Mama mkwe ameniuliza mimi na mtoto wake tulikutana wapi?

mjibu tu kilabuni,kwani si umeshamuoa,hatakunyang'anya mkeo,mimkwe mingine bwana


Anayeuliza swali ni "mke"si "mme".

Kwanini aseme klabuni hata kama hawajakutana klabuni.


Kwanini asimueleze ukweli?
 
Kwahiyo mkoa anaotoka mume wako unaitwa " Mkoani".

Nilijibu swali kuwa, mama mkwe hatukai nae, amekuja tu katika mji tunaishi lakini anaishi mkoani. Ni moja ya mikoa ya Tanzania.
 
Ok, Inategemeana amekuuliza katika mazingira gani? kama maongezi ya kawaida si unarespond tu tokana na kile mlichokuwa mnaongelea!! Lakini alipaswa kuuliza wakati wa Harusi.

Ndiyo utata unapokuja, ameniuliza baada tu ya salamu, hata hatukuwa kwenye hali ya utani.
 
Mkoani ni kwa mfano, wewe ukiwa una kaa ifakara, halafu mkweo anakaa Morogoro manispaa,
Hapo sasa ndio unasema mkweo anakaa mkoani wewe unakaa wilayani.

Asante sana, elimu haina mwisho leo nimejifunza jambo geni kutoka kwako. Kiswahili lugha kubwa.
 
umeulizwa swali rahisi lakini nadhani kwa kuwa moyo wako una hila ukataka kuleta timbwili la Fatuma Ndala Ndefu

Watu8 Sina timbwili la Fatuma Ndala Ndefu, huyu ni mama na ninamheshimu sana, tena ukizingatia tumekutana ukubwani, afadhali mama yangu angeweza kunitania kwani ananijua tangu nikiwa mdogo. Kama nilikuwa changu na mwanae alikuwa mteja wangu mzoefu akanogewa inapaswa kweli ayajue hayo?
 
Leo asubuhi, baada ya kumsalimia mama mkwe, ameniuliza mimi na mtoto wake tulikutana wapi? Nimeshindwa kumjibu kwasababu sijaelewa mantiki ya swali lake.

1. Akishajua itamsaidia nini?

2. Au hajaridhika kuwa mimi nina hadhi ya kuwa mkwe wake?

Huwezi kujua alikuwa na nia gani kuuliza hivyo, yeye mwenyewe ndio anajua kwa nini kauliza hivyo.
Kwa vile umesema ni mama mkwe wako, maana yake ni kwamba hiyo sio mara yenu ya kwanza kuonana, ingekuwa ni mara yenu ya kwanza kuonana then ingekuwa fifty fifty. Wazazi karibu wote(wa mke/ wa mume) wanaulizaga hilo swali behind the scene, lakini yeye ameuliza na wewe ukiwepo hiyo ndio tofauti, lakini maana ni ileile.
Wazazi wengi wanapenda kujua mtoto wao amempata wapi mwenza.
 
Wewe umeulizwa kirahisi tu kuwa "Ulikutana wapi na mwenzio?"...lakini akilini kwako ukaanza kujenga maswali mengiii
Labda na mimi nikuulize, ni kitu gani kinachokufanya ushindwe kulijibu hilo swali?

Watu8 Sina timbwili la Fatuma Ndala Ndefu, huyu ni mama na ninamheshimu sana, tena ukizingatia tumekutana ukubwani, afadhali mama yangu angeweza kunitania kwani ananijua tangu nikiwa mdogo. Kama nilikuwa changu na mwanae alikuwa mteja wangu mzoefu akanogewa inapaswa kweli ayajue hayo?
 
Hukumbuki mlikutana wapi? Kama unakumbuka mwambie tu, mbona simpo? Usijibu hayo maswali mengine ambayo hujaulizwa mkuu!
 
Leo asubuhi, baada ya kumsalimia mama mkwe, ameniuliza mimi na mtoto wake tulikutana wapi? Nimeshindwa kumjibu kwasababu sijaelewa mantiki ya swali lake.

