Mama Tibaijuka anatafutwa

Mama Tibaijuka anatafutwa

Kwangu hii ni fursa ngoja nijipange kulichukua jimbo 2015.
Mwaka huuu ccm watasema yote mabaya walio tufanyia watanzania ili ikifika 2014&2015 ni kukabidhi nchi kwa makamanda.
Kila anayeishi na ana akili anatamani mabadiliko yatakayoleta maendeleo na unafuu katika maisha. Lakini tatizo letu tulio wengi tunaweka matumaini makubwa kwenye msingi usiokuwepo. Na hilo ndilo tatizo kubwa sana la propaganda zisizo za kisayansi. Makosa mengine ni kwamba tunawahamasisha wasio na ushawishi katika lengo la dhamira yetu. Tukiendelea kwa mtindo huu wa matumaini ya kwenye vyombo vya habari, tukasahau kuwa ukweli uko mtaani na hakimu wa mwisho ni mwananchi wa eneo husika, basi ninaweza kukuhakikishia kuwa mabadiliko yatakayoshuhudiwa baada ya uchaguzi 2015 ni kupungua kwa wabunge wa upinzani bungeni. Na hivyo kama mwenzangu Sunshow unadunduliza kuwekeza kwenye hizo nafasi fikiria si mara mbili bali zaidi kabla hujapoteza pesa, mali na kujiletea msongo wa mawazo.
 
Mama Tibaijuka anatafutwa na wapiga kura wake wa Jimbo la Muleba,leo asbui kwenye kipindi cha Super Mix baadhi ya wapiga kura wake ambao walikua wakihojiwa na Kituo cha redio cha East Africa walisema kuwa tangu wamchague mbunge wao kuna maeneo hajapita kabisa,hasa maeneo ya vijijini,wanadai amewasahau na amehamia Dar es Salaam huku akionesha hana mpango nao.

Wapiga kura wa Mama Tibaijuka wakaenda mbali zaid na kusema,huduma muhim kama vile dawa kwenye zahanat wanakosa,ingawa wanaona magar yanashusha dawa lakin waendapo hospitalini au kwenye vituo vya afya husishia kuambiwa wakanunue kwani dawa hakuna.

Kuna mpiga kura wake mmoja alisema kuwa wakunga wanapata tabu sana kuwazalisha wake zao maana hata gloves hakuna,wao wanasema wanamhitaj mama Tibaijuka aende akawatembelee hasa huko vijijin ili wamueleze kero zao na azifanyie kazi,pia walilalamika kuwa hawashirikishwi kwenye kubuni miradi....

Hata hivyo mtangazaji alisema alipompigia sim mama Tibaijuka,simu haikupokelewa,sasa mimi kwakua niliisikia hii via redio nimeona bora niilete hapa,maana najua mama Tibaijuka ni memba wa JF kwa siku za karibuni.

Kwa sababu nilimskia Mtangazaji Zembwela akisema 'MAMA TIBAIJUKA POPOTE ULIPO KAMA UNATUSIKIA TUNAOMBA UJIBU HOJA ZA WAPIGA KURA WAKO.'

NAWASILISHA
EID NJEMA WADAU

Hatuwezi kukulaumu kwa kile ulichokiandika, inaonesha akili yako imeishia hapo. bado hujatambua umuhimu wa statics katika post??? na bado hujajua kuwa hutakiwi kabisa kuwa na haraka kw akupost habari ambayo ulitakiwa kwenda EARadio kutafuta kupata list kamil ya vijiji vinavyolalamika then ungekuja hapa mbele ya Dunia na kutweleza kuwa ni vijiji vingap kati ya vingap mama Tibaijuka hajafika.
Otherwise umejifunza, so usiharibu tena text time
 
Sunshow, Janeth Augustine, na denis charles mnakuwa hamko sahihi mkitoa majibu au kuchangia taarifa ya Mkoroshokigoli kwa kudhani kuwa ni mtu mbaya au mpinzani wenu. Saikolojia ya kawaida ya mtiririko wa taarifa na majibu yake inaonyesha kabisa kwamba yeye hana maslahi yoyote na Muleba au Ubunge wa Muleba zaidi ya kufikisha kile alichosikia Redioni. Kwa hiyo kilichotakiwa kufanywa ni kumuelewesha hali halisi tena kwa takwimu na hata picha (Kuona ni kuamini) badala ya kumshambulia.

