Mama Samia, jengo la BOT Mwanza tumepigwa

Nimeona hapa Governor wa BOT akiwasilisha gharama ya ujenzi wa jengo la BOT Mwanza ambalo limegharimu Bil.44
Hapa tumepigwa kwa mtu wa kawaida hilo jengo limegharimu kati Bil.3 na hadi 5 nyingine tumepigwa wazi wazi..
View attachment 1817321
Tupe mchanganua wako hilo jengo, limegharimu tofali ngapi na za gharama gani, sementi, bati,mbao, dirisha, vioo na mengineyo mengi Ndugu mtaalamu.
 
Watanzania sisi kila kitu tunajifanya ujuwaji. Hivi inaamana ni kweli hujuwi jengo kama la benki tena KUU huwa lina standard zake?
Siamini hilo jengo likipigwa bomu kama kuna kitu kitabaki! Gavana asituokote kwa kuhalalisha yasiyohalalika! 44 bil ni fyueza ndefu sana hiyo kwa jengo moja tu isee!
 
Eneo kubwa la hiyo benki ipo chini ya ardhi huku juu ni kama hewa tu chiniya ardhi ndio kuna kila kitu nazan umeelewa.
Ngoja nikawatafute wale jamaa wa de guzman labda tunaweza fanya the biggest bank robbery in tz history
 
  • Thanks
Reactions: _ID
Nimeona hapa Governor wa BOT akiwasilisha gharama ya ujenzi wa jengo la BOT Mwanza ambalo limegharimu Bil.44. Hapa tumepigwa kwa mtu wa kawaida hilo jengo limegharimu kati Bil.3 na hadi 5 nyingine tumepigwa wazi wazi.
===
Nimeambiwa kwamba shilingi bilioni 23.37 ni kwaajili ya ujenzi na shilingi bilioni 18.73 zimetumika kuweka mitambo na mifumo mbalimbali. Niitumie fursa hii kuipokenza Benki kuu kwa jengo hili zuri na la kisasa.

Mheshimiwa pamoja na sifa hizo ujenzi gharama kidogo imesisimua mishipa ya damu lakini hili tutalitazama jinsi tunavyokwenda kwa leo ni sherehe ya uzinduzi wa jengo. Fedha zimetumikaje, zimeendaje tutashikana huko.
Wewe ni shida
 
Acheni kujadili vitu msivyovijua. Benki huwa haiwi hivyo. Hujui imeenda kiasi gani upande mwingine (sina uhakika kama utachelewa ni upande upi ninaouzungumzia). Au ni njia ya kutafuta details namna benki zinavyojengwa? Hii hoja yapaswa ife kwa unyeti wake.
 
Sema lile jengo ni kalii ila bil 44 tumepigwa mchana kweupee
Kwa standard za majengo ya BOT,bila shaka hiyo gharama ni sahh,hata Kama walipiga ni kdogo Sana,majengo ya BOT ,Yana standard zake sio Kama haya magorofa ya kawaida ,Yale Yana standard zake mkuu,kujenga chumba kimoja tu kwa standard zao,umejenga nyumba ya vyumba vinne masters,sebule kubwa,stop,na jiko,fensi,na uwanja mkubwa wanyumba.sio kitoto zile mijengo.
 
Ila kweli haiwezekani kajengo kabaya na kakipuuzi kama hako kugharimu bil.44.5

Mama kaliona ila kavunga ataagiza timu kimya kimya.

Jengo la BOT Mbeya au Mtwara ni zuri kuliko hilo la Mwanza
 
Back
Top Bottom