Mama mkwe nakupenda sana ila bora uende

Mama mkwe nakupenda sana ila bora uende

Mbona simple tuu.? Kwa mujibu wako Mzozo ni chakula kuchelewa kupikwa na umesema mama mkwe kumzungumzia mkemwenzio huna shida nalo.kwani mchana anapika nani.? Si house girl.? Usipopika wewe mmeo hashibi.? Wewe huyo umemkuta ukubwani, huyo mkweo kakaa naye toka anazaliwa. So simply ukiamua kuingia vita na mama mkwe hutoshinda kamwe.

Kwani Kuna ubaya gani ukitoa idhini katika kipindi kwa housegirl apike chakula.? Hususan kipindi hiki ambacho mkweo yupo.? Weekend ukiwepo ama siku ukiwahi kurudi utapika. Sometimes inabidi ubadilike ili kuendana na mazingira, na ukifanya hivyo kama mumeo ni muelewa ataelewa umemaanisha nini.
Halafu baadae huyo huyo mama mkwe atasema mwanamke wa nyumba hyo hapiki kazi kuchelewa kirudi nyumbani... atasema kila leo mumewe anakula cha hauzgal... mwisho atamkuwadia na huyo hauzgal... hana dogo huyo mama!!!
 
Mimi sicheki na ma'mkwe..!akizingua tuh nampa maneno ya busara na Kwa kheri.
 
I know everythng,nishaexpirience maisha ya ndoa,so hakutokua na jipya kwangu
Hongera bora wewe unawaza ata kuolewa wenzio wanawaza kutuchuna wakidhani wanakukomoa bila kujua wanajikomoa wenyewe..!

Mwanaume km mti wa mwembe afu unaulinganisha na mpapai(girls).
 
Nimebahatika kutembelewa na mkwe wangu wiki kadhaa sasa,nilifurahi nikashukuru kwa kupata ugeni mzito ukizingatia kwamba nakaa na shemeji zangu hapa,mmoja anatafuta kazi mwingine yupo chuo anakaa hostel ila huwa anarudi hasa weekend.
Tabia ambazo amenionyesha na hakika niseme wazi tu kua zinanikera na kuukwaza moyo wangu na Mara hii naanza kujihisi unyonge sana ndani ya nyumba yangu
Huyu mwenzangu alizaaga mtoto kipindi cha nyuma huko katika pita pita za ujana na huyu mtoto yupo kwa mama Yake na anasoma boarding school na kila kitu kinalipiwa na baba yake hapa nami wala sina tatizo na hilo,sasa tangu mama mkwe aje akikaa na mwanae hadithi ni kumzungumzia huyo mama wa mtoto wee na kibaya zaidi anasema wazi kabisaa kua huwa anakwenda kumuona na kukaa hapo kwake yaani kwao na mumeo wangu,yaani anamsifu kabisaa kuwa anasaidia sana na anamshukuru!!
Mbaya zaidi baba watoto baada ya ajali mbaya aliyoipata na kupata tatizo La nyonga yupo tu haendi kazini zaidi Zaidi akitoka huwa anakwenda dukani kwetu kusaidia biashara, Mimi hutoka asubuhi kwenda job na kurudi jioni,na kutokana na heka heka za foleni najikuta Mara nyingine nachelewa kufika nyumbani mpaka saa 12 ndio naingia ila kawaida yangu ni ile ile kua chakula cha jioni napika mwenyewe hata Dada wa kazi hapa anafahamu hilo,mama mkwe nikichelewa hiyo kurudi anaanza maneno kua "sasa watakula saa ngapi? mwanae si atachelewa kunywa dawa? Kwa namna hii atapona kweli?" Yaani ni maneno juu ya maneno yeye anamfikiria mwanae mtu mzima hawa wajukuu walio wadogo hawaoni!!? Nifanyeje sasa? Niache kazi ili nimuhudumie mwanae ale saa 12 jioni badala ya saa 2 usiku au??
Nimekosa Uhuru na hamu ya mume wangu kwa kweli maana hata chakula kiwapo mezani nikimpakulia mwanae anakadiria kwa kuuliza "mbona kidogo sana? Atashiba kweli?" Inamaana Mimi nampunja mwanae!!? Mimi nikiyekaa nae miaka yote hii na watoto wote hawa nimpunje mwanae chakula lol!!?
Mama mkwe nakupenda sana,sana sana mamangu ila Tafadhari bila kusubiri siku nitakayoteleza na kufungua kunywa changu Leo ntamwambia mwanao bora uende!!
Roho mbaya inakusumbua kwani Mama yako akija mumeo sianamvumilia! na utambue kuwa kadiri binaadamu umri unavoenda akili zinarudi utoto tatizo wewe unashindana na mkweo
 
