Mama Rwakatare aichongea JamiiForums

Mama Rwakatare aichongea JamiiForums

kuna jambo moja linajitokeza hapa ni msuguano ama mapambano kati ya kizazi kinachotaka kuendelea kuishi kizamani na kizazi kipya. tahadhari kwa akina mama Rwakatare mkiendelea na mawazo yenu ya kizamani uchaguzi ujao mtapata shida sana kukubarika ktk jamii ya vijana ambao watakuwa ndiyo wapiga kura wengi.
 
Wewe rafiki yako akikuchangia pesa kwenye harusi yako inakuwa na yule mkeo/mumeo ni wake pia?
Ndio maana nilikataa kuchangiwa ili nifanye harusi! Nilioa tu. Vinginevyo waloochangiwa wana taabu kwelikweli. Waulize.
 
Kwa hili la Mama Rwakatare naona Mungu amebaliki Mtandao huu kujulikana sana kwa hivyo kauongezea nguvu ya watu kujua mambo mengi mtandaoni, hasa kajalia kjua uongo mwingi wa wachungaji FAKI wanaoumiza wananchi kwa kutegemea umaskini walionao au shida walizonazo, kama vile uzazi , Ukimwi. Mama anasema hata mwenye umri wa miaka 65 kwa miugiza ya mungu anaweza kuzaa
 
Ivi huyu mama kwanini asingefunga kula na kufanya maombi angalau hata kwa siku 3, ili jf ife automatically?

Au hana imani na mungu anayemuhubiri mpaka anaenda kushtaki bungeni?
 
..."jamiiforums, is a simple phbp based site that my 15 year old brother can set up by selecting a style and personalizing it via HTML within hours."...




JF inafanya kazi 90% zaidi ya maafisa usalama wanaosaka habari juu ya mawazo ya wananchi mitaani. Ukiingia JF utajua watanzania wanfikiria nini na wanataka nini na ndiyo maana ukiangalia sera mbalimbali nyingi zimekuwa zikitoka JF. JF inawasaidia akina JK kujua ni jinsi gani mambo yanavyoshughulikiwa katika nchi nyingine na hivyo kujifunza. JF has more positives to the ruling elites than negatives. It is a source of transparency. More people in the Govt nowadays afraid of being exposed on JF for their shady deals than they are afraiding of TAKUKURU or TISS. This helps to self-regulate the corrupts and lazy officials. A big boost to 'Wazalendo'

They will never ever shut JF, they tried it in 2007 (Jambo Forum) by printing it as Terror website and they failed. JF is not who owns it, JF is me and you are taking time to present their views freely without fear of intimidation from the corrupts!. They may not be able to shut our thoughts.
 
Huyu Cynthia Ngoye ndiye nani tena huko bungeni kwetu Dodoma; aliingia huko kwa kura ngapi na vipi utendaji wake jimboni kama atakua ni mbunge na pengine yule asiyeTEULIWA kiupendeleo?
 
Nami natia timu.

Huyu mama si mchungaji si lolote. Ni magumashi tu. Yupo kibiashara zaidi: kuwapumbaza akili wafuasi wake na kuwaibia huku wakichekelea.

Naamini baada ya upupu wake huu bungeni, atapungukiwa na wafuasi wake si chini ya asilimia 10 hivi.

Tetesi zinasema anatumia uchawi wa ki-nigeria kufanikisha mambo yake hapo kwenye banda lake analoliita kanisa.
 
Mama Lwakatare,
Internet Cencorship is hardly a dead issue, even The Goverment has no right to cencor
our community expression on the Internet. Stay to understand that this is a " Freedom of Speech "
Also you are free to do so, instead of accusing Jamiiforums. They are is no mean on it.
 
Wana JF kutokana na mtandao huu wa kijamii kuibua na kueneza siri za Serikali Wabunge wa CCM wameridhia Mtandao huo ufungwe kama ilivyokuwa Ze Utamu na Mtoa Hoja ni Mchungaji Getrude Lwakatale, Leo pia kapeleka swali lake Bungeni.

Waziri kaitetea JF na kuwashauri wabunge kuwa ni chombo cha habari cha kijamii.

