Ni changamoto kubwa pindi wazazi wakitengana na ukapaswa kuwasaidia wote

Alvajumaa

JF-Expert Member
Jul 5, 2018
4,953
6,071
Miaka imeenda sasa, wazazi walitengana muda sana, imefika muda wa sisi vijana wao kuwatunza na kuwapatia mahitaji madogo madogo.

Changamoto inakuwa kubwa hasa kama wazazi hawako pamoja na unapaswa kuwasaidia yaani ukipata chochote usema utume upande wa Mama upande mwingine unalalamika kwamba huwajali huwathamini, vice versa kwa upande mwingine.

Kama wangekuwa pamoja ni rahisi kwamba unachotuma kitawafaa wote kwa pamoja. Yote kheri sina tatizo na kuachana kwao maana maisha ya ndoa yana changamoto nyingi, kuna muda unawaza nimjengee Mama vyumba 2 baba nae akisikia nae anataka kujengewa vyumba 2 pesa hakuna aisee na haitoshi.

Kipato ni kidogo mara kusomesha mara familia, ndugu, jamaa mara wazazi aisee nanga inapaa.
 
Ukiwasaidia hakikisha unawasaidia kinacholingana...

Mfano; Kama unampa mama gari aina ya IST na baba naye mpe gari aina hiyohoyo...

Fanya kwa uwezo wako...

Utabarikiwa na Mungu
 
Miaka imeenda Sasa, wazazi walitengana muda sana, imefika muda wa sisi vijana wao kuwatunza na kuwapatia mahitaji madogo madogo,
Changamoto inakua kubwa hasa kama wazazi hawako pamoja na unapaswa kuwasaidia yaani ukipata chochote usema utume upande wa Mama upande mwingine unalalamika kwamba huwajali huwathamini, vice versa kwa upande mwingine...

Kama wangekua pamoja ni rahisi kwamba unachotuma kitawafaa wote kwa pamoja,
Yote kheri sina tatizo na kuacha kwao maana maisha ya ndoa yana changamoto nyingi, Kuna muda unawaza nimjengee Mama vyumba 2 baba nae akisikia nae anataka kujengewa vyumba 2 pesa hakuna aisee na haitoshi

Kipato ni kidogo mara kusomesha mara familia, ndugu, jamaa mara wazazi aisee nanga inapaa...
Ok sawa.
ni kweli
 
Kuna bestvyangu aliwaambia wazazi wake kama wanataka matunzo kutoka kwao ni lazima warudiane/waishi pamoja, yeye hana uwezo wa kuhudumia pande mbili,

Wale wazee iliwabidi waishi tu pamoja,hadi leo wanaishi pamoja.
 
Kuna bestvyangu aliwaambia wazazi wake kama wanataka matunzo kutoka kwao ni lazima warudiane/waishi pamoja, yeye hana uwezo wa kuhudumia pande mbili,

Wale wazee iliwabidi waishi tu pamoja,hadi leo wanaishi pamoja.
Hii kwangu sidhani kama inawezekana maana wazazi walitalikiana nikiwa na miaka 4, baada ya hapo maisha yote nimeishi na baba, mpaka Sasa Mimi ni mtu mzima 35

Sent from my Pixel 4 using JamiiForums mobile app
 
Hii kwangu sidhani kama inawezekana maana wazazi walitalikiana nikiwa na miaka 4, baada ya hapo maisha yote nimeishi na baba, mpaka Sasa Mimi ni mtu mzima 35

Sent from my Pixel 4 using JamiiForums mobile app
Yes kwako ni ngumu, wahudumie tu kwa urefu wa kamba yako,

Kuna mmoja pia kama wewe,kalelewa na baba na mama wa kambo, sasa kasoma na anafanya kazi,Changamota anajitolea tu,

mama mzazi akiona tarehe zinakaribia tu anatangaza shida,
 
Tupo 7, katika hao watatu wanasoma na nalipa ada, watatu wengine hali zao tia maji tia maji ... Siwezi kuwalaumu

Sent from my Pixel 4 using JamiiForums mobile app
Tofauti na watu wanavyokwambia utabarikiwa na kuongezewa, usipokuwa makini utashushwa chini uwe kama wao. Watu wa kusaidia ni wale ambao bado wana potential hao ndugu zako. Usipowapa msaada hao hawatosimama, ila wazazi walipambana vita yao hawakushinda. Sio kosa lako wao kuwa hivyo sasa wasaidie bila kujiumiza.

Tafuta ambaye alijitoa kusubiria mambo yake kwa ajili yako ndio umpe zaidi. Wazazi wakitengana huwa hawakupi uzito sawa. Kuna watu mzazi mmoja hakujenga ili mtoto asome, mwingine alitoa hela kidogo kuliganisha na kipato chake na hakuteseka kuitoa. Leo hii utawekaje mizani sawa ukiwapa chochote na huna uwezo mkubwa.

Tanzania ikipata shida Burundi ikatoa $1 million na Japan ikatoa $30 million aisee hiyo 1 ya Burundi inawauma sana, kuna vitu vingi vimesimama waitoe.

Wazazi wengine huplay victim card na kutishia laana na kulalamika. Na wengine timing yao inakuwa kuponda maisha sababu "si nilizaa". Wengine walipambana wakashindwa, ni maisha tu.
 
Back
Top Bottom