuwa anazungumza Kwa minajili Ya kisheria? Anawakilisha tamaduni zetu za kiafrika ,ndio maana mzazi anapomkataa mchumba ni tatizo harusi inakua ngumu kufanyika unless Ulazimishe Kwa nguvu, pia uwoya ameingia mkataba Mpya huku ule alioingia mwanzo na ndikumana haujavunjwa , uwoya amefunga ndoa Kabla ndikumana hajafa, sijui sheria inasemaje hapo
Kwahiyo nawe unaitaka sheria kama mimi? Ha ha ha ha ha ha
 
Amesema kuwa anazungumza Kwa minajili Ya kisheria? Anawakilisha tamaduni zetu za kiafrika ,ndio maana mzazi anapomkataa mchumba ni tatizo harusi inakua ngumu kufanyika unless Ulazimishe Kwa nguvu, pia uwoya ameingia mkataba Mpya huku ule alioingia mwanzo na ndikumana haujavunjwa , uwoya amefunga ndoa Kabla ndikumana hajafa, sijui sheria inasemaje hapo
Ndiyo maana kafunga ndoa ya kiislamu.
 
Ndiyo maana kafunga ndoa ya kiislamu.
Kwa hiyo ndoa Ya kiislam inafuta zingine zilizopo kisheria? Kwa hiyo unaweza kumzulumu muislam Mke na kwenda kufunga nae ndoa kwenye ukristo na muislam akafanya Hivyo kwa mkristo na isiwepo shida kisheria? Kwa ufahamu wangu mdogo kisheria ndoa yoyote iliyofungwa ktk dini yoyote ile inatambuliwa na sheria za nchi kama mkataba halali ,na ndio maana vyeti vyote vya ndoa vinatoka serikalini na kwenda misikitini na makanisani kwa ajili ya wanandoa kujaza, pale pana sehemu inayouliza ni ndoa ya wake wengi au mmoja unakata isiyohusika, ndoa iwe ya kiislam au kikristo lazima ivunjwe kwanza kupitia talaka ndipo ufunge nyingine , kwa wakristo kupitia mahakama maana madhehebu mengi hayavunji ndoa kiimani ila uwashauri waumini waende mahakamani usuluhishi ukishindikana kabisa

Ndikumana alikua na uwezo kabisa wa kwenda court ili ndoa ya uwoya na janja iwe declared null and void, nadhan Alisha give up hakutaka yote hayo
 
Kwahiyo nawe unaitaka sheria kama mimi? Ha ha ha ha ha ha
CHUKULIA MFANO HUU:
Timu ziingie uwanjani tayari kwa mpambano, refa anapiga kipyenga mechi ianze halafu mchezaji anatoa pasi ya kuanzisha mpira then timu pinzani wanaganda hawaendi kukaba wala mchezaji aliyepokea pasi ya kwanza nae hatoi mpira, wote wanaganda. Hadi dakika 45 zinaisha aliyeanzishiwa mpira hajatoa pasi, wala hakuna mchezaji anajishughulisha kuomba na vilevile hakuna adui aliyeenda kukaba mpira. Wote waliganda tu. Je, hapo mechi inachezwa au haichezwi? Pambano lipo au halipo?? Lakini timu zote zimefika uwanjani kwa wakati na jearsey zao na wamekaguliwa timamu kabisa kwa kuanza mpambano, na kila mchezaji kachu chumba chake kadiri ya namba yake.



NDOA: Sio suala la kuingia mkataba tubaina ya wanandoa, kuwepo kwa mkataba wa ndoa ni pamoja na kutekeleza masharti ya ndoa na makubaliano baina ya pande hizo mbili yaani bibi harusi na bwana harusi.

Mkataba wa kuoana hauezi kutekelezwa kwa kila mwanandoa kuishi kivyake, kujiendea anavyotaka (hata kama mwenza wake hatalalamikia). Kama wanaishi kivyao na jamii haioni wakiishi maisha ya wanandoa bas huo mkataba wa ndoa yao ni null and void kwasababu masharti ya ndoa hayajatekelezwa na kila upande umepuuzia (japo kuna wakati walienda kama wanataka kutekeleza ndoa yao, yaani kama mechi basi baada ya kipenga mchezaji alianzisha mpira kwa kutoa pasi, halafu wakaganda.

 
Back
Top Bottom