Mama Tibaijuka anatafutwa

Mama Tibaijuka anatafutwa

Mkoroshokigoli

JF-Expert Member
Joined
Dec 20, 2012
Posts
14,593
Reaction score
5,582
Mama Tibaijuka anatafutwa na wapiga kura wake wa Jimbo la Muleba,leo asbui kwenye kipindi cha Super Mix baadhi ya wapiga kura wake ambao walikua wakihojiwa na Kituo cha redio cha East Africa walisema kuwa tangu wamchague mbunge wao kuna maeneo hajapita kabisa,hasa maeneo ya vijijini,wanadai amewasahau na amehamia Dar es Salaam huku akionesha hana mpango nao.

Wapiga kura wa Mama Tibaijuka wakaenda mbali zaid na kusema,huduma muhim kama vile dawa kwenye zahanat wanakosa,ingawa wanaona magar yanashusha dawa lakin waendapo hospitalini au kwenye vituo vya afya husishia kuambiwa wakanunue kwani dawa hakuna.

Kuna mpiga kura wake mmoja alisema kuwa wakunga wanapata tabu sana kuwazalisha wake zao maana hata gloves hakuna,wao wanasema wanamhitaj mama Tibaijuka aende akawatembelee hasa huko vijijin ili wamueleze kero zao na azifanyie kazi,pia walilalamika kuwa hawashirikishwi kwenye kubuni miradi....

Hata hivyo mtangazaji alisema alipompigia sim mama Tibaijuka,simu haikupokelewa,sasa mimi kwakua niliisikia hii via redio nimeona bora niilete hapa,maana najua mama Tibaijuka ni memba wa JF kwa siku za karibuni.

Kwa sababu nilimskia Mtangazaji Zembwela akisema 'MAMA TIBAIJUKA POPOTE ULIPO KAMA UNATUSIKIA TUNAOMBA UJIBU HOJA ZA WAPIGA KURA WAKO.'

NAWASILISHA
EID NJEMA WADAU
 
"Wabunge wa ccm ni mzigo.."By samuel sita

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
"Wabunge wa ccm ni mzigo.."By samuel sita

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums

wale watu walivyokua wakilalamika inaonesha kabisa kwamba matumaini yao kwa mama Anna Tibaijuka yameyeyuka KAMA TANGU WAMCHAGUE MAENEO YAO HAJAPITA,HUYO SI MBUNGE TENA
 
Last edited by a moderator:
Waache wakome kilichowatuma kumchagua mtu ambaye ameishi hukooo miaka kibao ni nini. ina maana jimbo lote walikosa atakayewawakilisha.
 
Mamndenyi mwaka 2010 nilipokua nafatilia uchaguz mama Tibaijuka alipewa promo sana,waandishi walimfata hadi nyumbani kwenda kumhoji na blah blah kibao,na wahaya walizugwa kwa style hiyo tu,
mmoja wa wapiga kura wake nilimsikia akisema 'HUKU NDO NYUMBANI,TUNAMTAKA AJE DAR ANAFANYA NINI?'
 
Last edited by a moderator:
Atasoma thread, ameshazisikia hizo taarifa lakini HANA CHA KUPOTEZA!!

Alafu huyu Mh. Tibaijuka si alikuja hapa na tilalila kwamba alipanda ndege ya peke yake ili akawasikilize wananchi wake!!?? Iweje tena matatizo aliyotuambia kwamba yalikuwa sababu ya yeye kupanda ndege peke yake, ndio hayo hayo wananchi wanayalalamikia!!??

Ccm ni janga zaidi ya baa la njaa!!
 
Watu wa Muleba ni wanafiki sana. Wanamtafuta vipi Mbunge wao wakati juzi juzi tu alikuwa Muleba na Jakaya Kikwete hadi Jakaya Kikwete akalala kwake. Wanaboa sana watu wa Muleba
 
Watakoma,wao hawajui kama ccm wabunge wao wengi wamehama majimbon mwao?Watulie wasimlaum mtu
 
kwanza aje humu anijibie issue za viwanja vya wazi Sinza, land for equity na jengo refu karibu na ikulu njoo Prof.
 
Na ndege alipanda yeye peke yake hadi huko kukimbilia kusaidia kumbe anakula tu na wana ccm wenzake. fyuuuuuu
 
hakuna jipya hapo,hao wametengenezwa,no facts around
Siasa imejaa wanafiki na unafiki.

Ni vigumu kuunganisha mapokezi na shangwe kubwa iliyotolewa na wananchi kwa Rais akiwa ziarani Muleba, na mbele ya Wabunge wote wa Muleba kama wenyeji wake na malalamiko haya yaliyotolewa taarifa redioni. Ama Rais alipokewa na wenyeji wasio wenyeji au malalamiko haya kama kweli yapo basi yametoka kwa wenyeji ambao hawakuwepo wakati wa ziara ya Rais.

Siasa za Kagera ni pasua kichwa!
 
huyo mama ni hopeles kabisa hana uwezo wa kuwasaidiwa.2010 walidanganyika kuwa alikuwa un angewasaidia.sasa yamewakuta jimbo ni kama liko wazi kwa sasa.
 
wala simlaumu.huyu mama wabunge karibia wote wanaishi na kupiga dili dar,hata mbunge wangu wenje ndiko anakoishi.
saa nyingine tuache ushabiki jama
 
Kwanza MULEBA ata bus stand tu HAKUNA yani nia AIBU kwa mji ule kua na mbunge mtaalamu wa mipango miji lakini ata bus stand tu ya kisasa hakuna....Ata juzi TIBAIJUKA umeshindwa kumlilia mzee wa Ahadi JK na Magufuri wakujengee Bus Stand km za Mwanza? nadhani movement for change kamata mwenge na mkawashe uko ambako Tibaijuka hajawahi fika! Ata Bus stand hakuna!
Bus stand hakuna!
Bus stand hakuna!
Bus stand hakuna Muleba!
Bus stand hakuna Muleba!
Tibaijuka km jina lako lilivo huoni AIBU loh Stand
 
Back
Top Bottom