Chibolo
JF-Expert Member
- Oct 13, 2012
- 5,768
- 8,037
Ndugu wan
Jf.nawasalimu nyote.Kwa kuchangia tu kwenye maada hii,mm binafsi
ningeomba mtoa maada alipoleta maada angeikamilisha vizuri kwa
kubainisha ni zahanati zipi na vijiji gani vinavyomtafuta
mh.prof.tibaijuka.Kwanza kasema Mama Tibaijuka anatafutwa jimboni,kule
vijijini Muleba,angebainisha vijiji vile kwa majina ni vijiji gani
M.T.hajawahai kuvitembelea.Kwa faida ya wengi Takwimu zinaonyesha kuwa
Wilaya ya Muleba inavyo vijiji 167,ambapo kwa jimbo la Muleba
Kusini,onavyo vojiji 112,kati ya 167.Ni Ukweli usiopingika kuwa
M.T.amekuwa akifanya mikutano kwenye Kata yaan Makao makuu ya kata zote
25.za Jimbo zima.Ukweli wenyewe sio rahisi kuvifikia vijiji vyote kwan
hata wakati wa kampeni mikitano ya Wabunge hufanyika Makao makuu ya
kata. Pili Ndugu yangu mleta
maada,anaposema zahanati hazina madawa,ingekuwa vema akabainisha pia ni
zahanati zipi kwa majina.Ninavyojua wakati
Mh.Prof.Tibajuka,amekuja,11.june.2013,kwa Ndege ya Serikali,alitembelea
hospitali zote za Wilaya ya Muleba pamoja na zahanati lakini tatizo la
madawa halikusikika kwa wananchi.Hospitali zilizotembelewa ni pamoja na
Hosp.Teule ya Wilaya (Rubya hospital),Kagondo hispitalna Ndolage
Hospital.Kwa upande wa zahanati,alifika Kaigara iliyopo Muleba
Mjini,Kimeya Tarafa ya Kimwani,Rwantege tarafa ya Nshamba.Wagonjwa
wenyewe ndio walikuwa shahidi kwa vinywa vyao kuwa Madawa yalikuwepo ya
kutosha. Kama hiyo haitoshi,ni Juzi Mh.T.wakati wa Ziara ya Raisi
alitembelea wananchi wa Rulanda ambao wanajenga zahanat na Mh.Raisi
akawachangia Milion.3,akawambia kuwa atampa Mbunge wenu
azilete.Hivyohivyo Kasindaga kata ya Kyebitembe wanajenga Zahanati,Raisi
alichangia Mil.2.Habari njema zaidi Kasindaga Halmashauri wanaendelea
na ujenzi wa zahanati ile kwa 26.Milioni.Kote huko hakuna mahali walilia
madawa.Ndo nasema hivi huyu mleta maada ingekuwa vema akabainisha ni
vijiji gani na zahanati gani walipolalamikia upungufu wa madawa?,Nasema
hivyo Mh.Tibaijuka ametoka Muleba Jimboni na Mh.Raisi hilo tatizo hakuna
mahali lilipotajwa.Ni vema mtandao huu ukatumika kusema ukweli,kwani
itaweza kuisaidia kufuatilia na kutafuta ufumbuzi wa tatizo kama habari
ni ya kweli.Lakini ieleweke pia hata kusema Uongo ni ufisadi. *
Kwa nyongeza pale Kata ya
Biirabo,kuna mradi wa ujenzi wa Zahanati chini ya Halmashauri ambapo
Mh.Tibaijuka alichangia bati zote,lakini Halmashauri wakaamua kumalizia
kila kitu,mpaka sasa imeishaezkwa.Kule Buhangaza hivyohivyo.
* kuhusu
hoja ya bus stand hii imejengwa tangu 2003,kutoka eneo ilipokua
zamani.mpaka sasa standi hii ipo na imekamilika mabasi makubwa na madogo
yanatua,pale bila tatizo,huduma za msingi zipo zote maduka ya uhakika
na vyoo vya uhakika vimejengwa pale.kwa kufanya ulinganisho na standi
zote zilizo katika mkoa wa kagera wala huwezi amini hoja yako,mtoa
maada. * kitu muhimu
kinachopaswa kueleweka kwa watu wote na hasa wale wanaopost news,kwenye
mtandao wetu mtukufu,tujaribu kuheshimu usomi wetu,ambapo kusema ukweli
ni zaidi ya yote. Mwisho
ningeomba kama inawezekana tunapokuwa na thread nzuri na zenye uhakika
basi tujitahidi kuzitoa kwa kuweka wazi majina yetu wazi na sio yale ya
bandia,na niombe samahani kwa punctuation kwani niko vijijin na natumia
blackbery,mniwie radhu kwa hilo. Denis,
ktb/m.tibaijuka muleba.
we ni mwongo kabisa,madai ya wananchi ni ya msingi vituo vya afya havina madawa,mf.mdogo ni kituo cha afya kimeya ni miezi 9 sasa hakuna dawa wananchi wanapata huduma pale runazi kwenye pharmacy binafsi ya diwani wa chadema.