Unapokuwa PS au PR wa taasisi au mtu binafsi ni vema kupata A, B, C za Reputation Management. Hasa katika zama hizi za mitandao, Online Reputation Management skills ni kitu adhimu. Unaweza kudhani kwa kumshambulia mleta taarifa kwamba ndiyo unaeleweka au unamlinda muhanga (mtu au taasisi) lakini kumbe ukweli ni kinyume chake.
 
Last edited by a moderator:
Kwanza MULEBA ata bus stand tu HAKUNA yani nia AIBU kwa mji ule kua na mbunge mtaalamu wa mipango miji lakini ata bus stand tu ya kisasa hakuna....Ata juzi TIBAIJUKA umeshindwa kumlilia mzee wa Ahadi JK na Magufuri wakujengee Bus Stand km za Mwanza? nadhani movement for change kamata mwenge na mkawashe uko ambako Tibaijuka hajawahi fika! Ata Bus stand hakuna!
Bus stand hakuna!
Bus stand hakuna!
Bus stand hakuna Muleba!
Bus stand hakuna Muleba!
Tibaijuka km jina lako lilivo huoni AIBU loh Stand
mkuu hata ya mkoa ni kituko tena ya muleba nadhani ina unafuu ukilinganisha na ya bk mjini, btw nasikia kuwa anaanzisha mfumo wa stakabadhi ghalani kwenye kahawa kama njia ya kuzuia magendo ya kahawa kuuzwa uganda, wakati mfumo huo umefeli vibaya mno kule kwenye korosho hadi wakulima wanamwagia u.p.u.p.u viongozi wa vyama vya msingi.
 
Kwakupita tuu niwambie uyudenisi anajiabu kwa kumpa sifa mamatibajuka napenda kumuuliza.buligi,kayonza,lwiala, ichwandimi,rwazi,kasenyi,bumbile, kyota,kyamukwikwi,mjunwa ,ilemela,kabaguna,na katungulu,uko anapajua namatatizo walionayo anayajua? Wao wanajua jina tibajuka nazile picha alizogawa kwenyekipindi cha kampaini. Kuusu hosptal nenda kaigala dawa akuna na kuusu ziala ya rais wananchi ua awapewi nafasi yakuuliza maswali wao wanachokifanya ni kuandaa watu watakao uliza maswali walio ambiwa ndo maana uyu denisi k/b anajivunia kua mbona raisi alivo kuwepo awaja muuliza madai ayo acha unafiki wakishabiki wasiasa sema ukweli.
 
Kwanza MULEBA ata bus stand tu HAKUNA yani nia AIBU kwa mji ule kua na mbunge mtaalamu wa mipango miji lakini ata bus stand tu ya kisasa hakuna....Ata juzi TIBAIJUKA umeshindwa kumlilia mzee wa Ahadi JK na Magufuri wakujengee Bus Stand km za Mwanza? nadhani movement for change kamata mwenge na mkawashe uko ambako Tibaijuka hajawahi fika! Ata Bus stand hakuna!
Bus stand hakuna!
Bus stand hakuna!
Bus stand hakuna Muleba!
Bus stand hakuna Muleba!
Tibaijuka km jina lako lilivo huoni AIBU loh Stand

me najiuliza tu hivi hawa wabunge wakishateuliwa kuwa mawaizir huwa wanawaza nin?
 
Hatuwezi kukulaumu kwa kile ulichokiandika, inaonesha akili yako imeishia hapo. bado hujatambua umuhimu wa statics katika post??? na bado hujajua kuwa hutakiwi kabisa kuwa na haraka kw akupost habari ambayo ulitakiwa kwenda EARadio kutafuta kupata list kamil ya vijiji vinavyolalamika then ungekuja hapa mbele ya Dunia na kutweleza kuwa ni vijiji vingap kati ya vingap mama Tibaijuka hajafika.
Otherwise umejifunza, so usiharibu tena text time

