Mama mkwe ananing'angania

Mama mkwe ananing'angania

Anajua mkuu!

Sababu ya yeye kuja kwako ipo wazi kwamba anataka kufufua mahusiano.

Na wewe sasa cha msingi ni kumkalisha chini na kumueleza upya kinagaubaga bila kuuma maneno kwamba hayupo moyoni mwako tena.
 
Sababu ya yeye kuja kwako ipo wazi kwamba anataka kufufua mahusiano.

Na wewe sasa cha msingi ni kumkalisha chini na kumueleza upya kinagaubaga bila kuuma maneno kwamba hayupo moyoni mwako tena.

Nashukuru mkuu!
 
You were brave enough to say goodbye to her, now life has reward you with a new hello,so embrace the chance given by the mother in law!
 
jamaa utapata mpz atakaye kupenda kwa dhat kisa kutanguliza pesa.. tumia akir ww.. hao ndg mambo yatakuwa vilevile achana nao find mtu mwngne kwa makin usitangulize pesa ww huna hera pesa zpo 2
 
Hivi wewe umesoma chuo kipi? Mwanafunzi wa chuo ndio anaandika namna hii?

Hicho ni chuo cha makanjanja na wazee wako walipoteza wakati na fedha zao bure kukupa elimu ambayo huwezi kuitumia hata kwa kuandika sawa.

Kweli kabisa. huyu jamaa ni kama vile hajasoma chuo. Hata kama ulikuwa science lakini namiini hata kiswahili cha drs la sita kinatosha kuandika kwa mpangilio.
 
Sio zambi kuoa huyo shemeji yako, na kama wazazi wameridhia OA mkuu.
Kuna baadhi ya mila zetu za kiafrika zinaruhusu hiyo kitu na sometime hata mke akifa unapewa ndg yake wa karibu ili kulinda ukoo usipotee.
 
Naah don't jump the broom with the little sister. Just smash it and quit it and tell everybody that you did it.

And if the mother is easy on the eye, go right ahead and smash her too.

It's called buy one get two free. It doesn't get better than that.

Kwa kiswahili....ukipenda ua penda na boga lake.
 
aisee.......kwa hiyo mama mkwe anakung'angania!
 
Nilikuwa na mpenzi wangu tulisoma wote chuoni na tulipendana sana kiasi kwamba nilikuwa namgaramia kwa kiasi kikubwa na kuna kipindi aliumwa akalazwa hospitalini mimi nikawa siattend vipindi kwa ajili ya kumuhudumia yeye.

Zaidi nilishaenda nae kwao japo sikwenda kwa utambulisho rasmi lakini wazazi wake walielewa kuwa mimi ni mtarajiwa kwa binti yao!Wazazi wake walitokea kunipenda saana hasa mama mkwe ndiyo alikuwa ananipenda mpaka naogopa yani nikienda kwao napokelewa kama Rais vile sasa sijui ni kwa sababu nilikuwa naprovide mahela sana ila nachojua nilikuwa napendwa na hao wazazi!

Tuliporejea chuoni kwa masomo mwenzangu tabia yake ikaanza kubadilika akawa anaondoka chuoni sometimes haniagi na nikimpigia simu hapokei!mi nikawa nashinda kumtafuta kila kona ya hosteli bila kupata!Nikaja kuambiwa kuwa jamaa yangu wa karibu ambaye ni mfanya biashara alikuwa akitoka naye! Mi sikuamini!Hali iliendelea hivyo mpaka mimi nikaja kuhitimu masomo yeye nikamwacha akimalizia mwaka wake wa mwisho nilipoondoka mambo kwake yakazidi kuwa balaa alikuwa anatembea na yeyote atakayemtangulizia pesa!Nilikuja kusikia kuwa ametembea na mfagia vyoo vya hosteli akampa 60elfu! Hapo mi niliamua kumpiga chini baada ya kugundua ukweli wa mambo anayoyafanya! Sasa wazazi wake bado naendelea kuwa na mahusiano nao mazuri sometimes nawatumia pesa za matumizi licha ya kwamba wanajua binti yao sipo naye ktk mahusiano ya kimapenzi zaidi ya mawasiliano na tunaitana kaka na dada!

Sasa Mama yake alinipigia simu akaniuliza "endapo binti yake atakuwa amebadilika kitabia na akataka turudiane Je niko tayari?" Mi nimemjibu sipo tayari,Basi tokea hapo yule mama ananing'ang'aniza akanambia nimwoe hata mdogo wake na yule mdada niliyekuwa naye! Sasa wadau naomba ushauri nifanyaje manake napatwa na kigugumizi manake hata huyo mdogo wake ni mzuri sana wa umbo ila sijajua tabia yake!Na je ntakuwa sahihi endapo nitaoa mdogo mtu!?

kama ushawahi 'tembea' na huyo ambaye ndoto yenu haikutimia si vyema hata kidogo kwa huyo mdogo mtu
 
Nashukuru ndugu yangu manake wanataka niende mwezi huu eti nikawasalimie manake ni mda mrefu hawajaniona! Na mama mtu ananambia eti huyo mwanae ananipenda sana! Kinachonikatisha tamaa ni kabila lao na historia niliyoipata juu ya kabila lao! Wao ni" WAMBURU" kwao ni Karatu na mi nipo DSM ndiyo makazi yangu!Inakuaje hapo ndugu yangu!?

Mbulu!!!! Kimbia ufe
 
Back
Top Bottom