Mama Mchungaji alikuwa anatafuta AIRTIME ya JF naona tumempa ya kutosha, siku nyingine atafikiria mara mbili kabla hajaliparamia jamvi hili!
 
JF tupeni katuni zuri sana inayoonyesha huyu mama yetu alivyo na uwezo wa ajabu KUPITA NJIA ZOTE TATU kwa wakati mmoja bila kukatika msamba;

(1) Mfanya Biashara mkuu ni yeye, (2) Barabara Kuu ya malumbano ya kisiasa yumo, na (3) bado kule Kanisani bado vyeo vya Nabii Mkuu, Askofu na Mchungaji bado zinamsubiri.

Jamani kupita njia hizi zote kwa wakati mmoja u ewashinda wengi sana; Kamanda Masud Kipanya, Zero, Mpangala pamoja na Jemadari yao Mkuu Bwana Gaddo, hadi hapo - OVA!!

Katuni murua itue jamvini.


Mama Mchungaji alikuwa anatafuta AIRTIME ya JF naona tumempa ya kutosha, siku nyingine atafikiria mara mbili kabla hajaliparamia jamvi hili!
 
uyo mama alitaka nayeye asikike bungeni siku nyingi ajaongea,mwacheni ajui atendalo, kiboko yake kakobe.
 
shibe kitu kibaya sana
maana ukishibe utata na wengine wazidi kuwa na njaa
jf ndio kitaa chetu cha kutoa na kusoma kile kilicho ndani ya bongo zetu kwani
wengi wa viongozi wetu hawana mda wa kusikiliza sasa wakipita hapa wengi wao ushtuka kwa kile kilicho wakilishwa.ikifungwa jf itafunguliwa fj
 
Badala ya kuzungumzia maadili yahusuyo rasilimali za taifa mtu anazungumzia maadili ya watoto kuangalia internet? mbona nchi yetu kuna watu wana mawazo mgando hivi? Zama hizi ni za kuzungumzia nani anamiliki mtandao fulani? Nimeshtushwa sana! Na kwa hoja hiyo mtu anapata ze posho?
 
Mama Rwakatare Uje humu JF Tena kwa ID Tutakayoifahamu ni wewe! Uombe Radhi wana JF na WaTg kwa ujumla wao. Kwa kujaribu kuifunga kinywa, SAUTI ya WASIOKUWA NA SAUTI!
Usisubiri kikosi kazi kikufuate, kukuuliza, KUNANI?
 
Mama Rwakatare Uje humu JF Tena kwa ID Tutakayoifahamu ni wewe! Uombe Radhi wana JF na WaTg kwa ujumla wao. Kwa kujaribu kuifunga kinywa, SAUTI ya WASIOKUWA NA SAUTI!
Usisubiri kikosi kazi kikufuate, kukuuliza, KUNANI?
La sivyo halitaisha mpaka kieleweke.
 
Ila kweli viti maalum vya magamba vimekaliwa na MAZUZU... big-headers wth coconut fluids in it....
 
Labda kuongezea mheshimiwa naibu waziri kujibu swala la mheshimiwa Lwakatare ni kwamba ACCESS TO INTERNET IS A FUNDAMENTAL HUMAN RIGHT OF EVERY CITIZEN OF THE WORLD iliyokuwa registered mwezi september mwaka 2011. Hivyo kama wataifungia wajiandae kwenda kwa ocampo (ICC), UN Court of Human Right na European court of human right for prevention of human right. Naweka neno langu tu!!!
 
Haki hiyo imepitishwa tu hapo Mwaka jana UN kule New York kwenye kikao ambacho hata Mkuu wa Kaya naye alikua ni mjumbe. Sasa huyu mama wala hana habari na hilo.

Labda kuongezea mheshimiwa naibu waziri kujibu swala la mheshimiwa Lwakatare ni kwamba ACCESS TO INTERNET IS A FUNDAMENTAL HUMAN RIGHT OF EVERY CITIZEN OF THE WORLD iliyokuwa registered mwezi september mwaka 2011.

Hivyo kama wataifungia wajiandae kwenda kwa ocampo (ICC), UN Court of Human Right na European court of human right for prevention of human right. Naweka neno langu tu!!!
 
Back
Top Bottom