Unajua nini... inferiority complex ya mumeo ndo chanzo... kama wanaitana ndani jioni ndo wayaongee.. jua kuna malalamiko au maneno mumeo anaongea kwa mama yake ... ndo mama mtu anaanza kufanya ayafanyayo.... mumeo kwa kua haendi kazini anajiona hayuko productive basi hasira zake ndo zinaishia kusema sema... em chunguza sana ... na yote hayo akiyafanya reaction ya mumeo ikoje????
Kiufupi mwanzo wakati anafika hapa ile closeness nilijua ni vile hali ya mwanae na hawajaonana muda mrefu hivyo haikunipa taabu sana, Mimi sijui anamueleza nn mama yake ila nnachokiona ambacho kwangu ni kigeni huwa anakwenda chumba alichofikia mama yake anakaa huko wanaongeaa wee mpaka uwaite chakula,baada ya hapo Mimi huenda kulala na naweza shtuka saa 5 usiku mume hayupo yupo sebuleni wanaongea na bi mkubwa wake na kuangalia tv, Leo nimeshinda nyumbani nimepika mapema lakini mpaka saa hizi waliokula ni watoto tu sasa simuelewi kwa kweli
 
Aende tu Mkuu maana ntashindwa kumvumilia kwa kweli
Na asipoenda hiyo ndoa itavurugika, wakina mama mkwe issue, ndiyo wavunja ndoa kila kukicha, aende, tena fasta, si wewe tu mama, ilishanitokea na ya haya yakina mama mkwe, ila kama mwanaume nilisimama vyema mama mkwe hana hamu nami tena..
 
Hivi mama zenu majumbani kwao chakula cha usiku huwa wana kula saa ngapi? Maana Mimi hapa wakati taarifa ya habari ya saa 2 inaendelea chakula huwa tayari kwa kuliwa,hakuna siku niliyorudi saa 4 usiku, nipo radhi kugombana na boss wangu lakin niwahi kurudi maana na Mimi nina watoto wadogo wanahitaji kula mapema walale mapema na zaidi ya yote msichana wangu wa kazi ni kama ndugu yangu japo anatoka kijijini kwao lakini majukumu aliyo nayo ni mengi sana maana pamoja na kazi zote ananisaidia kulea mtoto wangu huyu mdogo wa mwisho hivyo nae bila shaka anahitaji mapumziko ya jiko angalau Mara moja kwa siku
Hata ukisema hauzgal apike... na bado ataongea atasema humpikii mumewe kazi kumuachia hauzgal...anagubu huyo hamna kitu ataacha kusema
 
Hapo panahitajika a high Diplomacy ya hali ya juu sana....

Usipo kuwa makini utaishia kupewa laani sisizo kuwa na mbele wala nyuma....

Tumia:
-Busara
-Hekima
-Akili

Usitumie hasira Kumaliza hilo tatizo.....
Good advice!

Barikiwa sana.Pia nimejifunza jambo.
 
Hapo tatizo ninaloliona mimi SIO MAMA MKWE WALA NINI. Tatizo hapo limetokana na MWANAMKE KUFANYA KAZI, NA MWANAUME KUWA JOBLESS.
Imeniuma sn nikiwa kma mwanaume, ila kiukweli NAJUTA KWANINI NIMEOA. Mwanaume labda uwe extraordinary kwenye kila kitu, ila ukishakuwa huna kitu/ huna income, ni matatizo sana.
Wewe dada ni MNYANYASAJI tu, huna lolote
 
Umenikumbusha hii
17932422_426334021065825_4241878931830996992_n.jpg

Uwiiii yaani kama naiona Malamba ilee
"Bora kurudi kwetu kwenda kula nyasi kwa amani, kuliko kula vinono vitani"
 
Hapo tatizo ninaloliona mimi SIO MAMA MKWE WALA NINI. Tatizo hapo limetokana na MWANAMKE KUFANYA KAZI, NA MWANAUME KUWA JOBLESS.
Imeniuma sn nikiwa kma mwanaume, ila kiukweli NAJUTA KWANINI NIMEOA. Mwanaume labda uwe extraordinary kwenye kila kitu, ila ukishakuwa huna kitu/ huna income, ni matatizo sana.
Wewe dada ni MNYANYASAJI tu, huna lolote
Shukrani, ila niliposema mwanaume yupo nyumbani sikumaanisha kua ni jobless !! Mwanzoni mwaka huu alipata ajali ya gari akiwa katika shughuli za kikazi na ndipo alipopata hilo tatizo la nyonga,hivyo basi mshahara anapata na wala si jobless ila yupo kwenye likizo ya ugonjwa
Unyanyasaji ninao Mimi tu pekee, shukrani matusi wanawake tumezoea,asante sana shemeji !!
 
