Amenipigia Abby nikambuka Aggy

Sean Paul

JF-Expert Member
Jun 16, 2013
807
2,107
Aggy ni mtoto aliyelelewa kanisani Pentecoste haswaa. Baba yake akiwa mtumishi wa hospitali ya kanisa hilo naye ni mzee wa kanisa kwa miaka mingi, bila kumuacha nyuma mkewe.

Mimi na Aggy tulikutana August mwaka 2012 sote tukiwa maafisa wa sensa ya watu na makazi wilaya moja ya mkoa wa Pwani kati ya hizi zinazozunguka mkoa wa Dar es Salaam. Nilikua bado nasoma chuko kikuu naye alikua kahitimua form 4 miaka 2 au 1 nyuma. Haikuwa kazi ngumu sana kumpata Aggy sababu alishaonesha kunizimia yeye mwenyewe. Penzi likaanza na likawa linaendelea vizuri. Kwa maelezo ya Aggy, mimi nilikua mwanaume wake wa pili baada ya huyo aliyefungua njia. Baadae kidogo, yaani 2013 akapata nafasi ya kujiunga JKT kwa hiyari akakaa sana huko. Niliendelea kuwasiliana naye alipokuwa JKT, lakini kuna kauli yake ilikua inanikwaza sana "tukionana lazima tupime HIV kabla ya majamboz". Nilishamueleza mimi sina tatizo juu ya hilo, lakini alikua karibu kila siku anakumbushia. Siku moja nikawa mkali, nikamwambia mama kwani unaniona mi malaya sana au vipi? Mbona hili suala kila siku unalisema sema, tumeshakubaliana kuwa tutapima, shida iko wapi?
Ilikua kama nimechokoza nyuki, simu ilikatwa na message za maneno ya hovyo zikaanza. Hii kwangu ilishakuwa red flag, ikabidi nimchane live. Mama mbona kama ulikuwa unatafuta sababu ya kugombana na mimi?
Kama ushampata afande huko kambini niambie tu usitafute ugomvi. Akasema poa, akinitafuta tena mimi basi mk**u wake ugeuke reli na train ipite. Nikasema La haula, mlokole wangu jeshi lishamfanya kuwa mhuni mpaka anaandika matusi hivi. Ukimya ukatawala na penzi likafia hapo.

SIku moja nasoma gazeti nikakuta jina lake ni kati ya watu waliochaguliwa kujiunga jeshi la polisi. So nikawa na info anaenda CCP Moshi. Ukimya ukaendelea. Mwaka 1 mbele yaani 2015, Aggy akanipigia akaniambia yuko Bukoba ni afisa wa polisi. Wakati huo tayari mimi naishi Mwanza. Aggy anaomba turudiane, nilikataa. Tukaishia kuwa marafiki na zaidi yeye ndio alikua ananitafuta. Baadae tukapotezeana tena.

Miaka 4 mbele yaani 2019, Aggy akanipigia tena. Safari hii akaja na taarifa mpya, kuwa alipata bwana akampa na mimba na mama yake mzazi (mama Aggy) alisafiri hadi huko BK kwenda kumsapoti alipojifungua. Lakini jamaa aliyempa mimba alionesha disrespect kwa mama mkwe na wala hakujali na alipomshauri akaombe radhi jamaa akamrusha rusha tu mpaka bi mkubwa akaondoka.......too good hawakuwa wakiishi pamoja na huyo bwana. Hakuweka wazi ni nini alifanya kwa mama mkwe , lakini pia suala la kwenda kutoa posa kwao jamaa haeleweki. Aggy kwa mara nyingine akauliza kama tunaweza kurudiana. Nikamwambia nimeowa na nina mtoto 1 na mke wangu mjamzito. Kama unaweza kuwa mchepuko karibu. Too bad mimi nilishahamishwa Mwanza nimerudishwa Dar. Akasema mwezi wa 7 anachukua likizo atakuja nimzagamue. Kumbe hata dalili ya ndoa sikuwa nayo. Akapotea tena hewani mpaka sasa sijui kama yu hai au amekufa.

Sasa leo tena amenipigia Abigael, x wangu tuliyetengana mwaka 2021. Huyu ni MD kwa sasa, turning 29 this Feb. Sikuwa na namba yake, baada ya kujitambulisha ndio nikajua ni yeye. Kajichekesha chekesha hapo, mara wifi hajambo na bla bla nyingi.......mwisho ntakutafuta baadae. Anataka nini?
 

Attachments

  • 37d0ae49f25243b780b256d0e5e7d686.jpg
    37d0ae49f25243b780b256d0e5e7d686.jpg
    29.4 KB · Views: 9
Back
Top Bottom