mwasita
JF-Expert Member
- Aug 5, 2016
- 371
- 378
Sema vyovyote vile unavyojisikia kusema lakini si mama mkwe kuniongezea mwanamke mwingine kwenye ndoa yangu NEVER EVER,kuto kukua kwa mtoto wake si kibali cha yeye kukaa na kumzungumzia mama wa mtoto wa mume wangu,hapa anatuanzishia migogoro ambayo nikiichekea hakika ntakuja kujuta,Mimi sitafutwi kupendwa ndugu yangu naitafuta heshima na utukufu kwa Allah maana dunia hii huwezi pendwa na wote
Kwanza Hongera kwa kutimiza majukumu yako katika familia yako ikiwa ni kuishi na wadogo wa mme wako kwa kipindi mlichoishi nao na pia Hongera kwa kipindi ulichovumilia ila elewa subira yavuta heri!
Fanya hivi:
Kaa uzungumze na mmeo umweleze jinsi ambavyo mama mkwe anakukwaza lakini usije ukamwaproach direct mama wa mwenzio pengine anafanya pasipo kujua kama anakukwaza na kama mmeo anayo hekima akiona kweli hoja zako ni muhimu pasipo upendeleo inabidi amwelimishe mama yake au basi mtashauriana namna nzuri ya kuhandle migongano ya aina hiyo au pengine yeye ndio atakusaidia kusolve tatizo hilo na familia ikaendelea kuwa moja na upendo uliokuwepo.
Mfano Mimi naamini katika uwazi na haki kama mzazi wangu akikosea ntamwambia tu kuwa mama/baba unamkwaza mtoto wa watu kwa namna hii unavyofanya hebu fikiria mtoto wako naye alikoolewa afanyiwe hivi vipi utajisikaje na pia mzazi wa mwenzangu akikosea ntasema ukweli ila siwezi kumconfront ntazungumza naye kama mzazi au pengine ataelimishwa na mwenzangu maana akiambiwa na mwanae anaweza kuelewa zaidi na kuujua ukweli zaidi.
Angalizo kwa wanawake wengine waondoe negative mentality kwa mama wakwe zao wengine hata hawajaingia ndoani wanawaza negatively kaeni mkijua nasi tunawaelewa mama zetu maana ni watu kama watu wengine kama ni mama mkorofi ntakuwa namjua hivyo ntakusaidia kutatua matatizo yatakayojitokeza.
Hivyo zungumza na mwenzio pengine atakusaidia kusolve tatizo hilo in the best way na familia yenu ikabaki moja na yenye upendo!