1. Akishajua itamsaidia nini?

2. Au hajaridhika kuwa mimi nina hadhi ya kuwa mkwe wake?
Swali hilo aliuliza akiwa ktk haligani, hasira, furaha,aukawaida? Vipi hali yako na yake kimaisha, nani mwenye hadhi ya juu zaidi ya mwenzie? Kwakuanzia hapo tutajua alichokua akikimaanisha.
 
alitaka mkutane wapi yeye
wakati mwingine wazazi na sie tuna mastress yetu
halafu tunayahamishia kwa watoto
mpeni alichofuata aweze kurudi kwake.
 
Kwanini asimuulize mwanae jamani! Na hata mwanae kimsingi hapaswi kumuuliza swali kama hilo. Wakwe wengine, mungu awasamehe tu

Kuna dalili wewe ndo una matatizo! Swali la ulikutana wapi na mwenzio linakuumiza kichwa? Au hukukutana nae?. Ungeulizwa kwanini ulimchagua huyu mwenzio ungepata jibu kweli? .
Ushauri, ktk maisha usipende kuwaza kuwa hata kwa kilicho wazi kina maani iliyojificha. Utagombana na watu utaharibu mahusiano yako. Kwa taarifa yako huyo mwenzio ni mtoto wa huyo aliyekuuliza hilo swali -mtoto wa nyoka ni nyoka,tarajia mwezio atakuwa akikuuliza maswali ya hivihivi.sasa nayo yatakunyima raha?
 
Mkoani ni kwa mfano, wewe ukiwa una kaa ifakara, halafu mkweo anakaa Morogoro manispaa,
Hapo sasa ndio unasema mkweo anakaa mkoani wewe unakaa wilayani.


Yeye anamaanisha kuwa mkoani ni mkoa mojawapo Tanzania.
 
Ndiyo utata unapokuja, ameniuliza baada tu ya salamu, hata hatukuwa kwenye hali ya utani.

Kuna maswali mengine halipatikani jibu mpaka muulizwaji nayeye aulize swali. Ulichotakiwa kufanya nawewe unge muuliza nini maana ya swali lake au alimaanisha nini ktk kukuuliza hivyo. Hapo ungepata maana na dhamira ya swali lake, kishaa jibu linge kuja lenyewe.
 
Hisia zako zinakutesa tu mwambie ukweli kwani akijua atafanyaje?

Sent from BlackBerry 9800 using JamiiForums
 
Mawazo mabaya huleta matokeo mabovu ukianza na fikra za kipuuzi namna hiyo hata hiyo ndoa utaiona chungu na hakuna jema utaliona kwa mama mkwe wako BTW HUYO NI MAMA YAKO KAMA ALIVO MAMA YAKO WA KUKUZAA.

(anaweza kuwa ni mtu wa utani alitaka akuchekeshe kitu huo ni mtizamo wangu KILA LA HERI)

uko sahihi mkuu pia nakubaliana nawewe..,,,unajua nn? tatizo watu wameshaweka pandikizi za chuki na fikra chafu juu ya mama mkwe/wakwe,,....mama ako mzazi angekuuliza kua huyo mumeo mlionana wapi pia ungeshindwa kumjib?,,..au kwasababu ni mama mkwe basi imekua nongwa?........tubadilike jaman
 
mmmh huyo mama analake jambo ili kumkata stim mwambie mlikutana bar usiku then mwanae akavutiwa na unywaji wako, mlipomaliza kunywa mkaingia disco kulimwaga sebene asubuhi mkajikuta mpo gest ndipo mwanzo mlipokutana kimwili.au ye anataka kujua sehemu tu? manake kukutana kuna maana zaidi ya moja.mama mkwe wengine bana looh

daaaa mkuu nimependa hilo jibu lakin inawezekana kauliza kwa maana nzur tu jaman tusifikirie mabaya kila siku jama
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom