Mchumi90
JF-Expert Member
- Mar 16, 2015
- 1,080
- 1,284
Kumekuwa na ukaguzi wa wafanyakazi hewa na madudu mengine wizara ya elimu. Natoa wito kwa Mama Ndalichako kutuma wakaguzi kwenye shule binafsi kikagua aina ya walimu wanaofundisha huko. Hili litaipunguzia serikali mzigo wa kuajiri walimu wote.
Kwa utafiti mdogo niliofanya wanaofundisha hizi shule hawana sifa za ualimu kama taaluma.
Ubaya wa hili ni kwamba wanaendesha mambo kienyeji na hawana ujuzi juu ya vitu vingi vilivyo ndani ya ualimu. Hata kuandika lesson plan au scheme of work hawawezi.
Pia kwa upande mwingine wanabania ajira kwa walimu wa kweli kutoka vyuo vinavyotambulika.
Ni kama itokee mtu aliyesomea uhasibu akafanye kazi ya lawyer, hapa lazima kuwe na mapungufu katika utendaji.
Nawasilisha, najua hili litafika kwa wahusika.