Kiufupi mwanzo wakati anafika hapa ile closeness nilijua ni vile hali ya mwanae na hawajaonana muda mrefu hivyo haikunipa taabu sana, Mimi sijui anamueleza nn mama yake ila nnachokiona ambacho kwangu ni kigeni huwa anakwenda chumba alichofikia mama yake anakaa huko wanaongeaa wee mpaka uwaite chakula,baada ya hapo Mimi huenda kulala na naweza shtuka saa 5 usiku mume hayupo yupo sebuleni wanaongea na bi mkubwa wake na kuangalia tv, Leo nimeshinda nyumbani nimepika mapema lakini mpaka saa hizi waliokula ni watoto tu sasa simuelewi kwa kweli
Fanya kuchunguza.... reaction za mumeo ndo zitakupa majibu... nachelea kusema ukianza kuongelea habari za mama mkwe kwa mwanae leo kibao kitakugeukia ... kuna kitu kinapikwa kua makini.. nenda mdogo mdogo utapata majibu yote... nashauri hata kama utaliongelea leo basi anza mbali upate kuona reaction ya.mwenzio usibwage lote
 
Fanya kuchunguza.... reaction za mumeo ndo zitakupa majibu... nachelea kusema ukianza kuongelea habari za mama mkwe kwa mwanae leo kibao kitakugeukia ... kuna kitu kinapikwa kua makini.. nenda mdogo mdogo utapata majibu yote... nashauri hata kama utaliongelea leo basi anza mbali upate kuona reaction ya.mwenzio usibwage lote
[emoji120] [emoji120]
 
Alamsiki, IshaAllah kesho M/Mungu akijaalia
 
Wewe ni ke au me? Nawewe ni mkwe mtarajiwa[emoji3]
Wanajisahau angalau umewakumbusha maana wanaangalia wenzao tu wamesahau nap wanaelekea huko huko. Biblia inasema msilaumu msije kulaumiwa ninyi. Hivyo anayelaumu leo ajiandae kulaumiwa pia kesho.
 
Hakuna urozi wala mavumba,sisi asili yetu hatutikiswi na mapenzi bora niende nikale michunga kuliko kutikiswa kusiko sababu
Umesema vyema sana sisi hapa tuna watoto tena wa 3 siwezi kusema wanangu ni zaidi, hapana maana mtoto ni mtoto kwa baba yake ila mama mkwe anataka kufanya kua yule wa nje ndie mtoto hawa wangu ni mashetani kitu ambacho kinanifanya nichume dhambi kwa kuanza kua na chuki na yule mtoto bure wakati nimemkuta kabla ya kuolewa na nilikubali, more mama mkwe anapotaka kunitawala kwa kuongea na mama wa mtoto kwenye simu kisha kumpa mwanae amsalimie inanikwaza mnoo, na sielewi dhamira yake kwangu
Hii comment nimekuelewa vizuri sana. Ukiolewa na mwanaume mwenye mtoto/watoto, mara nyingi tegemea ndugu wa mume wako kuside up na watoto wa nje, at least kwa familia chache nilizo-observe. Tena na hivi watoto wa nje ndo wakubwa afu ukute ni wa kiume, basi wao ndo wanaonekana kama warithi, wa kwako hawafai. Ndo hayo mtu unaanza kujenga na chuki. Itokee mumeo ndo aeanza kutangulia (God forbid), na hamna wosia, basi jiandae tu kisaikolojia mpendwa, utalia kwa mengi. Huwa sielewi hawa ndugu za waume zetu kugeuka maadui zetu once tukiolewa. Ukute hata huyo mdada alozaa na mumeo anapendwa tu kwa sababu yupo nje, siku na yeye akiolewa ataionja joto ya jiwe.

Huyo mama mkwe wako naona anavuka mipaka yake sasa. That's too much jamani akhuu
 
Back
Top Bottom