Janeth Augustine am sure una maslah ya ubunge wa mama tiba,me sina maslah,hebu soma post ya Mongororo hapo juu amekupa data maana yeye yupo huko,fanyien kazi malalamiko ya wapiga kura,ukinishambulia mimi haisaidii,na wala siwez kuhangaika kwenda east afrika redio,laiti kama nisingetaja kituo cha redio ndo ungathubutu walau kunihoji,nakushauri nenda studio za east africa redio waambie wakupe hiyo clip ili mjipange jins ya kuwasaidia wana-MULEBA kwani hapo kuna tatizo??kuna uadui?ni kuwekana sawa tu,mama amewasahau baadhi ya wana muleba na wanamhitaji hasa VIJIJINI
 
Last edited by a moderator:
Kwakupita tuu niwambie uyudenisi anajiabu kwa kumpa sifa mamatibajuka napenda kumuuliza.buligi,kayonza,lwiala, ichwandimi,rwazi,kasenyi,bumbile, kyota,kyamukwikwi,mjunwa ,ilemela,kabaguna,na katungulu,uko anapajua namatatizo walionayo anayajua? Wao wanajua jina tibajuka nazile picha alizogawa kwenyekipindi cha kampaini. Kuusu hosptal nenda kaigala dawa akuna na kuusu ziala ya rais wananchi ua awapewi nafasi yakuuliza maswali wao wanachokifanya ni kuandaa watu watakao uliza maswali walio ambiwa ndo maana uyu denisi k/b anajivunia kua mbona raisi alivo kuwepo awaja muuliza madai ayo acha unafiki wakishabiki wasiasa sema ukweli.

mkuu Mongororo naamini Janeth Augustine atakua amesoma comment yako huenda atamfikishia salam Mama Tibaijuka
 
Last edited by a moderator:
Sunshow, Janeth Augustine, na denis charles mnakuwa hamko sahihi mkitoa majibu au kuchangia taarifa ya Mkoroshokigoli kwa kudhani kuwa ni mtu mbaya au mpinzani wenu. Saikolojia ya kawaida ya mtiririko wa taarifa na majibu yake inaonyesha kabisa kwamba yeye hana maslahi yoyote na Muleba au Ubunge wa Muleba zaidi ya kufikisha kile alichosikia Redioni. Kwa hiyo kilichotakiwa kufanywa ni kumuelewesha hali halisi tena kwa takwimu na hata picha (Kuona ni kuamini) badala ya kumshambulia.

Unapokuwa PS au PR wa taasisi au mtu binafsi ni vema kupata A, B, C za Reputation Management. Hasa katika zama hizi za mitandao, Online Reputation Management skills ni kitu adhimu. Unaweza kudhani kwa kumshambulia mleta taarifa kwamba ndiyo unaeleweka au unamlinda muhanga (mtu au taasisi) lakini kumbe ukweli ni kinyume chake.

Ericus Kimasha nisaidie mdau,mimi sina maslah yoyote na muleba,lakin niliamin na naamini baadh ya watu wasioskiza redio jana leo watasoma,na bahat nzuri hata katibu wa mbunge bwana denis charles naye hakuskia hiyo habar jana,ila ameisoma leo jukwaan,na pia hata Janeth Augustine naye jana hakuiskia ila leo ameisoma,ndo changamoto zenyewe hizo
 
Last edited by a moderator:
wala simlaumu.huyu mama wabunge karibia wote wanaishi na kupiga dili dar,hata mbunge wangu wenje ndiko anakoishi.
saa nyingine tuache ushabiki jama

harafu hao wanaoitwa wapiga kura ni wapinzani wake tu, hakuna ushahidi wowote kuwa hao walikuwa ni wapiga kura wake, huu ni ushabiki tu.
 
hawa watu nilowaskia jana on east afrika redio wao ni wale wanaoish vijijin,ina maana mama huishi mjini,na wanasema tangu wamchague HAJAWATEMBELEA TENA WALITAJA NA MAJINA YAO,

Ndug yangu MkoroshoKigoli,
Hivi wewe ulisoma chuo gan? yaani kumskia mtu akiongea kupitia redio ndo unajua kuwa yuko kijiji?? je kama kaletwa mjini??
 
Ndug yangu MkoroshoKigoli,
Hivi wewe ulisoma chuo gan? yaani kumskia mtu akiongea kupitia redio ndo unajua kuwa yuko kijiji?? je kama kaletwa mjini??

Janeth Augustine hongera yako wewe uliyefika chuo,,,,maana unazid kuondoka kwenye mjadala,hata nikikutajia chuo nilichosoma haina maana,na nikisema sijasoma haina maana,,,,,kama unautaka ukweli zaid nimekwambia nenda east afrika redio,mikocheni,industrial area
 
Last edited by a moderator:
Kila anayeishi na ana akili anatamani mabadiliko yatakayoleta maendeleo na unafuu katika maisha. Lakini tatizo letu tulio wengi tunaweka matumaini makubwa kwenye msingi usiokuwepo. Na hilo ndilo tatizo kubwa sana la propaganda zisizo za kisayansi. Makosa mengine ni kwamba tunawahamasisha wasio na ushawishi katika lengo la dhamira yetu. Tukiendelea kwa mtindo huu wa matumaini ya kwenye vyombo vya habari, tukasahau kuwa ukweli uko mtaani na hakimu wa mwisho ni mwananchi wa eneo husika, basi ninaweza kukuhakikishia kuwa mabadiliko yatakayoshuhudiwa baada ya uchaguzi 2015 ni kupungua kwa wabunge wa upinzani bungeni. Na hivyo kama mwenzangu Sunshow unadunduliza kuwekeza kwenye hizo nafasi fikiria si mara mbili bali zaidi kabla hujapoteza pesa, mali na kujiletea msongo wa mawazo.

Kaka hapo umenena!
 
Sunshow, Janeth Augustine, na denis charles mnakuwa hamko sahihi mkitoa majibu au kuchangia taarifa ya Mkoroshokigoli kwa kudhani kuwa ni mtu mbaya au mpinzani wenu. Saikolojia ya kawaida ya mtiririko wa taarifa na majibu yake inaonyesha kabisa kwamba yeye hana maslahi yoyote na Muleba au Ubunge wa Muleba zaidi ya kufikisha kile alichosikia Redioni. Kwa hiyo kilichotakiwa kufanywa ni kumuelewesha hali halisi tena kwa takwimu na hata picha (Kuona ni kuamini) badala ya kumshambulia.

Unapokuwa PS au PR wa taasisi au mtu binafsi ni vema kupata A, B, C za Reputation Management. Hasa katika zama hizi za mitandao, Online Reputation Management skills ni kitu adhimu. Unaweza kudhani kwa kumshambulia mleta taarifa kwamba ndiyo unaeleweka au unamlinda muhanga (mtu au taasisi) lakini kumbe ukweli ni kinyume chake.

Ndug Ericus Kimasha, ushauri wako ni mzuri. Kimsingi nakubaliana nao katika dunia ya wastaarabu. lakini hapa janvini ustaarabu ni haba. Hapa mambo ni jicho kwa jicho, jino kwa jino. Online Reputation Management pia inategemea uelewa wa mtiririko wa Online Negative propaganda. kwa mfano; tayari umeniunganisha na katibu wa mama Tibaijuka, Ndug Denis Charles. Lakini wanaoshabikia habari hii hujawaunganisha na MkoroshoKigoli. Hii inaweza kutokana na kutotafsiri Online Character Assassination kama kampain chafu. Ni wazi kwamba mtangazaji wa EA Radio kwa sababu azijuazo yeye ameweka mazingira ya kupumbaza umma kwamba mama Tibaijuka haonekani jimboni kwake. Wachangiaji tuna haki ya kutoa maoni yetu juu ya jambo hili ambalo ni propaganda bila kujali imetokea wapi. Kuunganisha wapinga hoja kwamba hawamsaidii mtu ambaye anashambuliwa, in my opinion, haiwezi kuwa njia sahihi ya Online Reputation Management. Mimi kama mwanamke siwezi kukubali vyombo vya habari kusambaza propaganda chafu dhidi ya viongozi wanawake tena wenye uwezo. Na ndio hapo janvi linakuwa chombo muhimu kuliko redio au magazeti. Kila mtu anapewa elimu anayohitaji. Siamini kwamba mama Tibaijuka haendi jimboni kwake na hakutani na wapigakura wake. Vyombo vya habari huwa vinamuonyesha akiwa huko huko jimboni kwake tena vijijini ndani kabisa. Niliwahi kumuona kwenye TV akipanda mtumbwi kwenda visiwani ziwa victoria. Pia, niliwahi kumuona kwenye TV akimwajibisha mwenyekiti aliyeuza ardhi ya kijiji huko huko jimboni kwake-kata sizifahamu, labda katibu wake atusaidie. Nimewahi kumuona akiwa na wamasai huko Loliondo, mahali ambapo naamini viongozi waliowengi hawajawahi kufika.
Kama mimi nimeyaona hayo, kwa nini MkoroshoKigoli hakuyaona yote yale? Anatuletea kashifa za kupika dhidi ya kiongozi tena mwanamke tuikubali kama vile ni ukweli kutoka kwenye msaafu. Watu tumekuwa waelewa. Penye hila tunapaona, penye nia njema tunapatambua. Mbona Mh. MkoroshoKigoli hajawahi kutuletea sifa nzuri tunazozisikia kwenye redio na magazeti juu ta mama huyu ili tuzijadili? Anashabikia tu habari inapokuwa mbaya ndio wote tuijue.
Ndugu yangu Kimasha, wewe mwenyewe umekiri kwamba Siasa imejaa unafiki na wanafiki, uko sawa kabisa. Usishangae ukikuta kwamba MkoroshoKigoli na watangazaji wa kipindi cha Kabwela na the so called wapigakura wa mama Tibaijuka ni kitu kimoja. Wanajaribu kutulisha hii propaganda juu ya mama huyu amabye walio wengi wanakiri anaweza.
 
