Mama mkwe nakupenda sana ila bora uende

Mama mkwe nakupenda sana ila bora uende

Utajikuta una kazi kumlelea mwanae + Una kazi ya kumfurahisha mkwe +Una majukumu ya kifamilia. Mwishowe wengi wetu huchagua kuyanyamazia mambo haya kama njia ya kuepusha shari na kuwa wahanga wa furaha za wengine
Alafu hao unaosucrifice kwao angalau hata waione thamani ya ukifanyacho!!
 
Sina haja ya kupimana ubavu na mtu mwenye taswira ya kuijenga nyumba yangu lakini yule aliyeazimia kuibimoa lazima nimkemee maana ukicheka na nyani utavuna mabua
Tangu tulipofanikiwa kutoka kupanga chumba kimoja mpaka tukaja kupanga vyumba viwili na sebure ndipo nilipoanza kuishi na shemeji yangu mdogo wake anayemfuata na baadae akaniletea mwingine wote hawa nimewalea kama ndugu zangu,na mpaka hii Leo mmoja anatafuta kazi mwingine chuo,sio kwamba tulikua hatupishani tulipishana bila heshima ilikuwepo na lazima tufahamu kua heshima ni kitu cha bure hata kama labda namkosea huyu mama sio wa kuniingilia maamuzi ya nyumba yangu,sio wa yeye kuutumia karibu muda wangu wote kukaa chumbani kwake kuongea na mwanae,mchana Mimi nakua nipo kazini bora basi wangetumia muda huo lakini kwa makusudi tu jioni ndio wanaitana mazungumzo yasiyokwisha
Pole kwa kweli. Haya mambo ya wakwe huwa ni mtihani sana. Ongea na mumeo mweleze vile unakwazika na kukosa amani. Kama anakupenda mtasaidiana katika kutafuta suluhu
 
Wala uislam haulalishi vitendo vya huyu mama,Utamtii mzazi wako ktk mambo ambayo hayaendi kinyume na maamrisho ya Mola Mlezi,Je anachokifanya huyu mama kwa mmkwewe ni haq? Kwa vitendo vya huyu mama ni kama anataka kuisambaratisha ndoa ya mwanawe,Je wajua ktk halal zenye kumchukiza Allah ni yule mwenye kuoa na kuacha? Ktk uislam kuna haq za mume na haq za mke, Kwa mujibu wa mtoa mada haq zake ziko hatarini kwa huu mwenendo wamkwewe. KAMA ALICHOSEMA DADA HUYU NDIO UHALISIA! BASI MKWE NI TATIZO NA JUHUDI ZA HARAKA ZICHUKULIWE KABLA HALI HAIJAWA TETE
Nilishindwa kuongea zaidi maana mie sio muislamu so sijui hilo linakuwaje.
 
Hivi mama zenu majumbani kwao chakula cha usiku huwa wana kula saa ngapi? Maana Mimi hapa wakati taarifa ya habari ya saa 2 inaendelea chakula huwa tayari kwa kuliwa,hakuna siku niliyorudi saa 4 usiku, nipo radhi kugombana na boss wangu lakin niwahi kurudi maana na Mimi nina watoto wadogo wanahitaji kula mapema walale mapema na zaidi ya yote msichana wangu wa kazi ni kama ndugu yangu japo anatoka kijijini kwao lakini majukumu aliyo nayo ni mengi sana maana pamoja na kazi zote ananisaidia kulea mtoto wangu huyu mdogo wa mwisho hivyo nae bila shaka anahitaji mapumziko ya jiko angalau Mara moja kwa siku

Hicho unachokileta wewe ni mashindano yasiyo na sababu, kuna wakati mwingine maishani hupaswi kubishana na hayawani. Na si kila swali linajibiwa kwa jibu maswali mengine yanajibiwa kwa maswali.

Pia kuna wakati inabidi ubadilike wewe ili mradi uendane na jamii, ushasema kuwa hakai ataondoka, sasa ya nini kutunishiana misuli kwa jambo ambalo ni rahisi tuu kulitatua.? Muombe dada wa kazi akusaidie kupika kipindi hiki mkweo yupo. Akiondoka mtaendeleana ratiba zenu.
 
