Emma Kaisi
Taifa Imara online
Akiwa Waziri wa Ardhi, Mhe Profesa Anna Tibaijuka alikataa kuidhinisha mshahara wa Mkurugenzi wa NHC alioudai wa Dola za kimarekani 19, 500 kwa mwezi sawasawa na Shs milioni arobaini kwa mwezi Bodi ya Zhakia Meghiji liridhia lakini Tibaijuka akaikatalia kuwa hawezi kukubali kuidhinisha mshahara mkubwa kiasi hicho tena wa dola za kimarekani katika nchi ya sarafu ya shilingi. Mkurugenzi wa NHC akamkomalia na magazeti yalinunuliwa karibu yote kumchafua Prof Anna Tibaijuka.
Kwa hiyo jina la Tibaijuka lilipogundulika katika orodha ya mgao wa Rugemalira kwa fedha za ESCROW huko Mkombozi Bank magazeti yakamshughulikia ipasavyo mama huyo bila aibu wala huruma yakiongozwa na gazeti la Mwananchi na Citizen Nipashe na Mtanzania. Watanzania kama kawaida yetu tukameza propaganda hiyo chafu dhidi ya mama huyo aliyekuwa anaongoza wizara ngumu ya ardhi kwa weledi uadilifu na ujuzi mkubwa. Tibaijuka akasakamwa na mitandao ya ufisadi ndani ya Serikali ya awamu ya nne na waTanzania tukashindwa kuona kwamba mama huyo hatakiwi kwenye vikao vya maamuzi kwa hiyo mgao wa ESCROW ilikuwa kusingizio kumuondoa kwenye vikao hivyo ikiwemo Baraza la Mawaziri NEC na Kamati Kuu ya CCM.
Habari toka ndani ya vikao hivyo zilieleza kuwa alikuwa akichangia kwa uwazi hoja ndani ya vikao na hii haikumpendeza mkuu wa kaya wa awamu ya 4 Kwa hiyo tukadanganywa mama huyo ni fisadi akafukuzwa kazi ya uwaziri hadharani kama mbwa huku wanawake vijana wamekodishwa kumzomea wakati wa tendo hilo mbele ya taifa zima ukumbi wa Diamond Jubilee tarehe 22 Desemba 2014 kikao cha wazee wa DSM
Kila juhudi ilifanywa kumfikisha Mama huyo mahakamani lakini TAKUKURU haikuweza kuona kosa lolote dhidi yake kwa sababu alipokea mchango wa shule kwa nia njema na kuufikisha huko huko shuleni kama vile kila mtanzania apokeavyo mchango wa harusi au msiba au maendekeo na kuufikisha uendako.
Lakini mitandao ya ufisadi ndani ya serikali ya awamu ya nne ilikuwa na nguvu na hodari kwa mbinu za uongo. Walipoona TAKUKURU imeshindikana wakaibuka na mbinu mpya kumumaliza huyo mama. Kwa mara ya kwanza Rais wa awamu ya nne akaunda Baraza la Maadili chini ya Jaji Hamisi Msumi kusikiliza kesi za wabunge watuhumiwa wa mgao wa ESCROW katika Benki ya Mkombizi akiwemo Mhe Andrew Chenge na Mhe William Ngeleja. Hadi leo umma waTanzania haujawahi kuelezwa hukumu ya Baraza hilo lakini sidhani kama Jaji Msumi angelikuwa na ubavu wa kumpinga Rais Kikwete ambaye tayari alishamuhukumu hadharani Tibaijuka kwa ufisadi na kumfukuza uwaziri na kutoka vikao vya chama. Ni dhahiri Kikwete alitaka na kutegemea Jaji Msumi kuhalalisha kitendo chake cha kumtoa kafara Waziri Tibaijuka ili awalinde mafisadi halisi waliohamisha fedha za ESCROW kutoka Benki Kuu kwenda STANBIC. Hata Bunge lilitambua kuwa Tibaijuka na Chenge na Ngeleja hawakuhusika katika kuhamisha fedha hizo kutoka Benki Kuu. Wao walipokea mgao wa Rugemalira. Ni wanufaika lakini si wachongaji wa DILI hiyo. Wote watatu walimlalamikia Kikwete kuwaondoa kwenye NEC na Kamati Kuu na hadi sasa Kikwete kama Mwenyekiti wa CCM hajawahi kuwajibu.
Naamini ndiyo maana katika enzi za Serikali ya awamu ya tano isiyo na makandokando wala unafiki bali uwazi na ukweli tumeshuhudia wabunge wa mgao wa Escrow wakirejeshewa nafasi zao za uongozi katika Bunge. Mhe Chenge sasa ni Mwenyekiti wa Kamati ya Sheria ndogo na Mwenyekiti wa Bunge zima. Mhe William Ngeleja ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Sheria Ndogo. Mama Tibaijuka alisemekana kukataa kugombea nafasi yoyote ndani ya Bunge kwa kudai anataka kuwatumikia wapiga kura wake jimboni Muleba Kusini waliomuondolea aibu ya kuonewa na kumchagua tena kwa kushindo hata baada ya kuchafuliwa na kila mbinu ya kumuangusha kushindwa.
Kwa hiyo tunapompongeza Rais wetu Magufuli kuangalia ufisadi wa kimtandao unaolipa watendaji na viongozi mishahara minono ambayo baadaye wanagawana tuchambue zaidi maswala mbele yetu. Mishahara ya viongozi wote katika utumishi wa umma. itangazwe hadharani isiwe siri. Hakuna sababu ya kuwa na mishahara maalum na ya kutisha katika Benki Kuu, TRA, TPA. TANROADS, NSSF, PPF, nkd. Mbaya zaidi ni ufisadi wa Sekretetieti ya BIG RESULTS NOW ambayo ni mikubwa mno na iko katika dola za kimarekani Tunamuomba Rais Magufuli aitangaze yote.
Kwa wahanga wa kusimamua ukweli katika serikali ya awamu ya nne kama Mama Tibaijuka Chenge na Ngeleja tunaomba radhi na kuwashukuru wananchi walioliona hilo na kuwachagua kwa kishindo viongozi hao. Ukweli unashinda baada ya safari ndefu. Tusikate tamaa