Janeth Augustine,
Asante kwa kueleza kinagaubaga tashwishwi yako juu ya mtazamo wangu. Sitakueleza kwa nini waliounga mkono taarifa sikuwaunganisha bali nakupatia rejea zifuatazo uweze kutambua upande wangu katika tuhuma za namna hiyo zinazotolewa kwenye mitandao/vyombo vya habari tena zile zinatoka kanda ile ile!
Baada ya ya kusoma maelezo ya Mama Anna Tibaijuka kwenye uzi huu Siku Nilipotua kwa ndege Bukoba nikiwa peke yangu! nimegundua uzalendo unaanzia mbali. Na majungu ni kichocheo kikubwa katika kuchelewesha maendeleo kwenye jamii husika. Kuna haja ya kujihoji; tunafaidika nini kuwabomoa watu kwa upambe wetu? DJ Baraka ebu tujaribu kubadilika, tutafute na mazuri ya watu wetu, mkoa wetu na tuyatangaze. Kwa tabia hii ungekuwa unaishi katavi kwa Mzee Pinda ungeandika au kusingizia mabaya mangapi?
KAJUGUJUGU,
….. nakumbuka siku za nyuma kuingilia malalamiko ya mtu mmoja kutumia jina la Bukoba Wadau humu jamvini, kuanzisha mada za ugomvi wa Mayor na Mbunge huku akilalia upande mmoja. Ilibainika mtumiaji wa jina hapa JF hakuwa na uhusiano wala ridhaa ya MC Baraka-mmiliki na mwendeshaji wa BUKOBAWADAU. Ujio wa DJ Baraka katika uanzishaji wa mada zenye mlengo sawa na alizokuwa akianzisha Bukoba Wadau wa JF kipindi kile, unatia mashaka!. Si mchezo mzuri kwa sababu unachonganisha watu ndani ya Jamii. Na unaharibu sura ya chombo cha habari na kukifanya kionekane kinaendeshwa na watu wenye upendeleo.

Nitafurahi kama huyu DJ Baraka atajitokeza na kuweka bayana kutohusika kwake wala kutokuwa na mahsiano na Bukoba Wadau Blog.
Kuunganisha wapinga hoja kwamba hawamsaidii mtu ambaye anashambuliwa, in my opinion, haiwezi kuwa njia sahihi ya Online Reputation Management.
Sijawahesabu nyie kama wapinga hoja. Nimependekea mvae uhusika wa watetezi wa mtuhumiwa bila kumchukulia mleta taarifa kama mpinzani. Na nimeshauri juu ya njia sahihi ya kuidhohofisha hoja iliyomo katika taarifa yake. Katika maelezo yangu, nimemchukulia Mkoroshokigoli kama tarishi wa taarifa na si mleta hoja.