Alafu hao unaosucrifice kwao angalau hata waione thamani ya ukifanyacho!!
Alafu ni mambo madogo sana,lakini mazito kwa viumbe sisi,kupeana moyo,kuthamini juhudi za mwenza wako na kushukuru but we take things for granted.
 
Sio wanaume wote ni waelewa kama udhanivyo,kama umesoma pia mada nyingi humu utaligundua hilo. Ukideligate unachukuliwa kama mvivu,una dharau,hauyajui majukumu yako, nk.
espy, ni kweli sio wanaume wote waelewa. Kuna baadhi ya wanaume walichangia mada wakasema tangu wapo nyumbani kwao, mama ndiye alikuwa anampikia baba. Kwa hivyo lazima mke apike.

Kuna watu ambao hawakulelewa na baba na mama, na hayo waige lipi?

Mara nyingi nature ya kazi na muda wa kurudi ndiyo unadetermine nani apike. Lakini kusema mke lazima apike! Ahhh Tafadhali.

Kama unataka mke wako arudi akupikie, basi kubali kula muda atakao rudi.

Nadhani huu mjadala wa nani apike, baba na mama wakizungumza kwa hoja, basi hata baba anaweza kupika. Tatizo huwa ni nyumba nyingi za kupanga za bei ya kawaida hazina mandhari ya kijikonijikoni.
 
Kabla hujaanzisha mtiti mamii hebu anza kumshirikisha mumeo kwanza,halafu pima mzani kwa kuangalia anaegemea wapi maana kama mumeo hata kuamini au kukuelewa ujue vita na mama mkwe hutaiweza hata kama wewe ni mtanga , maana hapo utakua unapambana two against one na usiombe mumeo akawa hana msimamo hapo lazima jahazi lizame
 
Ahende tu maana anakutafutia sababu ipo siku atamleta mkwewe ambaye mwanae amemzalia mtt wa ujana
Pray part yako dada
 
Vita vya wanawake kwa ujumla huwa ni vigumu kweli kuviamua. Ukitaka uwe neutral inahitaji hekima ya ziada. Nadhani mume anawajua hawa wawili walivyo na tabia zao pia. Akishilikishwa ataweza tu kulitatua hilo.
 
Hiyo ni moja ya shida yangu,zipo nyingi tu ikiwamo kukulizwa mbona nampa chakula kidogo mwanae,wakati Mimi naishi nae miaka yote hii naujua ulaji wake, inamaana Mimi nampunja mwanae hahahahaa haki ya Mungu, M/Mungu anijaalie kuto fungua mdomo


Shemeji yetu huwa anajibu nini?
 
Wanawake mnajuana tabia zenu ni hizo hizo miaka yote , anayemlalamikia mwenzake leo, kesho naye atakuwa na tabia zile zile, hivyo sisi wanaume msituingize kwenye kesi zenu za kutengeneza.
Mvumiliane tu maana ni ninyi walewale.
 
seeeeeh mamawa brabraaaaaaaa nyingiiiiiiiiii sasa utamuigizia mwishowe utachoka kwa hali hio anakera mwambie mumeo filimbi ishapulizwa na ***** ya kuvuluga ndoa ss kabla hajamaliza kupuliza akaimalizie hukoooo kwa mumewe akakileee kibabu chake muda wa kumlea na kumcare mwanae ulishaisha saiz zamu yako kama anataka aende nae ila sio kuleta fujo ugenini mfyuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuu ZAKE
 
Aaaahg pole sana kwa yanayokukuta ila sababu ya kuujua uchungu wa mwanae nae anaumia labda kuona unachelewa,,,lakin pia angekusaidia tu hata kupika kabla ya kurud au kukuandalia viungo wewe ukifika unapika tu. Msamehe bure maana huyo ni mzaz wako pia.. Usisikilize wala kuumia sana kwa maneno kuhusu hyo mtoto mwngine,,we jali yakwako yaende...

Mi nampemda mama mkwe wngu mpka anajua mkwe ananipenda,,,nae nashukuru ananipenda snaaaaaaa mpka najua mkwe wngu ananipenda,, heshima na kujitambua na kuweka balance kwako na kwetu ndio siri kuu....
 
Back
Top Bottom