LadyAJ
JF-Expert Member
- Oct 21, 2015
- 7,173
- 9,656
- Thread starter
- #161
Hakuna urozi wala mavumba,sisi asili yetu hatutikiswi na mapenzi bora niende nikale michunga kuliko kutikiswa kusiko sababulol! hapo kwenye rangi unataka kufanya urozi? Usifanye urozi ila ongea na mumeo kwa lugha ya staha na kumwambia hupendi kinachoendelea. Kuzungumzia kuhusu mtoto wake wa nje ni muhimu lakini isiwe ni kila siku tena na huyo wa nje kusifiwa kamfanyia hili kamfanyia lile. Mwambie na nyinyi pia mna watoto mbona mama hawazungumzii. Kama mumeo ni muelewa atatafuta namna ya kuongea na mama yake ili maongezi hayo yapungue au yasiwepo kabisa au waongee wenyewe wakati wewe haupo.
Umesema vyema sana sisi hapa tuna watoto tena wa 3 siwezi kusema wanangu ni zaidi, hapana maana mtoto ni mtoto kwa baba yake ila mama mkwe anataka kufanya kua yule wa nje ndie mtoto hawa wangu ni mashetani kitu ambacho kinanifanya nichume dhambi kwa kuanza kua na chuki na yule mtoto bure wakati nimemkuta kabla ya kuolewa na nilikubali, more mama mkwe anapotaka kunitawala kwa kuongea na mama wa mtoto kwenye simu kisha kumpa mwanae amsalimie inanikwaza mnoo, na sielewi dhamira yake kwangu