Bado sitoshauri mwendo wa "jicho kwa jicho, jino kwa jino". Nikiambiwa niseme ukweli, mifano mizuri ya kutofanikiwa kwa mwendo wa namna hiyo ni sura inayopatikana kwenye jamii ya watu wa kawaida juu ya CCM kutokana na matukio ya namna hiyo hiyo yaliyoendeshwa na vijana wake (Lusinde, Nchemba na Nape). Akati akalakusiiga amazi......! Njia sahihi ni kuendelea kujipambanua kwa kauli safi, majibu ya kweli na sahihi yenye takwimu na viambatanisho pale inapowezekana. Uzoefu wangu mitandaoni, hasa hapa nyumbani, waanzishaji wa mada za uchochezi au za upotoshaji, karibu mara zote huwa hawaungwi mkono pale ukweli unapoletwa na kujidhiri, bali wao ndiyo uendeleza mjadala kwa kujiunga mkono. Sijui kama umenielewa kirahisi?

Endeleeni kujibu kistaarabu ili hata wasomaji waweze kuchambua pumba na mchele. Lakini nanyi mkiiga staili ya wapinzani wenu mtawachanganya hata wafuatiliji na kuwapa kazi ya ziada kuona utofauti kati yenu. Na mwisho wataona nyote ni wale wale. Hili likitokea anayekuwa ameshinda ni yule aliyefanikiwa kukufanya uonekane kuwa na wewe huna tofauti naye. Huwezi kuwalazimisha watu wote wakubaliane na wewe, lakini ukweli unayo nguvu ya kumfanya mtu kujua lipi siyo sahihi japo hata kwa utashi wake akiamu kuendelea kuamini na kushabikia lisilo sahihi. Wakati mwingine hata fisi hujampia jiwe......! Tusibadilishwe, Tusichoke.
 
Janeth Augustine, na denis charles nimelazimika kuwathibitishia kwa nini nilisema "mnakuwa hamko sahihi mkitoa majibu au kuchangia taarifa ya Mkoroshokigoli kwa kudhani kuwa ni mtu mbaya au mpinzani wenu" Nitajitahidi kufanya hivyo bila kuvunja Sheria ya JF.

Nataka muone mambo matatu yaliyo wazi kuhusu Mkoroshokigoli:

  • Kwanza ana maslahi na Mkoa wa Morogoro zaidi kuliko mkoa mwingine Tanzania
  • Pili ni mfuatiliaji sana wa habari kupitia Redio
  • Ni mtu anayependa kushirikisha taarifa za Redioni kwenye mitandao kwa watu wasio na muda wa kusikiliza Redio

Wadau nimepokea taarifa za kifo za mwenyekiti wa halmashauri ya WILAYA ya KILOMBERO bwana RAMADHAN KIOMBILE ambaye alikua anaumwa kwa muda mrefu sana amefariki leo,huyu jamaa alichaguliwa kuwa diwani na baadae madiwan walimchagua kuwa mwenyekiti wa halmashauri.

Kwa mara ya mwisho mwezi wa 10 nilikua kilombero(ifakara)niliambiwa kuwa amelazwa muhimbili.
Taarifa hizi nimepewa na mdau wake ambaye anaishi ifakara
Wadau,
Kwenye taarifa ya habari ya saa 4 niliskia wakitangaza kuwa huko tarafa ya MIKUMI wilaya ya kilosa mkoani Morogoro kuna hospitali ambayo wagonjwa wa kiume na wa kike wanalala wodi moja. Kadhia hii imesababishwa na uhaba wa wodi hospitalini hapo,jina la hospitali sikulishika kwakweli. wagonjwa hao wanadai kuwa hupata shida sana wanapotaka kubadilisha nguo
Chanzo: Redio One
Nimelipata jina la hiyo hospitali,inaitwa hospitali ya Mtakatifu KIZITO AU st Kizito HOSPITAL. Pia kuna mdau amenitonya kuwa Hospitali kuu ya wilaya ya KILOSA inakabiliwa na upungufu wa chakula na hivyo wagonjwa wanakosa chakula
 
Back
Top Bottom